Kitabu cha Ufunuo anasema, “Na kwenye paji la uso wake jina liliandikwa, FUMBO, BABELI MKUBWA, MAMA WA MALAYA NA MAKURUHI YA DUNIA. Na nikamwona mwanamke huyo akiwa amelewa kwa damu yao watakatifu, na damu ya mashahidi wake Yesu...” (Ufunuo 17: 5-6). Je, unajua jinsi ambavyo unabii huu hutimizwa? Je, unajua jinsi Mungu atakavyomwadibu yule Kahaba Mkuu wa Kitabu cha Ufunuo?
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Hukumu. Onyesha machapisho yote
Jumapili, 18 Agosti 2019
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 5 Maangamizo ya Shetani | Kwaya za Injili
Kitabu cha Ufunuo anasema, “Na kwenye paji la uso wake jina liliandikwa, FUMBO, BABELI MKUBWA, MAMA WA MALAYA NA MAKURUHI YA DUNIA. Na nikamwona mwanamke huyo akiwa amelewa kwa damu yao watakatifu, na damu ya mashahidi wake Yesu...” (Ufunuo 17: 5-6). Je, unajua jinsi ambavyo unabii huu hutimizwa? Je, unajua jinsi Mungu atakavyomwadibu yule Kahaba Mkuu wa Kitabu cha Ufunuo?
Iliyotazamwa Mara Nyingi : Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Have You Enjoyed the Joy of Gaining the Work of the Holy Spirit?
Ijumaa, 9 Agosti 2019
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili
Mwenyezi Mungu anasema, “Maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia, na upanga mkali ukatao kuwili, ambao unaweza kumshinda Shetani” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ni kama upanga wenye makali pande mbili, yanayoweza kushinda nguvu zote za uovu.
Ijumaa, 14 Juni 2019
Kuahidi Maisha Yangu kwa Moyo wa Ibada
Zhou Xuan Mkoa wa Shandong
Mnamo Aprili 3, mwaka wa 2003, niliambatana na dada mmoja kumtembelea muumini mpya. Muumini huyu mpya hakuwa na uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho na aliishia kuturipoti. Kwa sababu hiyo, askari wanne waovu wenye nguo za raia walikuja na kwa ugomvi kutuingiza sisi wawili katika gari lao na kutupeleka kwa kituo cha polisi. Njiani, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi mno, kwa sababu mwilini mwangu nilikuwa na peja ya mawasiliano, orodha isiyo kamili ya majina ya wanajumuiya wa kanisa letu, na daftari dogo. Niliogopa kwamba wale askari waovu wangeweza kugundua vitu hivi na niliogopa zaidi kwamba ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniita kupitia peja yangu ya mawasiliano, kwa hiyo mimi kwa mfululizo nilimwomba Mungu kwa haraka moyoni mwangu: “Mungu, ninapaswa kufanya nini? Ninakuomba Unipe suluhisho na usiruhusu vitu hivi viingie mikononi mwa askari hawa waovu.” Baada ya hili, nilichukua vitu hivi kutoka kwa mkoba wangu na kwa kimya kuviweka kiunoni mwangu na kusema kwamba tumbo langu liliuma na nilihitaji kutumia msala. Wale askari waovu wakaniapizia wakisema: “Wewe umejaa upuuzi!” Baada ya maombi yangu ya mara kwa mara, walimtaka askari mmoja wa kike anichunge nilipokwenda msalani. Nilipouondoa mshipi wangu, kifaa changu cha mawasiliano kilianguka na kwa urahisi nikakiokota na kukitupa katika bomba la maji taka. Kwa sababu niliogopa wakati huo kwamba huyo afisa wa kike angegundua mkoba kiunoni mwangu, sikuutupa katika bomba, lakini badala yake niliutia katika pipa la taka; nilidhani kwamba ningetumia msala tena usiku na kisha kuutupa ndani ya choo. Ilivyotukia, sikurudi kwa msala huo kamwe. Ilitukia kuwa wale askari waovu waliupata ule mkoba niliokuwa nimeutupa katika jaa la taka.
Wale askari waovu wakatufungia yule dada na mimi katika chumba kimoja na kutulazimisha tuvue nguo zetu zote ili waweze kutupekua. Walipekua hata kwa nywele zetu kuona kama tulificha chochote. Baada ya kumaliza kutafuta, walitutia pingu na kutufungia katika kile chumba. Ilipofika usiku, wale askari waovu walitutenganisha ili tuhojiwe kwa makini; waliniuliza: “Unatoka wapi? Jina lako ni nani? Ulikuja hapa lini? Unafanya nini hapa? Unaishi wapi? Unaamini nini? Jina la mtu uliye naye ni nani?” Kwa sababu hawakuridhishwa na majibu yangu, wale askari waovu walisema hivi kwa hasira: “Sisi huonyesha upole kwa wale wanaokiri na ukali kwa wale wanaobisha. Usiposema ukweli, utajilaumu mwenyewe! Sema! Ni nani anayekusimamia? Unafanya nini? Sema na tutakutendea kwa upole.” Nilivyoona jinsi walivyoonekana wakali kishetani, nilifanya uamuzi kwa kimya: kabisa sitakuwa Yuda, sitawasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike na sitazisaliti nia za familia ya Mungu. Walipoona kwamba hawakuweza kupata chochote kutoka kwangu, waliingiwa na wasiwasi na kuanza kunigonga na kunipiga mateke kwa ukali wakisema: “Kwa kuwa husemi chochote, tutakuadhibu kwa kukunyosha mikono na miguu!” Kisha ghafla kulikuwa na mlipuko mwingine wa kupigwa ngumi na mateke kwa ukali sana. Baadaye, mmoja wao akaniamuru niketi chini, na akanitia pingu na kuipinda mikono yangu kwelekea nyuma yangu kwa kukaza alivyoweza. Kisha akaweka kiti nyuma yangu na kutumia kamba kuifunga mikono yangu nyuma ya kiti. Alitumia mikono yake na akawekea nguvu zake zote kwelekea chini, akiweka shinikizo juu ya mikono yangu. Mara moja, mikono yangu ikahisi kama ingevunjika; iliumia vibaya sana hivi kwamba nilitoa yowe kali. Walikwenda mbele na nyuma jinsi hii kwa mikono yangu wakiniumiza bila kukoma kwa muda wa saa kadhaa. Baadaye, sikuweza kuvumilia na nilitikisika kutoka utosini hadi kidoleni. Walipoona hayo, wakasema: “Usijifanye kana kwamba wewe ni wazimu, tumeona hili mara nyingi kabla. Je, unadhani unamshtua nani? Je, unadhani kuwa kufanya hivi kutakuondoa kwa tatizo hili?” Waliona kwamba bado nilikuwa nikitikisika na askari mmoja mwovu akasema: “Nenda naye msalani na kumtia kinyesi kiasi kinywani mwake, angalia kama atakila au la.” Walitumia kijiti kuchotea kinyesi kiasi na kukifikicha ndani ya kinywa changu na kunifanya nikile; nilikuwa bado nikitoa pofu kwa kinywa na waliona kwamba bado nilikuwa nikitikisika, kwa hiyo waliniacha nishuke kutoka kwa kiti. Mwili wangu mzima uliumia bila kuvumilika kama kwamba nilikuwa na mito kutoka utosini hadi kidoleni na nilitoa yowe kwa maumivu nilipolala sakafuni nikiwa nimeduwaa. Baada ya muda mrefu, viganja vyangu na mikono viliaanza kusogea tena. Polisi hao waovu waliogopa kwamba ningegonga kichwa changu kwa ukuta na kujiua, kwa hiyo walinipa helmeti. Baadaye, waliniburuta na kunirudisha kwa kile chumba kidogo cha chuma. Nililia na kumwomba Mungu: “Ewe Mungu, mwili wangu ni dhaifu sana. Natamani kuwa Unilinde. Bila kujali jinsi Shetani anavyonitesa, ningependelea kufa kuliko kukusaliti Wewe kama Yuda. Sitawasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike au maslahi ya familia ya Mungu. Niko tayari kuwa shahidi Kwako ili kumuaibisha yule Shetani mzee.”
Siku ya tatu, wale askari waovu walichukua ile daftari dogo na orodha ya majina ya wanajumuiya wa kanisa niliyokuwa nimeitupa katika jaa la taka na kunihoji. Nilipoona vitu hivi, nilihisi hasa kutokuwa na raha na kujaa kujilaumu na majuto. Nilichukia kwamba nilikuwa na hofu sana na mwoga na kwamba sikuwa na ujasiri wa kutosha wakati huo wa kutupa mkoba ndani ya bomba la maji taka, jambo lililosababisha matokeo haya ya hatari. Nilichukia hata zaidi kwamba sikusikiliza mipango ya familia ya Mungu na kuleta vitu hivi wakati wa kutimiza wajibu wangu, jambo ambalo limelisababishia kanisa tatizo hili kubwa. Nilijua kwa kina kwamba nilistahili mateso niliyokuwa nikiyapitia siku hii na kwamba ilikuwa ni kuadibu kwa Mungu na hukumu vikinijia, na nilikuwa radhi kuvikubali. Nilikuwa radhi pia kumtegemea Mungu ili kumshinda Shetani. Wakati huu nilifikiri juu ya wimbo: “Sijali kuhusu njia iliyo mbele; ni kutenda tu mapenzi ya Mungu kama wito wangu. Wala sijali juu ya mustakabali wangu. Kwa kuwa nimechagua kumpenda Mungu, nitakuwa mwaminifu mpaka mwisho. Bila kujali jinsi hatari na shida zilivyo kubwa, au jinsi njia iliyo mbele ilivyo na mashimoshimo na ya kuparuza, kwa kuwa ninalenga siku ambayo Mungu atapata utukufu, nitatelekeza kila kitu na kujitahidi kwenda mbele” (“Kutembea Kama Askari kwa Njia ya Kumpenda Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliuimba wimbo huu kimya kimya na moyo wangu ulikuwa na imani na nguvu tena. Wale askari waovu wakaniuliza: “Je, vitu hivi ni vyako? Sema ukweli nasi, hatutakutendea bila haki. Wewe ni mwathirika na umedanganywa. Dini yenu ni Xie Jiao; Mungu mnayemwamini ni Mungu asiye dhahiri na yu mbali, ni ndoto za mchana. Chama cha Kikomunisti ni kizuri, na unapaswa kutegemea hicho chama na serikali. Ukiwa na shida yoyote, unaweza kuja kwetu na tutakusaidia kuitatua. Ukihitaji usaidizi kupata kazi, tunaweza kukusaidia pia. Kiri tu kila kitu juu ya kanisa lako; tuambie kile watu hawa walio kwa orodha yako wanachofanya. Wanaishi wapi? Ni nani mkuu wenu?” Nilitambua hila zao za uwongo na kusema: “Vitu hivi si vyangu, sijui.” Walipoona kwamba singefichua chochote, basi ilifichuka ni watu wa aina gani kamili na walinipiga kikatili na kuniangusha chini na kuendelea kunipiga kwa ukali sana na kutumia nguvu zao zote kuniburuta huku na huko wakitumia pingu zangu. Jinsi walivyozidi kuniburuta, ndivyo pingu zilivyozidi kujikaza na kuukata mwili wangu. Niliumia vibaya sana kiasi cha kulia kwa sauti kubwa na wale askari waovu wakasema kwa ukali: “Tutakufanya uonge, tutakuminya kidogo kidogo kama dawa ya meno ili kukufanya uzungumze!” Hatimaye, walichukua mikono yangu miwili na kuifunga ikielekea nyuma kwa kiti na kunifanya nikalie sakafu. Walinigonga na kuwekea nguvu zao na kugandamiza kwelekea chini juu ya mikono yangu; nilihisi maumivu yasiyovumilika na uchungu uliochoma kana kwamba mikono yangu ingevunjika. Wale askari waovu walinitesa na kunikemea: “Sema wazi!” Bila kusita nikasema: “Sijui!” “Usiposema wazi tutakuua; usiposema wazi basi usitarajie kuishi; tutakufunga jela kwa miaka kumi, miaka ishirini, maisha yako yote; usitarajie kutoka jela kamwe!” Niliposikia hivi, wazo fulani likanijia akilini mwangu ghafla: ni lazima niamue kuwa tayari kwenda jela maisha. Baadaye nilifikiri juu ya wimbo wa uzoefu: “Toa sadaka ya kupendeza mno kwa Mungu, nijidunduizie ile chungu zaidi. Simama na kwa uthabiti ushuhudie kwa Mungu, usikubali kushindwa na Shetani. Aa! Huenda vichwa vikavunjika na damu kuvuja, lakini hadhi ya watu wa Mungu haiwezi kupotea. Imani ya Mungu hupumzika kwa moyo, ni lazima niamue kumdhalilisha Shetani mzee” (“Ninataka Kuona Siku Ambapo Mungu Atapata Utukufu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Mungu alinipa nuru, akinifanya niwe imara na kuwa na ujasiri na akinipa imani na uamuzi kupitia kila kitu na kuwa shahidi kwa Mungu. Kwa sababu hiyo, hila za hao askari waovu hazikushinda; walinitesa mpaka wakachoka, kisha wakanirudisha kwa chumba cha chuma.
Siku chache baadaye, niliteswa na hao askari waovu mpaka nikawa sina nguvu. Nilikuwa katika mpagao wa usahaulifu kabisa na mikono yangu ilikuwa na ganzi. Katika kukabiliana na mateso haya katili na ya kinyama, niliogopa hasa kwamba hao askari waovu wangerudi na kunihoji. Mara tu nilivyofikiria hili, moyo wangu haukuweza kujizuia kutetemeka kwa hofu. Kwa kweli sikujua ni nini kingine wangetumia kunitesa, na sikujua ni lini masaili haya yangeisha. Niliweza tu kuendelea kuomba ndani ya moyo wangu kwa Mungu na kumwomba Mungu kuulinda moyo wangu na kunipa hiari na nguvu za kuvumilia mateso ili ningeweza kuwa shahidi kwa Mungu na kumfanya Shetani ashindwe kwa fedheha kamili.
Wakati wale askari waovu walipoona kuwa singekiri, waliungana na Brigedi ya Usalama wa Taifa na Shirika la Usalama wa Umma ili kunihoji. Kulikuwa na watu zaidi ya ishirini huko wakishika zamu kunihoji mchana na usiku wakijaribu kunilazimisha kukiri. Siku hiyo, askari wawili waovu kutoka kwa Brigedi ya Usalama wa Taifa ambao tayari walikuwa wamenihoji mara moja kabla walinijia na mwanzoni walizungumza kwa huruma wakisema: “Ukikiri ukweli, basi tutakuacha uende na tutahakikisha usalama wako. … Ni chama cha Kikomunisti tu kinachoweza kukuokoa, na Mungu hawezi kukuokoa ….” Wakati mmoja wao alipoona kwamba singetamka neno, aliingiwa na wasiwasi na kuanza kunipigia yowe kwa maneno machafu, akinilazimisha niketi sakafuni. Alinipiga teke kwa miguuni kwa nguvu alivyoweza akitumia viatu vya ngozi akisababisha maumivu yasiyoweza kustahimilika. Askari mwingine muovu akamwuliza: “Kunaendaje, anazungumza?” Alisema: “Yeye ni mkaidi sana, bila kujali unampiga kiasi gani na hatazungumza.” Huyo mtu akasema kwa ukali: “Kama hazungumzi, basi mpige hadi afe!” Yule askari muovu akanitishia akisema: “Hutazungumza? Basi tutakuua!” Nikasema: “Nimesema kila kitu ambacho nilihitaji kusema, sijui!” Alikasirika sana kiasi kwamba alionekana kuwa wazimu kabisa, kisha akanguruma kama mnyama wa mwitu na kuanza kunichapa na kunipiga mateke. Hatimaye alipata uchovu kwa kunipiga na kupata kamba kiasi cha unene wa kidole na kuiviringishia mkononi mwake mara chache. Kwa ukatili aliupiga uso wangu mijeledi tena na tena akisema: “Je, wewe humwamini Mungu? Wewe unateseka, kwa nini Mungu wako haji na kukuokoa? Kwa nini Yeye haji na kukufungua pingu? Mungu wako yuko wapi?” Niliyakereza meno yangu na kuvumilia maumivu. Niliomba kwa utulivu moyoni mwangu kwa Mungu: “Ee Mungu, ninapitia shida hii kwa sababu ya uasi wangu; ni kile ninachostahili. Mungu. Wakinipiga hadi kufa leo, kamwe sitakuwa kama Yuda. Nataka Uwe pamoja nami na kuulinda moyo wangu. Niko tayari kutoa maisha yangu ili kuwa shahidi Kwako na kumfedhehesha Shetani mzee.” Nilifikiria kuhusu wimbo: “Hakuna huruma katika kifo, na hakuna mshangao kwa hilo. Mapenzi ya Mungu huzidi yote. … Mungu aliniokoa na ameniwasilisha kwa Shetani, haya ndiyo mapenzi mazuri ya Mungu; moyo wangu utampenda Mungu wangu milele” (“Rudisha Upendo kwa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilifunga macho yangu na kuvumilia mateso ya Shetani na kupigwa. Wakati huo, ilikuwa ni kama nilisahau kuhusu maumivu yangu. Sikujua ni wakati upi mateso hayo yangeisha. Sikuthubutu kulifikiria, na sikuweza hata kutafakari juu ya hilo. Kitu pekee ambacho niliweza kufanya ni kusali bila kukoma na kumlilia Mungu. Maneno ya Mungu pia yalinipa imani ya mfululizo: “Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu” (“Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Msiwe na hofu ya wao wanaoua mwili, lakini hawana uwezo wa kuifisha roho: ila heri uwe na hofu ya yeye anayeweza kuiangamiza roho pamoja na mwili katika kuzimu” (Mathayo 10:28). Nilifikiri kuhusu jinsi joka kubwa jekundu lilikuwa tishio la bure tu lililoandikiwa kushindwa na mikono ya Mungu. Kama Mungu hakuyaruhusu, mauti hayangenijia; bila ruhusa ya Mungu, hakuna hata unywele wangu mmoja ungepotea. Pia nilifikiria kuhusu maneno haya ya Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” (“Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Nguvu ya neno la Mungu haina mipaka na imesababisha imani yangu kuongezeka; nilikuwa na azimio la kupambana na Shetani hadi mwisho. Yule askari muovu alipochoka kunipiga, aliniuliza tena: “Je, utasema?” Nilisema kikiki: “Hata ukinipiga hadi nife, bado sitajua!” Yule askari muovu aliposikia hayo, hakuweza kufanya chochote. Akatupa kamba na kusema: “Wewe ni mkaidi kweli, kama nyumbu. Kwa kweli wewe ni mzuri, huwezi kusema chochote hata ukifa. Ulipata kutoka wapi nguvu na imani nyingi jinsi hii? Wewe kwa kweli ni Liu Hulan zaidi ya Liu Hulan” Nilipomsikia akisema haya, ilikuwa ni kama nilimwona Mungu ameketi kwenye kiti Chake cha enzi kwa ushindi, akimwangalia Shetani akifedheheshwa. Nililia nusu na kumtukuza Mungu nusu: Ee Mungu, kwa kuitegemea nguvu Yako, ninaweza kumshinda Shetani, yule pepo! Kwa sababu ya ukweli huo, naona kwamba Wewe ni mwenye kudura na Shetani hana nguvu; Shetani daima atashindwa chini ya udhibiti Wako. Usipomruhusu, Shetani hataweza kunitesa hadi nife. Wakati huu, maneno ya Mungu yalinipa nuru tena: “Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote…. Tabia yake ni ishara ya mamlaka … ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui …” (“Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kupitia mateso katili ya joka kubwa jekundu, kwa kweli niliona upendo wa Mungu na wokovu kwangu na nilipitia nguvu na mamlaka ya neno la Mungu. Bila neno la Mungu kuniongoza kila hatua ya njia na kwa kutegemea tu nguvu yangu mwenyewe, haingewezekana kwangu kuyashinda mateso na kupigwa kwa joka kubwa jekundu. Vivyo hivyo, lilinifanya nione taswira yenyekuweza kudhuruiwa na iliyopondwapondwa ya joka kubwa jekundu. Nilikielewa kiini cha pepo cha unyama walo na kutojali kwalo kwa uhai na nililichukia na kulilaani ndani ya moyo wangu. Nilipenda kuvunja kabisa uhusiano wote nalo na kumfuata Kristo na kumtumikia Kristo milele.
Siku iliyofuata, askari waovu walikuja na kunihoji tena, kwa kweli walishangaa na kusema: “Ni nini kibaya na uso wako?” Nilipotazama katika kioo, sikuweza kujitambua; askari muovu alikuwa ameupiga uso wangu mijeledi kwa kamba siku iliyopita na ulikuwa umevimba sana na kuwa mweusi na bluu na kuwa kama panda. Nilipoona kuwa uso wangu ulikuwa umebadilika kabisa mpaka kutotambulika, nilihisi chuki kali kwa joka kubwa jekundu na nikafanya azimio langu kuwa shahidi. Sikuweza kabisa kuruhusu njama yake ishinde! Miguu yangu ilikuwa imepigwa vibaya sana kiasi kwamba sikuweza kutembea na wakati nilipokwenda msalani, niliweza kuona kwamba miguu yangu yote haikuwa na hali ya kawaida iliyobaki, kila kitu kilikuwa cheusi na bluu. Mmoja wa askari waovu akasema: “Hakuna haja ya wewe kuteswa hivi; ukiongea basi hutahitaji kuteseka; unajifanyia hivi mwenyewe! Lifikirie; kiri na tutakutuma nyumbani kwa mumeo na binti yako.” Baada ya kumsikia akisema haya, nilimchukia kabisa. Baadaye, walibadilisha mbinu zao na wakaanza kushika zamu kwa kutoniruhusu nilale mchana kutwa na usiku kucha. Nilipoanza kulala, wangepiga yowe na kupiga kelele kubwa ili kuniamsha; walijaribu kuivunja dhamira yangu kwa kutoniruhusu kulala ili nizungumze kwa usahaulifu, katika hali ya akili isiyobainika. Nilimshukuru Mungu kwa kunilinda. Ingawa wale askari waovu waliniweka kwa muda wa siku nne mchana na usiku, haikujalisha jinsi walivyonihoji, nilimtegemea Mungu kwa ustahimilivu na imani, na sio tu kwamba sikuwa na usahaulifu, lakini nilikuwa macho mno. Askari waovu waliponihoji tena na tena, wakasononeka zaidi na zaidi na wakawa wenye kukata tamaa. Walianza kutekeleza masaili ya shingo upande; walitoa matusi na kulalamika, walikasirikia kwamba nilikuwa nimewasababisha kupoteza hamu yao ya kula, kutopata mapumziko mazuri, na kuteswa na mimi, walihisi kuwa walikuwa na bahati mbaya sana. Hatimaye, yote waliyofanya yalikuwa kuniuliza maswali ya kawaida na hawakuwa tena na utashi wa kunihoji. Katika duru hii ya vita Shetani aliishia kushindwa tena.
Askari waovu hawakuachia hapo, walijaribu kunitongoza. Askari mmoja muovu alikuja na kuweka vidole chini ya kidevu changu, akachukua mkono wangu na kusema jina langu. Kwa sauti ya “upendo” akasema: “Wewe ni mzuri sana; haina thamani kuteseka sana hapa. Matatizo yoyote uliyo nayo, naweza kukusaidia kuyatatua. Imani yako kwa Mungu haijakupatia kitu. Nina nyumba mbili, siku moja, nitakuleta huko ili uwe na burudani; sisi wawili tunaweza kutengeneza ubia. Ukikiri, basi utakuwa huru. Chochote unachotaka, naweza kukusaidia. Sitakutendea bila haki….” Niliposikia uongo wake mbaya, mchafu sana, nilijihisi kuchafuka moyo na kwa nguvu zote nilimkataa. Hakuwa na chaguo jingine bali kuondoka kwa aibu. Hili lilinifanya niwaelewe kabisa hawa watu waliolaaniwa na wasio na aibu wanaodaiwa kuwa “polisi wa watu.” Ili kupata malengo yao wenyewe, wao hutumia mbinu zilizolaaniwa na za kishenzi bila aibu yoyote; hawana heshima yoyote au uadilifu; kwa kweli wao ni pepo wabaya na wachafu!
Hao askari waovu walikuwa na njama moja ya ujanja baada ya nyingine na waliitumia vibaya watu wa familia yangu kujaribu kunishurutisha, wakisema: “Unamwamini Mungu tu, hufikirii juu ya mume wako, binti, wazazi, na watu wengine wa familia; binti yako atakwenda shuleni siku fulani na kutafuta kazi. Unaamini katika Xie Jiao na hili litaathiri moja kwa moja matarajio yake ya mustakabali. Je, utaruhusu hili lifanyike kwake? Wewe humfikirii; Je, una moyo mgumu wa kumruhusu ahusike katika hili?” Kufuatia hili, walimleta mume wangu, binti, na shangazi ndani ili kuwaacha wajaribu kunishawishi. Nilipomwona binti yangu ambaye sikuwa nimemwona kwa miaka kadhaa, machozi yangu yalitiririka bila kuzuilika. Wakati huu, niliomba kwa nguvu zangu zote kwa Mungu: “Ee Mungu, nakuomba Uulinde moyo wangu, kwa sababu mwili wangu ni dhaifu mno. Wakati huu, siwezi kukamatwa na hila za Shetani na siwezi kujaribiwa na Shetani kuanguka katika hisia zangu; Siwezi kumsaliti Mungu au kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike; namwomba tu Mungu awe pamoja nami na kunipa imani na nguvu.” Shangazi akaniambia: “Fanya haraka na uzungumze, kwa nini wewe ni mjinga hivi? Ina thamani yoyote kupitia hili kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Ni nani atakayekushughulikia iwapo chochote kitatokea? Mama yako na baba yako wanahangaika juu yako, wana wasiwasi kila siku kukuhusu, hawawezi kula au kulala vizuri. Ni lazima utufikirie na urudi na kuishi maisha na sisi. Usimwamini Mungu. Angalia ni shida gani ulizopitia kwa sababu ya imani yako kwa Mungu; kwa nini unajisumbua?” Ingawa nilikuwa dhaifu, nililindwa na Mungu na nilitambua kuwa hili lilikuwa pambano la kiroho na niliweza kugundua hila za Shetani; maneno ya Mungu yalinikumbusha moyoni mwangu kwamba: “… lazima umridhishe Mungu licha ya kutotaka kuacha kitu chochote unachopenda, au kilio cha uchungu” (“Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, nilimwambia: “Shangazi, usijaribu kunishawishi, nimesema kila kitu ninachopaswa kuwaambia. Sijui nini kingine ninachopaswa kuwaambia. Wanaweza kunitendea kwa hali yoyote wanayotaka, ni juu yao. Hupaswi kujali kunihusu. Unapaswa kurudi!” Wakati wale askari waovu walipoona mwelekeo wangu imara, hawakuwa na uchaguzi mwingine bali kuiruhusu familia yangu irudi. Njama na mipango ya hao polisi waovu zilikuwa zimeshindwa, na walikuwa na hasira sana kwambawalisaga meno yao na kusema: “Kwa kweli wewe ni mkatili! Wewe una ubinafsi sana. Kwa hakika huna asili ya binadamu. Mungu wako yuko wapi? Kama Yeye ni mwenyezi sana, basi kwa nini Anaruhusu uteswe hapa? Kwa nini Mungu wako haji na kukuokoa? Kama kwa kweli kuna Mungu, basi kwa nini Yeye haji na kufungua pingu zako na kukuokoa? Mungu yuko wapi? Usidanganywe na uongo huu, usiwe mjinga. Hujachelewa mno kuamka na kuuona ukweli. Usipokiri, basi tutakupeleka gerezani kwa miaka mingi!” Uongo wa askari hawa waovu ulinifanya nifikirie kuonekana kwa Bwana Yesu akisulubishwa msalabani. Mungu mwenyewe alikuja na kuwa mwili ili kuwakomboa wanadamu wote; kila kitu Alichokifanya kilikuwa ni kwa manufaa ya mwanadamu; hata hivyo, alidhihakiwa, kukashifiwa, kushtakiwa, kukufuriwa, kutukanwa, na kuuawa na Mafarisayo na wale waliokuwa na mamlaka. Mungu alipitia fedheha mno ili kuwaokoa wanadamu, na hatimaye alitundikwa msalabani kwa ajili ya wanadamu. Maumivu yote ambayo Mungu alipitia ni kwa ajili ya wanadamu na leo maumivu ninayoyapitia ni maumivu ninayohitaji kuyapitia. Kwa sababu nina sumu ya joka kubwa jekundu, Mungu anatumia mazingira haya kwa upande mmoja ili kunipima, na kwa upande mwingine ili kuniruhusu kuelewa kwa hakika asili mbaya ya joka kubwa jekundu na, kulidharau na kulisaliti joka kubwa jekundu, na kumfuata Mungu kikamilifu. Kama vile tu neno la Mungu linavyosema: “Mungu anakusudia kutumia sehemu ya kazi ya pepo wachafu ili kuikamilisha sehemu ya mwanadamu, ili watu hawa waweze kufahamu matendo ya mapepo, na kuwawezesha watu wote wawafahamu kwa kweli mababu zao. Ni wakati huo tu ndipo wanadamu wanaweza kujinasua, sio tu kuwatoroka watoto wa mapepo, lakini hata zaidi mababu zao. Hili ndilo kusudi la asili la Mungu kulishinda kabisa joka kubwa jekundu, kufanya hivyo ili wanadamu wote wajue umbo halisi la joka kubwa jekundu, Aambue kinyago chake kabisa, na kuona umbo lake halisi. Hili ndilo Mungu anataka kutimiza, nalo ni lengo Lake la mwisho duniani ambalo Amefanyia kazi nyingi sana; Ananuia kulifanikisha hili ndani ya watu wote. Hili linajulikana kama ushawishi wa vitu vyote kwa ajili ya kusudi la Mungu” (“Sura ya 41” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili).
Hatimaye, wale askari waovu walinipeleka kwa kituo cha kizuizi na kunizuia kama mhalifu kwa mwezi mmoja. Katika mwezi huu, walinihoji mara moja zaidi. Kwa siku mbili mchana na usiku, hawakuniacha nilale na hawakunipa chakula cha kutosha. Wakati mwingine hawakunipa chakula chochote, lakini bado ilikuwa bure. Joka kubwa jekundu huwatesa na kuwaumiza watu jinsi hii bila kikomo! Wakati kuzuiliwa kwangu kulipofikia kikomo, walinihukumu miaka miwili ya marekebisho kupitia kwa kazi kwa “kuamini katika Xie Jiao na kuvuruga utaratibu wa jamii” bila ushahidi wowote. Kabla ya kwenda kambi ya kazi, familia yangu ilinitumia yuan 2,000 kwa ajili ya gharama za maisha, lakini zote zilibadhiriwa nao. Pepo hawa walikuwa kweli Shetani na pepo wabaya ambao walikuwa na kiu ya damu na uhai wa binadamu. Ulikuwa ni uovu kabisa! Katika nchi ya joka kubwa jekundu, hakuna sheria; chochote linachopinga, linaweza kuchinja na kunyonya lipendavyo; linaweza kuanzisha mashtaka ya jinai linavyotaka ili kuwadhibiti watu na kuwatesa watu. Joka kubwa jekundu huwasingizia na kuwanasa watu, huwaua watu wasio na hatia, hufanya kitu duni kuwa muhimu, na bila haki huwapachika watu sifa. Wao ni dhehebu halisi na la kweli, wao ni kikundi cha wahalifu wenye utaratibu na majambazi ambao huleta majanga na maafa kwa wanadamu. Kwa miaka miwili katika kambi ya kazi, niliona askari waovu wa serikali ya Kichina kimsingi huwadhulumu vibaya na kuwaamrishaamrisha wafanya kazi kama watumwa. Waliwalazimisha watu kula skonzi zilizookwa kwa mvuke na mchuzi wa mboga kila siku; mchana na usiku, walitulazimisha tufanye kazi ya ziada. Nilichoka kwa namna isiyovumilika kila siku na sikupokea fidia yoyote. Nilipokosa kufanya kazi nzuri, ningepata ukosoaji mkali na adhabu (vifungo virefu, kunyimwa chakula, kulazimishwa kusimama kimya). Wakati huu, hao askari waovu bado hawangeniruhusu niende, walinihoji wakijaribu kunilazimisha kukiri mazingira ya kanisa. Nililichukia vikali, nikitegemea imani na nguvu kutoka kwa Mungu, nikasema kwa hasira: “Mmenipiga na kuniadhibu; mnataka nini kingine? Nimesema kila kitu ninachopaswa kusema; mnaweza kunihoji kwa miaka kumi, miaka ishirini, na bado sitajua chochote. Mnaweza kusahau kuhusu hilo!” Waliposikia hili, wakasema kwa ghadhabu: “Huwezi kuponyeka, unaweza kusubiri hapa tu!” Hatimaye, hao askari waovu waliondoka kwa aibu na kushindwa.
Baada ya kupitia mateso ya kinyama ya joka kubwa jekundu na matendo ya kikatili pamoja na kuishi bila haki gerezani kwa miaka miwili, niliona kwa dhahiri kwamba tabia ya joka kubwa jekundu ni uongo, uovu, kiburi, na ukali. Ni chini ya mifugo. Wao hufikia kiwango cha kuweka mabango yakisema “uhuru wa kidini,” kisha wanakwenda huku na huko wakiwafuatilia na kuwatesa wateule wa Mungu kwa kila njia iwezekanayo. Wao kwa wayowayo huivuruga na kuivunja kazi ya Mungu. Wao ni wauaji ambao huua bila kupepesa jicho, wao ni majambazi ambao hupora kwa kisingizio cha “sadaka, haki, amani, na uadilifu.” Mwishowe, barakoa zao zimeambuliwa kabisa kupitia hekima ya kazi ya Mungu, na nyuso zao mbaya za pepo zimefunuliwa katika mwanga ili niweze kufungua mawanda yangu ya maono na kuamka kutoka katika ndoto yangu. Kama vile tu neno la Mungu linavyosema: “Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila kona, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi[b] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida[c]. Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Mwenyezi Mungu milele ni mwenye hekima, mwenye kudura na wa ajabu, na Shetani, joka kubwa jekundu, milele ni wa kusikitisha, mchafu na asiyeweza. Bila kujali jinsi alivyo mshenzi na mkosa nidhamu, na bila kujali jinsi hujitahidi na kuasi, daima atakuwa chombo cha Mungu kuwafundishia watu Wake wateule. Aidha, limehukumiwa kubagwa kuzimu na Mungu kama adhabu ya milele. Linajaribu kuvunja dhamira ya watu kupitia mateso yake ya kinyama ili watu waweze kujitenga na Mungu na kumtelekeza Mungu. Lakini limekosea! Mateso yake hutufanya tuone kwa usahihi kiini cha pepo. Ni jambo linalotuamsha kabisa kulisaliti kabisa na kuwa na imani na ujasiri kumfuata Mungu kwenye njia sahihi ya uzima. Daima nitamtegemea Mungu mwenye busara na mwenyezi. Kuanzia sasa kwendelea, bila kujali ni hatari zipi kemkem na shida zilizo kwa njia iliyo mbele, nitamfuata Mungu kwa uthabiti mpaka mwisho na kuwa na ushuhuda wa nguvu Kwake ili kuliaibisha joka kuu jekundu.
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “kutoweza kuwa.”
b. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo shetani hutumia huwadhuru watu.
c. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo shetani hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Alhamisi, 13 Juni 2019
Kuingiza kwenye Njia ya Imani katika Mungu
Juni 13, 2019Hukumu, Kazi-ya-Mungu, maneno-ya-Mungu, Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo, VitabuNo comments
Rongguang Mji wa Harbin, Mkoa wa Heilongjian
Mnamo mwaka wa 1991, kwa neema ya Mungu, nilianza kumfuata Mwenyezi Mungu kwa sababu ya ugonjwa. Wakati huo sikujua kitu chochote kuhusu kumwamini Mungu, lakini jambo la kushangaza ni kwamba, wakati wa kula na kunywa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, nilifurahia. Nilihisi kwamba maneno Yake yalikuwa mazuri sana, na nilipoimba au kuomba mara nyingi niliguswa na Roho Mtakatifu hadi kiwango cha kulia. Uzuri huo ndani ya moyo wangu, furaha hiyo ilikuwa ni kama kwamba tukio la furaha lilikuwa limenijia. Hasa katika mikusanyiko wakati wa kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, nilihisi kama nilikuwa nimevuka mipaka ya mwili na nilikuwa nikiishi katika mbingu ya tatu, kwamba kila kitu cha ulimwengu kilikuwa kimetupiliwa mbali. Siwezi kusema jinsi nilivyokuwa na furaha, jinsi nilivyoridhika moyoni mwangu. Nilihisi kwamba nilikuwa mtu mwenye furaha zaidi duniani. Kwa hivyo wakati huo niliamini kwamba kumwamini Mungu kulikuwa tu kufurahia neema Yake.
Wakati maneno mengi zaidi na zaidi ya Mungu yalikuwa yakitolewa (wakati huo yalikuwa yakitumwa kanisani siku zote, kifungu baada ya kifungu), pia nilijua zaidi na zaidi. Kisha, sikukamilishwa tena na kufurahi tu neema ya Mungu. Nilipoona “wazaliwa wa kwanza” wakitajwa katika maneno Yake na nikajifunza kwamba Mungu hutoa baraka kubwa kwa wazaliwa Wake wa kwanza, nilitafuta kuwa mmoja, nikitumaini kuwa siku zijazo ningeweza kutawala na Mungu. Baadaye, nilipoona katika maneno Yake kwamba muda Wake ulikuwa ukija hivi karibuni, nilihisi dharura zaidi, na kudhani: Nilikawia sana kumwamini Mungu; Je, sitakuwa na uwezo wa kupata baraka hii? Ninahitaji kuweka juhudi zaidi ndani ya hili. Kwa hivyo, nyumba ya Mungu iliponipangia kutekeleza wajibu, nilikuwa mwenye bidii sana. Sikuogopa shida. Niliamua kuacha kila kitu kumfuata Mungu ili niweze kupata baraka ya kuwa mwana wa kwanza. Kwa kweli, Mungu hakuwa amesema waziwazi katika maneno Yake kwamba tungeweza kuwa wazaliwa wa kwanza. Ilikuwa tu kwa sababu tulikuwa na malengo na tamaa zilizopita kiasi, tuliamini kwamba kwa kuwa Mungu alikuwa ametuita “wana” Wake na kwamba sasa Ametuinua, kwamba hakika tungekuwa wazaliwa wa kwanza. Hivi ndivyo nilivyoamini kwamba nilikuwa, kwa kawaida, nimekuwa mzaliwa wa kwanza. Baadaye niliona maneno ya Mungu ambayo yalikuwa yametolewa karibuni ambayo mara kwa mara yalitaja “watendaji-huduma,” na kulikuwa na maelezo zaidi na zaidi ya hukumu ya watendaji-huduma. Nilidhani mwenyewe: Kwa bahati ninamfuata Mwenyezi Mungu, vinginevyo ningekuwa mtendaji-huduma. Niliposoma kuhusu baraka za Mungu na ahadi za wazaliwa wa kwanza, niliamini kuwa sehemu ya hiyo ingekuwa yangu. Nilipoyasoma maneno Yake ya faraja na ya kuhimiza kwa mzaliwa Wake wa kwanza, nilihisi pia kwamba yalikuwa yakielekezwa kwangu. Nilihisi furaha hata zaidi hasa nilipoona yafuatazo “Maafa makuu hakika hayatawafikia wana Wangu, wapendwa Wangu. Nitawatunza wana Wangu kila wakati na kila sekunde. Hakika hamtavumilia uchungu na mateso hayo; badala yake, ni kwa ajili ya ukamilishwaji wa wana Wangu na utimizaji wa neno Langu ndani yao, ili kwamba muweze kutambua kudura Yangu, mkue zaidi katika maisha, mbebe mizigo kwa ajili Yangu karibuni, na kujitolea kabisa kwa ukamilisho wa mpango Wangu wa usimamizi. Mnapaswa kuwa na furaha na kuridhika na kushangilia kwa sababu ya hili. Nitawapa kila kitu, Nikiwaruhusu kuchukua usukani. Nitaiweka mikononi mwenu. Mwana akirithi mali nzima ya babake, je, ninyi wana Wangu wazaliwa wa kwanza mtaridhi zaidi kiasi gani? Kweli mmebarikiwa. Badala ya kuteseka kutokana na maafa makuu, mtafurahia baraka za milele. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!” (“Sura ya 68” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani: Je, ninaota? Mana hii ya ajabu kutoka mbinguni imeshuka juu yangu? Sikuweza kabisa kuthubutu kuamini, lakini nilihofu kuwa kaka zangu na dada wangesema kuwa imani yangu ilikuwa ndogo sana, kwa hivyo sikuthubutu kutoamini.
Siku moja, nilikwenda kwa furaha kushiriki katika mkutano, na nikaona kwamba viongozi wawili walikuwa wamekuja kanisani. Nilipokuwa katika ushirika nao, walisema kuwa walikuwa watendaji-huduma. Baada ya kusikia hayo, nilikuwa na hofu, na nikawauliza: “Ikiwa ninyi ni watendaji-huduma, si sisi wote ni watendaji-huduma?” Walisema ukweli bila kusita: “Takribani sisi sote nchini China ni watendaji-huduma.” Niliposikia wakisema hivi, moyo wangu ulihofu. Haiwezekani! Je, huu ni ukweli? Lakini nilipoona maonyesho yao nzito, yenye uchungu na kwamba nyuso za wengine pia zilikuwa za majonzi, sikuweza kuamini. Lakini nilibadili mawazo yangu na kufikiri: Kama viongozi, walikuwa wameacha familia zao na kazi zao, walikuwa wameteseka sana na kulipa thamani kuu sana kwa ajili ya kazi ya Mungu. Nilipungukiwa kabisa ikilinganishwa nao; kama wao ni watendaji-huduma, ningesema nini kingine? Mtendaji-huduma ni mtendaji-huduma, hivyo wakati huo, sikuhisi vibaya mno.
Baada ya kwenda nyumbani, nilichukua neno la Mungu tena na kuangalia kile Mungu alichokuwa na kusema kuhusu watendaji-huduma, na nikaona haya: “Wale wanaonitumikia, sikilizeni! Mnaweza kupokea baadhi ya neema Yangu wakati mnanitumikia. Yaani, ninyi mtajua kwa wakati kuhusu kazi Yangu ya baadaye na mambo ambayo yatatokea baadaye, lakini hamtafurahia hilo kabisa. Hii ni neema Yangu. Wakati huduma Yako imekamilika, ondoka mara moja na usikawie. Wale ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza hawapaswi kuwa wenye kiburi, lakini mnaweza kujivunia, kwa kuwa Nimewapa baraka za milele kwenu. Wale ambao ni walengwa wa uangamizaji hampaswi kujiletea shida au kuhisi huzuni kwa ajili ya hatima yenu; ni nani aliyekufanya kuwa mzawa wa Shetani? Baada ya kufanya huduma yako kwa ajili Yangu, unaweza kurudi tena kwenye shimo lisilo na mwisho kwa sababu hutakuwa tena na matumizi Kwangu na Nitaanza kuwashughulikia na kuadibu Kwangu. Mara Ninapoanza kazi Yangu huwa Sikomi kamwe; kile Ninachofanya kitatimizwa na kile Ninachotimiza kitadumu milele. Hili linatumika kwa wazaliwa Wangu wa kwanza, wanangu, watu Wangu, na hili linawahusu ninyi pia—Mimi kuwaadibu ninyi kutakuwa kwa milele” (“Sura ya 86” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Mara tu nilipoyasoma maneno haya nilizongwa na uchungu ambao sikuwa nimewahi kuhisi hapo awali. Nilifunga haraka kitabu cha maneno ya Mungu na sikujaribu kukitazama tena. Mara moja hisia za kusikitisha, za kuchanganyikiwa, za kutoridhika zote zilichemka ndani ya moyo wangu mara moja. Nilidhani: Jana nilikuwa katika susu ya furaha, lakini leo nimesukumwa nje ya nyumba ya Mungu. Jana nilikuwa mwana wa Mungu, lakini leo nimekuwa adui wa Mungu, mzao wa Shetani. Jana, baraka zisizo na kikomo za Mungu zilikuwa zikinisubiri, lakini leo shimo la kuzimu ni hatima yangu, nami nitaadhibiwa hata milele. Ikiwa Hatoi baraka, basi haijalishi, lakini kwa nini bado lazima Aniadibu? Nimekosea vipi tena? Haya yote ni ya nini tena? Sikuwa tayari kukabiliana na ukweli huu; sikuweza kukabiliana na aina hii ya ukweli. Niliyafumba macho yangu na sikuwa radhi kufikiri juu ya hayo tena. Nilitumaini sana kwamba ilikuwa ndoto tu.
Kuanzia hapo kuendelea, mara tu nilipojifikiria kuwa mtendaji-huduma, nilisikia maumivu yasiyoelezeka moyoni mwangu, na sikuthubutu kuyasoma maneno ya Mungu tena. Lakini Mungu ni mwenye hekima sana, na maneno Yake ambayo huwaadibu na kuwafichua watu hayaenei tu kwa fumbo, lakini pia ni unabii wa maangamizi ya siku za baadaye na vilevile mtazamo wa ufalme na mambo yanayofanana na hayo. Hivi vyote vilikuwa vitu ambavyo nilitaka kuvijua, hivyo bado singekwepa maneno Yake. Wakati wa kusoma maneno ya Mungu, maneno Yake makali sana yaliuchoma moyo wangu mara kwa mara, na sikuwa na budi ila kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye. Nilihisi kwamba ghadhabu kubwa ya hukumu ya Mungu ilikuwa daima juu yangu. Kando na maumivu, nilijua ukweli halisi wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Ilibainika kuwa nilikuwa mtoto wa joka kubwa jekundu, uzao wa Shetani, na lengo la uharibifu. Katika kukata tamaa, sikuthubutu tena kutumaini kwa tamaa baraka zozote, na nilikuwa tayari kukubali majaaliwa ya Mungu kwamba nilikuwa mtendaji-huduma. Nilipohisi kwamba ningeweza kutoa moyo wangu katika kuwa mtendaji huduma, Mungu tena aliyapanga mazingira yaliyofichua tabia potovu ambayo ilikuwa imefichwa ndani yangu. Siku moja nilipokuwa nikiyasoma maneno ya Mungu, niliona: “Baada Yangu kurudi Sayuni, wale walio duniani wataendelea kunisifu Mimi kama zamani. Wale watendaji huduma waaminifu wanabaki wakisubiri kutoa huduma Kwangu lakini kazi yao itakuwa imefika mwisho. Jambo bora zaidi wanaloweza kufanya ni kutafakari hali Yangu kuwa duniani. Wakati huo Nitaanza kushusha maafa juu ya wale ambao watakabiliwa na msiba mkubwa, lakini kama vile[a] wote wanaamini kwamba Mimi ni Mungu mwenye haki, basi bila shaka sitawaadhibu wale watendaji-huduma waaminifu nao watapokea tu neema Yangu” (“Sura ya 120” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilipoona hili, nilifikiri kwa siri: Sitafikiri tena juu ya haki ya mzaliwa wa kwanza na sitahitaji tena baraka nyingi. Sasa nitafuatilia tu kuwa mtendaji-huduma mwenye kumcha Mungu. Huu sasa ndio ufuatiliaji wangu wa pekee. Katika siku zijazo, bila kujali ni nini ambacho nyumba ya Mungu atanipangia mimi kufanya, nitakifanya kwa kujitolea kadiri ninavyoweza. Mimi kabisa siwezi kupoteza nafasi ya kuwa mtendaji-huduma mwaminifu tena. Kama hata sina uwezo wa kuwa mtendaji-huduma mcha Mungu lakini bali mtendaji-huduma tu, baada ya kumaliza huduma yangu ni lazima nirudi katika shimo la kuzimu au ziwa la moto wa jahanamu. Kwa hivyo yote ni ya nini? Sikuthubutu kuonyesha mawazo haya kwa mtu yeyote, lakini sikuweza kuepuka uchunguzi kutoka kwa macho ya Mungu. Niliyasoma maneno ya Mungu yaliyosema: “Hakuna awezaye kuielewa asili ya mwanadamu isipokuwa Mimi, na wote wanafikiria kwamba wao ni watiifu Kwangu, pasipo kujua kwamba utiifu wao ni mchafu. Uchafu huu utawaangamiza watu kwa kuwa wao ni njama ya joka kubwa jekundu. Hilo lilidhihirishwa na Mimi zamani sana; Mimi ni mwenyezi Mungu, na je, Mimi singeweza kufahamu jambo rahisi kama hili? Mimi ninaweza kupenyeza damu yako na mwili wako ili kuziona nia zako. Si vigumu Kwangu kuielewa asili ya mwanadamu, lakini watu hujaribu kuwa wajuaji, wakifikiria kwamba hakuna mtu ajuaye nia zao isipokuwa wao wenyewe. Je, hawajui kwamba, mwenyezi Mungu anaishi ndani ya mbingu na dunia na vitu vyote?” (“Sura ya 118” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Watu wengi zaidi sasa wanahodhi matumaini haba, lakini matumaini hayo yanapogeuka na kuwa masikitiko hawataki kuendelea zaidi na wanaomba kurudi. Nimekwisha kusema awali kwamba Simweki yeyote hapa kinyume cha mapenzi yake, lakini tahadhari kufikiria matokeo yatakavyokuwa kwako, ni huu ni ukweli, si Mimi kukutisha wewe” (“Sura ya 118” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma haya, moyo wangu ulikuwa ukipapa kwa nguvu. Nilihisi kwamba Mungu kwa kweli hubaini kila kipengele cha nafsi ya mwanadamu. Tunafikiria kitu na Mungu anajua; tunaweka tumaini kidogo katika mioyo yetu na Mungu anachukizwa. Wakati huo tu ndipo nilikuwa na moyo wa kumcha Mungu. Niliamua kwamba singeendesha tena shughuli na Mungu, ila kwa uaminifu, ningetenda kama mtendaji-huduma na kutii miundo Yake.
Baadaye tu ndipo nilijua kwamba uzoefu wangu kwa miezi hii mitatu ilikuwa jaribio la watendaji-huduma. Ilikuwa kazi ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ndani ya watu ya jaribio kwa maneno Yake. Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilielewa kuwa Mungu sio Mungu mwenye huruma na upendo tu, bali ni Mungu mwenye haki, Mungu mwenye uadhama ambaye havumilii makosa ya wanadamu. Maneno Yake yana mamlaka na nguvu, ambayo hayana budi ila kuzalisha moyo wa hofu kwa mwanadamu. Nilijua pia kwamba wanadamu ni viumbe wa Mungu, kwamba tunapaswa kuamini katika Mungu na kumwabudu Yeye. Hili ndilo lililo sawa na sahihi. Hakuna haja ya sababu, ya masharti, na hakupaswi kuwa na tamaa ya makuu au hamu iliyopita kiasi. Ikiwa watu wanaamini katika Mungu ili kupata kitu kutoka Kwake, basi aina hii ya imani ni kumtumia vibaya na kumdanganya. Ni maonyesho ya kukosa dhamiri na mantiki. Hata kama watu humwamini Mungu lakini hawapati chochote na baadaye kupata adhabu Yake, wanapaswa kumwamini. Wanadamu wanapaswa kumwamini na kumtii Mungu kwa sababu Yeye ni Mungu. Nilitambua pia kwamba mimi mwenyewe ni mwana wa joka kuu jekundu, kizazi cha Shetani, na mmoja wa wale watakaoangamia. Mungu ni Bwana wa viumbe vyote, na bila kujali Anavyonitendea mimi inastahili. Yote ni ya haki, na ninapaswa kuitii mipango na mipangilio Yake bila masharti. Sipaswi kujaribu kujadiliana na Yeye, na hata zaidi sipaswi kumpinga. Nilipokumbuka uzuzu wangu mwenyewe uliofichuliwa katika jaribio hili, niliona kwamba nilikuwa kweli mwenye aibu, na kwamba nilitaka tu kupata hadhi fulani ya juu, baraka nyingi, au hata kukaa bega kwa bega na Mungu na kutawala pamoja na Yeye. Nilipoona kwamba singepata baraka nilizozitarajia bali badala yake kupitia maangamizi, nilifikiria kuhusu kumsaliti Mungu. Mafafanuzi hayo ya wazi kabisa yalinifanya nione wazi kwamba lengo langu katika kumwamini Mungu lilikuwa kubarikiwa. Nilikuwa nikijaribu kufanya shughuli za kibiashara na Mungu kwa dhahiri. Kweli nilikuwa asiye na aibu, nikipigania hadhi na Mungu kwa ulafi—hilo lilitofautiana vipi na malaika mkuu? Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi, na nilikuwa nimepoteza kabisa mantiki ambayo mtu anapaswa kuwa nayo. Isingekuwa hekima hiyo katika kazi ya Mungu—kutumia jaribio la watendaji-huduma ili kunishinda, kuvunja tamaa yangu ya kupata baraka—bado ningekuwa nikikimbia katika njia isiyo sahihi ya kutafuta baraka. Nisingeweza kuelewa asili yangu iliyopotoka, na hasa singekubali hukumu na adhabu ya maneno ya Mungu kwa utiifu. Katika hali hiyo, nisingeweza kamwe kuokolewa au kukamilishwa.
Baada ya kupitia jaribio la watendaji-huduma, nilidhani sikuthubutu tena kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu ili kupata baraka, na nilidhani sikuthubutu tena kufanya mambo kwa nia ya kufanya shughuli na Mungu. Nilihisi kuwa kumtumia vibaya na kumdanganya Mungu kwa njia hii kulistahili kudharauliwa sana. Lakini wakati huo huo, nilikuwa na ufahamu kwamba Mungu kutumia jaribio hili kuokoa wanadamu ni nia Yake ya fadhili, na nilijua kuwa hakuna sehemu Yake ambayo humchukia mwanadamu. Upendo Wake kwa wanadamu haujabadilika tangu Alipoumba ulimwengu, hivyo, moyoni mwangu, nilikuwa tayari kufuatilia njia ya kuridhisha na kulipiza upendo wa Mungu katika imani yangu ya baadaye Kwake na kutimiza wajibu wangu. Hata hivyo, kwa sababu nia ya kupata baraka na kuendesha shughuli na Mungu imefanywa madhubuti sana katika mioyo ya watu, haiwezekani kutatua kabisa kwa kupitia jaribio moja tu. Baada ya muda fulani kupita, mambo haya yatajidhihirisha tena. Kwa hivyo, ili kutushinda zaidi na kabisa na kutuokoa, Yeye hufanya majaribio kadhaa ya mfululizo kwetu—jaribio la nyakati za kuadibiwa, jaribio la kifo, na majaribio ya miaka saba. Kati ya majaribio haya, nililopitia zaidi na kufaidika zaidi kutokana nalo lilikuwa jaribio la miaka saba la 1999.
Mnamo mwaka wa 1999, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa. Hii ilikuwa ni mwaka ambao injili ya ufalme ilienea sana, na nyumba ya Mungu ilihitaji kwamba tujaribu kumwokoa kila mtu aliyekuwa na uwezekano wa kuokolewa. Nilipoona utaratibu huu kutoka kwa nyumba ya Mungu, nilifikiri kazi ya Mungu ingekamilika mwaka wa 2000. Ili kujipatia roho zaidi na kupata hatima nzuri wakati ulipofika, nilijipa shughuli za injili kuanzia asubuhi hadi usiku. Kwa mintarafu ya maisha ya kanisa, nilikuwa nikihudhuria tu na kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati. Hata ingawa nilitambua kuwa nia zangu hazikuwa sawa, sikuwa na uwezo wa kudhibiti tamaa yangu ya kupata baraka. Wakati huo nilikuwa na shughuli nyingi, na nilihisi kuwa kufanya chochote kando na kazi ya injili kulikuwa kunanizuia, hata kula na kunywa neno la Mungu. Hivi ndivyo nilivyoanza kufanya kazi kwa ari kubwa, na bila ya kujua mwaka ulikuwa umekwisha. Nyumba ya Mungu ilikuwa imemchagua mtu wa mahali palepale ili kusaidia katika kazi, kwa hivyo nikarudi eneo la makazi yangu ya kudumu.
Nilidhani kwamba kazi ya Mungu itakapomalizika, janga kubwa hakika lingetokea, na hivyo baada ya kurudi nyumbani, nilisubiri tu janga nikiwa nyumbani kila siku, nikisubiri mwisho wa kazi ya Mungu. Nilipoona kwamba Sherehe ya Majira ya Kuchipua ilikuwa ikiwadia, kulikuwa na ushirika kutoka kwa kiongozi wa kanisa uliosema kuwa ni jambo la lazima kupitia miaka saba ya majaribio. Baada ya kusikia ujumbe huu, nilihisi kushtuka na moyo wangu ulikuwa katika msukosuko. Sikuwa na budi ila kuanza kujadiliana na Mungu: Miaka mingine saba imenikaribia—je, hii ni njia gani ya kuishi? Ee Mungu, ninakuomba Uniangamize mimi. Kwa kweli siwezi kuvumilia mateso haya tena! Siku iliyofuata, bado sikuweza kuepukana na mfadhaiko wangu. Nilidhani: Vyovyote vile, imekuwa miaka saba. Kesho ni siku nyingine—nitatoka na kuiondoa kutoka mawazo yangu. Mara tu nilipoingia kwenye basi, nilihisi Roho Mtakatifu alikuwa ndani yangu akishutumu: Wakati huo ulisema kwamba ungempenda Mungu hadi mwisho, kwamba hungemwacha kamwe, kwamba ungevumilia shida yoyote na Yeye. ... Je, wewe si mnafiki anayejaribu kumdanganya Mungu? Huku nikikabiliana na shutuma ya Roho Mtakatifu, sikuwa na budi ila kuning’iniza kichwa changu. Ilikuwa kweli. Awali, nilipokuwa nimefurahia neema ya Mungu, nilimpa ahadi, lakini sasa wakati ambapo kuna matatizo na ni lazima niyapitie, nataka kughairi neno langu. Hivyo si ahadi zangu ni za uongo tu? Mungu alinipa upendo mwingi sana, na sasa ninapokutana na mazingira ambayo sio kabisa kama ambavyo ninapenda nina hasira kubwa sana kiasi kwamba nataka kumghairi Mungu. Kwa kweli mimi ni mnyama asiye na shukrani, asiye bora kuliko mnyama! Nilipofikiri juu ya jambo hili, sikukuwa tena na hisia za kwenda nje, lakini nilirudi nyumbani na moyo mzito. Hata ingawa nilikuwa nimelazimishwa kuwa “mtiifu,” nilipofikiria ukweli kwamba bado kulikuwa na miaka saba iliyobaki katika kazi ya Mungu, niliweka huru katika moyo wangu na chochote nilichokifanya, sikuwa na haraka au wasiwasi. Nilitia bidii kila siku katika kutimiza wajibu wangu kana kwamba ilikuwa siku nyingine yoyote. Aina hii ya hali mbaya na yenye makabiliano ilinifanya nipoteze kazi ya Roho Mtakatifu hatua kwa hatua, na ingawa nilitaka kubadilisha hali yangu mwenyewe, sikuweza.
Siku moja, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno Yake yaliyosema: “Wakati baadhi ya watu walipotenda wajibu wao mara ya kwanza, walijaa nguvu, kana kwamba haingewahi kuishiwa na nguvu hizo. Lakini inakuwaje kwa kadri wanapoendelea ndipo wanapoonekana kupoteza nguvu hizo? Mtu waliokuwa wakati huo na mtu waliye sasa ni sawa na watu wawili tofauti. Kwa nini walibadilika? Sababu ilikuwa gani? Ni kwa sababu imani yao kwa Mungu ilienda njia mbaya kabla ya kufikia njia sahihi. Waliichagua njia mbaya. Kulikuwa na jambo lililokuwa limefichwa ndani ya kufuatilia kwao kwa kwanza, na kwa wakati mwafaka jambo hilo likaibuka. Nini kilikuwa kimefichwa? Ni matarajio yanayokuwa ndani ya mioyo yao wakati wakimsadiki Mungu, matarajio kwamba siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili taabu yao itafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilika na kwamba mateso yao yote yataisha” (“Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalinifanya nitafute mzizi wa tatizo hilo. Ilibainika kuwa nilikuwa na matumaini yaliyofichika ndani ya ufuatiliaji wangu, nikitumaini kwamba siku ya Mungu ingewadia hivi karibuni na kwamba singeweza kuteseka tena, kwamba ningekuwa na majaaliwa mazuri. Wakati huo wote, ufuatiliaji wangu ulitawaliwa na tumaini hili, na wakati ambapo matumaini yangu yalikuwa bure, niliteseka na kuvunjika moyo kiasi cha kumsaliti Mungu, hata kufikiri juu ya kuponyoka kupitia kifo. Ni wakati ule tu ndipo niliona kwamba nilikuwa nimemfuata Mungu kwa miaka mingi, lakini asili yake haikuwa kufuatilia njia ya kweli; daima nililenga siku ya Mungu, na nilikuwa nimefanya biashara na Yeye ili nipate baraka Zake. Hata ingawa wakati huo sikuwa na budi ila kukaa ndani ya nyumba ya Mungu na kutomwacha, ikiwa sikutatua uchafu ndani yangu, mapema au baadaye ningempinga na kumsaliti Mungu. Baada ya kuona hali yangu hatari, ndani ya moyo wangu nikamwuliza Mungu: Ninaweza kufanya nini ili kuondoa uchafuzi wa kutumaini siku ile? Kisha, nilisoma tena maneno ya Mungu, ambayo yalisema: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa? Mnafaa kuitembelea vipi njia iliyo mbele? Mnafaa kuufuatilia vipi ukweli? Kama hamfuatilii ukweli basi mnawezaje kuipata kazi ya Roho Mtakatifu? Pindi utakapopoteza kazi ya Roho Mtakatifu, basi utakuwa katika hatari kubwa zaidi. Mateso ya sasa si muhimu. Je, wajua yatakufanyia nini?” (“Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kutoka kwa maneno haya ya Mungu, niliweza kuona kwamba kuna maana kubwa kwa watu leo kuwa na uwezo wa kuteseka, lakini sikuweza kutambua maana ya mateso hayo kweli ilikuwa nini. Nilijua tu kwamba kama ningeweza tu kubaini maana ya mateso ndio ningeweza kwa kweli kubadilisha hali yangu ya kutarajia siku ya Mungu. Hii ilikuwa njia ya kuelekea katika azimio. Ingawa sikufahamu maana ya mateso wakati huo, jambo pekee ambalo ningeweza kufanya ilikuwa kufuatilia ukweli kabisa, kutafuta ukweli zaidi, kwa sababu ikiwa tu ningepata ukweli ndio ningeweza kuelewa kweli maana ya mateso, na ndipo basi ningeweza kuondoa uchafuzi huu ndani yangu.
Kama kwamba muda ulikuwa umeongeza kasi, nilipepesa na tayari ilikuwa mwaka wa 2009. Hiyo miaka saba ilikuwa imepita muda mrefu, bila mimi kugundua. Nilikuwa nimefika mbali hivyo na hatimaye nilihisi kwamba miaka hiyo saba haikuwa muda mrefu kama nilivyofikiri. Hiyo miaka michache, katika hukumu iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu, katika ufunuo wa majaribu ya Mungu na usafishaji, nilikuwa nimeuona uso wangu wa kweli. Niliona kwamba nilikuwa, mtoto wa joka kuu jekundu kabisa, kwa sababu nilijawa na sumu lake, kama vile sumu ya “Usiamke mapema ikiwa hakuna faida, faida huongoza katika kila kitu.” Huu ni uwakilishi bora zaidi wa sura ya joka kuu jekundu. Chini ya utawala wa sumu hii, imani yangu kwa Mungu ilikuwa tu kubarikiwa. Niliyotumia kwa ajili ya Mungu kilikuwa na mpaka wa muda, na nilitamani kuteseka kidogo na kupata baraka kubwa. Ili kuniondolea nia hii thabiti ya kubarikiwa na mtazamo wa kibiashara uliokuwa ndani yangu, Mungu alikamilisha majaribio mengi na usafishaji kwangu. Wakati huo tu ndipo uchafu katika imani yangu kwa Mungu ulipotakaswa. Na nikaona ndani ya ufunuo wa Mungu kwamba nilikuwa nimejaa tabia mbaya ya Shetani. Nilikuwa na kiburi, udanganyifu, ubinafsi na mwenye kustahili dharau, mzembe, na mwenye shingo upande. Yalinifanya nione wazi zaidi na zaidi hali yangu halisi, kuona kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani, kwamba nilikuwa mwana wa kuzimu. Kwamba ningeweza kumwamini Mungu na kumfuata Mungu wakati huo ilikuwa kweli kukuzwa na Yeye na neema, na kwamba ningeweza kukubali hukumu na kuadibiwa na Yeye vilikuwa baraka kubwa zaidi. Shukrani yangu kwa Mungu ilikua, mahitaji yangu yakawa madogo, utiifu wangu Kwake ukakua, na kujipenda kwangu mwenyewe kukapungua. Niliomba tu kuwa na uwezo wa kupoteza tabia yangu potovu ya kishetani, kuwa mtu ambaye anamtii na kumwabudu Mungu kweli. Tokeo hili dogo lilipatikana baada ya kazi nyingi ya Mungu isiyojulikana kiasi, ikiwa ni pamoja na jitihada Zake nyingi sana. Hadi leo, kupitia kazi ya Mungu, nimekwisha kufahamu kwamba wokovu wa watu kwa kweli si rahisi. Kazi Yake ni ya vitendo sana—kazi Yake ya kuwabadilisha na kuwaokoa wanadamu sio rahisi kama ambavyo watu wangefikiria. Hivyo, sasa mimi si kama mtoto mjinga, kutumaini tu kwamba siku ya Mungu itakuja kwa haraka, lakini daima ninahisi kuwa upotovu wangu ni mkubwa sana, kwamba ninahitaji sana wokovu wa Mungu na ninahitaji sana kupitia hukumu na kuadibiwa na Yeye, majaribio Yake na usafishaji Wake. Lazima sasa niwe na dhamiri kidogo na mantiki ambavyo vinapaswa kuwepo katika ubinadamu wa kawaida, na kikamilifu kuipitia kazi ya Mungu ya wokovu wa wanadamu. Mwishoni wakati ambapo nitaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kweli na kupokea furaha ya Mungu, moyo wangu utatimizwa. Sasa, ninapoangalia nyuma na kufikiri juu ya kile nilichofichua juu yangu wakati ambapo miaka hiyo saba ya majaribio ilinijia, ninahisi kwamba nina deni kubwa kwa Mungu, kwamba niliujeruhi moyo Wake sana. Kama kazi ya Mungu ingekamilika mwaka 2000, mimi, ambaye nilikuwa mchafu sana kabisa, hakika ningeangamizwa. Miaka saba ya majaribio kweli ilikuwa uvumilivu wa Mungu na huruma kwangu, na aidha, ilikuwa ni wokovu wa Mungu wa kweli zaidi na halisi zaidi kwangu.
Mara nilipokuwa nimetoka katika miaka hiyo saba na nilitafakari maneno hayo kutoka kwa Mungu ambayo sikuwa nimeyaelewa awali: “Je, ulijua kwamba kwa kumwamini Mungu huko Uchina, kuweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, kwamba wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. … Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi wa Mungu. Iliwahi kusemwa: ‘Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo.’ Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa?” Niliweza kuelewa maana kidogo ya maneno haya; niliweza hatimaye kuhisi kuwa mateso ni yenye umuhimu kweli. Ingawa niliteseka nilipopitia majaribio haya, baada tu ya kuteseka ndipo niliona kwamba kile nilichopata kilikuwa cha thamani sana, muhimu sana. Kwa kupitia majaribio haya, niliona tabia yenye haki ya Mwenyezi na uweza wa Mungu na hekima. Nilielewa ukarimu wa Mungu, na nilionja upendo wa kina, wa baba wa Mungu kwa watoto Wake. Pia nilipitia mamlaka na nguvu katika maneno Yake, na niliona ukweli wa kupotoshwa kwangu na Shetani. Niliona dhiki ya Mungu katika kazi Yake ya wokovu, kwamba Yeye ni mtakatifu na mwenye kuheshimiwa, na kwamba watu ni wabaya na wa kudharauliwa. Pia nilipitia jinsi Mungu anavyoshinda na kuwaokoa wanadamu ili kuwaleta kwenye njia sahihi ya kumwamini. Ninapolifikiria sasa, kama Mungu hakuwa amefanya kazi hii ngumu ya majaribio kwangu baada ya majaribio, nisingeweza kuwa na ufahamu huu. Dhiki na usafishaji vina manufaa katika ukuaji wa watu katika maisha yao. Kwa kuvipitia, watu wanaweza kupata kitu cha maana na cha thamani sana katika kipindi chao cha kumwamini Mungu—ukweli. Baada ya kuona thamani na maana ya mateso, mimi tena sina ndoto ya kuingia katika ufalme nikiwa nimeabiri motokaa, lakini nina nia ya kusimamisha imara miguu yangu na kupitia kazi ya Mungu, kufuatilia kwa kweli ukweli ili kujibadili.
Kwa kupitia miaka kadhaa ya kazi ya Mungu, ndipo sasa tu nina ufahamu mdogo wa vitendo wa maneno haya kutoka kwa Mungu: “Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu” (Dibaji wa Neno Laonekana katika Mwili). Kabla ya kupitia majaribio haya kutoka kwa Mungu, nilikuwa nimejaa nia kali ya kubarikiwa na mtazamo wa kishughuli. Hata ingawa nilijua kikanuni kuamini katika Mungu kulikuwa nini na lengo la imani katika Mungu lilikuwa nini, bado nilikuwa nimelenga tu kubarikiwa. Sikujali ukweli, sikuondoa tabia yangu potovu ili kuyakidhi mapenzi ya Mungu, au kumtambua Mungu kama lengo la ufuatiliaji wangu. Ni wakati ule tu ndipo nilielewa kwamba Mungu alipokuwa mwili kazi Yake ya msingi ilikuwa kutatua nia ya wanadamu ya kubarikiwa na mtazamo wao wa kishughuli. Ilikuwa ni kwa sababu mambo haya kweli ni vikwazo kati ya wanadamu na kuingia kwao kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Mambo haya yanapofichwa ndani ya wanadamu, hawatafuatilia ukweli. Hawatakuwa na lengo sahihi katika ufuatiliaji wao; watatembea katika njia isiyo sahihi. Hii ni njia ambayo haitambulikani na Mungu. Sasa, kazi ya Mungu ya kushinda na wokovu imeharibu ngome ya Shetani ndani yangu. Hatimaye sina wasiwasi tena, sina tena fikira za kupatia baraka au kupitia janga. Sifuatilii tena kwa uchungu tamaa zilizopita kiasi, na sizungumzii tena masharti au kutoa mahitaji ili kuepuka janga hilo. Bila uchafu huu, najihisi mwepesi, huru. Ninaweza kufuatilia ukweli kwa utulivu na kikamilifu. Hili ndilo tunda lililotokana na majaribio na usafishaji wa Mwenyezi Mungu. Ni kazi ya Mwenyezi Mungu ya majaribio na usafishaji ambavyo vimeniongoza kwenye njia ya kweli ya kumwamini Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali kazi zaidi ya majaribio ambayo Mungu hufanya, bila kujali jinsi usafishaji wenye maumivu ninaoupitia, nitatii na kukubali, na kuyapitia kwa kweli. Nitatafuta ukweli kutoka kwazo, na kufikia tabia isiyo na upotovu ili kukidhi mapenzi ya Mungu, ili kulipiza miaka mingi ya Mungu ya juhudi ya bidii.
Tanbihi:
a. Nakala asili inaacha “kama vile.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Jumatano, 12 Juni 2019
Hukumu ni Mwanga
Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.
Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: “Unaamini katika uwepo wa Mungu?” Nilijibu: “Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo.” Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu yako itarejea: ukiwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani ulipopotea kwa wakati mmoja, ukianguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na baba. Unatambua zaidi kuwa mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.
Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: “Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri.” Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?” (“Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninang’ang’ana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kumtegemea Mungu kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.
Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama “Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka.” Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikifuatilia ilikinzana na mapenzi ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: “Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako.” Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani. Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: “Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia.” Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “Kama ulitumia juhudi nyingi lakini bado Sikuchangamkii, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika uvunguvungu? Ikiwa, baada ya wewe kutumia vitu fulani kwa ajili Yangu, Sijatimiza mahitaji yako madogomadogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi au hata kuwa na ghadhabu na kunitusi?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena.” Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote kutafuta mahali salama, mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?” (“Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kulinifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, sikuwa na budi ila kuhisi aibu, kana kwamba sikuwa na mahali pa kujificha, na nilihisi kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na nilihitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: “Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu , pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako.”
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. … Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia hiziana asili ya aina gani? Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika “Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha”: “Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. … Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili” (“Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha I). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu. Alinihukumu na kuniadibu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.
Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.
Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu. Utukufu wote uwe kwa Mungu. Amina!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo