Jumamosi, 18 Mei 2019

4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?


4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Maneno Husika ya Mungu:
Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama. Lakini mwanadamu ni tofauti: Kutokana na kupata kiwango cha chini cha nguvu za Roho Mtakatifu, yeye huchukulia kwamba hakuna chochote kitakachobadilika; baada ya kupata ufahamu kidogo, hajipi msukumo wa kufuata nyayo za kazi mpya ya Mungu; licha ya kwamba ameona kiasi kazi ya Mungu, yeye anamchukulia Mungu kama kifaa, aina fulani ya umbo la sanamu ya mti, na anaamini kwamba Mungu atasalia kuwa hivyo daima kwani hali imekuwa hii tangu hapo awali na hata katika siku zijazo; akiwa amepata ufahamu wa kijuujuu, mwanadamu ni mwenye kiburi hivi kwamba hujisahau na kuanza kutangaza kwa fujo tabia ya Mungu na hali ya Mungu ambayo haipo; na akiwa na uhakika juu ya hatua moja ya Roho Mtakatifu, pasi kujali ni mtu wa aina gani ambaye anatangaza kazi mpya ya Mungu, mwanadamu huwa haikubali. Hawa ni watu ambao hawawezi kuikubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu; ni watu wenye kushikilia ukale sana, na hawawezi kukubali mambo mapya. Watu kama hawa ni watu wanaomwamini Mungu lakini wakati uo huo wanamkataa Mungu. Mwanadamu anaamini kwamba wana wa Israeli walikosea “tu kumuamini Yehova na kukosa kumuamini Yesu,” huku watu wengi wakiiga jukumu ambapo “humwamini Yehova tu na kumkataa Yesu” na “kusubiri kwa hamu kurejea kwa Masihi lakini wanamkataa Masihi ambaye ni Yesu”. Ndiyo maana, basi, watu wengi bado wanaishi chini ya mamlaka ya Shetani baada ya kukubali hatua moja tu ya Roho Mtakatifu na bado hawapokei baraka za Mungu. Je, si hii ni kutokana na uasi wa mwanadamu? … Hata ingawa wana “uaminifu wa hali ya juu” kwa maneno yaliyozungumzwa na Mungu; maneno yao na matendo yao bado hukera kwa sababu wao huipinga kazi ya Roho Mtakatifu, na kufanya uongo na uovu. Wale wasiofuata hadi mwisho kabisa, ambao hawazingatii kazi ya Roho Mtakatifu, na ambao wanashikilia kazi ya zamani hawajakosa tu kupata uaminifu kwa Mungu, bali kwa kinyume, wamekuwa wale wanaompinga Mungu, wamekuwa wale ambao wamekanwa na enzi mpya, na watakaoadhibiwa. Kuna wa kuhurumiwa zaidi kuliko wao?
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mwanadamu akiniita Yesu Kristo kila wakati, lakini hajui kuwa Nimeianza enzi mpya katika siku za mwisho na Nimeanza kazi mpya, na mwanadamu akingoja kwa shauku kuwasili kwa Yesu Mwokozi, basi Nitawaita watu kama hao wale wasioniamini. Wao ni watu ambao hawanijui, na imani yao Kwangu ni ya bandia. Je, watu kama hao wanaweza kushuhudia kufika kwa Yesu Mwokozi kutoka mbinguni? Wanachongoja si kufika Kwangu, bali ni kufika kwa Mfalme wa Wayahudi. Hawatamani maangamizo Yangu ya dunia hii nzee yenye uchafu, lakini badala yake wanatamani kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili, ndipo watakapokombolewa; wanamtazamia Yesu kuwakomboa wanadamu wote mara nyingine kutoka nchi hii iliyochafuliwa na isiyo na haki. Watu kama hao watawezaje kuwa wale wanaoikamilisha kazi Yangu katika siku za mwisho? Matamanio ya mwanadamu hayawezi kufikia mapenzi Yangu ama kutimiza kazi Yangu, kwani mwanadamu hutamani au kuthamini tu kazi ambayo Nimeifanya hapo awali, naye hajui kuwa Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mpya siku zote na si mzee kamwe. Mwanadamu anajua tu kuwa Mimi ni Yehova, na Yesu, naye hana fununu kuwa Mimi ni Mwisho, Yule ambaye Atawaangamiza wanadamu. Mwanadamu anachotamani na kujua tu ni kuhusu dhana yake mwenyewe, nayo ni yale tu ambayo anaweza kuyaona kwa macho yake mwenyewe. Hayako sambamba na kazi Ninayoifanya, bali hayatangamani nayo.
kutoka katika “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mkitumia dhana kupima na kufafanua Mungu kwa maneno, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiobadilika, na mkiwekea Mungu mipaka katika Biblia, na kumweka katika wigo wenye mipaka wa kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemshutumu Mungu. Kwa sababu katika mioyo yao, Wayahudi wa Agano la Kale walimtazama Mungu kama sanamu ya udongo, kana kwamba Mungu angeweza tu kuitwa Masihi, na Yule pekee anayeitwa Masihi ndiye Mungu, na kwa sababu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Alikuwa sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—wakimhukumu Yesu asiye na hatia kufa. Mungu alikuwa hajatenda uhalifu wowote, ilhali mwanadamu hakumsamehe Mungu, na kumhukumu Yeye kifo bila kusita. Na ndivyo Yesu Akasulubishwa. Mwanadamu kila wakati huamini kuwa Mungu habadiliki na humfafanua kulingana na Biblia, kana kwamba mwanadamu amebaini usimamizi wa Mungu, kana kwamba kila kitu Atendacho Mungu kiko mikononi mwa mwanadamu. Wanadamu ni wa kufanya mzaha kupita kiasi, wana kiburi kikubwa sana, na wote wana kipaji cha lugha ya kushawishi ya kujivuna. Bila kujali kiwango chako cha ufahamu kumhusu Mungu, bado Nasema kwamba humfahamu Mungu, kwamba hakuna walio wapinzani wa Mungu zaidi, na kwamba unamshutumu Mungu, kwa kuwa huna uwezo wa kuiheshimu kazi ya Mungu kabisa na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa kamili na Mungu. Ni kwa nini Mungu hatosheki kamwe na matendo ya mwanadamu? Kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu, kwa sababu ana dhana nyingi sana na kwa sababu badala ya kufuata uhalisi, maarifa yake yote ya Mungu yametolewa kwa chanzo kimoja, chenye ugumu na kisichobadilika. Hivyo, kwa kuwa amekuja duniani leo, Mungu Amesulubishwa kwa mara nyingine na mwanadamu.
kutoka katika “Waovu Lazima Waadhibiwe” katika Neno Laonekana katika Mwili
Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni zaidi, kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?
kutoka katika “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili

0 意見:

Chapisha Maoni