Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kanisa. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kanisa. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 12 Juni 2019

Hukumu ni Mwanga

Wokovu wa Mungu, Mkristo, Ushuhuda wa Maisha

Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.
Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: “Unaamini katika uwepo wa Mungu?” Nilijibu: “Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo.” Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu yako itarejea: ukiwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani ulipopotea kwa wakati mmoja, ukianguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na baba. Unatambua zaidi kuwa mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.
Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: “Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri.” Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?” (“Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninang’ang’ana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kumtegemea Mungu kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.
Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama “Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka.” Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikifuatilia ilikinzana na mapenzi ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: “Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako.” Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani. Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: “Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia.” Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “Kama ulitumia juhudi nyingi lakini bado Sikuchangamkii, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika uvunguvungu? Ikiwa, baada ya wewe kutumia vitu fulani kwa ajili Yangu, Sijatimiza mahitaji yako madogomadogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi au hata kuwa na ghadhabu na kunitusi?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena.” Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote kutafuta mahali salama, mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?” (“Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kulinifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, sikuwa na budi ila kuhisi aibu, kana kwamba sikuwa na mahali pa kujificha, na nilihisi kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na nilihitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: “Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu , pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako.”
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. … Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia hiziana asili ya aina gani? Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika “Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha”: “Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. … Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili” (“Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha I). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu. Alinihukumu na kuniadibu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.
Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.
Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu. Utukufu wote uwe kwa Mungu. Amina!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Ijumaa, 7 Juni 2019

Ni kwa Kuingia Katika Ukweli Mimi Mwenyewe tu Ndio Ninaweza Kuwasaidia Wengine

Ushuhuda wa Maisha, Wakristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu

Du Fan Mkoa wa Jiangsu
Hivi karibuni, kanisa moja lilikuwa linakipiga kura ili kumchagua kiongozi mpya, lakini kiongozi aliyeongoza alienda kinyume na kanuni za kanisa, akitumia njia yake mwenyewe kutekeleza upigaji kura. Wakati ndugu fulani wa kiume na wa kike walipotoa maoni yao, sio tu kwamba hakuyakubali, lakini alisisitiza kushikilia njia yake mwenyewe. Baadaye kanisa lilitupwa katika mchafuko kwa ajili ya vitendo vya kiongozi huyo. Nilipopata kujua, nilikasirika kabisa: Mtu anawezaje kuwa mwenye kiburi mno na wa kujidai? Kutekeleza wajibu wa kiongozi wa kanisa bila Mungu ndani ya moyo wake, kuangalia kwa dharau mipango ya kazi, kupinga na kukataa mapendekezo ya ndugu wa kiume na wa kike—ni nani mwingine wa kulaumiwa kwa mchafuko wa kanisa ila wewe! Papo hapo nilimtuma mtu kuwasiliana kwa karibu na kiongozi wa kanisa na, wakati ule ule, nikapitia neno la Mungu kutafuta ukweli unaohusika ambao ningeuibua na kiongozi ili kumridhisha kuhusu makosa yake. Baadaye usiku huo, nilikwenda na kukutana na kiongozi. Wakati wa ushirika, nikamwambia kwa sauti ya mashtaka, nikishindwa kuzuia hasira yangu mwenyewe. Nilishangaa kuwa, dakika kumi katika mkutano wetu, kiongozi ghafla aliinuka na kutimua nje akiwa na machozi machoni mwake. Ndugu aliyekuwa ameenda kumfuata alirudi baadaye kidogo na kusema, “Amekwenda na anajua amefanya makosa.” Nilikuwa siachilii, nikiguta kwa hasira: “Kuhusu suala muhimu jinsi hii la kanuni, uko tayari kuacha mambo tu kama hayajatatuliwa? Jinsi wewe ulivyo mwenye kiburi mno na wa kujidai! Unaenda kinyume na kanuni za kanisa na humruhusu mtu mwingine awe na maoni. Je! Unapaswaje kupata kitu chochote kifanywe wakati ujao? Ni matarajio ya hatari kweli! Hili halitakuwa sawa hasa, kama utatoka nje kwa hasira bila kusema, itanilazimu kukuandikia barua tu.” Papo hapo, nikaketi na kumwandikia barua ambamo kwa ishara nilikubali kuwa mtazamo wangu katika ushirikiano haukuwa bora na nikauliza msamaha wake. Katika barua hiyo, nilizungumzia pia masuala yake, nikitoa mfano wa kanuni ili kutambua tatizo hilo. Nilidhani kwamba nilikuwa nimeyashughulikia mambo vizuri sana. Kwa upande mmoja, nilionyesha kuwa niliweza kuacha ubinafsi wangu mwenyewe na kupata ufahamu wa kina kujihusu, wakati huo huo nikitumia ukweli kutatua masuala. Baada ya kuona jinsi nilivyoshughulikia mambo, kiongozi huyu bila shaka angeridhika na kupata ufahamu mpya, nilifikiri.
Siku moja, nilipokuwa nikiwasiliana kwa karibu juu ya jambo hili na kiongozi wangu, kiongozi aliniuliza jinsi nilivyoingia katika ukweli wakati wa kutatua suala hili. “Niliingiaje katika ukweli? Nilifanya kazi mbaya? Je! Matendo yangu yalikuwa yasiyofaa?” Nilijihisi kuchanganyikiwa kidogo. Kiongozi huyo aliendelea: “Sio suala la jinsi ulivyotatua suala hili vizuri, lakini badala yake, katika kutatua suala hilo, je, ulilitumia hadhi yako na uwezo kuwashawishi wengine au ulitumia ukweli kumkuza na kumshuhudia Mungu, na kuwaruhusu wengine kupata kujijua kwa kina? Kwa juu, inaonekana kama kwamba wewe ulikuwa ukiwasiliana kwa karibu katika neno la Mungu, lakini kwa kweli ulikuwa unajaribu kumfanya ashindwe na mtazamo wako tu. Kwa nini aliishia kwenda? Ni wazi kuwa aliondoka kwa sababu hakuweza kukubali hoja yako, hakuridhika. Kama tunajishughulisha tu na kuwasiliana ukweli kwa karibu na wengine na kupuuza kuzingatia upotovu wetu wenyewe, kupuuza kujijua wenyewe, na kufanya kazi kwa ajili ya kuifanya tu, huenda tusijifunze chochote kipya na kutopata mabadiliko yoyote katika tabia yetu wenyewe. Kwa maana hii, si sisi ni kama Paulo, ambaye alitoa mwongozo kwa wengine lakini, ambaye, katika huduma ya Mungu, alijishikilia zaidi njia zake potovu? Katika kiburi chake, akawa mtu ambaye alimwamini Mungu na bado alimpinga Mungu, akifikia mwisho wake kwa kuangamia kabisa.” Ushirika huu ulikuwa kama wito ukinitikisa kutoka kwa usingizi mrefu. Kweli, wakati Mungu alileta hali hii kwangu, sikutafuta ukweli au kutafuta nia ya Mungu, sikufikiria jinsi ya kuingia katika ukweli mwenyewe au kutafakari juu ya majibu yangu mwenyewe yenye mhemko kwa hali hiyo. Yote niliyoweza kufanya ilikuwa ni kufikiria jinsi ya kutatua matatizo ya watu wengine. Kwa maana hii, nilikuwa nikizingatia hamu ya Mungu ya kuwaleta wengine mbele Yake? Au badala yake nilikuwa nikitumia hadhi yangu kuwalazimisha wengine kuukubali mtazamo wangu? Nilipotoshwa na Shetani, bila ukweli, ubinadamu au sababu. Mimi pia nilikuwa mwathiriwa. Nilikuwaje bora kuliko mtu mwingine yeyote? Sikuwa na maarifa ya binafsi, ufahamu wa ukweli. Bila kutambua, nilikuwa nimechukua sauti kali na kukasirika, nikiitukuza hadhi yangu katika kuwaonya wengine. Kiburi changu cha kishetani na majivuno vilikuwa vimefichuliwa! Wakati dada yangu alipotimua akilia, sikufikiria juu ya matendo yangu, badala yake nikimchukia na kukasirika sana. Je, si tabia yangu ilifanana na vitendo vya kikatili vya joka kubwa jekundu?
Namshukuru Mungu kwa ajili ya uongozi Wake. Uzoefu huu ulinipa nuru kwa umuhimu wa kuingia katika uhalisi wa ukweli. Ni kwa kuingia tu katika uhalisi wa ukweli tunapoweza kupokea ulinzi wa Mungu na kutompinga Mungu. Katika mahubiri ilisemwa: “Watu wengi hugeuka viongozi wa uongo au wapinga Kristo kwa sababu hawafuatilii ukweli kwa kweli na, kwa sababu hiyo, hawana uhalisi hata chembe wa ukweli. Mara tu wanapopata hadhi na kuwa na mamlaka fulani wao huanza kutenda kwa utukutu, kuwa juu zaidi ya wote, kujipa hadhi juu ya wengine na kutamani radhi ya hadhi. Mwishowe, watu kama hao huchukiwa sana na kukataliwa na wateule wa Mungu, hatimaye wakishindwa kabisa. Hili linaweza kuwa labda tukio adimu? Kwa nini watu hawawezi kujirudi? Kuna haja gani ya kumwamini Mungu ili kupata mamlaka tu, kushika madaraka na kutamani radhi ya hadhi? Hii ni tabia ya watu wa ubinafsi, duni na waovu, ni tamaa duni ya wale wanaoitembea njia ya mpinga Kristo” (“Unapaswa Kupata Uzoefu na Kuingia kwa Uhalisi wa Ukweli wa Neno la Mungu Ili Uweze Kupata Ukamilifu wa Mungu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Kupitia kifungu hiki niligundua kwamba wale ambao hawaingi katika ukweli, baada ya kupata hadhi, watajitangaza kuwa mfalme na kwa majivuno watatumia hadhi yao kuwakandamiza, kuwasingizia, na kuwadhibiti wengine. Hatimaye watakuwa viongozi wa uongo na wapinga Kristo. Sio mamlaka yaliyowaharibu watu hawa, lakini matokeo yasiyoepukika ya kushindwa kutafuta ukweli! Ingawa inaweza kuonekana kama uzoefu huu haukuwa mbaya sana, hali yangu ya akili na asili ya kweli katika kumpinga Mungu bila kukanushika inaashiria kwamba nilikuwa nikiitembea njia ya upinzani kwa Kristo. Kama sikuwa na mwelekeo wa Mungu, bila shaka singekuwa nimetambua upumbavu wangu na bado ningekuwa nikiishi katika hali ya kujidai. Kuendelea kupitia njia hiyo, hatimaye ningefichuliwa na kufutwa! Wakati ninapofikiria jinsi mambo yangeishia, jambo hili huniogofya. Jinsi niliyoitembelea nilivyopitia matatizo, nikimwamini Mungu kwa miaka mingi sana na bado kutoweza kujua jinsi ya kuingia katika uhalisi kama Paulo, ambaye aliishi ndani ya dhana ya kufikiriwa, lakini aliendelea kumwamini na kumtumikia Mungu kulingana na tabia yake ya kawaida na asili iliyopotoka. Nisipogeuza hali ya mambo ya leo, huenda nikajipata nimehukumiwa kwa laana ya milele. Katika siku zijazo, nahitaji kuweka umuhimu zaidi juu ya kuingia binafsi na ukimbizaji wa ukweli.
Muda mfupi baada ya haya yote kufanyika, nilipokea barua kutoka kwa dada ambayo ilianza kwa kusema kuwa alikuwa na shida kuelewa ukweli na kuomba mwongozo wangu. Baada ya kusoma barua hiyo, nilipandwa na hasira tena: Wewe ni mtu mwenye kiburi jinsi gani! Huwezi kushirikiana vizuri na hao viongozi wa kanisa na wafanyakazi. Kila wakati wanapokupa mapendekezo wewe hutoa tu udhuru, ukiendelea kufanya mambo kiholela. Kazi ya injili unayowajibikia haijafanikiwa na makanisa daima hutoa taarifa juu ya hali yako. Leo unaniandikia kuniuliza mwongozo: Una uhakika unaweza kukubali mwongozo wangu? Unafikiri kwamba kila kitu ambacho umekifanya kimekuwa cha kufaa na sawa na kushindwa kwako kote kumesababishwa na watu wengine kutoweza kutenda ukweli: Ni kiasi gani unajijua mwenyewe? … Jinsi nilivyozidi kufikiria, ndivyo nilivyozidi kukasirika, ningehisi miale ya ghadhabu ikiwaka moyoni mwangu: Si uliniomba nikupe mwongozo? Nimekuwa nikitaka kuzungumza nawe kwa muda sasa, leo hatimaye nina nafasi. Nikaandika kazi zangu za sasa na kuanza shughuli za kutafuta maneno ya Mungu yanayohusiana na hali yake ambayo ningeweza kudondoa ili kumshawishi. Ilielekea kwamba, nilivyozidi kutafuta vifungu vilivyofaa, ndivyo nilivyozidi kuvikosa—nilikanganyika na vilikopotelea vifungu vyote ambavyo kwavyo nilikuwa na ufahamu fulani. Nilipokuwa tu nimeanza kupata wasiwasi, ghafla nilihisi kufedheheka: Ni wapi unatafuta neno la Mungu? Hapa mtu huyu yuko mbele yako, huwa unaingiaje katika ukweli? Kwa nini daima unajaribu kutatua matatizo ya watu wengine? Umefichua nini ndani yako? Wakati huo, moyo wangu ulitulizwa na nikaanza kufikiria kwangu mwenyewe: Je! Umesahau tayari kilichotokea wakati wa mwisho? Usifanye kazi kwa ajili ya kufanya tu—tatua masuala yako mwenyewe kabla ya kujaribu kuwasaidia wengine. Wakati huu, nilifikiria nyuma kifungu hiki cha neno la Mungu: “Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwako kutojijua. Kwanza ponya ugonjwa wako mwenyewe, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. … Je, maisha ya mtu ambaye hawezi kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu yanaweza kukomaa? Hapana, hayawezi. Lazima uishi kwa kutegemea maneno Yangu kila wakati. Katika maisha, lazima maneno Yangu yawe kanuni yako ya vitendo. Yatakusababisha kuhisi kuwa kufanya mambo kwa njia fulani ni kile Mungu anafurahia, na kufanya mambo kwa njia nyingine ni kile Mungu anachochukia; polepole, utakuja kutembea katika njia sahihi” (“Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Lazima uwe na ufahamu wa watu ambao huwa na ushirika nao na ushirika kuhusu masuala ya kiroho katika maisha, ni hapo tu unapoweza kuruzuku maisha kwa wengine na kufidia mapungufu yao. Hupaswi kuchukua sauti ya kuhubiri nao, ambao kimsingi ni msimamo mbaya kuwa nao. Katika ushirika ni lazima uwe na ufahamu wa mambo ya kiroho. Lazima uwe na hekima na kuwa na uwezo wa kuelewa ni nini kilicho katika mioyo ya watu wengine. Lazima uwe mtu mwafaka kama utawatumikia wengine na lazima ufanye ushirika na kile ulicho nacho” (“Sura ya 13” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalikuwa wazi kama ziwa la mlimani na yalinisaidia kutambua upungufu wangu mwenyewe: Wakati ninapokumbana na hali yoyote, huwa sina ufahamivu wangu kamwe na huwa siweki umuhimu wowote juu ya kile ninachokifichua ndani yangu. Kimsingi, sina Mungu ndani ya moyo wangu na sijui jinsi ya kumtegemea Yeye. Aidha, sielewi maneno mengi sana ya Mungu na siwezi kuona vitu au kutenda kulingana na maneno ya Mungu. Mungu hutaka kwamba tuishi kulingana na neno Lake wakati wote wa kila siku na kwamba tulichukue neno la Mungu kama mwongozo ambao tunapaswa kujiongozea. Yeye hutaka kwamba tufanye kile Anachopenda na kuacha kile ambacho hakiambatani na nia Yake. Je, si Mungu huyachukia yale niliyoyafichua kujihusu leo? Je, matendo yangu leo yalikuwa yakitimizaje wajibu wangu? Hapana, kwa dhahiri nilikuwa nikitenda uovu. Baadaye nilisoma “Kanuni za Kuwasaidia Wengine Kwa Moyo wa Upendo,” na kanuni ya kwanza ilisema: “Ni lazima utofautishe aina tofauti za watu kulingana na neno la Mungu. Kwa wale ambao kwa kweli humwamini Mungu na kuukubali ukweli, ni lazima uwasaidie kwa moyo wa upendo na uaminifu.” (Utendaji na Mazoezi kwa Mwenendo Wenye Maadili). Nilipata pia maneno haya ya Mungu, “Neno la Mungu linahitaji nini kama kanuni ya kuwatendea wengine? Kipende kile ambacho Mungu anapenda, kichukie kile ambacho Mungu anachukia. Hivyo ni kusema, watu wanaopendwa na Mungu ambao kweli hufuatilia ukweli na wanaofanya mapenzi ya Mungu, ndio watu ambao unapaswa kuwapenda. Wale ambao hawafanyi mapenzi ya Mungu, wale wanaomchukia Mungu, wale wasiomtii Mungu, na wale wanaodharauliwa na Mungu, ndio watu tunaopaswa kuwadharau na kuwakataa. Hicho ndicho neno la Mungu linahitaji” (“Ni kwa Kujua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa sababu Mungu anatupenda, Yeye huwa mwili na kujificha Mwenyewe kwa unyenyekevu, akifanya chochote ili kuuokoa binadamu wote. Yeye huchukia vipengele viovu vya wanadamu, lakini husikitikia udhaifu wao, bila kuwashughulikia watu kamwe kuhusu upotovu wao, lakini daima Akiwatia moyo watu kwa maonyo madogomadogo ya ari, mafundisho yasiyokwisha na upendo ili watambue makosa ya njia zao na kutafuta njia mpya ya kwendelea mbele. Mungu hunipa neema Yake, huniinua na kuniruhusu kutimiza wajibu huu ili niweze kupenda kile ambacho Mungu hupenda, kuwasaidia na kuunga mkono ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa moyo wenye upendo wanapokabiliwa na shida na kuwatendea watu wote kwa moyo mwaminifu. Mimi, hata hivyo, nilikwenda kinyume na kanuni Zake: Kwa sababu tu nilikuwa na hadhi ndogo na niliona kuwa wengine walikuwa wameonyesha upotovu wao kiasi, nilikosa kuuhurumia udhaifu wao, lakini badala yake nilitumia neno la Mungu kama silaha ya kuwakandamiza na kuwalazimisha wakubaliane nami. Si hiki ni kitendo cha chuki? Kwa ghafla nilihisi kutahayarishika na kuaibika juu ya kiburi na ujinga wangu. Baadaye, nilisoma kifungu cha neno la Mungu kutoka kwa Kanuni ya 43, “Kanuni ya Kushiriki Kutoka Moyoni”: “‘Kushiriki na kuwasiliana kuhusu uzoefu’ kunamaanisha kuzungumza kuhusu kila wazo katika moyo wako, hali yako, uzoefu wako na maarifa ya maneno ya Mungu, na pia tabia potovu ndani yako—na baada ya hayo, wengine wanatofautisha, na kukubali mazuri na kutambua kile kilicho hasi. Huku tu ndiko kushiriki, na huku tu ndiko kuwasiliana kwa kweli” (“Ili Kuwa Mtu Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kupitia kula na kunywa neno la Mungu, nilijifunza jinsi ya kuwasiliana kwa karibu na dada yangu kwa namna ambayo ingekuwa ya manufaa kwake. Wakati huu, nilipochukua kalamu, nilihisi msisimko wa upendo ukifurika ndani yangu. Nilihisi hamu kubwa ya kuufunua moyo wangu katika majadiliano na dada yangu. Wakati huu, nilijadili utambuzi wangu juu ya tabia yangu yenye kiburi na asili yangu ya majivuno na katili—sikuwa nimewatendea ndugu wa kiume na wa kike kwa usahihi, nikikosa kuonyesha upendo na huruma kwao. Katika barua niliandika yafuatayo: Kwa hakika namshukuru Mungu kwa kukuweka mbele yangu, akiniruhusu kuona uovu ndani ya moyo wangu. Kama kiongozi, sina ukweli au uhalisi. Sistahili kuwa kiongozi, kwa sababu nilishindwa kuwajibikia wajibu ambao Mungu alinipa—nilishindwa kutenda kama mtumishi mbele ya Mungu. Badala yake, nilichukua wajibu wangu kama cheo cha mamlaka, hadhi, nikijiona kuwa juu ya wengine. Nilipoona barua yako, nilijaa dharau na hukumu, na hata nikaamini kwamba nilikuwa na mamlaka ya kukupogoa na kukushughulikia. Jinsi nilivyokuwa na kiburi na majivuno! Kwa ukweli, upungufu wako ulikuwa pia upungufu na makosa yangu. Wakati mimi na ndugu zangu wa kiume na wa kike hatuwezi kufanya kazi pamoja kwa mpangilio wa kuridhisha, huyu ni Mungu akionyesha ukweli kwamba maafa haya yote ya dhiki yalikuwa matokeo ya kutoweza kwangu kuingia katika ukweli kwa ushirikiano wenye kuridhisha. Asante Mungu kwa ufunuo huu, ambao ulinisaidia kutambua kwamba licha ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi, bado sijapata ufahamu juu ya wokovu wa Mungu wa wanadamu. Bado sijaielewa nia ya Mungu katika kuwaokoa wanadamu. Sijui ni kwa njia gani mwanadamu anapaswa kuokolewa na kukamilishwa. Kutokana na haya, katika hali yoyote ninayoweza kuikabili, sijaweza bado kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, kushughulikiwa na kupogolewa. Badala yake, daima mimi hugaagaa katika mambo ya juujuu. Kama haungekuwa umenituma barua hii kunifichua, singekuwa nimeona asili ya suala langu. Hebu sote tufanye mazoezi ya kuingia katika uhalisi wa ukweli siku zijazo.
Wakati kwa kweli nilipoiacha nafsi yangu, nikaja kujijua na kujichangua, na kutumia hali halisi ambayo nina uzoefu nayo kuwasiliana kwa karibu na kuingia katika ukweli na dada yangu, nilijihisi kuwa na mwenye hekima kabisa na kuwa na amani na kuona kuwa hakukuwa na umbali na utengano kati yetu. Kwa kweli niliona alama ya baraka ya Mungu katika hali ambazo nilitenda ukweli. Ni kwa njia ya mwongozo wa mfululizo wa Mungu na kupata nuru tu, ambapo mimi, ambaye ningeweza kuzungumza juu ya ukweli tu lakini sio kuutumia, ambaye nilipitia uzoefu kwa kutoonyesha hisia bila kuingia katika uhalisi wa ukweli, polepole nilianza kuboreka. Niliona tabia takatifu na ya haki ya Mungu katika uzoefu wangu wa zamani. Kama vile tu kifungu katika mahubiri kilisema, “Popote palipo na upotovu, patakuwa na hukumu, popote palipo na uovu, patakuwa na kuadibu” (“Zile Hatua Tatu za Kazi ya Mungu tu Ndizo Kazi Kamili ya Wokovu wa Wanadamu” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha). Pia nilikuja kuwa na ufahamu zaidi na zaidi kwamba hukumu ya Mungu na adabu ndivyo tu tunavyovihitaji. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu ni zawadi ya wokovu mkubwa na neema. Ni kwa kupokea hukumu hii na kuadibiwa tu tunapoweza kupokonywa kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, tuondoe giza, tutafute mwanga na ukweli, tuingie katika ukweli, na tutende ukweli. Naomba kwamba hukumu na adhabu ya Mungu vinifuate popote nitakapokwenda, ili niweze kupata usafi na kuishi kama mwanadamu wa kweli.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumatano, 5 Juni 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kupitia Upendo Maalum wa Mungu

Uzima wa kanisa, Mkristo

Jiayi Mji wa Fuyang, Mkoa wa Anhui
Asili yangu ni ya kiburi hasa; bila kujali ninafanya nini, mimi daima hutumia werevu na ujuzi wa kubuni ili kuonyesha akili yangu na kwa hiyo mara kwa mara hukiuka mipango ya kazi ili nifanye mambo kwa njia yangu mwenyewe. Mimi ni mwenye kiburi hasa kuhusu kuchagua watu kwa cheo fulani. Ninaamini kuwa nina talanta ya kipekee na umaizi ambavyo hunisaidia daima kumchagua mtu sahihi. Kwa sababu ya hili, nilipomchagua mtu, singechunguza kwa dhati ili kuelewa hali zote za mtu niliyetaka kumchagua. Pia singewapima kwa makini watu ambao ninataka kuchagua kulingana na maadili yanayohusiana. Matokeo ya hili yalikuwa ni kwamba niliishia kuwachagua watu fulani wenye hila na udanganyifu waliozungumzia tu masomo na mafundisho ili kujichukulia majukumu muhimu katika kanisa. Hili lilisababisha hasara kubwa kwa kazi na pia kwa maisha ya ndugu zangu wa kiume na wa kike. Hatimaye, kutokana na ukosefu wangu wa kazi halisi katika huduma ya Mungu, nilikataliwa na Mungu. Nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kuondolewa kwa huduma.
Nilipopata habari kwamba ningepaswa kubadilishwa, niliduwaa. Ilikuwa vigumu kufikiria kwamba jambo kama hili lingenitokea. Baadaye, nilianza kutomwelewa Mungu na kumhoji: Kanisa lilinibadilisha na halikunipa kazi yoyote. Ilionekana kama shida yangu ilikuwa mbaya sana. Iliwezekana kwamba ningefukuzwa. Watu wengine walikuwa wamefukuzwa hapo zamani kwa sababu walikuwa wamefanya kazi bila uangalifu na walimdanganya Mungu na walidakiza pakubwa na kusumbua kazi ya kanisa. Na wengine walikuwa wapinga Kristo kwa sababu walijitukuza, wakajishuhudia, na wakashindana na Mungu kwa ajili ya watu Wake waliochaguliwa. Hata zaidi si ningefukuzwa leo kwa sababu nimefanya kazi kwa kuzembea, nikamdanganya Mungu, nikajiinua, nikajishuhudia, na nikadakiza pakubwa na kusumbua kazi ya kanisa? Kwa kuona baa hili nililolisababisha, nilitetemeka kwa hofu. Moyo wangu ukasema mfululizo: Nimekwisha. Wakati huu nimekwisha kabisa. Nilikuwa nimempinga na kumkosea Mungu mara nyingi. Mungu bila shaka hangeninusuru. Ingawa Mungu alikuwa amesema kuwa Yeye anafanya kila kitu anachoweza kuwaokoa wanadamu, ilihusika na wale ambao walikuwa wamepotoka kidogo na wale waliofanya makosa madogo. Mtu mwenye kiburi na mwenye majivuno kama mimi mwenyewe ambaye hakuweza kumtambua Mungu na kutenda aina zote za dhambi bila shaka angepatwa na adhabu ya Mungu. Hata kama ningejitahidi kufanya mwanzo mpya, Mungu hangenisamehe, kwa sababu matendo yangu yalikuwa yamesababisha Mungu kupoteza tumaini nami na kumhuzunisha Yeye mno sana…. Pasipo kujua, nilizama katika maumivu na kukata tamaa.
Katika maumivu yangu makubwa, nilitamani kuwa kanisa lingenipa fursa nyingine ya kutimiza wajibu fulani. Lakini kila wakati wazo hili lilipokuja katika mawazo yangu, maneno “dhambi nzito” yangetangua na kugubika dalili yoyote ya matumaini. Maumivu, kujilaumu, mapambano, na matamanio yangu yalinitesa, yakanisababishia maumivu mengi kiasi kwamba sikutaka kuishi. Nilikaribia kuchanganyikiwa katika kukata tamaa kwangu. Wakati huu tu, nilisoma neno la Mungu likisema, “Mungu hapendi waoga; Anapenda watu wenye azimio. Hata kama umeonyesha upotovu mkubwa, hata kama umepitia barabara nyingi zilizopinda, au hata ikiwa njiani umekuwa na makosa mengi au umemkataa Mungu—au kuna watu wengine ambao wanamkufuru Mungu mioyoni mwao au wanamlaumu Yeye, wana mgogoro naye—Mungu hatazami jambo hili. Mungu huangalia tu ikiwa siku moja mtu ataweza kubadilika au la. … Ni kwamba mapenzi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ni ya kweli. Anawapa watu fursa za kutubu na fursa za kubadili, na wakati wa mchakato huu, Anawaelewa watu na Anajua udhaifu wao kwa kina na kiwango cha upotovu wao. Anajua kwamba watajikwaa. … Anaelewa matatizo ya kila mtu, udhaifu, pamoja na mahitaji yake. Hata zaidi, Anaelewa shida gani kila mtu atakabiliwa nazo katika mchakato wa kuingia katika mabadiliko, na aina zipi za udhaifu na kushindwa zitakazotokea. Hili ni jambo ambalo Mungu anaelewa zaidi. Ndiyo maana inasemwa Mungu huona ndani ya vina vya mioyo ya watu. Haijalishi wewe ni dhaifu kiasi gani, mradi huliachi jina la Mungu, mradi humwachi Mungu au njia hii, daima utakuwa na fursa ya kufikia mabadiliko katika tabia. Na ikiwa tuna fursa ya kufikia mabadiliko katika tabia basi tuna matumaini ya kuendelea kwetu kuishi. Ikiwa tuna matumaini ya kuendelea kwetu kuishi, tuna matumaini ya kuokolewa na Mungu” (“Ni Nini Maana ya Mabadiliko Katika Tabia na Njia Kuelekea Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilisikiliza pia maneno haya kutoka kwa mahubiri, “Mungu anafanya yote Anayoweza ili kuwaokoa wanadamu. Hasa wakosaji, watu hudhani kuwa wamepita kiwango cha kuokolewa, lakini Mungu hayuko tayari kukata tamaa juu yao na bado anataka kuwaokoa. Watu wengine wana makosa makubwa. Mungu aliwaambia, 'Unahitaji tu kurudi kwa kujitolea ulikokuwa nako kabla na kufuatilia ukweli. Bado Nataka kukuokoa.' Bila kujali ni makosa gani uliyo nayo, mradi una dhamira ya kutomwacha Mungu kamwe na hamu ya kutafuta wokovu, basi Mungu hatakata tamaa na wewe” (“Jinsi ya Kujua Kristo Ndiye Ukweli, Njia, na Uzima” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha II). Maneno haya yalionekana kuwa umande mzuri ambao ulirowesha ukame wa kudumu katika moyo wangu. Niliangua kilio na kumamia. Sikutambua ni mara ngapi “haiwezekani” liligeuka bila kutarajia kuwa bora. Mungu alisema kwamba bado Anataka kuniokoa nisipoacha ukimbizaji wangu, nitafute kutubu, na nisiondoke au kumtelekeza Yeye bila kujali hali yangu. Sikuweza kujizuia kusujudu mbele ya Mungu: “Ee Mungu! Ninakuamini na kukufuata, na bado ninakupinga na kukuasi kila mara. Mara kwa mara mimi hutenda kulingana na mapenzi yangu ninapotekeleza wajibu wangu, na mimi hudakiza na kuvuruga kazi ya kanisa; lakini umenivumilia na kunisamehe. Umenipa fursa nyingine ya kutubu na kuokolewa. Ee Mungu! Upendo Wako umeondoa kutoelewa kwangu na maswali yangu Kwako. Umesababisha moyo wangu unaokufa kupona na kuinuka kwa kutoka kwa uhasi wa kuzidi kiasi, maumivu na kukata tamaa. Umeitia moto tena tamaa yangu ya uzima mara nyingine —kutafuta wokovu. Ee Mungu! Upendo Wako kwangu ni wa kina sana, ni mkubwa sana! Kwa sababu ya upendo Wako kwangu, umesamehe makosa yangu yote, umesamehe ukinzani wangu wote na upinzani. Umefanya kazi Yako ya wokovu kwangu kupitia uvumilivu Wako mkubwa. Ee Mungu! Wewe ni mkubwa sana, ni mzuri sana! Siwezi kunena ninapokabiliwa na Upendo wako, naona haya na siwezi kuonyesha uso wangu. Ninajisikia kwa undani kwamba ningeona haya kuishi katika uwepo Wako. Kwa wakati huu, naweza tu kukutumia shukrani na sifa zangu za dhati. Ninaweza tu kukupa Wewe wimbo wa moyo wangu: “Upendo wako umenifanya nisiweze kuchagua kitu kingine chochote, sitakuacha Uwe na wasiwasi tena kunihusu. Watu wapotovu hufurahia upendo Wako mno. Wewe ndiwe upendo pekee moyoni mwangu, pekee ninayempenda, ninayemheshimu sana, na kumtegemea. Bila upendo Wako, nina maumivu tu na siwezi kuendelea kuishi. Ni furaha iliyoje kukujua Wewe maisha yangu yote. Bila kujali hali zangu zikoje, nitazifuata nyayo Zako na kufuatana Nawe ili kukufariji. Nikiwa katika maumivu makali, mimi pia nataka kuwa shahidi na kukuridhisha Wewe. Kuteseka na usafishwaji husababisha moyo wangu kuwa karibu na Wewe. Nina furaha milele kuwa na Wewe moyoni mwangu.”
Baada ya kuondosha mawazo yangu mabaya kuhusu Mungu, nilianza kutulia na kuchunguza tabia yangu ya zamani: Katika kazi yangu, sikuwahi kamwe kumtegemea Mungu wala kumheshimu. Sikutafuta mapenzi ya Mungu na sikufanya kulingana na mipango ya kazi au mahitaji ya kanisa. Nilitegemea kabisa akili yangu mwenyewe, sifa za ndani, na ujuzi wa kufanya mambo kwa njia yangu mwenyewe. Sikuwahi kamwe kuona au kushughulikia mambo kulingana na neno la Mungu, na sikutafuta kanuni za kazi yangu. Nilitegemea hisia zangu na mawazo yangu ili kuamua na kukisia. Sikuwahi kamwe kushauriana na wengine na mara nyingi nilifanya mambo yangu mwenyewe. Hata kama nilishauriana na wengine, ilikuwa tu ili kwamba ningeonekana kuwa mnyenyekevu. Kwa uhalisi, tayari nilikuwa na mpango katika mawazo yangu na kwa sababu ya hili, mara chache niliyashirikisha mawazo ya watu wengine. Singeweza kutekeleza mipango ya kazi kutoka walio juu vizuri kama hawangefuata mawazo yangu na kama mtu angejaribu kunishughulikia na kunipogoa, hata zaidi sikuwa tayari kulikubali. Mimi hasa nilitaka kuwa bora zaidi; bila kujali nilichokifanya nilitaka kuwapita wengine. Niliamini kwamba nilikuwa bora zaidi kuliko kila mtu na kwamba hakuna kazi katika kanisa ambayo sikuweza kufanya na kwamba kila kitu nilichokifanya kilikuwa kizuri. … Kwa sababu ya kudhibitiwa na asili yangu ya kiburi, nilitegemea asili ya Shetani ambayo ilikuwa ndani yangu kucharuka katika kazi yangu kwa miaka mingi. Kimsingi sikutafuta ukweli na sikusisitiza kujijua. Nilitafuta nafasi nzuri kikamilifu, na nilitaka kuwa kiongozi mkuu. Kwa ajili ya hilo, sikuelewa kikamilifu tabia ya Mungu wala kiini cha Mungu. Sikuwa hata na kiwango kidogo cha heshima au uchaji kwa Mungu. Nilitenda kwa uzembe mbele ya Mungu na hakuna kilichonizuia. Ningethubutu kusema chochote na kufanya chochote. Sikutambua kwamba nilikuwa nikichukua nafasi ya mchungaji wa uongo; nilikuwa nachukua njia ya kumtumikia Mungu huku nikimpinga. Ingawa ndugu wa kiume na wa kike walinikumbusha mara nyingi, sikukubali msaada wao uliokuwa na nia nzuri. Nilikuwa na kiburi mno na niliendelea katika njia zangu. Kwa sababu ya nyakati nyingi nilipompinga Mungu na nikaenda kinyume na Yeye, niliichochea hasira ya Mungu na hatimaye niliondolewa kwa huduma, ambayo ilinielekeza kujiwazia.
Baada ya kuchunguza jambo hili, hatua kwa hatua nilianza kuamka kutoka kwa mzubao wangu. Wakati huu wote, Mungu alikuwa ameweka mawazo mengi katika mambo yote yaliyonipata kwa nia ya kunikomboa. Sikuweza kujizuia kusujudu tena mbele ya Mungu: Ee Mwenyezi Mungu, nakushukuru Wewe! Ingawa kubadilishwa wakati huu kulihisi tu kama kufa na maumivu yangu yalikuwa yasiyolinganishika, kulitumika kama kisingizio cha mimi kupata uzoefu wa upendo Wako mkubwa na wokovu kwangu. Kama singekuwa nimebadilishwa wakati huu, ningekuwa bado ninaishi ndani ya dhana na mawazo yangu mwenyewe, nikiendelea kufanya mambo kwa njia isiyo sahihi. Bado ningeamini kwamba kutelekeza familia yangu na kazi ili kufanya kazi katika kanisa kulikuwa kukuhudumia kwa uaminifu. Singekuwa nimetafakari juu ya mwenendo wangu, na singetambua kwamba huduma yangu ilikuwa kukupinga Wewe. Kama mambo yangeendelea jinsi hii, ningekuwa tu mwenye kiburi na mwenye majivuno. Hatimaye ningekuwa nikikupinga kama mpinga Kristo na ningepaswa kukabiliwa na adhabu yako. Ee Mungu, upendo Wako kwangu ni mkubwa sana na halisi! Ubadili wa leo ni jinsi Unavyotaka kuniokoa kwa hakika. Upendo wako wa kuadibu umeushinda moyo wangu. Ninakushukuru Wewe kutoka moyoni mwangu kwa kuniokoa na kunilinda. Ninakushukuru Wewe hata zaidi kwa kunisababisha kwa hakika kupata uzoefu kupitia kwa ufunuo Wako kwamba tabia Yako ya haki haiwezi kuvumilia kosa; ninakushukuru kwa kuniruhusu nione mapenzi makubwa ya baba Uliyo nayo katika vipigo vikatili na majaribu machungu ya mwanadamu. Wakati huo huo, umeniruhusu pia kutambua kiini changu kipotovu na kuona kwamba nimepotoshwa sana na Shetani. Asili ya kiburi imekita mizizi kwa kina ndani yangu na ninahitaji sana kuadibu Kwako, hukumu, majaribu, usafishwaji, na hata adhabu Yako na laana ili kunisafisha na kuniokoa. Ni kwa njia ya kazi hii tu ambapo ninaweza kuibuka na heshima kuu Kwako na kulindwa na kutakaswa. Ee Mungu, tangu siku hii kwendelea, niko tayari kutafuta ukweli kwa bidii na kwa kweli kuitii kazi Yako. Nitakubali hukumu Yako na kuadibiwa. Bila kujali jinsi gani Wewe hunitendea, nitajiweka chini Yako kikamilifu na kuikubali mipango Yako. Sitaelewa visivyo wala kulalamika. Nitakuwa mtu halisi na kuishi na thamani na kusudi.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumapili, 2 Juni 2019

Maana Halisi ya Uasi Dhidi ya Mungu

Zhang Jun Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning
Katika siku za nyuma, niliamini kuwa “uasi dhidi ya Mungu” ilimaanisha kumsaliti Mungu, kuacha kanisa, au kuutelekeza wajibu wa mtu. Nilidhani tabia hizi hufanyiza uasi. Kwa hiyo, wakati wowote niliposikia kuhusu watu wakihusika katika tabia hizo, ningejikumbusha kwamba sipaswi kuasi dhidi ya Mungu kama walivyofanya. Aidha, nilikuwa mwangalifu katika jitihada zangu zote na nilishikilia kazi zote nilizopewa na kanisa. Sikurudi nyuma kutoka kwa wajibu wangu wakati niliposhughulikiwa na kupogolewa wala kuondoka kutoka kanisani nilipojaribiwa, bila kujali shida. Kwa hiyo, niliamini kwamba sikuwahi kuasi dhidi ya Mungu kamwe. Nilihisi kuwa nilikuwa nimepata hadhi fulani tayari na nilikuwa na hakika kwamba ningemfuata Mungu mpaka mwisho na hatimaye kufanikisha wokovu.
Siku moja wakati wa ukuzaji wa roho, nilisoma hili katika mahubiri: “Kuna aina mbalimbali za uasi dhidi ya Mungu. Aina moja ya uasi ni kuenda kinyume na mapenzi Yake au kwenda kinyume na maneno Yake; aina nyingine ni kuwa na tabia ya kiburi, kukosa Mungu katika moyo wa mtu, na hivyo kujivunia na kuwa na uhasama na Mungu—huu ni uasi wa kutomtii na kutomjali; kuna aina moja zaidi, ambayo ni uasi wa kumsaliti na kumtelekeza Mungu. … Tabia za uasi ambazo sisi huziongelea mara kwa mara katika ushirika hurejelea hasa aina mbili za kwanza. Hii ni kwa sababu wale ambao humsaliti na kumtelekeza Mungu hawako ndani ya mawanda ya wokovu wa Mungu, na tabia za uasi zilizotajwa katika maneno ya Mungu pia ni za aina mbili za kwanza; aina ya tatu ya uasi haijatajwa. Hatupaswi kuelewa visivyo au kutafsiri vibaya dhamira za Mungu, tukiamini kuwa ni kumsaliti tu au kumtelekeza tu kunakoweza kuitwa kuasi dhidi ya Mungu, kana kwamba kwenda kinyume na neno Lake au kuwa na tabia ya kiburi si aina ya uasi. Huu ni ufahamu wa upande mmoja kabisa! Hivyo uasi hasa ni nini? Watu wanapaswa kuutambuaje? Kwa mujibu neno la Mungu, vitu vyote ambavyo havilingani na Mungu ni maadui Wake, na vitu vyote vinavyoenda kinyume na maneno ya Mungu vinaasi dhidi ya maneno Yake. Kuasi dhidi ya maneno ya Mungu ni kuasi dhidi ya Mungu, na kutenda kama adui Yake pia ni kuasi dhidi Yake. Yaelekea kuwa kanuni hizi mbili hazilingani na dhana za kibinadamu, lakini hiki hasa ni kiini cha tatizo” (Ushirika Kutoka kwa wa Juu). Baada ya kusoma ushirika, nilitambua kuwa kuasi dhidi ya Mungu haikuwa kumsaliti Yeye tu, kutelekeza kanisa, au kuziacha kazi za mtu. Badala yake, kukiuka mapenzi ya Mungu au neno Lake, na kumpinga Yeye pia ni aina za uasi. Chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, nilianza kutafakari juu ya matendo yangu. Mungu hutaka tufuatilie ukweli na kubadilika katika tabia tunapotimiza wajibu wetu. Hata hivyo, nimelenga kazi na kupata hadhi ya juu ndani ya kanisa ninapotimiza wajibu wangu. Mungu hutusihi tufanye kazi zetu kwa uaminifu, tufuate mapenzi Yake wakati tunapokabiliwa na shida, na tuunyime mwili ili kuutenda ukweli. Hata hivyo, mimi daima hutafuta njia ambayo inahitaji jitihada kidogo kuliko zote katika kutimiza wajibu wangu, nikimdanganya Mungu na utepetevu wangu. Mimi huujali tu mwili wangu wakati wa shida, kulalamika juu ya matatizo na kuzembea katika wajibu wangu. Hata nimefikiria kukata tamaa kabisa kama njia ya kuutoroka wajibu wangu. Mungu huhitaji uaminifu kamili na kujitolea kamili. Mbele ya Mungu, mawazo yangu mara nyingi hushughulika na familia yangu na jamaa zangu. Mungu hutusihi tujifunze mafundisho katika vitu vyote na kuingia katika ukweli wa neno Lake ili tuweze kukamilishwa na Mungu. Wakati ninapokabiliwa na watu au mambo yasiyofaa, mimi husita kwa fikira kwamba vitu vyote ni sehemu ya mpango wa Mungu na hujipata daima nikiyumba kati ya mema na mabaya. Mungu hututaka tuingie katika ukweli na kukubali wokovu wa Mungu katika hali mbalimbali na majaribu ya shida ambayo Yeye ametupangia. Ninapokabiliwa na kushughulikiwa, kupogolewa, kipingamizi, au kushindwa, mimi huelewa visivyo na kumlaumu Mungu. Mimi huhisi kukata tamaa kuelekea barabara iliyo mbele, kupoteza imani kwa Mungu, na hata hufikiria kuacha kanisa. Mungu hutusihi tuwe makini, watu wa vitendo na wa kufaa katika maisha yetu ya kiroho. Mimi, hata hivyo, mara nyingi hutumia kanuni na taratibu, na kutenda kaida za dini. Mungu hutusihi tumtukuze na kumshuhudia Yeye katika kazi yetu na kuwaleta watu mbele Yake. Hata hivyo, mimi hujitukuza na kujishuhudia mwenyewe, nikiwaleta wengine mbele yangu ili wanipende na kunistahi. Mungu hutusihi tutumie ukweli ili kutatua matatizo yetu. Mimi huwa ninajigamba na kuzungumza juu ya elimu na mafundisho ya dini, kuwawekea wengine mipaka kwa kutumia kanuni, kutatua matatizo kulingana na njia za mwanadamu, na kuwakandamiza wengine kwa kutumia hadhi. Mungu hutusihi tufanye kazi zetu kwa mujibu wa mipango ya kazi. Kwa kawaida mimi hufanya kazi yangu kwa msingi wa nia zangu, kufanya vitu kwa njia ambayo ninaona kuwa inafaa. … Si vitendo hivi vyote vinakiuka mapenzi ya Mungu na neno Lake na viko katika upinzani kwa Mungu? Si vitendo hivi hufanyiza uasi dhidi ya Mungu?
Kwa wakati huu, siwezi kujizuia kujisikia mwenye hisia ya woga. Yaelekea kuwa niliasi dhidi ya Mungu bila kufahamu katika vitendo vyangu vyote huku nikiamini kwa kukosea kuwa uasi ulikuwa na maana ya kulisaliti kanisa, kulitelekeza kanisa, au kuziacha kazi za mtu. Kwa kujipujua nilifikiri kwamba kimo changu kiliniruhusu kuasi dhidi ya Mungu. Nimekuwa mgeni kwangu mwenyewe, na ufahamu wangu wa neno la Mungu ni wa urahisi na wa juu juu. Maneno ya Mungu yanasema, “Mungu ameifunua asili na kiini cha mwanadamu, lakini mwanadamu anafahamu kwamba njia yake ya kuyatenda mambo na njia yao ya kusema ni yenye mawaa na yenye kasoro; kwa hiyo ni kazi yenye kutumia juhudi nyingi kwa watu kutia ukweli katika vitendo. Watu wanafikiria kwamba makosa yao ni udhihirisho wa muda tu, ambao unafunuliwa bila kujali, badala ya kuwa ufunuo wa asili yao” (“Kuifahamu Asili na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana” (“Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Hilo ni kweli pasipo mashaka. Si mimi kabisa ni aina ya mtu wa kuhangaika juu ya mambo madogo bila kuelewa kwa dhahiri asili yangu? Tabia za watu hutawalwa na asili yao, na tabia yao ni dhihirisho la asili yao. Ikiwa uasi umeandikwa katika lugha ya mficho ndani ya asili ya mwanadamu, basi mtu ataasi dhidi ya Mungu bila kuepuka. Hili si suala la kuwa na tahadhari. Lakini, sijajishughulisha na kuitambua asili yangu. Badala yake, nimeridhishwa na kushikilia matendo fulani ya nje, ambayo hunizuia kutafuta ukweli na kubadilisha tabia yangu, ingawa nimemfuata Mungu kwa miaka mingi. Kwa kawaida nimeishi na asili ya uasi. Nikiendelea kufanya hivyo, kwa kuzingatia mazingira mazuri, bila kuepuka nitatawaliwa na asili yangu, kulisaliti na kuliacha kanisa. Hii ni njia hatari kweli!
Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea ukweli kuhusu imani zangu zenye makosa kuhusu uasi dhidi Yako. Uliniruhusu nielewe kwamba kutelekeza na kukiuka neno Lako ni aina za uasi, na ukanionyesha kuwa mimi niko katika hatari ya kuasi dhidi Yako, kukusaliti, na kukutelekeza. Kutoka leo kwendelea, niko tayari kuzingatia neno Lako na kulenga juhudi zangu kwa kutafakari juu ya maana halisi ya neno Lako, ili kwa kweli kuelewa kiini cha ukweli na kujiruhusu kuingia na kutenda ukweli kwa usahihi. Nitajitahidi kutetea neno Lako katika hali zote na kurekebisha ukaidi wangu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumamosi, 1 Juni 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mawazo Kuhusu Kubadilishwa

Yi Ran Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu. Kwa hiyo sikuweza kujua asilani jinsi mtu fulani aliyetafuta ukweli sana angeweza kubadilishwa. Inawezekana kwamba yeye alizungumza juu ya maonyesho yake mwenyewe ya upotovu sana, na hivyo kiongozi wake kwa makosa alimchukua kuwa mtu asiyefuatilia ukweli, na kumbadilisha? Kama hili ndilo lililotokea kweli, basi si fursa ya mafunzo kwa mtu ambaye alikuwa anafuta ukweli imeangamizwa?
Nilipokuwa tu nikihisi kukanganywa sana kuhusu hili, nilisoma kifungu hiki katika mpango wa kazi uliotolewa na kanisa: “Familia ya Mungu huamua kufundisha na kutumia watu kulingana na asili yao. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hufuatilia ukweli, basi familia ya Mungu kabisa haitamtelekeza, kama mtu yu tayari kufuatilia ukweli, basi bila shaka atapitia mabadiliko. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hakifuatilii ukweli, ni mzembe kwa majukumu yake na ni ambaye haipitii barabara sahihi, basi si mzuri wa kufundisha na wala Mungu hawezi kukamilisha aina hii ya mtu. Kwa mtu ambaye Mungu hataki kumkamilisha, familia ya Mungu pia haiwezi kumfundisha. … Hivyo ushughulikiwaji wa watu ni lazima ujongelewe kwa mujibu wa mahitaji ya kazi ya Mungu na kiini cha watu. Hii tu ndiyo njia ya kufaa ya kufanya kazi pamoja na Mungu na kwa hakika kumtumikia Mungu. Kama njia hii ifaayo ya kufanya kazi pamoja na Mungu haitumiwi, basi kazi ya Mungu inavurugwa na mapenzi ya Mungu inakiukwa kabisa” (“Kushirikiana Maswali Kadhaa” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Kujaribu mara kwa mara kuelewa maneno haya, nilielewa kwamba kulikuwa na kanuni zilizokuwa zikifanya kazi kama kanisa lilikuwa likimpandisha mtu cheo au kumbadilisha. Nilielewa kwamba ulikuwa ukijongelewa kwa mujibu wa mahitaji ya kazi ya Mungu na kiini cha watu, na sio kutumia watu kwa upofu au kuwabadilisha watu upendavyo. Aidha, kanisa huwa haliwabadilishi watu kwa msingi wa kuwa walionyesha upotovu, lakini badala yake huamua mambo kwa msingi wa asili yao. Kama kiini cha mtu ni kile ambacho hutafuta ukweli, basi bila shaka kanisa halingemwacha, bila shaka halingemtelekeza au kumwangamiza mtu yeyote akitafuta ukweli. Kwa hiyo nilikwenda mbele ya Mungu kuomba na kutafuta mwongozo: “Ee Mungu! Najua kwamba nimepotoshwa sana na Shetani, na sina ufahamu wa kazi Yako, nikiwa na dhana nyingi ndani yangu na maoni mengi ambayo hayawezi kupatana na Wewe. Leo, chini ya mwongozo Wako, sasa ninajua kuwa kama ni katika kuchagua, kufundisha au kubadilisha watu, kanisa huyajongelea yote kwa mujibu wa mahitaji ya kazi Yako na kiini cha watu. Lakini bado sielewi vizuri kiini cha dada aliyebadilishwa, na matokeo yake ni kuwa nina maoni juu ya utaratibu wa kanisa. Ninakuomba Unielekeze na kuniongoza, niruhusu nipate kuona kwa dhahiri ili, katika kazi yangu tangu sasa na kwendelea, nisiweze kuvuruga kazi Yako kwa sababu ya kupotoka kwangu na makosa yangu.”
Nilipokuwa nimekwisha kuomba, nilichukua utaratibu wa kazi na, chini ya uongozi wa Mungu, nilisoma maneno haya: “Kwa kusoma maneno ya Mungu, wale wanaofuatilia ukweli wanaweza kupima hali yao potovu dhidi ya maneno ya Mungu. Ushirika wao juu ya maneno ya Mungu haufanyiki tu ili kuzungumza juu ya kuelewa maneno ya Mungu, bali pia kuzungumza juu ya kujielewa wenyewe. Bila kujali ni upotovu upi unaonyeshwa, wanaweza kuufichua wazi ili ndugu wa kiume na wa kike waweze kufanikisha kitu halisi, wakati huo huo wakitatua upotovu wao wenyewe. Huu pia ndio utaratibu bora ya kabisa wa kuwaongoza watu kwenye maneno ya Mungu. … Wale wote ambao huzungumza tu kuhusu maana halisi na ambao hawana uhalisi, hawastahili kuwa viongozi katika familia ya Mungu. Kiongozi na mfanyikazi wa aina hii wanapaswa kubadilishwa” (“Kumtumikia Mungu ni Lazima Mtu Ajifunze Jinsi ya Kutambua Watu wa Kila Aina” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu). Maneno haya yalinifanya nielewe kwamba kwa kusoma maneno ya Mungu, wale ambao kwa kweli hutafuta ukweli wanaweza kupima hali yao wenyewe potovu dhidi ya maneno ya Mungu, kuwa na ufahamu wa kweli wa kiini cha maneno ya Mungu, na wanaweza kuelewa kwa hakika asili na nafsi ya upotovu wao wenyewe. Ushirika wao unaweza kufichua njia halisi ya watu na unaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Zaidi ya hayo, wakati huo huo wa kutatua matatizo ya wengine, wanaweza pia kutatua matatizo yao wenyewe, na kulenga kuingia kwao katika maisha na mabadiliko yao katika tabia.
Wakati huu, nilianza kukumbuka kinaganaga mwenendo na utendaji ulioendelea kuwepo wa dada aliyebadilishwa. Ingawa wakati wa kutatua matatizo ya watu wengine alizungumza kwa umbuji na kwa urefu, akitumia maneno yaliyofikiriwa na yaliyoelezwa kwa ufasaha, hakuwa ametatua ugumu wa kuingia kwake katika maisha na daima aliishi katika hali ya kujidai, akijihisi kujivuna mno, akiamini kwamba alifanya kila kazi vizuri. Kwa kweli, kazi yake ilifanywa vibaya. Kama kile alichopata na kushirikiana kwa kweli kilikuwa ufahamu wa kiini cha kweli, kwa nini hakuweza kutumia ufahamu wake ili kujisaidia? Kiongozi alipoonyesha hali yake ya makosa, kuchukua kwa uzito kabisa na kuchangua matatizo makubwa yaliyokuwemo katika kazi yake, na kushirikiana naye kuhusu hilo, ingawa kwa nje alikubali kwa kichwa chake mara kwa mara, akionyesha kukubali kwake na nia yake ya kufanya hivyo kwa kanuni, yeye hata hivyo kwa siri aliendelea katika njia zake za zamani kwa ukiukaji wa kanuni hiyo, akifanya mambo jinsi alivyotaka akidhuru kazi tena. Wakati alipokuwa akishughulikiwa, ingawa sura yake ya nje ilionyesha kuwa alikuwa na huruma sana, baadaye hakufanya mabadiliko yoyote kabisa. Ingawa alizungumzia ufahamu wake wa nafsi yake mwenyewe na kutoa upotovu wake mwenyewe waziwazi, matokeo yake yalikuwa kwamba alifanya wengine kumtegemea, kumpa heshima sana, akiwaleta watu mbele yake. Njia yake ya kutoa vitu nje waziwazi haikuweza kumletea mtu yeyote faida yoyote kabisa. Ingeweza tu kuwadhuru watu na kuwadanganya. … Niliweza kuona kutoka kwa utendaji wake wa kuendelea kuwepo kwamba, ingawa alikuwa amefanya kazi kwa miaka mingi na kujiandaa na ufahamu mwingi halisi, tabia yake katika maisha haikuwa imepitia mabadiliko yoyote kabisa. Kwa kinyume chake, alikuwa ashakuwa mwenye kiburi na majivuno zaidi na zaidi. Ni sasa tu ninapotambua kwamba hakuwa mtu ambaye alitafuta ukweli, wala hakuwa mtu ambaye alipokea ukweli halisi au aliyefanya ushirika kwa werevu. Bila shaka hakuwa mzuri wa kufundisha na, kama angekuwa amewekwa katika cheo yake, angechelewesha tu kazi ya kanisa na kuwaharibu ndugu zake wa kiume na wa kike. Kubadilishwa kwake kwa kweli kulikuwa ni haki ya Mungu na ilikuwa njia nzuri zaidi ya Mungu kumwokoa. Vinginevyo, bado angeweza kudanganywa na sura yake ya nje na hangeweza kuona makosa ya njia zake, mwishowe akianguka katika adhabu ya Mungu.
Ni kwa njia ya jambo hili tu nilipoona jinsi nilivyoelewa kiasi kidogo cha ukweli, nikilenga tu maana halisi ya mipango ya kazi na ukweli, kuwa tu na maarifa ya kinadharia. Hakika sikuwa nikilenga juu ya kuelewa mapenzi ya Mungu katika mipango ya kazi, wala sikuwa na ufahamu muhimu wa ukweli. Kwa hivyo sio tu kwamba niliishia kutoweza kuelewa kabisa viini vya watu, lakini kwa kinyume chake nilihofia kwa kiburi kwamba mtu ambaye alitafuta ukweli alikuwa amebadilishwa kwa makosa.
Ee Mungu! Ninatoa shukurani kwa ajili ya ufunuo Wako na kupata nuru ambavyo vilinifanya nione ufukara wangu mwenyewe, upofu na jinsi nilivyokuwa wa kusikitisha, vilivyonifanya kutambua kwamba bila ukweli, mtu hawezi kuelewa kabisa kiini cha suala hili, badala yake akidanganywa tu na sura ya nje. Ni kwa kuelewa ukweli tu, mtu anapoweza kufanya kazi muhimu vyema. Ee Mungu! Kuanzia leo kwendelea, napenda kufanya jitihada nyingi katika ufuatiliaji wangu wa ukweli, kutafuta mapenzi Yako katika vitu vyote, kufanya vitu kama Unavyohitaji na hivi karibuni kuwa wa manufaa Kwako.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo