Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video-za-Nyimbo-na-Kucheza. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video-za-Nyimbo-na-Kucheza. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 18 Januari 2018

Sifa Kamili | Dansi ya Kilatini ”Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu”

Tukuzeni Ufanikishaji wa Kazi ya Mungu

Kazi kubwa ya Mungu hubadilika haraka sana, vigumu kuipima, kuridhisha kwa mtu. Angalia kandokando yako, si kama awali, kila kitu ni kizuri na kipya. Kila kitu kimehuishwa, vyote vimetengenezwa upya, vyote vimetakaswa. Tunamsifu Mungu, tukijawa furaha, nyimbo za sifa zinapepea mbinguni Kwake. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Watu wote msifuni Mungu kwa vigelegele.
Sifa kwa matendo ya Mungu ya ajabu, isifuni hekima Yake, isiyoshindwa. Isifuni tabia Yake yenye haki, msifuni kwa kuwa ni Mungu mwaminifu. Kazi halisi ya Mungu imebadilisha tabia yangu ya kutotii. Nimeadhimiwa na kazi iliyoteuliwa ya Mungu, kushuhudia kwa matendo Yake matakatifu. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Kuimba sifa Kwake kutoka kwa nyoyo zetu zenye furaha. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Kuimba sifa kwa Mungu kutoka kwa nyoyo zetu zenye furaha.
Wale wanaompenda Mungu, mtiini daima, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa neno Lake. Baada ya kuacha dhambi zao na uchafu, wote huwa watakatifu. Kuwa na ushuhuda kwa jina takatifu la Mungu, baada ya kuutosheleza moyo wa Mungu. Uadilifu na utakatifu kujaa katika ulimwengu huu, kila mahali ni pazuri na papya. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Kuimba sifa Kwake kutoka kwa nyoyo zetu zenye furaha. Mtukuzeni Yeye! Imbeni utukufu kwa jina Lake! Kuimba sifa kwa Mungu kutoka kwa nyoyo zetu zenye furaha.
Tukuzeni ufanikishaji wa kazi ya Mungu, Mungu ametukuzwa kikamilifu, wote na yeyote anafanya kutii, kila mmoja ana mahali pa mwisho pa kupumzika. Watu wa Mungu, watakatifu hata zaidi, humtukuza Mungu wa kweli. Pamoja na Yeye, wametota kwa furaha. Wametota kwa furaha. Mtukuzeni! Pamoja, sisi humtukuza! Nyimbo zetu za sifa hazitafika kikomo kamwe. Mtukuzeni! Pamoja, sisi humtukuza! Nyimbo zetu za sifa hazitafika kikomo kamwe, hazitafika kikomo.
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Jumamosi, 18 Novemba 2017

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana | "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"


Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu

Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha;
ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka.
Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya.
Eneo kubwa la ulimwengu limejaa kusifu; tunapiga ukelele na kuruka kwa shangwe.
Milima yajiunga na milima na maji mengi kujiunga na maji mengi, ndugu wote wa kiume na kike ni wandani.
Twamsifu Mungu bila kukoma. Viumbe wampenda Mungu,
wakija, mbele ya kiti chake cha enzi kwa furaha kuabudu pamoja.
Mungu Amefichua katika Sayuni kwa ulimwengu uadilifu Wake na utakatifu Wake.
Watu wote wa Mungu wanachangamka kwa furaha, wakimtukuza Mungu bila kukoma.
Msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Haleluya! Msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo,
Kumpenda Mungu, lazima kwanza tutoe moyo wa kweli.
Imbeni na kucheza kumsifu Mwenyezi Mungu.
Sauti inayosifu yapasua mbingu.
Acha sisi, waume kwa wake, wazee kwa vijana, tuwahi pamoja.
Watoa nyimbo nami natoa ngoma, uimbe nami nishirikiane.
Aliyetiwa aibu ni shetani—joka kubwa jekundu; lililotukuzwa ni jina la Mwenyezi Mungu wa kweli.
Tumeona tabia adilifu ya Mungu kutoka kwa kazi Yake.
Mwenyezi Mungu ni Mungu mwadilifu. Watu wote wa Mungu wameiona sura Yake tukufu.
Sisi sote hufuata kumpenda na kumtosheleza Mungu, tukipenda kuwa waaminifu Kwake milele.
Msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Haleluya! Msifuni Mungu, msifuni Mungu!
Njooni! Hebu tumsifu Mungu!
Njooni! Hebu tumsifu Mungu!
Kuja!

Milima inashangilia na maji mengi yanacheka,
mataifa yote na watu wote wanacheka kwa furaha. Mtazamo mpya ulioje!
Hiyo mbingu mpya, dunia mpya, na ufalme mpya!
Tunacheza na kuimba nyimbo mpya kwa Mungu; tumefurahi sana!
Nyimbo nzuri sana zaimbiwa Mungu, ngoma za madaha zaidi zawasilishwa kwa Mungu.
Moyo mnyofu umeinuliwa juu kwa Mungu, moyo wa kweli umetolewa juu kwa Mungu.
Watu wote wa Mungu na vitu vyote watamsifu Yeye milele bila kukoma. Ha!
Lo! Sayuni ni tukufu sana!
Makao ya Mungu hung'aa kwa miale ya mwanga. Utukufu wake hung'aa kotekote ulimwengu mzima.
Mwenyezi Mungu huvaa tabasamu, na hukalia enzi Yake akitazama umbo jipya la ulimwengu mzima. Ala!
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Alhamisi, 16 Novemba 2017

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani”

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Furaha katika Nchi Nzuri ya Kanaani”

Nimerudi kwa familia ya Mungu, mchangamfu na mwenye furaha.
Mikono yangu imemshika mpendwa wangu, moyo wangu ni miliki Yake.
Japo nimepitia Bonde la Machozi, nimeyaona mapenzi ya Mungu.
Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku, Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.
Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.

Katika nchi hii iliyobarikiwa ya Kanaani, yote ni mabichi, yote ni mapya,
yakifurika na nafsi ya uhai ya maisha.
Maji ya uzima hutiririka kutoka kwa Mungu wa vitendo, hunifanya niruzukike na maisha.
Naweza kufurahia baraka kutoka mbinguni, hakuna tena kutafuta, kuchakura, kuwa na uchu.
Nimewasili katika nchi iliyobarikiwa ya Kanaani, furaha yangu haina kifani!
Upendo wangu kwa Mungu huniletea nguvu isiyoisha.
Sauti za kusifu hupaa juu mbinguni, zikimwambia upendo wangu wa ndani.
Ni haiba ilioje mpendwa wangu aliyo nayo! Uzuri Wake huiteka roho yangu.
Manukato ya mpendwa wangu hunifanya nione ugumu wa kumwacha.

Nyota mbinguni zatabasamu kwangu, jua lanikubali kutoka juu.
Pamoja na mwanga wa jua, na mvua na umande, tunda la uzima hukua kwa uthabiti na ubivu.
Maneno ya Mungu, mengi na ya fahari, hutuletea sikukuu tamu.
Riziki nzima na ya kutosha ya Mungu hutufanya tutosheke.
Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu; upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
Nchi ya Kanaani, ulimwengu wa maneno ya Mungu; upendo Wake hutuletea furaha isiyokoma.
Harufu nzuri ya matunda hujaa hewani.
Ukikaa hapa kwa siku chache, utapapenda kuliko chochote kingine.
Hakuna wakati utataka kuondoka.
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,
Mwezi wa fedha hunurisha mwanga wake. Mzuri na mchangamfu, ni maisha yangu.
Uliye mpendwa moyoni mwangu, uzuri Wako umepita maneno yote.
Moyo wangu u katika mapenzi matamu Nawe, siwezi kujizuia kuruka kwa furaha.
Daima Uko moyoni mwangu, nitakuwa nawe maisha yangu yote.
Moyo wangu hukutamani Wewe daima; kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
Ee mpenzi moyoni mwangu! Nimekupa mapenzi yangu yote.
Moyo wangu hukutamani Wewe daima; kukupenda Wewe hufurahisha moyo wangu kila siku.
Ee mpenzi moyoni mwangu! Nimekupa mapenzi yangu yote.
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho.

Jumapili, 12 Novemba 2017

Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video



Kama Nisingeokolewa na Mungu

I
Kama nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu, nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio. Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani, kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje. Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu leo, wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu. Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimechanganywa kuhusu imani yangu, nikiwa ningali katika nafasi tupu nikisukuma siku, bila kujua imani yangu iwe kwa nani. Hatimaye nimeelewa mikono ya upendo ya Mungu imeshika yangu safarini. Sitaweza kwenda na kupotea njia kwa sababu niko kwa mwendo huu mwangavu kukaa. Hatimaye nimeelewa dhamira ya Mungu, yenye ari kwa mtu. Fikra danganyifu kuondolewa kabisa, nitampa Mungu mwili wangu na roho yangu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo,

II
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu hapa leo, wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu. Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimechanganywa kuhusu imani yangu, nikiwa ningali katika nafasi tupu nikisukuma siku, bila kujua imani yangu iwe kwa nani. Hatimaye nimeelewa mkono wa upendo wa Mungu umeushika wangu safarini. Sitaweza kwenda na kupotea njia kwa sababu niko kwa mwendo huu mwangavu kukaa. Hatimaye nimeelewa dhamira ya Mungu, yenye ari kwa mtu. Fikra danganyifu kuondolewa kabisa, nitampa Mungu mwili wangu na roho yangu.
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya


Jumatatu, 6 Novemba 2017

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu


Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

I
Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji.

II
Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure, upendo wa Mungu umemzunguka. Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru, huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu. Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake. Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo, yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

III
Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu, Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake. Ni uangalizi wa aina gani huo? Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu. Anamtumainia mtu kuamini katika, kuamini katika na kuyatii maneno Yake. Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu.

IV
Akiwa na tumaini hili la kwanza, Mungu aliyasema maneno yafuatayo: "Matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kuyala: Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mema na mabaya, msiyale: kwa maana siku mtakapoyala matunda ya mti huo hakika mtakufa." Maneno haya rahisi, yakisimamia mapenzi ya Mungu, yaonyesha kuwa kumjali mtu kulikuwa tayari katika moyo Wake.

V
Hivyo, kwa maneno haya rahisi, tunaona kilicho moyoni mwa Mungu. Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima? Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa. Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu, utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa, utajihisi mwenye heri na furaha.

VI
Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu? Utakuwa mwaminifu Kwake? Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako? Moyo wako utasogea karibu na Yeye? Kutokana na haya tunaona, jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu. Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu.
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana Katika Mwili
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Upendo wa Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"


Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada "Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki"

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale,
na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki.
Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga
ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga,
wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.
Mungu atawaacha wote wanaotafuta kuuona mwanga tena
na utukufu Aliokuwa nao katika Israeli,
kuona kwamba Mungu tayari ameshuka chini juu ya wingu jeupe miongoni mwa watu,
na kuona mawingu mengi meupe, na kuona vishada vya matunda,
kumwona Yehova Mungu wa Israeli, Mungu wa Israeli,
kumwona Mkuu wa Wayahudi, kumwona Masihi Aliyengojewa,
na kuonekana kamili kwa Yeye aliyeteswa na wafalme katika enzi zote.
Mungu atafanya kazi ya ulimwengu mzima na kufanya kazi kubwa,
akifichua utukufu Wake wote na matendo Yake yote kwa mwanadamu
katika siku za mwisho.
Mungu ataonyesha uso Wake uliojaa utukufu
kwa wale ambao wamemngoja Yeye kwa miaka mingi,
kwa wale ambao wametamani kumuona Yeye akija juu ya wingu jeupe,
kwa Israeli ambayo imemngoja Aonekane kwa mara nyingine tena,
kwa watu wote wanaomtesa Mungu.
Ili wote wajue kwamba Mungu kwa muda mrefu uliopita Ameuchukua utukufu Wake
na kuuleta katika Mashariki.
Hauko katika Uyahudi, kwa maana siku za mwisho tayari zimewadia!
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.