Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukweli. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ukweli. Onyesha machapisho yote
Ijumaa, 9 Agosti 2019
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 2 Mamlaka ya Neno la Mungu | Kwaya za Injili
Mwenyezi Mungu anasema, “Maneno Yangu ni ukweli, uhai, njia, na upanga mkali ukatao kuwili, ambao unaweza kumshinda Shetani” (Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ni kama upanga wenye makali pande mbili, yanayoweza kushinda nguvu zote za uovu.
Jumanne, 6 Agosti 2019
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 1 Matukio ya Kuzimu | Kwaya za Injili
"Kwaya ya Kichina Onyesho la 13" Clip 1 Matukio ya Kuzimu | Kwaya za Injili
Je, unafikiria kuna kuzimu? Je, kuzimu iko namna gani hasa? Tafadhali fuatilia dondoo hii ya video!
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake.
Jumatano, 31 Julai 2019
Neno la Mungu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli” (Dondoo)
Neno la Mungu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye
Anayemwamini Mungu Kweli” (Dondoo)
Mwenyezi Mungu anasema, “Kuchunguza kitu cha aina hii sio vigumu, lakini kunahitaji kila mmoja wetu ajue ukweli huu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana Mungu Hupata mwili, Ataleta mbele kazi Anayopaswa kufanya, na kwa maana Mungu Amepata mwili, Ataonyesha kile Alicho na Ataweza kuuleta ukweli kwa mwanadamu, kumpa mwanadamu uhai, na Amwonyeshe mwanadamu njia.
Ijumaa, 19 Julai 2019
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 100
Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote.
Jumatano, 10 Julai 2019
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103
Julai 10, 2019Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho-Mtakatifu, sauti-ya-Mungu, ukweli, VitabuNo comments
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103
Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami.
Jumatatu, 1 Julai 2019
"Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance
Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia,
mchangamfu na mwenye nguvu za ujana,
Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu.
wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.
Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake.
Tunakubali uchunguzi wa Mungu, tunaishi mbele Yake.
Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku,
Ijumaa, 28 Juni 2019
Wimbo wa Dini “Watu Waaminifu Tu Ndio Wana Mfano wa Binadamu” | Asante kwa Upendo na Wokovu wa Mungu"
Juni 28, 2019maneno-ya-Mungu, sauti-ya-Mungu, ukweli, Upendo-wa-Mungu, Video, Video-za-Nyimbo-za-DiniNo comments
Wimbo wa Dini “Watu Waaminifu Tu Ndio Wana Mfano wa Binadamu” | Asante kwa Upendo na Wokovu wa Mungu
Kwa ajili ya umaarufu na faida niliacha viwango vyote vya kutenda,
na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.
Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.
Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.
Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,
bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.
Alhamisi, 27 Juni 2019
Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God
Juni 27, 2019neno-la-Mungu, Tabia-ya-Mungu, ukweli, Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu, VideoNo comments
Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God
Mwenyezi Mungu anasema, “Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi. Kwa hivyo, kabla ya kuuamua mwisho wenu, Ninafaa kuwaambia kwanza baadhi ya mambo, ambayo ni yenye umuhimu mkubwa sana kwenu. ... Katika maisha yenu, Naona mengi ambayo mnafanya ambayo hayana uhusiano na ukweli, kwa hivyo Nawaambia moja kwa moja muwe watumishi wa ukweli na wala si kutawaliwa na maovu na ubaya. Msikanyage ukweli na kuchafua sehemu yoyote ya nyumba ya Mungu. Hili ndilo onyo Langu kwenu.”
Husika: Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki "Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19"
Jumatano, 12 Juni 2019
Hukumu ni Mwanga
Zhao Xia Mkoa wa Shandong
Jina langu ni Zhao Xia. Nilizaliwa katika familia ya kawaida. Kutokana na ushawishi wa misemo kama “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” na “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” sifa na heshima zikawa muhimu sana kwangu. Kila kitu nilichofanya kilikuwa ili kupata sifa, pongezi, na upendezwaji wa watu wengine. Baada ya kuolewa, malengo niliyojiwekea yalikuwa: Nitaishi maisha ya kitajiri zaidi kuliko wengine; Ni lazima nisiruhusu mtu yeyote kusema mambo hasi kuhusu jinsi ninavyowatendea wazee au kuhusu tabia na mwenendo wangu; na nitahakikishia mtoto wangu ataingia katika chuo kikuu cha kifahari na ana matarajio mazuri, ili kuongeza fahari zaidi katika heshima yangu. Kwa hivyo, sikuwahi kugombana na wakwe wangu. Mara nyingine, wakati walisema maneno makali kwangu, ningehisi nimekerwa mno mpaka ningejificha na kulia badala ya kuwapa uhasi. Wakati niliona wengine wakiwanunulia wazazi wao nguo wakati wa Mwaka Mpya wa Kichina na sikukuu zingine, ningeenda mara moja kumnunulia mama mkwe wangu baadhi, na ingekua pia ya ubora wa hali ya juu. Wakati jamaa walikuja kunitembelea, ningesaidia kununua vyakula na kupika. Hata wakati ilikuwa ngumu na ya kuchosha kiasi bado ningekuwa radhi kabisa. Nikihofia kuwa ningekuwa na utajiri kiasi kuliko wengine, niliacha mtoto wangu wa kike nyuma mwezi mmoja baada ya kumzaa na kurudi mara moja kazini. Matokeo yake yakawa, binti yangu alipata maumivu ya utapiamlo na akawa tu ngozi na mifupa kwa sababu hangeweza kunywa maziwa ya matiti yangu. Hali yake iliimarika tu baada ya sindano 100 za lishe, ilhali nilikuwa nimechoka sana kiasi kwamba nilikuwa na maumivu ya mgongo kila siku. Ingawa ilikuwa ngumu na yenye kuchokesha, nilivumilia shida hizo na nilijitolea kwa bidii kwa ajili ya kupata sifa nzuri. Katika miaka michache tu, nikawa mkwe maarufu katika kijiji, na familia yangu ikawa tajiri na kuonewa kijicho na watu walio karibu nasi. Matokeo yake yakawa, wakwe zangu, majirani, jamaa na marafiki wote walinisifu sana. Katika kukabiliwa na sifa na taadhimu kutoka kwa wale walio karibu nami, kiburi changu kilitoshelezwa sana. Nilihisi shida zangu wakati wa kipindi cha miaka michache iliyopita hazikuwa za bure, na nilikuwa nimefurahishwa sana kindani. Hata hivyo, maisha yangu ya utulivu yalikatishwa baada ya shemeji wangu kuolewa. Mke wake alinena nami kwa kejeli daima, akisema kuwa nilikuwa na nia fiche kwa kumtendea mama mkwe wetu vyema kwa sababu nilikuwa nataka tu mali yake. Yeye alikuwa akisema kila mara kuwa mama mkwe wetu alikuwa na upendeleo kwani alitupa sisi vitu vingi zaidi kuliko alivyowapa wao, na mara nyingi tulikuwa tukigombana kwa sababu ya haya. Nilihisi kuudhika mno na nilitaka kubishana naye hadharani ili kulalamika kutokuwa na hatia kwangu, lakini ingeweza kuharibu picha nzuri niliyokuwa nimejenga ndani ya mioyo ya watu. Kwa hivyo, ningejizuia kwa lazima, na wakati singeweza kuvumilia tena ningekuwa na kilio kikubwa kwa faragha. Baadaye, wifi huyo alisukuma bahati yake kwa kumiliki ardhi iliyosambazwa kwa upande wangu wa familia, iliyonifanya nitingike kwa hasira na nisikule au kunywa kwa masiku. Nilitaka hata pia kupambana naye hadi suluhu ipatikane. Hata hivyo, nikifikiria kwamba ingeweza kunifanya kupoteza heshima, kuharibu sifa yangu, na kufanya wale walio karibu nami kunidharau, nilimeza hayo yote, lakini ndani nilihisi nimekazwa mno kiasi kwamba nilikuwa na maumivu. Nilionekana mwenye majonzi na nilitanafusi siku nzima, nikihisi kama ilikuwa chungu sana na ya kuchosha kuishi na kutojua wakati kungekuwa na mwisho kwa maisha kama hayo.
Mwisho wa binadamu kweli ndio mwanzo wa Mungu. Pindi wakati nilikuwa na maumivu na kuhisi mnyonge, Mwenyezi Mungu alinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu. Siku moja, jirani yangu aliniuliza: “Unaamini katika uwepo wa Mungu?” Nilijibu: “Nani asiye? Ninaamini Mungu yupo.” Kisha akasema kwamba Mungu anayeamini ndiye Mungu pekee na wa kweli aliyeumba ulimwengu na vitu vyote, na kwamba mwanzoni, binadamu waliishi katika baraka za Mungu kwa sababu walimwabudu Mungu, lakini baada ya wao kupotoshwa na Shetani, hawaabudu tena Mungu na ndivyo basi wanaishi chini ya laana na maumivu kwa Mungu. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho alikuja kuwapa watu ukweli na kuwaokoa kutoka kwenye lindi kuu la taabu. Kwa kuongezea, pia aliwasiliana uzoefu wake mwenyewe wa kumwamini Mungu. Baada ya kusikiza mawasiliano yake, nilihisi kuwa nimepata msiri wangu wa karibu sana, na singeweza kujizuia kuelezea maumivu yote moyoni mwangu. Baadaye, alinisomea kifungu cha neno la Mungu: “Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu yako itarejea: ukiwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani ulipopotea kwa wakati mmoja, ukianguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na baba. Unatambua zaidi kuwa mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalitiririka ndani ya moyo wangu kama mkondo wenye joto, yakituliza moyo wangu wenye uchungu na huzuni, na singeweza kuzuia machozi yangu kumwagika. Wakati huo huo, nilihisi kama mtoto aliye na mateso aliyepotea na aliyerudi kwa ghafla katika kumbatio la mama yake. Kulikuwa na msisimko usioweza kusemeka na mhemuko katika moyo wangu. Niliendelea kumshukuru Mungu, kwa sababu alinichukua katika nyumba Yake na kunijalia wakati sikuwa na pengine pa kwenda. Nitafuata Mungu kwa moyo na roho yangu! Tangu wakati huo, nilisoma maneno ya Mungu, nikamwomba Mungu, na niliimba nyimbo za kumsifu Mungu kila siku, mambo yalilonifanya kutulia hasa katika moyo wangu. Kwa kuhudhuria mikutano, niliona kuwa ndugu walikuwa kama familia kubwa, ingawa wao hawana uhusiano wa damu. Uingiliano wao ulikuwa wa kawaida na wazi, ulikuwa umejaa uelewa, ustahamilivu, na uvumilivu, na haukuwa na wivu, mgongano na kupanga njama au kisingizio na unafiki. Hawakuwadhulumu maskini ilhali wakipenda matajiri, na wote waliweza kutendea kila mtu na unyofu na usawa. Moyo wangu ungehisi huru hasa wakati tuliimba nyimbo za kumsifu Mungu pamoja. Kwa sababu hiyo nilipendezwa na maisha haya ya kanisa yenye upendo na ukunjufu, ya haki na yenye furaha. Nilisadiki kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu pekee wa kweli na nilifanya uamuzi wangu kuwa ningemfuata hadi mwisho.
Kupitia kusoma maneno ya Mungu, nilielewa hamu ya haraka ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu kwa kiwango kikubwa kiwezekanavyo, na kuona kwamba ndugu wengi walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kujitoa na kujitumia kwa ajili ya kueneza injili ya ufalme. Hivyo basi pia nikajihusisha kikamilifu katika kuhubiri injili. Ili kunitakasa na kunibadili mimi, Mungu alilenga asili yangu mbovu na alitekeleza adabu na hukumu Yake juu yangu mara kwa mara. Wakati mmoja, nilikwenda kuhubiri injili kwa aliyeweza kuwa mwaminifu. Ilikuwa msimu wa kilimo wenye shughuli nyingi wakati huo. Baada ya kuona jinsi alivyokuwa na shughuli nyingi za kilimo, nilienda kufanya kazi pamoja naye huku nikimpa ushuhuda wa kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Nani angejua ya kwamba baada ya kuzungumza naye kwa siku tatu mtawalia angekuwa hana nia ya kuukubali tu na badala yake angenikaripia: “Wewe huna haya hata! Mimi tayari nilisema siyaamini haya, na bado huachi kuhubiri.” Maneno yake yaliniumiza sana. Uso wangu ulichomeka ni kama nilikuwa nimechapwa makofi mara kadhaa hadharani, wakati moyo wangu uliuma na wimbi baada ya wimbi la maumivu hafifu yasiyo makali. Nilifikiria: Nilikuja kukuhubiria kwa nia njema na nilijichokesha nilipokusaidia na kazi yako hadi mgongo wangu ulipata maumivu, na bado badala ya kukubali hayo, ulinitendea hivi. Wewe ni katili kweli! Nilihisi nimeaibishwa mno na sikutaka kuzungumza naye tena, lakini pia nilihisi kuwa hii haikuwa inaambatana na nia za Mungu, kwa hivyo niliomba kwa ukimya moyoni mwangu na nilizuia maumivu yangu ya kindani ili kuendelea kuongea naye nilipokuwa nikimsaidia na kazi yake. Hata hivyo, haidhuru kwa bidii gani niliwasiliana sikuweza bado kumfikia. Niliporomoka kama mpira uliotolewa upepo niliporudi nyumbani. Maneno ya mlengwa wa mahubiri yangu yaliendelea kujitokeza kichwani mwangu. Nilivyofikiria zaidi kuhusu hayo ndivyo nilivyoteseka zaidi: Mbona ninajisumbua? Yote niliyoyapata kama malipo ya nia yangu njema yalikuwaa kuzomewa, kukashifiwa, na kunyanyaswa. Kwa kweli hii sio haki kabisa! Hakuna mtu aliyewahi kunitenda namna hii. Kueneza injili ni uchungu na ngumu kabisa! Hapana, siwezi kwenda nje kuhubiri injili tena! Ikiwa nitaendelea kuhubiri sitabaki na heshima yoyote ya kuona mtu yeyote. Wakati tu nilipohisi nimekosewa sana na mwenye maumivu kiasi kwamba sikuwa na hiari tena ya kuhubiri injili, maneno ya Mungu yalinipatia nuru: “Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? … Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, ‘Njia iko wapi?’ Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia , ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe?” (“Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Mistari katikati ya maneno ya Mungu yote yalifichua hangaiko Lake na huzuni Yake yenye masikitiko na ya kuwajali watu wasio na hatia. Mungu hawezi kuvumilia kuona watu walioumbwa kwa mikono Yake mwenyewe wakidanganyika na kuumizwa na Shetani. Mungu anaendelea kusubiri kwa hamu sana kwa wanadamu kurudi katika nyumba Yake hivi karibuni ili wapokee wokovu mkubwa amewafadhili. Ilhali wakati nilipopatwa na maneno machache makali kutoka kwa mlengwa wangu wa mahubiri, nilihisi nimekosewa na kuteswa na nililalamika kuhusu shida na mateso hayo. Nilikuwa hata tena sina radhi ya kushirikiana kwa sababu nilikuwa nimefedheheka. Dhamiri na mantiki yangu ilikuwa wapi? Ili kutuokoa sisi watu potovu katika siku za mwisho, Mungu ameendelea kuwindwa na kuteswa na serikali kwa kila mara, kutelekezwa, kushutumiwa, kukufuriwa na kukashifiwa na jamii ya dini, na kuelewa visivyo na kupingwa na sisi wafuasi wa Mungu. Yale machungu na aibu Mungu amepitia ni mengi sana, ni mengi kabisa! Hata hivyo, Mungu hakuachana na wokovu Wake wa wanadamu, na aliendelea kutoa mahitaji ya wanadamu katika utulivu. Upendo wa Mungu ni mkubwa sana! Nafsi yake ni nzuri sana na yenye ukarimu! Taabu zangu leo haziwezi kulinganishwa na mateso ambayo Mungu amepitia kwa ajili ya kuokoa mwanadamu! Nilikumbuka kuwa mimi nilikuwa pia mwathiriwa, mtu yule aliyekuwa amedhuruiwa na Shetani kwa miaka. Kama Mungu hangekuwa amenyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu, ningekuwa bado ninang’ang’ana kwa uchungu katika giza, nisiweze kupata mwanga na matumaini ya kuishi. Kwa kufurahia wokovu wa Mungu, ninapaswa kuubeba aibu na maumivu ili kufanya lote liwezekanalo kushirikiana na Mungu, kutekeleza wajibu wangu vizuri, na kuleta watu wale wasio na hatia na bado wanadhuruiwa na Shetani mbele za Mungu. Hii ni ya thamani na ya maana zaidi kuliko kazi yoyote duniani, na ni ya kufaa haijalishi ni mateso ngapi yanapaswa kuvumiliwa! Nilipofikiria juu ya haya, sikuhisi tena kwamba kuhubiri kwa injili ni kitu chenye uchungu, na badala yake nilihisi mwenye bahati kuwa na uwezo wa kuratibu na injili ya ufalme. Huu ulikuwa heshima yangu na pia kuinuliwa na Mungu. Nilifanya uamuzi wangu: Bila kujali aina gani ya shida nitakayopatana nayo katika kazi yangu ya injili, nitajitolea yangu yote na kumtegemea Mungu kuwaleta watu zaidi na zaidi wenye shauku ya Mungu mbele Yake ili kufariji moyo Wake! Baadaye, nilijirusha mwenyewe tena katika kazi ya injili tena.
Kufuatia kipindi cha mafunzo, kila nilipokutana na mlengwa wa mahubiri ambaye alikuwa na mtazamo mbaya au aliyeninenea maneno makali wakati wa kutekeleza wajibu wangu, ningekuwa na uwezo wa kukabiliana na hilo kwa njia sahihi na kuendelea kushirikiana na moyo wa upendo. Kwa sababu ya haya, nilihisi nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninajali tena kuhusu heshima na hadhi. Lakini wakati Mungu aliweka mazingira mengine ya kunijaribu kulingana na kile nilichohitaji katika maisha, nilifichuliwa kabisa tena. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinijulia hali hivi karibuni na pia alizungumzia nia za Mungu za wakati uliopo na njia ya utendaji. Wakati niligundua wakati wa mazungumzo kuwa alikuwa anahamishwa katika kanisa lingine ili kutimiza wajibu wake, singeweza kujisaidia kuhisi wimbi la msisimko: Kuna uwezekano kuwa nitafanywa kuwa kiongozi wa kanisa baada ya yeye kuondoka. Ikiwa ndivyo, ni lazima kabisa nishirikiane vizuri! Wakati tu nilipokuwa ninahisi furaha kisiri, dada huyo alisema kuwa dada mwingine katika kijiji changu angetutembelea kesho. Nilikuwa na wasiwasi mara tu niliposikia hayo: Anakujia nini? Yeye ndiye atafanywa kuwa kiongozi mpya wa kanisa? Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi: Hajakuwa akimwamini Mungu kwa muda mrefu kama vile nimefanya, na pia anakuja kutoka kijiji hicho kama mimi. Ikiwa yeye atafanywa kiongozi, basi heshima yangu itakuwa aje? Ndugu wataniona namna gani? Kwa hakika watasema kuwa mimi huwa sifuatilii ukweli kwa kiwango chake. Sikuweza kuacha kufikiria juu ya hayo. Niligaagaa na kugeuka kitandani usiku, nisiweze kulala. Wakati wa mkutano siku iliyofuata, nilitia makini mara kwa mara sauti na mtazamo wa kile kiongozi alikuwa akisema kwa sababu nilitaka kujua kwa hamu ni nani angechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa kanisa. Kila wakati kiongozi huyo aliniangalia alipozungumza, nilihisi tumaini la kufanywa kuwa kiongozi. Sura yangu ingejawa na furaha na ningekubali kwa kichwa na kukubaliana na chochote alichosema. Kwa upande huo mwingine, wakati wowote kiongozi huyo alitazama dada huyo mwingine alipokuwa akizungumza, ningekuwa na uhakika kuwa dada huyo angetajwa kama kiongozi, na ningehisi huzuni na kuwa na masumbuko makali kwa sababu ya hilo. Wakati wa siku hizo chache, nilikuwa nimeteseka kwa ajili ya heshima na hadhi sana hadi nikawa na wasiwasi na kuchanganyikiwa. Nilipoteza hamu yangu ya kula na hata nikahisi kama muda ulikuwa unapita hasa polepole, ni kama ulikuwa umeganda. Kiongozi wa kanisa aliweza kuona hali niliyokuwa katika, kwa hivyo alipata kifungu cha neno la Mungu niweze kusoma: “Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu.” “Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza…. Kadiri unavyotafuta zaidi kwa njia hii ndivyo utavyovuna kidogo zaidi. Kadiri ilivyo kubwa zaidi tamaa ya mtu ya hadhi, ndivyo itabidi washughulikiwe kwa uzito zaidi na ndivyo zaidi lazima wapitie usafishaji mkubwa. Mtu wa aina hiyo hana thamani kabisa! Lazima ashughulikiwe na ahukumiwe vya kutosha ili aache hilo kabisa. Mkifuatilia kwa njia hii mpaka mwisho, hamtavuna chochote. Wale ambao hawafuatilii maisha hawawezi kubadilishwa; wale ambao hawana kiu ya ukweli hawawezi kupata ukweli. Hulengi kufuatilia mabadiliko ya kibinafsi na kuingia ndani; daima wewe hulenga tamaa zile badhirifu na vitu vinavyozuia upendo wako kwa Mungu na kukuzuia kufika karibu na Yeye. Je, vitu hivyo vinaweza kukubadili? Je, vinaweza kukuleta katika ufalme?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[a]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila mstari wa maneno ya Mungu uligonga moyo mwangu, ukinifanya nihisi kuwa Mungu alikuwa kando yangu, akifuatia kila neno na mwenendo wangu. Singeweza kujizia ila kujitafakari kwa mawazo na utendaji wangu siku hizi mbili zilizopita. Niligundua kuwa mtazamo wangu wa ufuatiliaji ulikuwa mbovu sana na uliathiriwa na misemo kama “Kama vile mti unavyoishi kwa sababu ya gome lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma mahali popote anapoishi, kama vile bata bukini hunena kilio chake popote anapoburuka.” Siku zote nilitaka hadhi ili nipate kushinda sifa zaidi kutoka kwa wengine, kilichosababisha mimi kuteseka kwa ajili ya heshima na hadhi kiasi kwamba nilikuwa na wasiwasi na kuchanganyikiwa, nilipoteza hamu yangu ya kula na singeweza kulala, na nilijifanya kuonekana mpumbavu. Hali kama hiyo ilitengenezwa na Mungu kulingana na hali yangu. Ilikuwa upendo wa Mungu ukiniangukia. Kazi ya Mungu leo ilikuwa ya kuniokoa, kunisaidia kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani ili nipate kupata wokovu. Njia niliyokuwa nikifuatilia ilikinzana na mapenzi ya Mungu. Singekuwa na uwezo wa kupokea idhini ya Mungu hata kama ningemwamini hadi mwisho. Ningeachwa bila chochote! Kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa ukimya: “Ewe Mungu! Niko radhi kutii kazi Yako, kutembea katika njia sahihi ya kuamini Mungu kwa mujibu wa mahitaji Yako, na kutia juhudi kwa neno Lako ili kufikia kuelewa ukweli na kuachana na tabia yangu mbovu. Bila kujali kama nimefanywa kiongozi, nitafuatilia ukweli na kutia makini kwa kubadili mambo yangu ambayo hayakidhi malengo Yako.” Baada ya kuelewa makusudi ya Mungu, nilihisi hasa utulivu moyoni mwangu na nilifurahia kuwasiliana bila kujali maudhui yalikuwa gani. Baada ya mkutano, kiongozi wa kanisa alisema kuwa, kulingana na mapendekezo ya wengi wa ndugu, dada huyo angekuwa kiongozi mpya wa kanisa, na kuwa ningeweza kuratibu na kazi yake. Nilikuwa na utulivu sana ndani na kukubali bila kusita, kukubali kufanya kazi kwa upatanifu na dada huyo ili kutimiza wajibu wetu.
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu wakati huu, nilipata ujuzi fulani juu ya mwelekeo wangu wa kuzingatia heshima na hadhi, na nilikuwa radhi kuachana na mwili wangu na kumwamini Mungu na kutekeleza wajibu wangu kulingana na mahitaji Yake. Hata hivyo, uchafu wangu uliotokana na sumu za Shetani zilikuwa zimezama sana. Kina cha nafsi yangu bado kilikuwa kinatawaliwa na ushawishi wa Shetani. Ili kuniokoa vyema kutoka kwa madhara ya Shetani, Mungu aliinyoosha mikono Yake ya wokovu kwangu tena. Siku moja, niliambiwa kuwa kulikuwa na dada katika kanisa ambaye hakuwa katika hali nzuri, kwa hiyo nilishauriana na dada niliyeshirikishwa naye kuhusu jinsi ya kutatua shida hii. Kwa sababu dada niliyeshiriki naye hakuhisi vizuri, nilikwenda peke yangu kutatua tatizo hilo baada ya majadiliano yetu. Nilimtafuta dada huyo usiku uo huo ili kuwasiliana naye, na tatizo hilo lilitatuliwa haraka sana. Moyo wangu ulibubujikwa kwa furaha wakati huo, nikifikiri kuwa kiongozi wa ngazi ya juu angenisifu kwa hakika kwa sababu nilikuwa nimetia jitihada nyingi sana. Hata hivyo, wakati tu nilipokuwa nikisubiria habari njema, kiongozi wa ngazi ya juu aliandika barua akitaka kuelewa hali ya dada huyo. Nilifikiria ilikuwa ni kunisifu, kwa hiyo niliifungua kwa furaha na kuisoma. Lakini nilipoona kuwa kile kilichokuwa ndani ya barua kilikuwa hasa cha kuuliza dada mwenzi vile alivyoshughulikia tatizo hilo, mara moja nikawa mwenye uchungu: Kwa uwazi ni mimi niliyeshughulikia suala hilo. Mbona usiniandikie kuniuliza juu ya hilo? Inaonekana mimi sina nafasi katika moyo wa kiongozi na ninadharauliwa. Mimi ni msichana wa kibaraka tu. Haijalishi jinsi ninavyofanya vyema sipati sifa njema yoyote kwa sababu hakuna mtu anayelizingatia kwa makini. Nilivyofikiria zaidi juu ya hilo, ndivyo nilihisi zaidi nilikuwa nimekosewa na kuhuzunika. Nilihisi nimefedheheshwa. Wakati huu, dada yangu mwenzi alikuwa na barua mkononi mwake na alikuwa karibu kuzungumza nami. Singeweza kuzuia hisia zilizokuwa ndani yangu na nikampigia kelele: “Kiongozi wa ngazi ya juu hajui jinsi suala hili lilivyotatuliwa. Hujaelewa haya? Nililifanya kazi kwa bidii kwa muda mrefu lakini hakuna hata mmoja aliyesema neno jema kulihusu, na hatimaye wewe bado ulipata sifa zote. Mbele ya kila mtu, mimi ni mtu tu wa kutumwa na kusaidia. Haijalishi ninaliwekea jitihada gani, hakuna mtu atakayelifurahia.” Baada ya kusema haya, nilihisi mwenye kudhulumiwa sana hadi nikaangua kilio. Wakati huo, maneno ya Mungu yalirudiarudia katika masikio yangu: “Kama ulitumia juhudi nyingi lakini bado Sikuchangamkii, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika uvunguvungu? Ikiwa, baada ya wewe kutumia vitu fulani kwa ajili Yangu, Sijatimiza mahitaji yako madogomadogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi au hata kuwa na ghadhabu na kunitusi?” (“Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya kushutumu ya Mungu yalinituliza polepole, na mawazo yangu yalifumbuka sana pia. Tukio ambalo lilikuwa limetoka kutokea liliendelea kucheza tena katika mawazo yangu kama sinema. Ufunuo wa Mungu ulinifanya kuona kwamba asili yangu ni ya kutisha na ya hatari sana, na kwamba imani yangu kwa Mungu na kutekeleza kwa wajibu wangu haukuwa wa kuridhisha Mungu au kupokea idhini Yake, mbali kupokea sifa na taadhimu kutoka kwa watu wengine. Mara tu matamanio yangu hayakuwa yakitoshelezwa, ningekuwa mwenye kujaa chuki; asili yangu ya unyama ungejitokeza, na kumsaliti Mungu ikawa jambo rahisi sana kufanya hata zaidi. Wakati huu, niliona kuwa nimevuka mipaka sana na kwamba nilikuwa mkatili. Maumivu niliyoyahisi yalikuwa ya kuhuzunisha sana. Nilipotubu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu, nilifikiri nilikuwa nimebadilika na sikuwa ninaishi tena kwa sababu ya heshima na hadhi, na pia ningeweza kushirikiana na dada huyo. Lakini katika ufunuo Wako leo, kwa mara nyingine tena nimeweza kufunua ubaya wangu wa kishetani, daima nikihisi kuwa sikuwa na hadhi kati ya watu na kuteseka kwa sababu jitihada zangu hazikusifiwa na wengine. Ee Mungu, Shetani kweli alikuwa amenidhuru sana. Hadhi, sifa, na majivuno yote yakawa pingu zangu. Ninaomba kuwa Unaweza kuniongoza kutoka kwa ushawishi wa Shetani tena.” Baadaye, niliona kati ya maneno ya Mungu yafuatayo: “Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote kutafuta mahali salama, mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani?” (“Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila neno la hukumu ya Mungu lilinidunga kwa uchungu ndani ya moyo wangu kama upanga mkali, likichangamsha roho yangu na kunifanya kutambua kwamba nilitekeleza wajibu wangu sio ili kumtukuza Mungu na kumshuhudia, lakini kwa sababu daima nilitaka kujionyesha, kujishuhudia mwenyewe, na nilikuwa na ndoto ya kuwa bora kuliko watu ili waweze kunienzi na kuniheshimu. Kulikuwa na uchaji wowote wa Mungu ndani ya moyo wangu? Nilichofuatilia hakikuwa sawa na kile cha malaika mkuu aliyemsaliti Mungu? Mimi ni kiumbe kilichoumbwa kilichopotoshwa kabisa na Shetani. Mbele ya Mungu, mimi ni kama uchafu, funza. Ninatakiwa kuwa ninamwabudu Mungu na kutimiza wajibu wangu nikiwa na uchaji moyoni mwangu wakati wote, lakini sikushughulika na kazi ya uaminifu, na nilitaka daima kutumia kutekeleza wajibu wangu kama fursa ya kujionyesha na kujishuhudia mwenyewe. Mungu angewezaje kutochukia na kusinywa na haya? Mungu ni mtakatifu sana na mkuu, amejaa mamlaka na uongozi, na bado anabaki kuwa mnyenyekevu na kujisetiri, hafichui utambulisho Wake kamwe ili kuwafanya watu kumtazamia na kumstahi. Badala yake, Anaendelea kwa ukimya kujitolea Kwake kote ili kuwaokoa wanadamu, kamwe hajitetei Mwenyewe au kudai sifa njema, na kamwe hadai chochote kutoka kwa wanadamu. Unyenyekevu, uadilifu, na kutokuwa na ubinafsi kwa Mungu kulinifanya nione kiburi, kuwa duni, na ubinafsi wangu, sikuwa na budi ila kuhisi aibu, kana kwamba sikuwa na mahali pa kujificha, na nilihisi kwamba nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na nilihitaji sana wokovu wa hukumu, adabu, jaribio na usafishaji wa Mungu. Kwa hivyo nilianguka tena mbele ya Mungu: “Ewe, Mwenyezi Mungu! Kupitia uadibu na hukumu Yako ninaweza kuona uasi wangu , pamoja na uadilifu Wako na ukuu. Kuanzia sasa kuendelea, wakati ninapotekeleza wajibu wangu ninatumaini tu kutenda kama mwanadamu wa adabu aliye na moyo unaokuogopa Wewe, na kutupa tabia yangu ya kishetani kwa kutegemea maneno Yako.”
Baada ya kupitia adabu na hukumu ya Mungu mara kwa mara tena, maoni yangu juu ya ufuatiliaji yamebadilika hatua kwa hatua, lakini tabia ya maisha yangu haikuwa bado imepata mabadiliko kweli. Ili kunitakasa kabisa zaidi na kunisababisha kutembea kwenye njia ya sahihi ya uzima, Mungu mara nyingine tena alinipa wokovu Wake. Baadaye, nilichaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa, nikishirikiana na dada mwingine kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na kushindwa kwangu kwa awali, niliendelea kujikumbusha kila wakati kwamba nilihitaji kukubaliana na dada huyo ili kufanya kazi ya kanisa vizuri. Mwanzoni, ningekuwa nikijadili kila kitu na dada huyo na kufuatilia mwongozo wa Mungu pamoja, kwa hivyo tulifanikisha matokeo katika vipengele vyote vya kazi. Lakini baada ya muda fulani, niligundua kuwa dada huyo alikuwa na tabia nzuri za asili, mawasiliano yake ya ukweli yalikuwa wazi na ya kuangaza, na uwezo wake wa kikazi ulikuwa sawa kuliko wangu. Wakati wa mikutano, ndugu walikuwa wote radhi kusikiliza mawasiliano yake na wote walitafuta ushauri wake walipopatwa na shida. Nilipokabiliwa na mazingira kama hayo, nilikuwa tena nimetegwa katika mtego wa Shetani na kupumbazwa nayo: Dada huyo ni bora zaidi kuliko mimi kwa kila namna na anapendwa na ndugu bila kujali mahali anaenda. Hapana! Ni lazima nimpite kwa vyovyote vile, na niache ndugu waone kwamba mimi niko chini yake. Kwa sababu hii, nilijishughulisha kanisani kila siku mtawalia, nikipanga mikutano ya ndugu na haijalishi ni nani aliyepata matatizo ningekimbia kwao kuwasaidia kutatua suala hilo. … Inawezekana kuwa nilionekana kuwa mwaminifu na mtiifu kutoka nje, lakini malengo yangu ya ndani ingewezaje kuepuka macho ya Mungu? Uasi wangu ulifufua hasira ya Mungu, na kama matokeo nilianguka katika giza. Sikupata nuru niliposoma maneno ya Mungu, sikuwa na cha kusema wakati wa kuomba, niliwasiliana bila kusisimua wakati wa mikutano, na hata niliogopa mikutano na ndugu zangu. Nilikuwa nimefungwa kabisa na heshima na hadhi. Nilipitia kila siku bila kidokezo, ni kama nilikuwa nimebeba mzigo mkubwa mgongoni mwangu na singeweza kupumua kutokana na kubanwa. Singeweza pia kubaini tena baadhi ya masuala ya kanisa, na utendaji bora wangu wa kazi yangu ukashuka kwa kasi. Nilipokabiliwa na ufunuo kama huo kutoka kwa Mungu, sikujaribu kujijua na pia sikuwa radhi kuzungumza kwa nyofu kwa ndugu kuhusu hali yangu na kutafuta ukweli ili kuutatua, kwa hofu kuwa wangenidharau. Baadaye, kuadibu na nidhamu ya Mungu ikaniangukia. Tumbo yangu ilianza kwa ghafla kuniuma sana hadi singeweza kukaa au kusimama kwa amani. Mateso ya magonjwa na kutoridhika kutokana na kutopata hadhi kuliniacha nikizungukazunguka katikati ya maisha na kifo. Kutokana na kukataa kwangu kuyakubali matatizo yangu na kushindwa kwangu kushirikiana kwa kazi ya kanisa, kanisa halikuwa na budi ila kunibadilisha na kunituma nyumbani ili ibada ya kiroho na kujitafakari. Baada ya kupoteza hadhi yangu, nilihisi kama nilikuwa nimehukumiwa jehanamu. Kihisia, nilizama hadi katika kiwango changu cha chini kabisa na kuhisi kuwa nilikuwa nimeaibika kabisa. Niliteseka hata zaidi ndani hasa wakati nilipowaona ndugu wote wakitekeleza kikamilifu wajibu wao, wakati nilikuwa nimepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na sikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wowote. Kwa uchungu, sikuweza kujisaidia ila kujiuliza: Mbona kuna wengine wanaamini Mungu na wanaelewa ukweli zaidi na zaidi, ilhali ninaendelea kumuasi na kumpinga Mungu mara kwa mara tena kwa sababu ya heshima na hadhi? Nilimsihi Mungu mara nyingi anielekeze nipate chanzo cha kufeli kwangu. Siku moja, niliona yafuatayo kati ya maneno ya Mungu: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia hiziana asili ya aina gani? Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuongezea, inasema katika “Mahubiri na Ushirika kuhusu Kuingia Katika Maisha”: “Kiini na asili ya Shetani ni usaliti. alimsaliti Mungu tangu mwanzo kabisa, na baada ya kumsaliti Mungu alidanganya, akapotosha, akachezea, na akatawala wanadamu duniani walioumbwa na Mungu, akijaribu kuwa sawa na Mungu kama na kuanzisha ufalme tofauti. … Unaona, asili ya Shetani sio ile inayosaliti Mungu? Kutoka kwa yote ambayo Shetani amefanyia wanadamu, tunaweza kuona wazi kwamba Shetani ni kwa kweli pepo mbaya anayepinga Mungu na kwamba asili ya Shetani ni ile inayomsaliti Mungu. Haya yote ni kamili” (“Jinsi ya Kupata Ujuzi wa Asili Yako Potovu” katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha I). Nikizingatia haya maneno, singeweza kujizuia kutetemeka na hofu. Niliona kwamba yale niliyoyaishi kwa kudhihirisha yalikuwa kwa sura ya Shetani kabisa, na nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno, na asiyemwabudu Mungu hata kidogo. Mungu aliniinua ili nitekeleze wajibu wangu kanisani, ili nipate kuwaleta ndugu mbele za Mungu nikiwa na uchaji Kwake moyoni mwangu, na kuwafanya watu wawe na nafasi ya Mungu katika mioyo yao, na pia kuwa na uchaji na kumtii Mungu. Lakini nilipokabiliwa na kuinuliwa na Mungu, sikutia maanani nia ya Mungu katika kutekeleza wajibu wangu, na sikuhisi mzigo kuwasaidia ndugu kuingia katika maisha. Badala yake, nilitaka kila mara kuwafanya watu waniangalie kwa makini na kunisikiliza, na kwa ajili ya matamanio yangu, nilijaribu kila mara kujiinua bila kujalisha popote nilipoenda. Nilikuwa hata mwenye wivu kwa waliokuwa wazuri na mwenye husuda kwa wakakamavu, na nilishindana kwa ukaidi na wengine kwa ajili ya ukuu. Kutoka nje, nilikuwa ninashindana na wanadamu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipigana dhidi ya Mungu. Hili ni jambo ambalo huudhi sana tabia ya Mungu. Alinihukumu na kuniadibu, kunirudia na kunifundisha nidhamu, na kuninyang’anya hadhi ili kunifanya nijitafakari na kutubu. Niliona kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa ya kina sana na makubwa sana! Singeweza kujizuia kuhisi majuto na kujilaumu ndani, na hata zaidi nilichukia ya kwamba upotovu wangu ulikuwa wa kina sana. Nilifuata Mungu lakini sikufuatilia ukweli, na badala yake nilifanya kazi kwa bidii bila kufikiri tu kwa sababu ya hadhi na heshima. Nilikuwa nimeshindwa kabisa kuishi kulingana na mapenzi na wokovu wa Mungu. Kadri nilivyojichungua, ndivyo nilivyoona wazi zaidi kuwa misemo niliyoishi kulingana nayo, kama vile “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha jina lake nyuma popote akaapo, kama vile bata bukini hutetea popote arukapo,” yalikuwa uongo yaliyotumiwa na Shetani ili kuwapotosha na kuwadhuru wanadamu. Nilitambua kwamba Shetani alitumia mambo haya kuduwaza nafsi za watu, kupotosha mawazo yao, na kuwafanya kukuza mitazamo mbaya kuhusu maisha, kuwafanya wajitahidi kwa vyovyote vile kufuatilia vitu bure kama vile hadhi, umaarufu, utajiri na heshima, na hatimaye kupotea kutoka kwa na kumsaliti Mungu, ili waweze wote kuzingatia uwongo wake na kuifanyia kazi na kuangamizwa na kudhuruiwa kwa hiari. Nilikuwa mmoja wa watu hao ambao walikuza mtazamo mbaya wa maisha kwa msingi wa udanganyifu wa Shetani, nikawa mwenye kiburi, majivuno, dharau, na asiyekuwa na mahali pa Mungu moyoni mwangu. Niliishi katika upotovu na kumtendea Mungu kama adui. Sasa, sipaswi tena kuenda kinyume na Mungu wakati ninafurahia rehema Yake. Nitajirekebisha kabisa, nitaacha Shetani kabisa, nitampa Mungu moyo wangu kabisa, na kuishi kwa kudhihirisha mtu wa kweli ili kufariji moyo wa Mungu. Baada ya hapo, nilitaka kujua jinsi ya kuendelea na njia yangu ya baadaye, na jinsi ya kufuatilia ukweli ili kukidhi mapenzi ya Mungu. Asante kwa Mungu kwa kuniongoza tena. Kisha niliona maneno ya Mungu: “Leo, hata kama wewe si mfanyikazi, unapaswa kuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kujiwasilisha kwa mipango yote ya Mungu. Unapaswa kuwa na uwezo wa kutii chochote Mungu anachosema, na upitie kila aina ya madhila na usafishaji, na ingawa wewe ni dhaifu, moyoni mwako unapaswa bado uwe na uwezo wa kumpenda Mungu. Wale ambao huchukua jukumu katika maisha yao wako tayari kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na mtazamo wa watu kama hawa kuhusu harakati ni ule sahihi. Hawa ndio watu ambao Mungu anahitaji. … Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kama kioleza, maneno ya Mungu yalinipa nuru moyoni mwangu, yakinionyesha njia ambayo ninapaswa kuchukua. Mungu anatarajia kuwa watu, bila kujali kama wana hadhi na wamefikwa na hali gani, wanaweza kufanya kila wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanaweza kutii upangaji na utaratibu wa Mungu na kutafuta kupenda na kumtosheleza Mungu. Hii ndiyo njia sahihi zaidi ya ufuatiliaji na pia ni njia ya ukweli ya uzima ambayo kiumbe kilichoumbwa kinapaswa kupitia. Hivyo basi niliamua mbele ya Mungu: Ee Mungu, asante kwa kunionyeshea njia ya ukweli ya uzima. Hadhi yangu ya awali ilikuwa kutokana na kuinuliwa na Wewe. Kutokuwa na hadhi leo pia ni kwa sababu ya haki Yako. Mimi ni kiumbe kidogo tu kilichoumbwa. Kuanzia sasa kuendelea, ninataka tu kufuatilia ukweli na kutii mipango Yako yote.
Baadaye, hali yangu ikarudi kawaida haraka kutokana na kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa. Kanisa tena lilinipangia kazi linalonifaa. Pia, nilizingatia kufuatilia ukweli katika kutekeleza wajibu wangu, wakati wowote kitu kilifanyika ningetafuta nia ya Mungu, ningejaribu kujijua mwenyewe, na kupata maneno yanayoambatana na ya Mungu ili kukitatua. Nilipokabiliwa na vitu vilivyohusisha heshima na hadhi, hata ingawa ningekuwa na mawazo fulani katika akili yangu, kwa kupitia maombi na neno la Mungu ningetafuta ukweli na kujitelekeza mwenyewe, na polepole niliweza kuwa na uwezo wa kutodhibitiwa na mambo haya na ningetekeleza wajibu wangu nikiwa na utulivu wa akili. Wakati niliona baadhi ya ndugu ambao hawakuwa wamemwamini Mungu kwa muda mrefu kama mimi wakiaminishwa na agizo, ningeweza, kwa kutafuta ukweli, kuelewa kwamba wajibu ambao unatekelezwa na mtu umejaaliwa na Mungu, na kwamba ninapaswa kutii mipango ya Mungu. Matokeo yake yakawa, niliweza kuwa na uwezo wa kuichukulia kwa njia sawa. Wakati ndugu walinishughulikia na kufichua asili yangu na kiini, ingawa nilihisi nimepoteza heshima, niliweza kuwa mtiifu kutumia sala. Hii ni kwa sababu upendo wa Mungu umeniangukia, na umefaidika sana katika kubadilisha tabia yangu ya maisha. Hapo awali, nilitia maanani katika heshima yangu sana kupindukia na sikuwa radhi kufichulia yeyote, kwa hofu kwamba wengine wangenidharau. Sasa, ninafanya mazoezi ya kuwa mtu mwaminifu kwa mujibu wa mahitaji ya Mungu, na kama nina shida yoyote nitafungua roho yangu kwa ndugu, jambo ambalo hunifanya kuhisi hasa nimefarijika na mwenye furaha katika kina cha roho yangu. Nikiyaona haya mabadiliko ndani yangu, singeweza kujisaidia ila kumshukuru na kumsifu Mungu, kwa maana mabadiliko haya yanaletwa kwangu na kazi ya adabu na hukumu ya Mungu ya siku za mwisho.
Nimemfuata Mwenyezi Mungu kwa miaka kadhaa sasa. Nikifikiria awali, ilikuwa ni sumu za Shetani ambazo zilikuwa zimemomonyoa nafsi yangu. Nilikuwa nimeishi chini ya miliki ya Shetani na niliangamizwa na kupumbazwa naye kwa miaka mingi. Sikujua thamani na maana ya maisha. Sikuweza kuona mwanga, wala sikuweza kupata furaha ya ukweli na shangwe. Nilizama katika dimbwi la simanzi na sikuweza kujinasua. Sasa, ni kupitia adhabu na hukumu ya mara kwa mara niliweza kuachana na madhara ya Shetani na kufikia faraja na uhuru. Nimepata tena dhamiri na mantiki yangu, na pia nina lengo sahihi la kufuatilia, kufuata Mungu katika njia ya ukweli na yenye kung’aa ya uzima. Kupitia adabu na hukumu ya Mungu, kwa kweli nilipitia upendo wa Mungu usio na ubinafsi na wa kweli, na kufurahia baraka na kupokea upendo ambao ulimwengu wa mwanadamu hauwezi kufurahia. Ni Mungu pekee anayeweza kumwokoa mwanadamu kutokana na bahari ya mateso ya Shetani, na ni kazi ya adabu na hukumu tu ya Mungu inayoweza kuwatakasa wanadamu kutokana na sumu za Shetani ndani yao na kuwafanya waishi kulingana na mfano wa mtu wa kweli na watembee katika njia ya ukweli ya uzima. Adabu na hukumu ya Mungu ni nuru. Ni rehema kubwa kabisa, ulinzi bora kabisa, na utajiri wenye thamani zaidi ya maisha ambayo Mungu amewapa watu. Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “… adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu!” (“Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Asante kwa adhabu na hukumu ya Mungu kwa kuniokoa na kuniruhusu kuzaliwa upya! Katika njia yangu ya baadaye ya kumwamini Mungu, nitajizatiti kufuatilia ukweli, kupokea zaidi adhabu na hukumu zaidi ya Mungu, na kutoa kabisa sumu za Shetani ili kupata utakaso, kupata ujuzi wa kweli wa Mungu, na kuwa mtu ambaye kwa kweli anampenda Mungu. Utukufu wote uwe kwa Mungu. Amina!
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Jumatatu, 10 Juni 2019
Mchakato wa Mbadiliko wa Muumini Mwenye Kiburi
Zhang Yitao, Mkoa wa Henan
“Mungu, kazi Yako ni ya vitendo sana, imejaa haki na utakatifu sana. Umekuwa ukifanya kazi kwa muda mrefu kwa subira, yote kwa ajili yetu. Katika siku za nyuma, nilimwamini Mungu lakini sikuwa na mwenendo wa binadamu. Nilikuasi na kuumiza moyo Wako bila kujua. Nimejaa aibu na majuto na ninapaswa kukushukuru Wewe. Ni sasa tu ninapotambua hili. ... Bila Hukumu Yako kali, singekuwa na leo, na nikikabiliwa na upendo Wako wa kweli nina shukrani na kuwiwa na Wewe. Ilikuwa ni kazi Yako ambayo iliniokoa na kusababisha tabia yangu kubadilika. Bila huzuni na uchungu, moyo wangu umejaa furaha” (“Ewe Mungu, Upendo Ambao Umenipa Ni Mkubwa Mno” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kila wakati ninapoimba wimbo huu, mimi hufikiria juu ya wokovu wa Mungu kwangu kupitia miaka hii yote, na nimejaa shukrani Kwake. Ilikuwa ni hukumu ya Mungu na kuadibu vilivyonibadilisha. Lilinifanya—kuwa mwana mwenye kiburi, kutaka makuu, mwasi—kuonekana kidogo zaidi kama mwanadamu. Kwa kweli ninatoa shukrani kwa ajili ya wokovu wa Mungu kwangu!
Nilizaliwa mashambani. Kwa sababu familia yangu ilikuwa maskini na wazazi wangu walikuwa waaminifu, mara nyingi walikuwa wakidanganywa. Kuanzia wakati nilipokuwa mdogo watu waliniangalia kwa dharau, na kupigwa na kudhulumiwa kulikuwa matukio ya kawaida. Hili mara nyingi lilinifanya kuhuzunika kiasi cha kutokwa na machozi. Niliweka kila kitu nilichokuwa nacho katika masomo yangu ili kwamba nisingelazimika kuishi maisha ya aina hiyo tena, ili wakati wa baadaye ningepata kazi kama afisa wa serikali, kuwa mtu mwenye madaraka, na kila mtu angeweza kunipa heshima kubwa. Lakini mara tu nilipomaliza shule ya kati na nilikuwa nikijiandaa kwa mtihani wa kuingia shule ya sekondari, Mapinduzi ya Kitamaduni yakaanza. Kundi la wanafunzi lenye hadhi ya kijeshi la Red Guards likaasi, wafanyakazi wakagoma, wanafunzi wakagoma. Kila siku ilihusika katika mapinduzi. Ilikuwa vurumai, watu walikuwa na hofu, na mfumo wa mtihani wa kuingia chuo ulipigwa marufuku. Kwa hivyo, nilipoteza fursa ya kutahiniwa kuingia shuleni. Nilihangaika—nilihisi vibaya kana kwamba nilikwisha kuwa mgonjwa kwa uzito kabisa. Baadaye, nilifikiria: Ingawa siwezi kutahiniwa kuingia shuleni au kuwa afisa wa serikali, nitafanya kazi kwa bidii ili kupata pesa. Almradi nina pesa, watu wataniheshimu sana. Kuanzia hapo kuendelea, nilikuwa natafuta njia za kutengeneza pesa kila mahali. Kwa kuwa familia yangu ilikuwa masikini, sikuwa na fedha zozote za kuanza kufanya biashara. Kupitia kwa jamaa na marafiki, niliweza kukopa Yuan 500 ili kuanzisha duka la kuuza nyama ya nguruwe iliyopikwa kwa mvuke. Wakati huo nyama iligharimu senti sabini tu kwa ratili moja, lakini baada ya kununua vifaa nilivyohitaji, kile kilichobaki kutoka kwa hiyo Yuan 500 hakikuwa cha kutosha hasa. Kila wakati nilipokuwa na mapato kiasi yalikwenda moja kwa moja kwa ufadhili wa biashara hiyo. Mara nilipokuwa nimepata pesa zozote ningelipa deni langu. Nilivumilia shida nyingi ili niweze kuishi maisha bora zaidi kuliko wengine. Kutoka asubuhi hadi mwishoni mwa siku, sikuwa na wakati wa ziada. Baada ya miaka kadhaa ya kazi ngumu, ujuzi wangu ukawa mzuri zaidi na zaidi, na biashara yangu ilikuwa inasitawi zaidi na zaidi. Familia yangu kwa haraka ikawa na mali zaidi, na watu wengi wananiangalia kwa wivu.
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 1990, kulikuwa na mtu fulani katika kijiji chetu ambaye alizungumza nami kuhusu kumwamini Yesu. Nilisikiliza mahubiri machache kwa kutaka kujua, na nikaona kwamba wakati ndugu huyu wa kiume aliyekuwa akihubiri alikuwa akizungumza, watu wengi walimheshimu. Nilikuwa na wivu usioaminika kuhusu tukio hilo la yeye kuzungukwa na kupendwa na umati. Nilifikiria mwenyewe: Kama ningeweza kuwa mtu kama huyo, sio tu kuwa kila mtu angenipenda mno, lakini ningeweza kupata neema ya Bwana na kupewa thawabu na Yeye. Hilo lingekuwa jambo la ajabu sana! Kutokana na mawazo haya, nilianza kumwamini Bwana Yesu Kristo, na nilijiunga na kanisa la nyumbani. Baada ya hilo, nilifanya kazi kwa bidii kujifunza Biblia, hasa kutafuta maarifa ya Biblia, nikizingatia kukariri vifungu fulani, na kwa haraka sana nilijua sura nyingi maarufu na aya kwa moyo. Niliisoma sura ya 16, aya ya 26 ya Injili ya Mathayo ambapo Bwana Yesu alisema: “Kwani mwanadamu atafaidika na nini, ikiwa ataupata ulimwengu mzima, na apoteze nafsi yake mwenyewe? au mwanadamu atabadilisha nafsi yake na nini?” Kisha nikasoma pia juu ya Bwana Yesu akimwita Petro, na mara moja alizitupa nyavu zake za uvuvi na kumfuata Kristo. Nikafikiria mwenyewe: Kuwa na pesa za kutosha ili kuishi ni vyema; nikichuma zaidi, itakuwa na faida gani nitakapokufa? Nikitaka kupata sifa za Bwana, ni lazima nifuate mfano wa Petro. Kwa hiyo nikaacha biashara yangu, na kuanza kujishughulisha kanisani muda wote. Nilikuwa na shauku sana wakati huo, na kwa kupitia kwa jamaa na marafiki zangu nilikuwa nimehubiri kwa watu 19 kwa muda mfupi, na kisha hiyo idadi ilipanuliwa hadi watu 230 kupitia hao 19. Kisha, nikasoma maneno ya Bwana Yesu: “Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni” (Mathayo 7:21). Nikajihisi mwenye kukinai hata zaidi. Kwa msingi wa kile nilichoelewa kutoka kwa maana halisi ya maneno Yake, niliamini kwamba nilikuwa tayari naifuata njia ya Bwana, kwamba nilikuwa kwa njia ya kuyafuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, na katika enzi yenye kufuata wakati ufalme wa Mungu umefanikishwa, ningetawala kama mfalme duniani. Chini ya utawala wa lengo la aina hii, shauku yangu ikawa hata zaidi. Niliweka azimio langu kwamba nilipaswa kufuata maneno ya Yesu kwa uthabiti ya “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” na “kuwa na uvumilivu na subira,” na vile vile kuongoza kwa mfano, na kutoogopa kustahimili shida. Wakati mwingine nilipoenda nyumbani kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike, ningewasaidia kubeba maji, kuwasha mioto, na kufanya kazi ya shamba. Walipokuwa wagonjwa ningeenda kuwatembelea. Walipokuwa hawana pesa za kutosha ningewasaidia kutoka kwa akiba yangu mwenyewe; ningemsaidia yeyote aliyekuwa anapitia shida. Kwa haraka nilipata sifa ya ndugu zangu wote wa kiume na wa kike na vilevile ya viongozi wa ngazi za juu katika kanisa. Mwaka mmoja baadaye nilipandishwa cheo kuwa kiongozi wa kanisa, kuyaongoza makanisa 30. Nilikuwa nimesimamia waumini takriban 400. Mara nilipokuwa nimepata cheo hiki, nilijihisi mashuhuri. Nilihisi kuwa kazi yangu yote ngumu na jitihada hatimaye zilikuwa zimezaa matunda, lakini wakati huo huo niliunda msimamo wa juu zaidi katika moyo wangu: kufuatilia cheo cha juu zaidi, kupata sifa na upendo wa watu hata wengi zaidi. Kupitia mwaka mwingine wa kazi ngumu, nikawa kiongozi wa ngazi ya juu wa kanisa, nikiongoza wafanyakazi wenzangu katika wilaya tano, nikiongoza makanisa 420. Baada ya hapo nilikuwa na woga zaidi wa kuzembea, kwa hiyo nilizingatia hasa tabia yangu nzuri kijuujuu, na kuanzisha taswira yangu miongoni mwa wafanyakazi wenzangu na ndugu wa kiume na wa kike. Kwa kibali cha wafanyakazi wenzangu na ili ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniheshimu, nilikataa chakula badhirifu katika kanisa, na nikapiga marufuku mawasiliano yote baina ya washiriki wa jinsia tofauti na matendo ya hatari. “Uadilifu wangu na hisia za haki” zilipata uungwaji mkono na kibali kutoka kwa wafanyakazi wenzangu na ndugu wengine wa kiume na wa kike. Asili yangu ya kiburi pia ilituna na kufika kiasi cha kutoweza kudhibitika. Juu ya hayo, nilijua vizuri baadhi ya vifungu vya kawaida zaidi vya Biblia, na wakati nilipokuwa nikikutana na kuhubiri kwa baadhi ya viongozi wa kanisa wa ngazi za chini na wafanyakazi wenzangu, ningeweza kuvitongoa vifungu bila kutazama Biblia yangu kwa msingi wa sura na nambari za mstari tu. Ndugu zangu wa kiume na wa kike kwa kweli walinipenda sana, kwa hiyo siku zote nilikuwa na kauli ya mwisho katika kanisa. Kila mtu alinisikiliza. Siku zote nilifikiri kwamba niliyoyasema yalikuwa sahihi, kwamba nilikuwa na ufahamu wa juu. Kama ulikuwa ni utawala wa kanisa, kuainisha makanisa, au kuwakuza viongozi wa kanisa na wafanyakazi wenzangu, sikujadiliana mambo na wengine. Nilichokisema daima kilikuwa na thamani; kwa kweli nilikuwa na utawala wa mfalme. Wakati huo hasa nilifurahia kusimama kwa mimbari, nikinena kwa umbuji na bila kukoma, na kila mtu alipokuwa akinitazama kwa upendezewaji, hiyo hisia ya kufurahi sana ilikuwa ya kunipendeza mno na ilinifanya kusahau kila kitu. Mimi hasa nilihisi hili wakati niliposoma sura ya 12, mistari ya 44 na 45 ya Injili ya Yohana: “Yesu akatoa sauti na kusema, Yeye anayeniamini, haniamini mimi, ila yeye aliyenituma. Na yeye anayeniona mimi anamwona yule aliyenituma.” Nilihisi hili pia niliposoma sura ya 3, mstari wa 34: “Kwani yeye ambaye Mungu amemtuma huyasema maneno ya Mungu: kwa kuwa Mungu hampi Roho kwa kipimo.” Kwa kweli nilifurahia hili, na kwa kujipujua niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu, kwamba Mungu alikuwa amenipa Roho Mtakatifu, na mapenzi ya Mungu yalionyeshwa kunipitia. Niliamini kwamba kwa sababu ningeweza kufafanua maandiko, ningeweza kuyaelewa “mafumbo” ambayo wengine hawakuweza kuyaelewa, kwamba ningeona vidokezo ambavyo wengine hawangeweza kuviona. Nilijali tu kuhusu kujitosa mwenyewe katika furaha iliyoletwa na cheo changu, na nilikuwa nimesahau kabisa kwamba nilikuwa kiumbe tu, kwamba nilikuwa tu chombo cha neema ya Bwana.
Kanisa lilipoendelea kukua, sifa yangu pia ilikua, na kila mahali nilikoenda nilifuatiliwa na polisi kwa kushiriki katika shughuli zisizoruhusiwa za kidini. Kutokana na mateso haya kutoka kwa serikali, sikuthubutu kurudi nyumbani. Ningeweza kujificha kwa muda, lakini sio milele, na wakati mmoja nilishikwa na polisi wakati niliporudi kuchukua nguo. Nilihukumiwa miaka mitatu ya ufundishwaji tena kwa njia ya kufanya kazi. Katika kipindi hicho cha miaka mitatu nilipitia kila aina ya mateso na maumivu makali ya ukatili. Siku hizo kwa kweli nilihisi zilikuwa kama miaka, na ilihisika kama safu ya ngozi ilikuwa imeambuliwa kutoka kwa kichwa hadi kwa vidole. Lakini baada ya kuachiliwa, bado niliendelea kuhubiri injili kwa ujasiri mkubwa, sawa tu na wakati wowote, na pia nilirudishiwa nafasi yangu ya kazi ya asili. Baada ya miezi sita mingine, niliwekwa kizuizini tena na serikali ya mitaa na kuhukumiwa miaka mitatu ya ufundishwaji tena kwa njia ya kufanya kazi. Baada ya kunitesa kwa kila njia iliyowezekana, waliniweka kwa kituo cha kizuizi kwa siku zingine 70. Baada ya hapo, niliwekwa katika kambi ya kazi ambapo nilikuwa nikibeba matofali. Wakati huo ulikuwa ni mwezi wa saba unaofuata kuandama kwa mwezi na hali ya hewa ilikuwa ya joto ya kumfanya mtu kujisikia vibaya. Halijoto katika tanuru lilikuwa takriban nyuzi 70 sentigredi na nililazimika kutengeneza matofali zaidi ya 10,000 kila siku. Njaa yangu ikichanganywa na mateso yaliyotangulia ya kikatili yalikuwa yameufanya mwili wangu kuwa dhaifu mno. Sikuweza kuvumilia aina hiyo ya kazi katika joto, lakini walinzi wenye dhuluma hawakujali kuhusu yoyote ya hayo. Wakati sikuweza kuzikamilisha kazi zangu, walinifunga pingu mikononi mwangu nyuma yangu, walinilazimisha kupiga magoti, na kuniweka chupa katika makwapa yangu na nyuma ya magoti yangu. Kisha wakanipiga na midukuo ya umeme mpaka pingu zikachimba ndani ya mwili wangu. Ulikuwa uchungu usiofikirika. Nikitolewa mhanga kwa kikatili, nilikuwa nimekamilisha siku saba tu za kazi nilipozirai ndani ya tanuru. Sikuokolewa hadi baada ya saa 52, lakini nilikaribia kuwa punguani. Mbali na kuwa na fahamu na kuweza kuona na kusikia, sikuweza kufanya chochote. Sikuweza kula, kuzungumza, kutembea, au hata kwenda msalani. Baada ya kuharibiwa jinsi hii na Chama cha Kikomunisti, asili yangu ya kiburi ilikuwa imeshindwa kwa kiasi kikubwa. Hiyo nguvu ya uwezo na kiburi niliyokuwa nayo katika kanisa ilikuwa imetoweka tu. Nilikwisha kuwa mwenye huzuni na kukosa rajua; nilikuwa nikiishi katikati ya mateso yasiyo na mipaka na hali ya kutokuwa na msaada. Baadaye watu katika kituo cha kizuizi walikuja na wazo lililopindika na kupata daktari kutengeneza taarifa za udanganyifu zikisema kwamba nilikuwa na “maradhi ya kinasaba.” Walimwita mke wangu na wakamwambia anichukue na kunipeleka nyumbani. Ili kuitibu hali yangu, kila kitu nyumbani mwetu kiliuzwa, na wakati jamaa zangu walipokuja kuniona walipiga kijembe, wakawa fidhuli na kufanya mzaha. Nikikabiliwa na hali hii, nilivunjika moyo na nilihisi kwamba dunia ilikuwa yenye uovu sana, kwamba hapakuwa na upendo wa familia au mapenzi kati ya watu, kwamba kulikuwa tu na mateso ya kikatili na shutuma …. Nikikabiliwa na mateso ya ugonjwa huu wa kuumiza, hakukuwa na matumaini katika maisha yangu na sikujua jinsi ningeweza kuendelea.
Nilivyokuwa tu nikizama katika kukata tamaa, Mwenyezi Mungu akaninyoshea mkono wa wokovu. Nilipokuwa nimerejea nyumbani kwa zaidi ya mwezi mmoja, ndugu wawili wa kiume walikuja kunihubiria injili ya Mungu ya siku za mwisho na kwamba Alikuwa akishughulikia hatua mpya ya kazi, kupata mwili Kwake kwa mara ya pili ili kuwaokoa wanadamu. Wakati huo sikuamini yote kabisa, lakini kwa sababu sikuweza kuzungumza, nikatafuta vifungu fulani vya Biblia kuwaonyesha. Hivi ndivyo nilivyowakanusha. Walinijibu kwa upole: “Ndugu, wakati unamwamini Mungu unapaswa kuwa na moyo wa utafutaji wa unyenyekevu. Kazi ya Mungu ni mpya daima; daima inasonga mbele, na hekima Yake haiwezi kueleweka na wanadamu, kwa hiyo hatuwezi kushughulika mno katika siku za nyuma. Ikiwa unashikilia kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema utaweza kuingia katika Enzi ya Ufalme? Licha ya, yale Bwana Yesu aliyoyasema katika Biblia yote yana maana yake na muktadha.” Kisha, walinifungulia maneno ya Mwenyezi Mungu ili niyasome, na baada ya hapo wakapata unabii mwingi katika Biblia ili nisome juu ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Kwa njia ya maneno ya Mungu na ushirika na ndugu zangu wa kiume, nilikuja kuelewa maana ya jina la Mungu, ukweli wa ndani katika hatua Zake tatu za kazi, kusudi Lake katika usimamizi Wake wa wanadamu, siri za kupata Kwake mwili, ukweli wa ndani katika Biblia, na zaidi. Hivi ni vitu ambavyo sikuwahi kusikia kuvihusu katika maisha yangu, na pia vilikuwa mafumbo na ukweli ambavyo sikuwa msikivu kwavyo wakati nilipokuwa ninajitahidi sana kujifunza Biblia kwa miaka yote hiyo. Niliisikiliza kwa furaha; niliridhishwa kabisa. Baada ya hayo, ndugu zangu walinipa kitabu cha maneno ya Mungu, wakisema: “Baada wewe kuwa bora wa afya, unaweza kuhubiri injili kwa wafanyakazi wenzako na ndugu wa kiume na wa kike.” Kwa furaha sana nilikubali kitabu cha maneno ya Mungu. Wakati huo, niliweza tu kulala kitandani siku nzima na kusoma maneno ya Mungu. Nilihisi hamu na furaha kama ya samaki akirudi kwa maji. Nilifurahia na nikaidhinisha. Baada ya muda mfupi, afya yangu ilikuwa ikiboreka hatua kwa hatua. Ningeweza kutoka nje ya kitanda na kutembea huku na kule kiasi, na niliweza kujitegemea zaidi katika maisha yangu. Baada ya hapo nilikuwa nikiishi maisha ya kanisa nyumbani mwangu, na nilikuwa na mikutano mara mbili kila juma.
Sikuwa nimefikiria kuwa katika maisha yangu ya baadaye ya kanisa tabia yangu ya kiburi ingefunuliwa kabisa. Kupitia Maneno Yake na watu mbalimbali, masuala na mambo, kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji Wake kwangu na upogoaji wa vipengele fulani vyangu, Mungu alisababisha moyo wangu wa kiburi, mkaidi kushushwa kidogo kidogo. Wakati mmoja kanisa lilimpangia msichana mdogo wa miaka 17 au 18 kuja kukutana nami. Alikuwa binti ya ndugu fulani wa kiume kutoka dhehebu langu la awali, na awali nilipokuwa kiongozi wa kanisa nilikuwa nimekwenda nyumbani kwake mara kwa mara. Nikafikiria mwenyewe: Ni nini kibaya na mipango ya kiongozi wa kanisa? Kufanya mtoto aje kuniongoza—wananiangalia kwa dharau? Chini ya kanuni ya asili yangu ya kiburi, nikasema kwa dharau: “Nimemwamini Mungu kwa miaka mingi zaidi ya umri wako. Nilipokuwa nikienda nyumbani kwenu ulikuwa na miaka michache tu. Ningecheza nawe wakati huo, lakini sasa unakuja kunielekeza ….” Dada yangu mdogo alikasirika kutokana na kile nilichokisema, na hakuthubutu kuja tena. Wiki iliyofuata dada tofauti mdogo alikuja. Alikuwa mdogo sana pia na alitoka kwa kijiji jirani. Sikusema chochote, lakini niliwaza: Ikiwa ni idadi ya miaka au sifa za kumwamini Mungu, elimu ya Biblia, au uzoefu katika uongozi wa kanisa, mimi ni bora zaidi kukuliko katika kila kipengele! Kutokana na umri wako, naweza kuona kwamba umekuwa muumini kwa miaka mitatu au minne na si zaidi. Nimeamini kwa miaka 21. Je, unawezaje kuwa na sifa zinazostahili kunielekeza? … Lakini ni nani angeweza kujua kwamba huyu dada mdogo alikuwa akieleza kwa ufasaha mno—alizungumza kwa uwazi na kwa ukali. Wakati tukikutana, mara moja alifungua matamshi ya Mungu na kusoma kwa sauti: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. … Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani. Unaweza kuelewa wazi asili yake kutoka kwa mienendo hii” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yaliuchoma moyo wangu kama upanga wa makali kuwili, yakinijeruhi moja kwa moja. Ulikuwa ni ufunuo mkali wa malengo yangu yenye kustahili dharau na utendaji mbaya katika vitendo vyangu vya kumwamini Mungu, na pia kiini cha kweli cha asili yangu. Nilikuwa nimejaa aibu na sikutaka chochote zaidi ya kutoweka tu. Juu ya kile kilichofichuliwa katika maneno ya Mungu, nilipofikiria juu ya kile nilichofichua, ni hapo tu nilipotambua kwamba asili yangu ilikuwa ya kiburi sana na kwamba kimsingi nilikuwa nikiwa na uhasama kwa Mungu. Katika siku za nyuma, ili watu wanistahi na kunipenda, kuwa mtu aliye na mamlaka juu ya wengine, kuwa katika daraja la juu, nilifanya bidii kwa kusoma Biblia na kutia kila kitu katika kujiandaa na elimu ya Biblia. Kwa sababu ya hili, nilipata hadhi na cheo ambavyo nilikuwa nimeviota tu pamoja na uungwaji mkono na kila mtu. Nilipata raha kutokana na kupendwa na wengine, na nilihubiri ili kuridhisha majivuno yangu mwenyewe. Kupitia kwa ukiritimba wangu wa mamlaka, nilijifichua na kujionyesha. Nilikuwa naridhika daima kufaidika na hisia ya kuwa na furaha sana nilipokuwa nikisimama kwa mimbari, na hata kwa kujipujua niliitumia aya kutoka kwa Biblia kujishuhudia na kujiinua mwenyewe. Niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu. Nilikuwa na kiburi dhalimu. Siku hiyo, nilimwangalia huyo dada mdogo kwa dharau, nikitumia miaka yangu mingi ya kuhubiri kwa manufaa yangu. Niliamini kwamba kwa sababu nilikuwa nimemwamini Mungu kwa miaka mingi zaidi na nilikuwa na elimu kubwa zaidi ya Biblia, uzoefu mkubwa zaidi katika uongozi wa kanisa, nilikuwa bora zaidi kuliko kila mtu. Sikumchukua yeyote kuwa muhimu, na niliwakadiria kwa upungufu na kuwadharau hao dada wawili. Nilipozungumza niliwaudhi wengine, na kwa kiburi nilipoteza hisi yangu na ubinadamu wa kawaida. Ni hapo tu nilipotambua kwamba ufuatiliaji wangu ulikuwa katika upinzani kwa Mungu na kumpinga Yeye. Nilikuwa nikishindana na Mungu kwa hadhi. Kiini cha asili yangu kilikuwa ni mfano bora kabisa wa Shetani. Nikikabiliana na maneno ya Mungu, singeweza kutoridhishwa. Nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu, nina kiburi sana. Nilipokuwa na hadhi nilikuwa mwenye majivuno sana, na wakati nilipokuwa sina hadhi bado sikumsikiliza yeyote. Nilitumia sifa zangu za zamani na mamlaka kuwatawala watu, kuwaangalia kwa dharau. Mimi nina utovu wa haya sana! Leo nilipokea wokovu Wako. Niko radhi kukubali ufichuzi na hukumu katika maneno Yako.”
Baada ya hapo, huyo dada tena alifungua kifungu cha maneno ya Mungu ili nisome. Yalikuwa: “Hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu, haijalishi jinsi anavyojaribu kuonekana mwenye kuhurumiwa machoni Pangu, Sitawahi kamwe kuwa na huruma kwake, kwa kuwa mwanadamu hana ufahamu wa kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, tofauti kati ya ukweli na yasiyo ya kweli. Hisia ya mwanadamu ni usiohisi chochote, ilhali bado anataka apate baraka; ubinadamu wake si wa kuheshimika lakini bado anataka kumiliki ukuu wa mfalme. Ataweza kuwa mfalme wa nani, na hisia kama hiyo? Jinsi gani yeye na ubinadamu kama huo ataweza kukaa kwenye kiti cha enzi? Mwanadamu kwa kweli hana aibu! Yeye ni mdhalili wa kujivuna tu! Kwa wale kati yenu mnaotaka kupokea baraka, Ninawashauri kwanza mtafute kioo na kuangalia picha zenu mbaya—je, una kile kinachohitajika kuwa mfalme? Je, una uso wa mwanadamu ambaye anaweza kupata baraka? Hakujawa mabadiliko hata madogo katika tabia yako na wewe hujaweka ukweli wowote katika vitendo, ilhali bado unatamani kuona siku ifuatayo ikiwa ya ajabu. Unajihadaa mwenyewe!” (“Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kuyasikia maneno ya Mungu, sikuweza kuyazuia machozi kutiririka usoni mwangu. Nilihisi kwamba kila sentensi ya maneno ya Mungu ilinyakua moyo wangu, kwa ukali nilihisi hukumu Yake, na nilihisi aibu hasa. Tukio baada ya tukio la ukimbizaji wangu wa aibu wa kutawala kama mfalme katika kanisa langu la zamani lilionekana mbele yangu: Miongoni mwa ndugu zangu wa kiume na wa kike nilikuwa mwenye majivuno sana, niliwaamrishaamrisha watu, nilitaka kudhibiti kila kitu, na sikukosa tu kuwaleta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele ya Mungu na kuwasaidia kumjua Yeye, lakini niliwafanya wanitendee kana kwamba nilikuwa juu sana, mkuu sana …. Jinsi nilivyozidi kufikiri juu ya hilo, ndivyo nilivyozidi kuhisi kwamba matendo yangu yalimchukiza Mungu, kwamba nilikuwa wa kuchosha, nisiyestahili, na kwamba niliwasikitisha ndugu zangu wa kiume na wa kike. Wakati huo nilihisi aibu kupita kadiri. Niliona kuwa gharama niliyokuwa nimelipa kwa ajili ya tamaa zangu za kutaka makuu haikuwa na thamani yoyote. Ukimbizaji wangu mbaya wa hadhi na kupewa heshima na wengine ulikuwa wa upuuzi. Nilikuwa nakurupuka pote mchana na usiku; nilistahimili shida, nilifanya kazi kwa bidii, na nikaenda jela. Niliadhibiwa na kuteswa, na nilikuwa karibu kufa. Haikunifanya kuwa na ufahamu wa Mungu; kinyume chake, asili yangu ya kiburi iliongezeka zaidi na zaidi, kumweka Mungu karibu yangu kulipungua zaidi na zaidi kiasi kwamba nilifikiri kwa kujidanganya kwamba ningetawala kama mfalme wakati Ufalme wa Mungu umefanikishwa. Wakati huo huo, nilitambua pia kwamba wakati nilipokuwa nimeteswa na Chama cha Kikomunisti katika kanisa langu la awali, Mungu alikuwa akitumia hilo ili kunifanya niweze vyema zaidi kuikubali kazi Yake katika siku za mwisho. Vinginevyo, kulingana na fahari kuu na hadhi yangu katika kanisa langu la awali, kwa msingi wa ukweli kwamba sikumweka Mungu karibu nami na tabia yangu ya kujivuna, singeweza kabisa kuiachilia hali yangu kwa urahisi na kumkubali Mwenyezi Mungu. Bila shaka ningekuwa mtumishi mwovu aliyezuia kurudi kwa wengine kwa Mungu, aliyempinga Mungu na hatimaye angepata adhabu Yake! Sikuweza kujizuia kumshukuru Mungu kwa dhati kwa ajili ya wokovu Wake, na msamaha Wake mkubwa kwangu. Kwa hiyo nikawa bila makeke zaidi kwa sababu ya kile kilichofichuliwa kupitia kwa maneno ya Mungu, na sikuthubutu tena kuwa mfidhuli na muhali na ndugu zangu wa kiume na wa kike.
Chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu ugonjwa wangu ukapungua hatua kwa hatua. Ingawa sikuweza kuzungumza vizuri, ningeweza kuendesha baiskeli na kufanya kazi kidogo katika mambo ya kawaida. Hata hivyo, kwa sababu asili yangu ya kiburi ilikuwa madhubuti mno, Mungu mara nyingine tena alinipangia watu wapya na mambo ya kunihukumu na kunibadilisha. Siku moja, kiongozi wa kanisa alinipangia wajibu wa kukaribisha. Baada ya kusikia hili nilihisi kutotaka sana kulifanya hilo. Niliamini kuwa kutenda kazi ya kukaribisha ilikuwa ni kutumia vibaya uwezo wangu, lakini sikuweza kukataa, kwa hiyo nilikubali shingo upande. Nilipokuwa nikikaribisha, baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike walikuwa wakikutana nyumbani kwangu na kunifanya kulinda mlango ili kulinda mazingira yetu. Mara nyingine tena mawazo yangu ya ndani yalitokea: kutenda tu kama mwenyeji, kulinda mlango—nitapata nini kutoka hili? Nilifikiria wakati wa nyuma. Niliposimama nyuma ya mimbari nilikuwa na majivuno sana, lakini katika kazi yangu leo sikuwa na ujasiri wowote au hadhi yoyote. Cheo changu kilikuwa cha chini sana! Hivyo baada ya muda fulani, upinzani wangu wa ndani ukawa mkubwa zaidi na zaidi, nilihisi kukosewa zaidi na zaidi, na sikuwa radhi tena kutimiza wajibu huo. Kiongozi wa kanisa alipopitia wakati fulani baadaye, sikuweza kulizuia tena. Nikasema: “Unahitaji kunipa wajibu mwingine wa kutekeleza. Ninyi nyote mnahubiri injili na kulitunza kanisa, lakini mimi niko nyumbani nikitenda kama mwenyeji na kulinda mlango—nitapata nini wakati wa baadaye?” Huyo dada akatabasamu na kusema: “Umekosea. Mbele ya Mungu, hakuna wajibu mkubwa au mdogo, hakuna hadhi kubwa au ndogo. Bila kujali ni wajibu gani tunaotekeleza, kila mmoja wetu ana kazi. Kanisa ni kitengo kimoja chenye kazi tofauti, lakini ni mwili mmoja. Hebu tuangalie kifungu kimoja cha maneno ya Mungu.” Kisha akanisomea kifungu hiki: “Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye. Kwa sasa hakuna hata mmoja wenu aliye mkamilifu. Wakati mwingine mnaweza kutekeleza aina moja ya kazi na wakati mwingine mnaweza kutekeleza mbili; mradi tu mnampa Mungu nguvu zenu zote na kujitoa kwa ajili Yake, hatimaye mtafanywa wakamilifu na Mungu” (“Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusikiliza maneno haya ya Mungu na ushirika wa huyu dada, moyo wangu ukatulia na kuchangamka. Niliwaza: Huwa kwamba Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi tofauti ya kila mmoja. Yeye haangalii kama watu wana hadhi au la ama ni wajibu upi wao hutekeleza, kile ambacho Mungu hukamilisha ni mioyo ya watu na utii wao. Kile Anachoangalia ni kama wao huishia kupata mabadiliko katika tabia. Bila kujali wao hutekeleza wajibu upi, almradi wao huufanya kwa moyo wao wote na ni wacha Mungu kabisa, na wakitupilia mbali tabia yao potovu wao wenyewe wanapotekeleza wajibu wao, wanaweza kukamilishwa na Mungu. Ingawa watu hufanya kazi mbalimbali katika kanisa, lengo daima ni kumridhisha Mungu. Wote wanatimiza wajibu wa uumbaji. Kama watu wanaweza kumtazama Mungu na kutimiza wajibu wao bila nia za kibinafsi au uchafu, hata kama wengine huuangalia kwa dharau wajibu wanaoutimiza na kufikiri si wa thamani sana, machoni mwa Mungu unatunzwa na kuthaminiwa. Watu wakitekeleza wajibu wao ili kuridhisha nia zao wenyewe na tamaa zao, bila kujali ukubwa wa kazi yao na ni wajibu gani wao hutimiza, hautampendeza Mungu. Baada ya hapo, niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu. Usifanye wajibu wako ili ubarikiwe tu, na usikatae kutenda kwa kuogopa kupata laana” (“Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilielewa kutoka kwa maneno haya ya Mungu kwamba kama kiumbe, ibada ya Mungu ni sawa na sahihi. Sistahili kuwa na chaguo langu mwenyewe, na sifai kabisa kujadili masharti ama kufanya shughuli na Mungu. Kama imani yangu kwa Mungu na utimizaji wa wajibu wangu ni ili kupata baraka ama taji, aina hii ya imani haiko katika dhamiri na maana nzuri. Imetoka kwa mtazamo usiofaa. Nilisita kufanya “kazi ndogo” na kutimiza “wajibu mdogo”—si huko bado ni kuwa chini ya utawala wa matarajio ya kiburi kufuatilia baraka na kupewa heshima na wengine? Katika mawazo yangu, niliamini kwamba nikiwa na hadhi na mamlaka ningeweza kuongoza, na kwamba jinsi nilivyofanya kazi zaidi ndivyo Mungu angezidi kufurahi, na ndivyo ningepokea sifa ya Mungu na kutuzwa na Yeye. Hivyo bado singetaka kuachana na hadhi, na daima nilikuwa nikitafuta kufanya kazi kubwa na kutekeleza majukumu makubwa ili mwishowe ningepokea taji kubwa. Vilevile nilielewa visivyo mapenzi ya Mungu na sikuridhishwa na wajibu uliopangwa na kanisa. Nililalamikia juu ya jambo hilo na hata niliamini kuwa kutimiza wajibu wa mwenyeji kulikuwa ni kutumia vibaya ujuzi wangu, kwamba ilikuwa ni njia ya kuniangalia kwa dharau. Nilikuwa na kiburi sana na mjinga! Chini ya hukumu ya maneno ya Mungu, mimi kwa mara nyingine tena niliona aibu. Na pia kwa sababu ya kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu, nilielewa mapenzi Yake. Nilijua ni mtu wa aina gani Mungu humpenda, na ni mtu wa aina gani Yeye hukamilisha, na ni mtu wa aina gani humchukiza Yeye. Nilipata moyo wa utii kwa Mungu. Baada ya hapo niliweka mapenzi yangu mbele ya Mungu na nilikuwa radhi kuwa mdogo kabisa, mtu asiyejitanguliza kabisa katika kanisa, ili kuukamilisha wajibu wangu kama mwenyeji, kuyalinda mazingira yetu, kuwaruhusu ndugu zangu wa kiume na wa kike kukutana katika nyumba yangu kwa amani bila kusumbuliwa. Ningeufariji moyo wa Mungu kwa njia hii.
Kwa njia ya uzoefu huu, niligundua jinsi maneno ya Mungu yalivyo makubwa, kwamba Yeye amenyesha ukweli na mapenzi Yake yote ili kuwaokoa wanadamu. Tunahitaji tu kusoma kwa bidii maneno Yake ili kuufahamu ukweli katika mambo yote, kuyaelewa mapenzi Yake, kutatua mawazo yetu wenyewe na imani. Kutoka hapo na kuendelea, nilikuza kiu zaidi ya maneno Yake, na nikaanza kuamka saa kumi au saa kumi na moja kila asubuhi kusoma maneno Yake. Baada ya muda fulani, niliweza kukumbuka sehemu moja ya maneno Yake, nikapata ufahamu wa mapenzi Yake, na kweli niliyafurahia moyoni mwangu. Baadaye, kulikuwa na ndugu wa kiume aliyekuwa na wajibu wa kazi ya injili ambaye alikaa nyumbani yangu mara nyingi. Mara nyingi alipokuwa akihubiri injili na kukabiliwa na matatizo, aliniulizwa kutafuta maneno ya Mungu ili kuyatatua. Aliona kwamba mimi ningeweza kuyapata haraka sana, na mara tu alipojipata katika matatizo angeniuliza kumsaidia kupata baadhi ya maneno kutoka kwa Mungu. Alinipenda kweli. Bila kukusudia, asili yangu ya kiburi ilianza kujifaragua mara nyingine tena. Nilifikiria mwenyewe: licha ya ukweli kwamba una wajibu wa kuhubiri injili, bado inabidi nikusaidie kutatua masuala. Hujasoma neno la Mungu kama vile nimesoma, na hulielewi jinsi ninavyolielewa. Mimi tayari nimepata ukweli. Kama ningekuwa na madaraka ya kuhubiri injili, waziwazi ningekuwa bora katika hilo kuliko ulivyo. Hivyo katika moyo wangu nilianza kumwangalia kwa dharau huyu ndugu yangu, na baada ya muda hata nilianza kutomthamini. Baadaye, kiongozi wa kanisa alikuja nyumbani kwangu na kuniuliza: “Umekuwa ukiendeleaje hivi karibuni?” Kama nimejaa imani, nilimjibu: “Nimekuwa mwema. Mimi husoma maneno ya Mungu na kuomba kila siku. Yule ndugu ameona kwamba ninaelewa neno la Mungu kiasi, kwa hiyo yeye daima hutaka nimsaidie kutafuta maneno kutoka kwa Mungu ya kutatua masuala ….” Kiongozi wa kanisa alisikia kiburi katika kile nilichokisema, na akachukua kitabu cha maneno ya Mungu na kusema: “Hebu tusome vifungu vichache vya maneno Yake” Mungu anasema: “Kwa sababu hadhi yao ilivyo kubwa zaidi, ndivyo tamaa yao ya makuu ilivyo kubwa zaidi; kadiri wanavyofahamu mafundisho zaidi, ndivyo tabia zao zinavyokuwa zenye majivuno zaidi. Kama, katika kumwamini Mungu kwenu, humwufuati ukweli, na badala yake mnaifuata hadhi, basi ninyi mko hatarini” (“Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). “Bila kujali ni kipengele kipi cha uhalisi wa ukweli umesikia, ukikitumia kama kigezo, utayatekeleza haya maneno katika maisha yako mwenyewe, na kuyashirikisha katika matendo yako mwenyewe, kwa hakika utapata kitu, na kwa hakika utabadilika. Ukiingiza maneno haya ndani ya tumbo lako, na kuyakariri katika ubongo wako, basi hutawahi badilika. … lazima uweke msingi mzuri. Kama, kule mwanzoni kabisa, uliweka msingi wa barua na mafundisho, basi utakuwa katika shida. Ni kama wakati watu hujenga nyumba ufuoni: Nyumba hiyo itakuwa katika hatari ya kuanguka bila kujali umeijenga kwa urefu gani, na haitadumu sana” (“Ili Kuwa Mtu Mwaminifu, Unapaswa Kujiweka Wazi kwa Wengine” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusikia maneno haya ya Mungu, niliona aibu kabisa. Nikagundua kuwa asili yangu mwenyewe ya kiburi ilikuwa inaibuka tena. Katika imani yangu kwa Yesu katika siku za nyuma, nilikuwa nimezingatia kupata elimu ya kina na kuelewa nadharia katika Biblia, na nilitumia hilo kama msingi wa kuwa mtu mwenye majivuno sana, kwa kuwa na kiburi zaidi na zaidi. Sasa nilikuwa na bahati niliweza kusoma ukweli mwingi katika maneno ya Mungu, lakini nilikuwa nimeirudia njia yangu ya zamani na nilikuwa nikitegemea akili yangu. Nilikuwa nimekariri sentensi kadhaa kutoka kwa maneno Yake na niliamini kuwa nilikuwa nimepata ukweli; mara nyingine tena nikawa mwenye kiburi na singemsikiliza mtu yeyote. Nilichuana na wengine kwa ajili ya hadhi na nilishindana nao. Kwa kweli ilikuwa ni aibu sana! Kuelewa nadharia katika maneno inaweza tu kuwafanya watu kuwa na kiburi, lakini ni wale tu wanaojua ukweli wa maneno ya Mungu watakaoweza kubadilisha tabia zao na kuishi kama binadamu. Ndugu huyo wa kiume alikuwa amemwamini Mungu kwa muda mrefu kuniliko, na alelewa mengi kuniliko, lakini aliweza kuomba msaada wangu kwa unyenyekevu. Hii kwa kweli ilikuwa ni nguvu yake, na lilikuwa ni tunda lililotokana na uzoefu wake wa kazi na neno la Mungu. Si kwamba tu sikujifunza kutoka kwake na kuzingatia kuweka neno la Mungu katika matendo maishani mwangu, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu sahihi, lakini nilimwangalia kwa dharau na kutomthamini. Kwa kweli nilikuwa na kiburi, kipofu, na mjinga! Moyo wangu wakati huo ulikuwa na maumivu sana. Nilihisi kwamba asili hii yangu ya kiburi ilikuwa ya aibu na mbaya kwa kweli. Ilikuwa ya kuchukiza mno! Na aina hii ya kiburi kwa kiasi kilichokosa mantiki yote huichukiza tabia ya Mungu kwa urahisi sana. Bila kujibadilisha, bila kufuatilia ukweli kwa ukweli ningekuwa tu nimejiangamiza mwenyewe. Nilipotambua yote haya, nilihisi kwa kweli kuwa hukumu na kuadibu katika maneno ya Mungu yalikuwa kweli upendo Wake na wokovu kwangu. Hili lilinisababisha kuhisi chuki kwa asili yangu ya kiburi, na nilielewa kwamba katika imani yangu katika Mungu, napaswa kutembea njia sahihi ya kufuatilia ukweli na kufuatilia mabadiliko katika tabia.
Hilo lilipokuwa limepita, nilianza kujiangalia ndani kwa ajili ya mizizi ya kiburi changu na ukosefu wa mantiki, kwa kile kilichokuwa kikiyaongoza mawazo yangu, kile kilichonifanya mara kwa mara kufichua asili yangu ya kishetani ya kiburi. Siku moja, niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kila kitu ambacho Shetani hufanya ni kwa ajili yake. Anataka kumpita Mungu, kujiondoa kwa Mungu na kushika mamlaka mwenyewe, na kumiliki vitu vyote ambavyo Mungu ameumba. Baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, alikuwa mwenye kiburi na majivuno, mchoyo na mwovu, na alijishughulisha na faida zake pekee. Kwa hivyo, asili ya mwanadamu ni asili ya Shetani. … Asili ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa ya kishetani ndani yake. Wakati mwingine wewe mwenyewe huelewi vizuri, lakini unaishi kwa kutegemea hilo kila wakati. Na unafikiri kuwa ni sahihi sana yenye mantiki sana. Falsafa ya Shetani inageuka kuwa ukweli wa mwanadamu, na watu wanaishi kwa mujibu wa falsafa yake kabisa bila ukinzani hata kidogo. Kwa hivyo, mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na anaishi kwa falsafa ya shetani katika vipengele vyote. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu” (“Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nikitafakari maneno haya ya Mungu, moyo wangu ulichangamka zaidi na zaidi. Niliwaza: Inatukia kwamba baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, asili yetu pia ilikuwa ya kiburi vilevile, kaidi vilevile, na bila ya ibada ya Mungu kama Shetani mwenyewe, na sisi hufuatilia wengine kutuheshimu na kutuabudu kana kwamba sisi ni Mungu. Kupitia ushawishi wa kijamii na maneno maarufu kutoka kwa watu mashuhuri, Shetani ameweka kufikiri kwake, falsafa yake ya maisha na sheria zake za kudumu ndani ya moyo wa binadamu, kikiwa kitu ambacho watu hutegemea katika maisha yao; hivi vinayaongoza mawazo ya wanadamu, vikitawala matendo yao, na vikiwasababisha wawe na kiburi na muhali zaidi na zaidi. Nilitafakari juu ya ukweli kwamba tangu nilipokuwa mtoto nilionewa na kubaguliwa na nilianza kuwahusudu wale waliokuwa na mamlaka na hadhi. Aidha, sheria za kishetani za kudumu za “Watu hupambana kwenda juu, lakini maji hutiririka kwenda chini,” “Mimi ni Bwana wangu mwenyewe kote mbinguni na duniani,” “kuinuka juu ya wengine,” na “Mtu anafaa kuwaletea mababu zake sifa njema” vilikuwa vimepandwa kwa udhabiti katika moyo wangu kuanzia umri mdogo, vikiyatawala maisha yangu. Kama ilikuwa nje katika ulimwengu au katika kanisa, nilikuwa nafanya kila linalowezekana kufuatilia hadhi na sifa; nilikuwa natafuta kuwa na kimo cha juu kuliko wengine, kuwa mwenye madaraka juu ya wa wengine. Nikiwa nimetiwa sumu na mambo haya, nikawa mwenye kiburi zaidi na zaidi kiasi kwamba nilikuwa na majivuno na daima neno langu lilikuwa ni kauli ya mwisho. Nilikuwa na kiburi kiasi kwamba niliamini kwamba nilikuwa nimetumwa na Mungu, na nilifikiri kwamba ningetawala kama mfalme pamoja na Mungu. Kwa sababu ya sumu hizi, nilijiona mwenye hadhi ya juu sana; nilijiona kama mkubwa kwa kweli. Daima ningeweka sifa zangu za kuwa muumini wa muda mrefu nilipokabiliwa na ndugu zangu wa kiume na wa kike na kulinganisha nguvu zangu na udhaifu wa watu wengine. Ningewadunisha na kuwaangalia kwa dharau. Sikuweza kuwatendea kwa haki, na sikuwa na ufahamu wa asili na ukweli wa upotovu wa Shetani kwangu. Sumu ya Shetani ilikuwa imenifanya kuwa na kiburi kiasi kwamba nilikuwa nimepoteza mantiki yangu ya binadamu. Kama Shetani tu, nilitaka kutwaa mamlaka katika kila kitu. Nilitaka cheo kilichoinuliwa ili kuwatawala wanadamu. Hizi sumu za Shetani zilinidhuru vibaya mno, kwa kina sana, hivi kwamba kile nilichokuwa nikiishi kwa kudhihirisha kilikuwa ni mfano wa shetani, ibilisi! Nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu, siko radhi tena kuishi kwa msingi wa mambo haya. Nimeteseka mno kwa sababu ya mambo hayo, nimekuwa nikiishi katika ubaya usiostahimilika na nimekuchukiza Wewe. Ee Mungu, niko radhi kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli, kuwa mtu ambaye kwa hakika ana dhamira na mantiki, kuishi kwa kudhihirisha mwenendo wa mtu wa kweli, kuufariji moyo Wako. Ee Mungu, nakuomba Usichukue hukumu na kuadibu Kwako mbali na mimi, naomba kazi yako initakase. Mradi inawezekana kunibadilisha, kunifanya nikue na kuwa Wako hivi karibuni, niko radhi kukubali hata hukumu kali zaidi na kuadibu kutoka Kwako na kuadibiwa kwa nidhamu Yako.”
Siku moja, nilisoma maneno ya Mungu yakisema: “Mungu hana mambo ya ukamilifu wa kibinafsi na umuhimu wa kibinafsi, au yale wa kujiona na kiburi; Hana mambo yasiyo aminifu. Yote yanayomuasi Mungu yanatoka kwa Shetani; Shetani ni chanzo cha ubaya na uovu wote. Sababu kwamba mwanadamu anayo sifa sawa na ile ya Shetani ni kwa sababu mwanadamu amelagaiwa na kufinyangwa Shetani. Kristo hajawahi kupotoshwa na Shetani, hivyo Anazo tu tabia za Mungu na hakuna hata moja ya Shetani” (“Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni” katika Neno Laonekana katika Mwili). Moyo wangu ulisisimuliwa mara nyingine tena. Mungu ni wa fahari sana na mkuu, lakini mnyenyekevu sana na aliyejificha. Kamwe huwa Hajishaui, na Yeye kamwe hawi na kiburi katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Yeye daima hufanya kazi yote inayohitajika na mwanadamu kimya kimya, Akivumilia fedheha kubwa na maumivu bila kuiona kama ni shida. Badala yake, Yeye huteseka na huzunishwa kutokana na binadamu kuishi chini ya miliki ya shetani na kufungwa kwa falsafa zake. Yeye hutumia juhudi zote iwezekanavyo ili tu kuwaokoa wanadamu kutoka kwa ushawishi wa Shetani ili watu waweze kupata uzima, waishi kwa uhuru na bila vizuizi, na wanaweza kuzikubali baraka Zake. Mungu ni mkuu sana, mtakatifu sana, na katika maisha Yake hakuna vipengele vya kujidai na majisifu, Kwa sababu Kristo Mwenyewe ni ukweli, njia, na uzima. Yeye ni mkuu na vilevile mnyenyekevu na mzuri. Kuona kile Kristo alicho nacho na alicho, nilihisi hata zaidi kwamba nilikuwa na kiburi na mtovu wa haya, na nilitamani kufuata mfano wa Kristo, ili kufuatilia kuishi kulingana na mwenendo wa mtu sahihi ili kumridhisha Mungu. Baada ya hapo, nikifuata mfano wa Kristo na kuishi kulingana na mwenendo wa mtu wa kweli likawa ndilo lengo nililofuatilia.
Baadaye, kulikuwa na wakati ambapo nilisoma kifungu cha maneno ya Mungu na sikuweza kukielewa. Sikujua kilimaanisha nini, lakini kwa ajili ya kujiepusha na aibu, sikuwa radhi kujiweka kando na kutafuta ushirika na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Nilihofia kuwa wangeniangalia kwa dharau kwa sababu nilikuwa nimezoea kutatua masuala ya watu wengine na kamwe sikuwa nimetaja matatizo yangu mwenyewe ili kutafuta msaada kutoka kwa wengine. Baadaye, nilitambua kwamba kutotaka kwangu kukubali ushirika bado ulikuwa ni utawala wa asili yangu ya kiburi na kutotaka kuangaliwa kwa dharau na wengine. Niliasi dhidi ya mwili ili kutafuta ushirika na ndugu zangu wa kiume na wa kike. Sikuwa nimewahi kudhania kwamba hawakukosa tu kuniangalia kwa dharau, lakini kwa subira waliwasiliana nami mapenzi ya Mungu, na shida yangu ilitatuliwa kwa haraka sana. Kulikuwa na wakati mwingine ambapo ndugu mmoja alinituma nipeleke barua iliyohusiana na kazi ya kanisa. Kwa sababu ya kiburi changu na kwamba nilikamilisha kazi hiyo kwa msingi wa mawazo yangu mwenyewe, haikuwasilishwa kwa wakati wake. Alipoona kuwa ingechelewesha kazi, huyu ndugu akawa na wasiwasi sana. Alinishughulikia na kunifichua. Wakati huo nilikuwa na wasiwasi sana na niliona aibu, lakini nilijua pia kwamba hili lilikuwa ni Mungu akinishughulikia na kuvipogoa vipengele vyangu. Ilikuwa ni Mungu akipima kama nilikuwa na utii au la, na kama ningeweka ukweli katika matendo au la. Nilimwomba Mungu: “Ee Mungu, leo nilishughulikiwa na ndugu yangu, niliona wasiwasi. Nilitaka pia kulipinga kwa sababu katika siku za nyuma, daima nilikuwa katika cheo cha juu na nikiwakaripia wengine, na sikuwa nimewahi kutii ukweli. Daima niliishi kwa kudhihirisha sura ya Shetani. Sasa, nina uzoefu mwingi sana wa kazi ya Mungu na ninaelewa kwamba mtu ambaye anaweza kukubali kushughulikiwa na kupogolewa ndiye wa maana zaidi. Huyu ni mtu ambaye ni mtiifu kwa Mungu na anayemwogopa Mungu. Ni mtu wa aina hii tu aliye na uadilifu na mwenendo wa binadamu. Sasa niko radhi kuunyima mwili wangu mwenyewe na moyo wa kumpenda Mungu. Niko radhi Wewe uusisimue moyo wangu, ulikamilishe azimio langu.” Baada ya maombi hayo, nilihisi sana amani na utulivu katika moyo wangu. Niliona kuwa lile Mungu alilolifanya lilikuwa kubwa, na kwamba kupitia kwa watu, matukio, na mambo, Alinisaidia kujitambua ili niweze kubadilika haraka iwezekanavyo. Kuanzia sasa kwendelea, niko radhi kumtafuta Mungu zaidi, kumtegemea Mungu ili kutimiza wajibu wangu vizuri iwezekanavyo. Baada ya hapo, ndugu yangu alikuwa na wasiwasi kwamba ningekuwa sitaki kukubali yote haya, hivyo aliwasiliana nami juu ya mapenzi ya Mungu. Niliongea kuhusu utambuzi wangu juu ya uzoefu wangu mwenyewe. Tulicheka pamoja kuhusu hilo, na kutoka moyoni mwangu nilitoa shukrani kwa wokovu wa Mungu, kwa Yeye kunibadilisha. Utukufu wote uwe kwa Mungu!
Kwa hiyo, kupitia muda baada ya muda wa hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu, tabia yangu ya kiburi ilibadilika hatua kwa hatua. Ningeweza kuwa mtu asiye makeke, ningeweza kwa subira kuwasikiliza wengine wakiongea, na ningeweza kutilia maanani mapendekezo ya wengine. Ningeweza kukusanya maoni ya ndugu zangu wa kiume na wa kike juu ya masuala fulani, na ningeweza kushirikiana kwa upatanifu nao. Chochote kilichotokea, sikuwa tena na kauli ya mwisho, na sikuwa tena na kiburi na kutokuwa radhi kuwasikiliza wengine. Hatimaye nilikuwa nimepata ubinadamu kidogo. Tangu wakati huo, nahisi kwamba nimekuwa mtu wa kawaida zaidi. Mimi huishi maisha bila shida, kwa furaha sana. Naushukuru wokovu wa Mwenyezi Mungu kwangu. Bila wokovu Wake, bado ningekuwa napambana kwa uchungu katikati ya giza na dhambi bila kuweza kamwe kutoka kwa upotovu. Bila wokovu ya Mungu, asili yangu ingekuwa imekuwa tu ya kiburi zaidi na zaidi, hata nikiwafanya watu kuniabudu kama Mungu, kiasi cha kuikasirisha tabia ya Mungu na kupata adhabu Yake lakini bila mimi kulitambua. Kupitia muda baada ya muda wa hukumu na kuadibu kwa Mungu, niliona kwamba upendo Wake ni halisi sana, na kwamba daima Ametumia upendo Wake kunishawishi, akinisubiri ili nijigeuze. Bila kujali ni jinsi gani nilivyokuwa muasi, bila kujali ni jinsi gani nilivyokuwa mgumu kushughulikiwa, ni malalamiko mangapi na suitafahamu nilizokuwa nazo za Mungu, Hakuwa amewahi kamwe kulifanya kuwa suala kubwa. Bado kwa bidii Alikuwa ameanzisha kila aina ya mazingira ili kuuamsha moyo wangu, kuiamsha roho yangu, kuniokoa kutoka kwa mateso ya Shetani, kuniruhusu niishi katika mwanga wa Mungu, kutembea njia ya kweli ya maisha ya binadamu. Mungu kwa subira alingoja zaidi ya miaka 20 na kulipa gharama isiyo kifani kwa ajili yangu— Upendo wa Mungu kweli ni mkubwa na hauna mwisho! Sasa, hukumu na kuadibu kwa Mungu vimekuwa hazina yangu; pia ni chanzo cha thamani cha utajiri kutoka kwa uzoefu wangu na ni kitu ambacho sitaweza kukisahau kamwe. Mateso haya yalikuwa na thamani na maana. Ingawa bado sijafikia matakwa ya Mungu, ningali naufuatilia kwa matumaini mabadiliko katika tabia, na niko radhi kwa kina sana kupitia uzoefu wa hukumu ya Mungu na kuadibiwa. Naamini kuwa kwa hakika Anaweza kunigeuza kuwa mtu wa kweli anayeweza kukubaliana na mapenzi Yake.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo