Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo huruma. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo huruma. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 29 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote.

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Tamko la Thelathini na Sita

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, kila kitu chini ya mbingu hung’aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika miisho ya ulimwengu vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli wamefungua mapazia yao, kuhuishwa, kama kuamka kutoka kwa ndoto, kuchipuka kwa kuvunja uchafu!
Ah! Mungu mmoja wa kweli, Huonekana mbele ya dunia. Je, nani anathubutu kumpokea kwa upinzani? Kila mmoja hutetemeka kwa hofu.

Jumamosi, 10 Novemba 2018

Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"


Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote.

Jumapili, 4 Novemba 2018

Tamko la Arubaini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe. Msiwe na hamu sana ya matokeo ya haraka, kazi Yangu si kitu ambacho kinaweza kufanywa mara moja. Ndani yake kuna hatua Zangu na hekima Yangu, hivyo hekima Yangu inaweza kufichuliwa. Nitawawezesha kuona ni nini kinachofanywa kwa mikono Yangu—kuadhibu uovu na kuzawadi mema. Mimi hakika Simpendelei mtu yeyote. Ninakupenda kwa dhati wewe unayenipenda kwa dhati, na ghadhabu Yangu daima itakuwa pamoja na wale wasionipenda kwa dhati, ili kwamba waweze kukumbuka daima kwamba Mimi ni Mungu wa kweli, Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu.

Jumamosi, 3 Novemba 2018

Tamko la Arubaini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Mwenyezi Mungu mwenye haki—Mwenyezi! Ndani Yako hakuna chochote kabisa kilichofichwa. Kila fumbo tangu zamani hadi milele, ambalo binadamu hawajawahi kufichua, ndani Yako linadhihirika na kwa jumla kuwa wazi. Hatuhitaji tena kutafuta na kupapasa, kwa maana leo nafsi Yako inadhihirika wazi kwetu, Wewe ndilo fumbo ambalo limefichuliwa, na Wewe ni Mungu aliye hai Mwenyewe, na kwa leo Umekuja uso kwa uso na sisi, na kwa sisi kuona nafsi Yako ni kuona kila fumbo la ulimwengu wa kiroho.

Jumatano, 31 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Sita

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. Kwa wale Ninaowapenda, Nitawapenda daima mpaka mwisho kabisa na upendo hautabadilika kamwe. Kwa wale Ninaowachukia, moyo Wangu hauguswi hata kidogo bila kujali ni wazuri kiasi gani. Hii ni kwa sababu wao sio Wangu na hawana sifa Zangu na hawana uzima Wangu.

Jumapili, 28 Oktoba 2018

Tamko la Tisini na Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni. Hili linamaanisha kwamba tutarudi kutoka kwa nyama hadi kwa mwili wa awali. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kurudi Sayuni.” Hii pia ndiyo maana ya kweli na lengo la mpango Wangu mzima wa usimamizi, na hata zaidi sehemu muhimu zaidi ya mpango Wangu wa usimamizi, ambayo hakuna anayeweza kuizuia, na ambayo itatimizwa mara moja. 

Jumatatu, 18 Desemba 2017

Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Mwenyezi Mungu alisema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote."
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.