Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho-Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 20 Oktoba 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo 1)

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo 1)


Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.”
Tazama Video: Wimbo wa Kuabudu "Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu" | Manifestation of Power of God

Jumamosi, 5 Oktoba 2019

Neno la Mungu: Sura ya 87

Neno la Mungu: Sura ya 87

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu! Wale wanaomtumikia Shetani, yaani, uzao wa Shetani (hii inahusu wale ambao wanamilikiwa na Shetani.Wale wanaomilikiwa na Shetani kwa hakika wana uhai wa Shetani, na kwa hivyo wanaitwa kuwa uzao wa Shetani) wanaomba rehema miguuni Pangu, wanalia na kusaga meno yao, lakini Siwezi kufanya kitu kama hicho cha kijinga! Ninaweza kumsamehe Shetani? Ninaweza kuleta wokovu kwa Shetani? Haiwezekani! Ninafanya kile Ninachosema na Siwezi kujuta kamwe!
Chochote Ninachosema kinakuja kutukia, si hivyo? Lakini ninyi bado kila mara hamniamini, mnashuku maneno Yangu, na kufikiri kwamba Ninawafanyia mzaha. Hiyo kwa kweli ya dhihaka. Mimi ni Mungu Mwenyewe! Mnaelewa? Mimi ni Mungu Mwenyewe! Ikiwa Sina hekima na sina nguvu, Ninaweza tu kufanya na kusema kama inavyonipendeza? Lakini bado hamniamini. Nimesisitiza mara kwa mara kwenu, na Nimewaambia mara kwa mara. Ni kwa nini wengi wenu bado hawaamini? Kwa nini bado mna mashaka? Kwa nini mnamshikilia kabisa mawazo yenu wenyewe? Yanaweza kukuokoa? Ninatenda kile ninachosema. Nimewaambia mara nyingi: Angalieni maneno Yangu kuwa ni ya kweli na msishuku. Je, mmechukulia maneno Yangu kwa uzito? Wewe peke yako huwezi kufanya chochote, lakini huwezi kuamini katika kile Ninachotenda. Ni nini kinaweza kusemwa juu ya mtu kama huyo? Kusema wazi wazi, ni kama kwamba Sikuwahi kuwaumba kamwe, ambayo ni kusema, wewe hujahitimu katika kila hali kuwa mtumishi Wangu. Kila mtu lazima aamini maneno Yangu! Wote wanapaswa kupitia jaribio—Sitamuacha mtu yeyote kukwepa. Bila shaka, hii ni isipokuwa wale wanaoamini. Watu wanaoamini maneno Yangu kwa hakika watapata baraka Yangu, ambayo utapewa kulingana na kile unachoamini, na itatimizwa ndani yako. Wana Wangu wazaliwa wa kwanza! Sasa, Ninaanza kuwapa baraka Zangu zote. Mtaanza kuvitupa vifungo vyote vinavyochukiza vya mwili kidogo na kidogo: ndoa, familia, kula, kuvaa, kulala, majanga yote ya asili (upepo, jua, mvua, dhoruba inayouma, shida ya kuanguka kwa theluji, na mambo mengine yote mnayochukia). Ninyi mtasafiri baharini, ardhini, na angani bila kuathiriwa na vizuio vya anga, wakati, au jiografia, kujifurahisha kikamilifu katika kumbatio Langu la upendo, mkiwa na wajibu juu ya kila kitu chini ya utunzaji Wangu wa upendo.
Ni nani asiyejivunia wana Wangu wazaliwa wa kwanza ambao Nimewafanya wakamilifu? Ni nani asiyelisifu jina Langu kwa ajili ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza? Kwa nini sasa Ninataka kuwaonyesha siri nyingi sana? Mbona si katika wakati uliopita, lakini leo? Hii yenyewe pia ni siri, wewe unajua? Kwa nini Sikusema hapo nyuma kuwa China ni taifa Nilililolilaani? Na kwa nini Sikuwafichua wale wanaonitumikia? Leo Nawaambieni hili: Leo, kwa maoni Yangu, kila kitu kimetimilika—Ninasema hili kuhusu wana Wangu wazaliwa wa kwanza. (Kwa kuwa leo wana Wangu wazaliwa wa kwanza wametawala pamoja nami, sio tu kuoneka, lakini kwa kweli wanatawala pamoja nami. Kwa sasa, ni kwa yeyote ambaye Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake ambaye kwa hakika anatawala pamoja nami, na hii inafichuliwa sasa, sio jana, wala kesho.) Leo Ninafichua siri zangu Zangu zote katika ubinadamu wa kawaida kwa sababu wale watu ambao Nataka kuwafichua wamefichuliwa, na hii ni hekima Yangu. Kazi Yangu imeendelea hadi hatua hii: Yaani, kwa wakati huu ni lazima Nitekeleze mpango wa maagizo ya utawala Niliyoamua juu ya wakati huu. Kwa hiyo, Ninawatunukia wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wana, watu, na watumishi wa huduma muhuri unaofaa tu, kwa sababu Nina mamlaka na Nitahukumu na kutatawala kwa ukali. Ni nani anayethubutu kutonifanyia huduma kwa utii? Ni nani anayethubutu kunilalamikia? Ni nani anayethubutu kusema kwamba Mimi si Mungu wa haki? Najua, asili yenu ya kipepo imefichuliwa kwa muda mrefu mbele Yangu: Kwa yeyote Ninayekuwa mwema kwake, ninyi mnamwonea wivu na mnamchukia. Hii ni asili ya Shetani kabisa! Mimi ni mwema kwa wana Wangu—je, unathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Naweza kukufukuza kabisa. Kwa bahati nzuri wewe unanifanyia huduma na sasa sio wakati; vinginevyo, Ningekuwa nimekufukuza!
Aina ya Shetani! Acheni kuwa washenzi! Msiseme tena! Msitende tena! Kazi Yangu imeanza kufanywa kati ya wana na watu Wangu waliochaguliwa, na tayari inaenea katika mataifa yote, makundi yote, madhehebu yote, na kazi zote za maisha nje ya China. Ni kwa nini wale wanaonipa huduma kila mara huzuiwa kiroho? Ni kwa nini hawaelewi kamwe mambo ya kiroho? Ni kwa nini kila mara Roho Yangu haifanyi kazi kwa watu hawa? Kwa ujumla, Siwezi kutumia nguvu nyingi sana juu ya wale ambao Sikuwaamulia kabla au kuwagua. Mateso Yangu yote ya awali, bidii Yangu ya kazi ya ulinzi imekuwa kwa wana Wangu wazaliwa wa kwanza na sehemu ndogo ya wana na watu, na zaidi ya hayo, pia wamekuwa kwa niaba ya kukamilika kwa ufanisi wa kazi Yangu ya baadaye, ili mapenzi Yangu yasizuiliwe. Kwa sababu Mimi ni Mungu Mwenye busara Mwenyewe, Nimepanga vizuri kila hatua. Mimi sijitahidi kwa vyoyote kubaki na mtu yeyote (hii inaelekezwa kwa wale ambao hawakuchaguliwa au kuamuliwa kabla), na Sitamuangusha mtu yeyote kwa bahati (hii inaelekezwa na waliochaguliwa na kuamuliwa kabla): Hii ni amri Yangu ya utawala, ambayo hakuna mtu anayeweza kuibadilisha! Kwa wale ambao Ninawachukia, Mimi ni mkatili; kwa wale Ninaowapenda, Ninawalinda na kuwahifadhi. Kwa hiyo, Ninatenda kile Ninachosema (Ninaowachagua, wamechaguliwa; Ninaowaamulia kabla, wameamuliwa kabla; haya ni mambo Yangu ambayo Nimeyapanga kabla ya uumbaji).
Nani anaweza kubadilisha moyo Wangu? Isipokuwa Mimi kufanya kulingana na mipango Ninayofanya Nitakavyo, ni nani anathubutu kutenda kwa pupa na kutotii amri Yangu? Hizi ni amri Zangu za utawala, na ni nani anayethubutu kuondoa moja yao kutoka Kwangu? Wote lazima wawe katika amri Yangu. Watu wengine wanasema, mtu huyo ameteseka sana, na ni mwaminifu na anafikiria moyo Wangu kabisa, lakini kwa nini hakuchaguliwa? Hii pia ni amri Yangu ya utawala. Nikisema mtu anaupendeza moyo Wangu, basi mtu huyo anaupendeza moyo Wangu na ni yule Ninayempenda; Nikisema kwamba mtu ni mtoto wa Shetani, basi mtu huyo ni yule Ninayemchukia. Usimpendekeze mtu yeyote! Je, unaweza kumng’amua? Haya yote yanaamuliwa na Mimi. Mwana ni mwana daima, na Shetani ni Shetani daima, ambayo ni kusema, asili ya mwanadamu haibadiliki. Isipokuwa Mimi Niwafanye wabadilike, wote watafuata aina yao wenyewe na hawawezi kamwe kubadilika!
Ninafichua siri Zangu kwenu kazi Yangu inavyoendelea. Leo, kazi Yangu imeendelea hadi hatua gani, je, mnajua kwa kweli? Je, mtafuata kwa kweli uongozi wa Roho Wangu kufanya kile Ninachofanya na kusema kile Ninachosema? Ni kwa nini Nasema kuwa China ni taifa ambalo Nimelilaani? Kwanza, Niliwaumba Wachina wa leo kwa sura Yangu. Hawakuwa na roho, na mwanzoni wao walipotoshwa na Shetani na hawangeweza kuokolewa. Kwa hivyo Niliwakasirikia watu hawa na nikawalaani. Ninawachukia watu hawa zaidi, na Ninakasirika wanapotajwa kwa sababu ni watoto wa joka kubwa jekundu. Kutokana na hili mtu anaweza kufikiria wakati ambapo nchi za dunia zimetwaa kwa nguvu China. Bado ni vivyo hivyo leo, na yote imekuwa laana Yangu—hukumu Yangu yenye nguvu zaidi dhidi ya joka kubwa jekundu. Hatimaye, Nikawaumba aina nyingine ya watu, ambao pamoja nao Niliwaamulia kabla wana Wangu wazaliwa wa kwanza, wana, watu, na wale wanaonifanyia huduma, kwa hivyo kile Ninachofanya leo Nilipanga kitambo kufanya. Kwa nini wale walio katika mamlaka nchini China wanatesa mara kwa mara na kuwadhulumu ninyi? Ni kwa sababu joka kubwa jekundu halifurahii laana Yangu na ananipinga. Lakini ni chini ya aina hii ya mateso na tishio hasa kwamba Mimi huwakamilisha wana Wangu wazaliwa wa kwanza kurudisha mashambulio dhidi ya joka kubwa jekundu na watoto wake. Baadaye Nitawaainisha. Baada ya kusikiliza maneno Yangu, je, mnaelewa umuhimu wa kuwaruhusu kutawala pamoja nami? Ninaposema kwamba joka kubwa jekundu limesononeshwa kabisa hadi kifo chake, pia ni wakati wana Wangu wazaliwa wa kwanza watawale pamoja nami. Mateso ya joka kubwa jekundu ya wana Wangu wazaliwa wa kwanza hutoa huduma sana Kwangu, na wakati wana Wangu wanapokua na wanaweza kusimamia masuala ya nyumba Yangu, basi watumishi waovu (watenda huduma) wataondolewa. Kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza watakuwa wakitawala pamoja nami na watakuwa wametimiza makusudi Yangu, Nitawasukuma watenda huduma mmoja baada ya mwingine kwenye ziwa la moto na kibiriti: Kwa vyovyote vile wanapaswa kwenda! Ninafahamu kikamilifu kwamba aina ya Shetani pia anataka kufurahia baraka Zangu, na hataki kurudi chini ya miliki ya Shetani, lakini Nina amri Zangu ya utawala ambazo kila mtu lazima azingatie na ambazo zinapaswa kutekelezwa, na hakuna mtu anayeachiliwa. Baadaye, Nitawaambieni amri Zangu za utawala moja baada ya nyingine, msije kukosea.

Alhamisi, 5 Septemba 2019

Sauti ya Mungu : Sura ya 93

Sauti ya Mungu : Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe.

Jumatatu, 2 Septemba 2019

Maneno ya Mungu : Sura ya 94

Maneno ya Mungu : Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni.

Jumanne, 27 Agosti 2019

Sauti ya Mungu : Sura ya 96

Sauti ya Mungu : Sura ya 96

Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee.

Jumamosi, 3 Agosti 2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 97

Maneno ya Mungu | Sura ya 97

Nitafanya kila mtu aone matendo Yangu ya ajabu na kusikia maneno Yangu ya hekima. Ni lazima iwe kila mtu na ni lazima iwe juu ya kila suala. Hii ni amri Yangu ya utawala na ni ghadhabu Yangu. Nitahusisha kila mtu na kila jambo ili watu wote kutoka mwisho mmoja wa ulimwengu hadi mwingine wataona kwa macho yao wenyewe, la sivyo Sitaacha kamwe.

Jumapili, 28 Julai 2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 98

Sauti ya Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote.

Jumatatu, 22 Julai 2019

Sauti ya Mungu | sura ya 99

Sauti ya Mungu | sura ya 99

Kwa sababu mwendo wa kazi Yangu unaongeza kasi, hakuna anayeweza kuenda mwendo sawa na nyayo Zangu, na hakuna anayeweza kupenya akili Yangu, lakini hii ndiyo njia tu ambayo lazima isafiriwe. Hii ni “wafu” yaani wakati Ninapoongea kuhusu kufufuliwa kutoka kwa wafu (inarejelea kukosa uwezo wa kufahamu mapenzi Yangu, kukosa uwezo wa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Yangu. Haya ni maelezo mengine ya “wafu”, na hayamaanishi kutelekezwa na Roho Wangu).

Jumanne, 16 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 101

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 101

Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka

Jumamosi, 13 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102

Nimeongea hadi kwa kiwango fulani na kufanya kazi hadi kwa kiwango fulani; ninyi nyote mnapaswa kuelewa mapenzi Yangu na kwa viwango tofauti muweze kuzingatia mzigo Wangu. Sasa ndicho kipindi muhimu kutoka katika mwili kuingia katika dunia ya roho, na ninyi ndio watangulizi kwa kutagaa enzi, wanadamu wa ulimwengu wanaovuka miisho ya ulimwengu. Ninyi ni wapendwa Wangu zaidi; ninyi ndio Ninaowapenda.

Jumatano, 10 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami.

Ijumaa, 5 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 105

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 105

Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu). Ni njia ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu ya joka kubwa jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu. Katika kila kipindi muhimu, yaani, katika kila awamu ya mpito ya mpango Wangu wa usimamizi, baadhi ya watu lazima waondolewe; wanaondolewa kulingana na utaratibu wa kazi Yangu.

Alhamisi, 4 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 106

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 106

Wale wasioyajua maneno Yangu, wale wasioujua ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale wanaokataa uungu Wangu wote wataangamizwa hadi wasikuwepo. Hakuna atakayeachiliwa kutokana na hili, na wote lazima wapitie hili kwa sababu ni amri Yangu ya utawala, na ndicho kifungu kikali zaidi cha amri Yangu. Wale wasioyajua maneno Yangu ni wale ambao wamesikiliza yale ambayo Nimesema wazi, ilhali bado hawayajui, kwa maneno mengine wale ambao hawaelewi masuala ya kiroho (kwa kuwa Sijaumba sehemu hii ya mwili kwa ajili ya wanadamu, Sihitaji mengi kutoka kwao; Nahitaji tu kwamba wasikilize maneno Yangu na kisha wayaweke katika matendo).

Jumatano, 3 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.)Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi.

Jumanne, 2 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 108

Ndani Yangu, wote wanaweza kupata raha na wote wanaweza kuwa huru. Wale walio nje Yangu hawawezi kupata uhuru na furaha kwa sababu Roho Wangu hayuko pamoja na watu hawa. Watu hawa wanaitwa wafu wasio na roho. Nami Nawaita wale walio ndani Yangu watu walio hai wenye roho. Wao ni Wangu, na watarudi kwenye kiti Changu cha enzi. Wale ambao hutoa huduma na wale ambao ni wa ibilisi ni wafu wasio na roho, nao wanapaswa kuangamizwa hadi wawe katika hali ya kutokuwepo. 

Ijumaa, 21 Juni 2019

Neno la Mungu | Sura ya 116

Neno la Mungu | Sura ya 116
Kati ya maneno Yangu, mengi huwafanya watu kuhisi woga, mengi huwafanya watu watetemeke kwa hofu; bado mengine mengi sana huwafanya watu kuteseka na kukata tamaa, na bado mengine mengi husababisha uangamizaji wa watu. Wingi wa maneno Yangu, hakuna mtu anayeweza kuelewa au kufahamu vizuri. Ni wakati tu Ninapowaambia maneno Yangu na kuyafichua kwenu sentensi baada ya sentensi ndipo mnaweza kujua hali ya jumla; ukweli wa mambo maalum ya hakika, bado hamuelewi. Basi, Nitatumia ukweli kufichua maneno Yangu yote, hivyo kuwaruhusu mpate ufahamu wa juu zaidi.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Kuzaliwa Upya

Ushuhuda wa Maisha, Wakristo, Kanisa la Mwenyezi Mungu

Yang Zheng Mkoa wa Heilongjiang
Nilizaliwa katika familia maskini ya vijijini iliyokuwa nyuma kimaendeleo katika kufikiri kwao. Nilikuwa ovyo kutoka utotoni na hamu yangu ya hadhi ilikuwa hasa yenye nguvu. Baada ya muda, kupitia ushawishi wa jamii na mafunzo ya kitamaduni, nilichukua aina zote za sheria za Shetani za kuponea moyoni mwangu. Aina zote za hoja za uwongo zililea matamanio yangu ya sifa na hadhi, kama vile kujenga nchi nzuri ya asili kwa mikono yako miwili, umaarufu utakufanya kuishi milele, watu wanahitaji nyuso kama mti unavyohitaji ganda lake, kujiendeleza na kuwa juu, mtu anapaswa kuleta heshima kwa mababu zake, nk. Haya hatua kwa hatua yakawa maisha yangu na yakanifanya kuamini kwa thabiti kwamba almuradi tunaishi katika ulimwengu huu, itabidi tufanye kazi ili tuheshimiwe na wengine. Haijalishi tuko katika kikundi kipi ni lazima tuwe na hadhi, inapasa tuwe waliojitokeza zaidi. Kwa kuishi hivi tu ndio tunaweza kuwa wenye uadilifu na heshima. Kuishi maisha kwa njia hii tu ndiko kuna thamani. Ili kutimiza ndoto yangu, nilijifunza kwa juhudi sana katika shule ya asili; kupitia dhoruba na magonjwa, sikuwahi kukosa kuhudhuria darasa. Siku kwa siku, hatimaye nilifikia shule ya kati kwa njia hiyo. Nilipoona kwamba nilikuwa ninaelekea kukaribia ndoto yangu zaidi na zaidi sikuthubutu kuzembea. Nilijiambia mara kwa mara kuwa ilibidi nihimili, kuwa ilibidi nijionyeshe vizuri kwa walimu na wanafunzi wenza. Hata hivyo, wakati huo tu, jambo lisilotazamiwa lilifanyika. Kulikuwa na kashfa kuhusu mwalimu wetu mkuu na mkuu wa shule iliyosababisha vurumai. Walimu na wanafunzi wote walijua kuhusu hiyo. Siku moja darasani, mwalimu huyo alituuliza kama tulikuwa tumesikia kuhusu hiyo na wanafunzi wote wengine walisema “Hapana.” Mimi peke yangu ndiye nilisema kwa uaminifu “Nilisikia.” Kuanzia wakati huo kuendelea, mwalimu huyo aliniona kama mwiba kwa upande wake na mara kwa mara angetafuta vijisababu vya kufanya mambo yawe magumu kwangu, ili kunichukulia hatua kali. Wanafunzi wenza walianza kujitenga nami na kuachana na mimi. Walinifanyia mzaha na kuniaibisha. Hatimaye, sikuweza tena kuvumilia mateso ya aina hiyo na nikaachana na shule. Hivyo ndivyo ndoto yangu ya kujiendeleza na kuwa juu ilivyovunjwa. Nikifikiria kuhusu siku zangu za baadaye huku uso wangu ukiwa kwenye ardhi na mgongo angani, nilihisi huzuni na ghamu isiyoelezeka. Nilifikiri: Inaweza kuwa kwamba maisha yangu yatapitwa kama kawaida tu? Bila hadhi, bila ufahari, bila mafanikio. Haja gani basi ya kuishi namna hii? Kwa kweli sikuwa radhi kukubali ukweli huo wakati huo lakini sikuwa ninajiweza kubadilisha hali zangu. Wakati tu nilipokuwa nikiishi katika uchungu na kutokuwa na matumaini ambayo singeweza kujinasua kwayo, Mwenyezi Mungu aliniokoa na kutia tena tumaini moyoni mwangu ambayo ilikuwa imezimwa. Kutoka wakati huo nilianza maisha mapya kamili.
Ilikuwa Mechi mwaka wa 1999, na kutoka kwa fursa ya bahati niliisikia injili ya siku za mwisho ya Mwenyezi Mungu. Nilipata habari kuwa Mungu mwenye mwili alikuwa amekuja duniani na Yeye Mwenyewe alikuwa akiwazungumzia na kuwaongoza wanadamu ili kutuokoa kutoka kwenye miliki ya Shetani, kuturuhusu kutupa maisha yetu ya kuwa na maumivu, ya kuwa wenye dhambi, kuishi katika mbingu na ardhi mpya. Na kutokana na ushirika wenye ustahamilivu na uangalifu kutoka kwa ndugu zangu, nilisikia ukweli mwingi ambazo sikuwahi sikia hapo awali, kama vile: mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, fumbo la Mungu kuwa mwili, kwamba watu waliopotoshwa wanahitaji wokovu wa Mungu mwenye mwili, ni aina gani ya hisi uumbaji wanapaswa kuwa nayo, jinsi ya kumwabudu Bwana wa uumbaji wote, jinsi ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wako halisi, kile ambacho kweli ni maisha ya binadamu…. Nilivutiwa sana na ukweli huu na ulinifanya kabisa kuamini kuwa hii ilikuwa kazi ya Mungu wa kweli. Siku hiyo ndugu zangu pia waliimba wimbo wa uzoefu wa maisha, “Nikifikiri juu ya Siku Chungu za Nyuma na Utamu wa Hivi Sasa, Nampenda Mungu Hata Zaidi”: “Ee Mungu wa vitendo! Nakuomba usikize hadithi yangu. Mimi hulia ninapokumbuka ya kale; moyo wangu ulikuwa wenye giza na bila mwanga; maisha yangu yalikuwa bila matumaini, sikuweza kuzungumza juu ya mateso katika maisha yangu, niliweza tu kupitisha siku bila kujiweza. Ingewezaje kutosababisha moyo wangu maumivu? Ee Mungu wa vitendo! Nisikilize, ninapofikiria mambo ya kale, moyo wangu una maumivu. Ilikuwa Shetani ibilisi aliyekuwa akinidhuru, akinifanya mpotovu na wa kuanguka. Maneno Yako yalinipa nuru na kuniongoza kutoka giza. Ee Mungu wa kweli! Ee Mungu wa kweli! Ninakupenda kutoka ndani ya moyo wangu.” Hii iliangaza nafsi yangu ambayo kwa muda mrefu ilikuwa gizani kama mwali wa mwanga, na singeweza kujizuia kuangua kilio. Miaka mingi ya ukandamizaji, udhalimu, na huzuni ilionekana kuachiliwa huru kwa ghafla. Moyo wangu ulihisi kuwa mwepesi zaidi. Mbali na msisimko huu, nilikuwa mwenye shukrani hata zaidi kwa Mungu kwa kunichagua kutoka miongoni mwa mamilioni ya watu, kukubali nafsi yangu iliyochoka, na yenye huzuni kupata mapumziko vuguvugu. Kutoka wakati huo maisha yangu yakabadilika kabisa. Sikuwa tena mwenye huzuni na wa kuvunjika moyo, ila niliweka akili yangu yote katika kusoma neno la Mungu, kwenda kwenye mikutano, na kushiriki juu ya ukweli. Kila siku ilikuwa kamili na yenye furaha. Baadaye niliinuliwa na Mungu na kuanza kutimiza wajibu wa kuhubiri injili. Kwa sababu nilikuwa mwenye shauku kabisa na mwenye mawazo mema na ukweli kuwa nilikuwa wa uhodari fulani, baada ya kipindi cha muda kazi yangu ilikuwa inazaa matunda kweli. Nilipata sifa kutoka kwa kiongozi wangu wa timu ya injili, na ndugu katika kanisa pia walinienzi. Wangekuwa kila mara wakija kuniuliza kuhusu mambo hawakuwa wakielewa kuhusu kuhubiri injili. Bila kutambua nilianza kuwa wa kujiona kidogo, na nilifikiri: Nimefaidika kwa upesi sana kanisani ile sifa na hadhi niliyotarajia duniani kwa miaka mingi sana. Sehemu yangu ya “ushujaa” hatimaye imepata mahali pake! Nikiona kufanikiwa kwangu nilihisi kama aliyetimiza sana na nilijitahidi hata zaidi kutimiza wajibu wangu. Haijalishi nilikumbana na shida kubwa kiasi gani, ningefanya niwezavyo kuishinda. Haidhuru nini kanisa lililonipangia kufanya, nilitii kwa hiari na kufanya kadri ya uwezo wangu kuikamilisha. Mara nyingine kiongozi wa kanisa alinishughulikia na kupogoa vipengele vyangu kwa sababu sikuwa nimetenda kazi yangu vyema. Haidhuru nilikuwa nimepinduka aje, kijuujuu singeweza kujitolea visababu kwa ajili yangu. Ijapokuwa niliteseka kabisa sana kiasi wakati wa kipindi cha muda huu, mradi nilikuwa na hadhi kati ya ndugu zangu na nilikuwa ninaheshimiwa nao, nilihisi kuwa ilikuwa sawa kabisa kupitia mateso hayo. Lakini Mungu anaweza kubaini kila sehemu ya watu. Ili Aweze kubadilisha maoni yangu yenye kasoro kuhusu maisha na maadili ya binadamu, ili kutakasa uchafu katika imani yangu kwa Mungu na kutekeleza wajibu wangu, Mungu alitekeleza hukumu na adabu pamoja na majaribio na usafishaji kwangu.
Hiyo ilikuwa mwaka wa 2003, wakati nilipopandishwa cheo kutenda kama kiongozi wa timu yetu ya kiinjili. Pamoja na upandaji cheo huu katika hadhi yangu, upeo wangu wa kazi pia ulienezwa, na nilihisi hata zaidi nimejifurahisha: Dhahabu hung’aa kila mahali. Nina dhamiria kutenda kazi yangu vyema na kupanda kwa hatua ili ndugu zangu waweze kunionea kijicho na kunipenda hata zaidi. Hiyo ingeweza kuwa vyema sana! Wakati nilipofika mahali nilipopaswa kutekeleza wajibu wangu, kiongozi huyo alitia maanani kuwa nilikuwa nimechukua aina hii ya kazi karibuni na nilikosa uzoefu na pia methodolojia, kwa hivyo alikusanya pamoja viongozi wengine kadhaa wa timu ya injili kutoka maeneo ya karibu ili tuweze kujifunza kutoka kwa kila mmoja. Lakini wakati wa ushirika, niliona kuwa wote walikuwa wazee kuliko mimi na kwamba walikuwa wa uhodari duni. Wakati wa ushirika kuhusu maneno ya Mungu pia hawakuzungumza kwa uwazi kama nilivyofanya. Singeweza kujizuia kuwa mwenye kiburi na sikufikiri chochote kuwahusu hata kidogo. Nilihisi kwamba kwa hakika ningeweza kufanya kazi nzuri kwa kutegemea nguvu zangu. Baada ya mkutano nilienda mara moja kwa kila timu ili kupata ufahamu wa kazi yao. Nilipogundua makosa fulani na mambo yaliyoachwa katika kazi zao na kwamba baadhi ya ndugu hawakuwa na uwezo wa kuhubiri injili na kuwa na ushuhuda wa Mungu, nilikuwa na wasiwasi na pia hasira. Singeweza kujizuia kuwakaripia ndugu zangu: “Kutekeleza wajibu wenu namna hii kweli kunaweza kuambatana na mapenzi yake Mungu? Hamtaki kulipa gharama lakini mnataka kuokolewa na Mungu. Mtu wa aina hii ana busara yoyote? …” Na wakati mwingine katika ushirika ningejionyesha, nikiambia kila mtu jinsi nilivyokuwa nimeshiriki katika kazi ya kiinjili, kuhusu matokeo yote niliyoyapata. Nilipoona wivu kwenye nyuso za ndugu zangu, nilijigamba sana na nilihisi kuwa nilikuwa nimewajibika zaidi kuliko wengine. Baada ya muda, ndugu zangu mara zote wangejadiliana masuala yoyote na mimi na sikulenga hata tena kuomba Mungu au kumtegemea Yeye. Na sikukosa tu sikuhisi woga, lakini nilifurahia hilo. Hatimaye, nilipoteza kabisa kazi ya Roho Mtakatifu na kwa kweli sikuweza tena kufanya kazi. Mwanzoni mwa mwaka wa 2004 kanisa liliniondoa kwenye wajibu wangu na kunifanya nirudi nyumbani ili nikatafakari kiroho. Nikiwa nimekabiliwa na tokeo hili, ilikuwa ni kama kwamba nilianguka haraka sana katika shimo la kina kirefu. Mwili wangu wote ulikuwa mlegevu na dhaifu kutokana na hisia kali ya kuvunjika moyo, na sikuweza kujizuia kufikiri: Ilikuwa ni vizuri sana wakati nilipoanza kutekeleza wajibu wangu mara ya kwanza. Na sasa, nikirudi katika aibu hii, nitawezaje kukabili familia yangu na ndugu katika makazi yangu ya kudumu? Watanifikiria aje? Watanifanyia mzaha, wataniangalia kwa dharau? Mara tu nilipofikiria kuhusu kupoteza heshima na hadhi yangu katika akili za watu wengine nilihisi kama nilikuwa karibu kukata tamaa. Nilikuwa nikiishi katika uhasi ambayo singeweza kujinasua kutoka na sikuweza hata kuendelea kusoma maneno ya Mungu. Katikati ya uchungu huu, sikuweza kutomwomba Mungu: “Ewe Mungu! Nimekuwa dhaifu sana sasa na roho yangu iko gizani kwa sababu sina uwezo wa kukubali ukweli kuwa nilibadilishwa cheo. Pia sitaki kutii mipango ya kanisa lakini ninafahamu kuwa chochote Unachofanya ni chema na kina mapenzi yako ya ukarimu. Niko radhi kupata nuru Yako na kuelewa mapenzi Yako.” Baada ya kuomba, maneno haya ya Mungu yaniletea nuru: “Katika kutafuta kwenu, mna dhana, matumaini, na siku za baadaye nyingi sana za kibinafsi. Kazi ya sasa ni ili kushughulikia tamaa yenu ya hadhi na tamaa zenu badhirifu. Matumaini, tamaa ya[a]hadhi, na dhana yote ni mifano bora kabisa ya tabia ya kishetani. … Ingawa mmefikia hatua hii leo, bado hamjaiacha hadhi, lakini daima mnapambana kuuliza kuihusu na kila siku mnaichunguza, kwa hofu kubwa kwamba siku moja hadhi yenu itapotea na jina lenu litaharibiwa. … Sasa nyinyi ni wafuasi, na mna ufahamu fulani wa hatua hii ya kazi. Hata hivyo, bado hamjaweka kando tamaa yenu ya hadhi. Wakati hadhi yenu iko juu mnatafuta vizuri, lakini wakati hadhi yenu iko chini hamtafuti tena. Baraka za hadhi daima ziko katika fikira zenu. Kwa nini watu wengi hawawezi kujitoa nje ya uhasi? Je, si daima ni kwa sababu ya matarajio ya kuvunja moyo?” (“Mbona Huko Tayari Kuwa Foili[b]?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ile hukumu iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu ilinipa utambuzi wa ghafla wa ukweli usiopendeza, na kunifanya kuelewa kwamba kazi ya Mungu wakati huo ulikuwa kushughulikia matamanio yangu ya hadhi, kunifanya kuingia katika njia ya kufaa katika maisha. Nikifikiria nyuma kwa wakati tangu nilipoanza kutekeleza wajibu wangu, nilikuwa vyema sana wakati nilikuwa na hadhi. Nilikuwa na ujasiri sana na sikuogopa mateso wala dhiki. Nilipokumbwa na mtu akinishughulikia au kupogoa vipengele fulani kunihusu sikuzuia hilo. Lakini tena, baada ya kuachiliwa na nilibidi kurudi nyumbani sikuweza kujinasua kutoka kwa uhasi wangu. Niliona kwamba kwa nje ilionekana kuwa nilikuwa nikitekeleza wajibu wangu, lakini kwa kweli nilikuwa nikipeperusha bendera ya kutekeleza wajibu wangu wakati nilipokuwa nikisimamia mambo mwenyewe. Ilikuwa kabisa kumtumia Mungu kukidhi matamanio yangu ya kibinafsi ambayo yalikuwa yamefichwa kwa miaka mingi—kuenda mbele na kuheshimika sana. Na haikuwa kufuatilia ukweli na ilikuwa hata zaidi si kutekeleza wajibu wa kiumbe ili kutimiza Mungu. Wakati nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu na nikaona upungufu wa ndugu zangu, sio tu kwamba sikuwasaidia kutokana na upendo, lakini nilitegemea hadhi yangu kuwakashifu. Nilijiinua kwa makusudi, nikajisimamia kama shahidi kwa nafsi yangu, na nilikuwa na wasiwasi wa kila mtu kuniheshimu na kunienzi. Kuanzia mwanzo hadi mwisho, nilikuwa na lengo moja tu katika mawazo na matendo yangu—huku hakukuwa kumpinga Mungu bila kuficha? Wanadamu waliumbwa na Mungu, kwa hivyo tunapaswa kumwabudu na kumtazamia. Mioyo yetu inapaswa tu kuwa na hadhi ya Mungu, lakini nilikuwa mtu mchafu na mwovu, mwenye hali ya chini aliyetaka kuwa na nafasi katika mioyo ya wengine. Huku si kukuwa na kiburi mno? Hii si ya kufedheheshana na kuwa kinyume na Mungu? Hii tabia si kosa kubwa kwa tabia ya Mungu? Nilipofikiri hayo, sikuweza kujisaidia kutetemeka na hofu kwa sababu ya asili yangu yenye kiburi. Ilitokea kuwa tayari nilikuwa katika hali hiyo hatari ya kuwa kwenye uelekeo wa adhabu ya Mungu! Tabia ya Mungu ni ya haki na takatifu na haivumilii makosa ya binadamu. Angewezaje kuvumilia kuniruhusu mimi, mtoto huyu mwasi, kuvuruga tele na kufadhaisha kazi Yake? Hapo tu ndipo nilipobaini kwamba kuachiliwa kulikuwa ni uvumilivu mkubwa na upendo mkubwa wa Mungu. Vinginevyo, ningefanya maovu zaidi na makuu hadi kiwango ambacho Hangeweza kunisamehe. Kisha kungekuwa kumechelewa mno. Nilipofikiri zaidi juu ya hilo ndivyo nilivyoogopa zaidi, na ndivyo nilivyohisi zaidi kuwa nilikuwa na deni ya Mungu sana. Sikuweza kujizuia kusujudu mbele Yake na kuomba: “Ee Mungu! Asili yangu ni ya kiburi sana, ya kijuujuu sana. Sijafuatilia ukweli wakati wa kutekeleza wajibu wangu, na sijafikiri kulipiza upendo Wako. Nilikuwa nikijishughulisha nikikimbia hapa na pale kwa ajili ya sifa na hadhi, na nilidhamiria kuwa mbele kanisani, kwa hivyo ningewezaje kukosa kujikwaa na kuanguka wakati wa kutekeleza wajibu wangu nikiwa na nia hiyo? Kama hukumu na kuadibu Kwako, na ushughulikiaji na kupogoa Kwako hakungenijia kwa wakati ufaao, hakika ningeendelea katika njia ya adui ya Kristo. Mwishowe ningeharibu nafasi yangu ya wokovu. Ee Mungu! Ninakupa shukrani kwa ajili ya rehema Yako na wokovu Wako kwangu. Kuanzia siku ya leo kwendelea, niko tayari kuachana na matamanio yangu makuu na kufuatilia ukweli, na kukubali zaidi hukumu na adabu Yako, kupata mabadiliko katika tabia yangu potovu hivi karibuni.” Nuru na mwongozo wa Mungu uliniondoa katika uhasi wangu na kuniruhusu kutambua kiasi asili yangu ya kiburi na kiini changu cha kumpinga Mungu. Pia nilipata ufahamu kiasi wa tabia ya haki ya Mungu, na nilihisi ufunguliwaji mno katika moyo wangu. Nilikuwa pia radhi kuendelea kutafuta ukweli katika mazingira yoyote ambayo Mungu angeniandalia, na kuelewa kwa undani zaidi mapenzi Yake.
Katika ufuatiliaji wangu baada ya hayo, niliona maneno kutoka kwa Mungu yaliyosema: “Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika” (“Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kama kiumbe wa Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu, na kutafuta kumpenda Mungu bila kufanya chaguo lingine kwa kuwa Mungu anastahiki upendo wa mwanadamu. Wale ambao wanatafuta kumpenda Mungu hawapaswi kutafuta faida zozote za kibinafsi au lile ambalo wanatamani binafsi; hii ndiyo njia sahihi kabisa ya ufuatiliaji” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalikuwa tayari yamewaambia watu kwa uwazi kabisa na kwa njia inayoeleweka mapenzi na mahitaji yake yaliokuwa yapi ili wanadamu wangeweza kuelewa njia mwafaka ya ufuatiliaji na njia gani iliyo mbaya. Wakati huo niliweka sifa na hadhi juu ya kila kitu, lakini kwa kweli, Mungu hakuangalia jinsi hadhi ya mtu ilivyokuwa juu, ni aina gani ya ukubwa aliokuwa nao, au alipitia kiasi gani cha mateso katika imani yake kwa Mungu. Aliangalia kama alifuata ukweli na alikuwa na ufahamu wa kweli wa Mungu au la. Wale walio na ukweli lakini hawana hadhi ya juu pia wanaweza kupata sifa Yake, lakini wale wasiokuwa na ukweli na wana hadhi ya juu ndio ambao Mungu huwachukia na kuwakataa. Hii ndiyo tabia Yake Mungu ya haki na utakatifu. Hadhi haiwezi kuamua majaliwa ya mtu, wala si ishara ya wokovu wa mtu katika imani yao kwa Mungu. Hasa sio alama ya mtu ambaye amekamilishwa na Mungu. Lakini mara mingi nilikuwa nimetumia hadhi yangu kupima thamani yangu na furaha yangu kuu ilikuwa kuheshimiwa na kupendwa na wengine. Hii haikuwa kinyume kabisa na mahitaji ya Mungu? Kutoamini Mungu hivi haikuwa bure bilashi kabisa? Singeweza tu kutoweza kuokolewa na Mungu, lakini mwishowe ningekumbwa na adhabu ya Mungu kutokana na njia zangu mbaya. Wakati huo, kile ambacho Mungu alikuwa ameniaminisha nacho kilikuwa kuniruhusu niingie katika ukweli, kuwa na uwezo wa kufuatilia mabadiliko katika tabia, kufuatilia utiifu kwa na upendo wa Mungu, na mwishowe kuokolewa na kukamilishwa na Yeye. Huu tu ndio uliokuwa njia mwafaka. Baada ya kuelewa haya yote, moyo wangu ulijawa na shukrani kwa Mungu. Shukrani kwa hukumu na adabu Yake iliyonitoa katika njia mbaya na kunipa nuru ili nipate kuelewa mapenzi Yake, kuniruhusu hatimaye kuona kwa wazi hatari na matokeo ya kufuatilia sifa na hadhi. Hapo tu ndipo niliweza kuamka na kugeuka kwa wakati ufaao. Kupitia tukio hilo nilikuwa na ufahamu kiasi wa maoni yangu yenye makosa kuhusu kufuatilia, nikaelewa ukweli kiasi pamoja na nia zake Mungu za ukarimu, na hali yangu ya akili ilipata nafuu mara nyingine tena. Nilijitosa katika kutekeleza wajibu wangu tena.
Mnamo Julai mwaka wa 2004 nilikwenda eneo ya mbali katika milima na kushirikiana na ndugu huko kuhusu kazi ya injili. Wakati nilianza hiyo kazi, nilitia maanani kushindwa kwangu kwa awali kama mafunzo. Nilijikumbusha mara nyingi kutofuatilia sifa wala hadhi lakini kutekeleza wajibu wangu kwa uaminifu kama kiumbe, kwa hivyo wakati kulikuwa na masuala ambayo sikuelewa au sikuwa na hakika nayo, ningejitoa na kutafuta kikamilifu ndugu yangu ili tufanye ushirika, ili tuyajadili na tuyatatue. Lakini kadri kazi yangu ilivyoendelea kuzalisha matunda zaidi na zaidi, asili yangu ya kiburi ilijitokeza tena na nilianza kutia maanani taswira yangu binafsi na hadhi yangu tena. Wakati wa mkutano siku moja, mwanachama wa timu ya mahali hapo ya kiinjili aliniambia kwa furaha: “Kwa ajili ya wewe kuja hapa tumewabadili waumini zaidi….” Kinywa changu kilisema kuwa haya yalikuwa matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu, lakini moyoni mwangu nilifurahishwa sana nami. Baada ya mkutano kukamilika na nikarudi kwa nyumba ya mwenyeji wangu, niliketi juu ya kitanda changu na kuchezesha tena katika akili yangu kila tukio la kazi yangu wakati huo. Singeweza kuzuia kujipongeza, nikifikiri: Inaonekana nina uwezo wa kweli katika kazi hii. Almuradi ninaendelea kufanya kazi kwa bidii, bila shaka ninaweza kupandishwa cheo tena. Nilijiona basi kama shujaa kabisa, na hadhi ya Mungu ilikuwa tayari imeniondoka moyoni mwangu. Wakati wa kutekeleza wajibu wangu baada ya hayo, nilianza kushindana kupata hadhi na kulinganisha vyeo na wafanyikazi wenzangu. Nilianza kujionyesha kwa wazi mbele ya ndugu zangu kama kwamba matokeo yoyote kutoka kwa kazi yetu yalikuwa yote kwa sababu ya jitihada zangu. Wakati tu nilipokuwa nikirudi nyuma katika lindi kuu hatua moja kwa nyingine, Mungu mara nyingine tena alininyoshea mkono wa wokovu kwangu. Jioni moja nilipatwa na homa kubwa kwa ghafla. Halijoto yangu ilifikia digrii 102 na hata baada ya kunywa dawa kwa siku kadhaa sikupata afueni. Nilienda hospitalini kupata unyweshaji, lakini hali yangu haikukosa kupata nafuu tu lakini ikawa mbaya zaidi. Sikuweza kushikilia chochote tumboni, hata maji. Hatimaye, nilikuwa mgonjwa kitandani na nilihisi kama kwamba nilikuwa nimetimia kifo. Katika mateso ya maradhi hayo, sikuweza tena kufikiri aina gani ya hadhi ningekuwa nayo siku zingefuata. Nilipiga magoti haraka na kumwomba Mungu: “Ewe Mungu! Huu ugonjwa unaonijia ni mapenzi Yako yenye ukarimu pamoja na tabia Yako yenye haki. Sitaki kutokuelewa au kukulaumu; ninakuomba tu unipe nuru na Uniangazie tena, uniruhusu nipate kuelewa mapenzi Yako ili niweze kuelewa hata zaidi upotovu wangu mwenyewe.” Baada ya kuomba, moyo wangu ulikuwa na amani zaidi. Wakati huo tu, maneno haya ya Mungu ghafla yalinijia: “Asili zenu za majivuno na kiburi huwaelekeza kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kuasi na kumpinga Kristo, na kufichua uovu wenu, hivyo basi kuleta kwenye mwangaza fikra zenu, mawazo, tamaa nyingi na macho yaliyojaa ulafi” (“Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kila moja ya maneno haya kutoka kwa Mungu yalidunga moyo wangu kama upanga; yaligonga katika mahali pangu pa kunifisha. Kila aina ya ubaya wa kiburi niliokuwa nimefichua ulinijia kwenye akili kwa uwazi mkubwa. Moyo wangu ulikuwa na uchungu na niliaibika na kufedheheshwa kupindukia. Ilikuwa hapo nilipoona kwa wazi kuwa ilikuwa ni asili yangu yenye kiburi ambayo ilisababisha dhamiri yangu kupoteza utendaji wake wa asili hadi sikuwa na uwezo wa kutii na kumwabudu Mungu mara kwa mara kwa uaminifu. Hii ilinisababisha daima kuhodhi lengo na matamanio, na punde tu nilipopata fursa ningeshindania hadhi, na nilitaka kujionyesha na kuwakandamiza wengine. Singeweza tu kuwa mtu mwenye tabia nzuri. Ilikuwa wazi kuwa matunda yoyote ya kazi yangu yalitegemea kazi ya Roho Mtakatifu; ilikuwa ni baraka za Mungu. Hata hivyo, bila haya niliiba utukufu wa Mungu, kutumia hiyo fursa kujiinua, na kufurahia ndugu zangu kuniheshimu na kuniabudu: Niligeuka kuwa mwenye kiburi sana kiasi kwamba nilipoteza busara yangu. Hapo tu ndipo nilitambua kwamba asili hii yangu ya kiburi ilikuwa hasa ndio kiini cha upinzani wangu kwa Mungu. Ikiwa singeitatua, singewahi kufikia utiifu kwa Mungu au uzatiti wa kutimiza wajibu wangu.
Chini ya uongozo wa Mungu, mara nyingine tena nilifikiria maneno Yake: “Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo, jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha, basi hajivunii nafsi yake mwenyewe sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama alivyokuwa hapo awali. Yeye huhisi, ‘Lazima nitende baadhi ya maneno ya Mungu kwa njia yenye ari na yenye kuhusika na mambo halisi. Kama sivyo, siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.’ Kwa hakika yeye hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Kwa wakati huu ni rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye huonekana kuwa na mfanano fulani wa mwanadamu” (“Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalinielekeza kwa njia ya utendaji na kuingia ndani, na kama nilitaka kuacha kabisa mawazo yangu ya sifa na hadhi, ingebidi kutia juhudi katika kujua asili yangu mwenyewe. Wakati ningeweza kuona kweli vile nilivyokuwa duni, bure, ningeweza kuwa mtu mtulivu na singekuwa tena na kiburi. Kisha, ningeweza kufuatilia ukweli nikiwa imara kabisa. Ukweli ni kuwa, Mungu kunitia adhabu hii ya hukumu na adabu, pigo hili na nidhamu, ilikuwa kwa ajili ya mimi kuwa na ufahamu wa kweli wa nafsi yangu mwenyewe na utambulisho wangu wa asili na hadhi. Ilikuwa ili kuniruhusu kuwa na ujuzi wa kibinafsi mbele ya Mungu, ili niweze kutambua umasikini wangu wa roho, hali yangu ya kutokuwa na thamani. Ilikuwa kuniruhusu kutambua kwamba kile nilichohitaji kilikuwa ni ukweli, wokovu wa Mungu, ambapo ningeweza kuanguka chini mbele ya Mungu na kuwa mtu mwenye tabia njema. Ilikuwa ili niweze kutekeleza wajibu wangu kumtosheleza Mungu na kutofuatilia tena hadhi, hivyo kuumiza moyo Wake. Chini ya uongozi wa maneno Yake nilikuwa na njia ya kuenda mbele pamoja na ujasiri wa kufuatilia ukweli. Hata ingawa nilikuwa nimepotoshwa sana na Shetani na asili yangu ya kiburi ilikuwa madhubuti sana, almuradi nilikuwa na uwezo wa kukubali na kutii hukumu na adabu wa Mungu na majaribu na usafishaji Wake, kutoka hapo kutambua asili yangu mwenyewe na nafsi, na kisha kufuatilia ukweli bila kuchoka, bila shaka ningeweza kufumua vifungo na mateso ya sifa na hadhi, na kuingia katika njia ya kuokolewa, ya kukamilishwa. Baada ya kumrudia Mungu, nilipata nafuu kutoka kwa ugonjwa wangu ndani ya siku mbili. Hii ilinifanya kugundua hata zaidi kwamba alikuwa ametumia ugonjwa huo kama njia ya kunifundisha nidhamu. Haikuwa kunifanya niteseke kwa makusudi, wala hakukuwa na adhabu yoyote ndani yake—ilikuwa ni kuamsha moyo wangu ulioganda, kunifanya kuacha ufuatiliaji wangu wenye kasoro haraka iwezekanavyo na niingie katika njia ya kweli ya kumwamini Mungu. Nilisisimuliwa sana na kuamshwa na mapenzi ya Mungu. Kwa unyoofu mno nilimpa Mungu shukrani zangu na sifa.
Baada ya kupona kutoka kwa ugonjwa wangu nilijirusha tena katika kazi. Niliamua kimoyomoyo kuwa wakati nitakapopatana na jambo litakalohusisha sifa au hadhi, hakika ningemshuhudia Mungu. Miezi kadhaa baadaye, niligundua kuwa timu nyingine ya kiinjili ilikuwa inapata matokeo mazuri sana na ilikuwa imeshuhudia matendo fulani ya ajabu ya Mungu, na ilikuwa imefanya muhtasari wa baadhi ya matukio yao yenye mafanikio na njia zao za utendaji. Hata hivyo, kazi niliyokuwa nikishiriki katika ilikuwa ikididimia. Nilipoona masikitiko katika nyuso za ndugu zangu, hasa niliposikia dada mmoja akisema “Sasa sisi tunafurahia wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu lakini hatuwezi kuwa na ushuhuda wa kazi Yake. Kwa kweli sisi tumewiwa Kwake,” na kila mtu hawangeweza kujizuia kulia, moyo wangu ulikuwa una maumivu sana. Sikujua jinsi ya kujiondoa katika mashaka hayo, na nilimwomba Mungu mara kwa mara: “Ewe Mungu! Sisi sote ni wanyonge wakati tunakabiliwa na matatizo ya kiutendaji, lakini ninajua kuwa huyu ni wewe anayejaribu imani yetu, anayepima mapenzi yetu. Lakini kimo changu ni kidogo mno na siwezi kabisa kuubeba mzigo huo. Ninakuomba unipe nuru ili nielewe mapenzi Yako. Niko radhi kutenda kulingana na mwongozo Wako.” Baada ya kuomba, wazo lilinijia kwa ghafla: Ninafaa kumwuliza mfanyakazi mwenza hapo aje ashirikiane nasi katika ushirika ili tuweze kupata baadhi ya nguvu na tajriba zake. Kwa njia hiyo ndugu pia wataweza kufurahia kupata nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu na kujua jinsi ya kufanya kazi zao za injili. Nilijua kwamba mawazo haya yalitokea kutoka kwa mwongozo wa Roho Mtakatifu, lakini bado nilikuwa na mashaka moyoni mwangu. Nilifikiri: Nilikuwa na uwezo zaidi kuliko ndugu huyo kwa kila namna na wakati tulipokuwa kwenye mikutano pamoja ningemdharau, lakini sasa, utendaji wake ni bora kuliko wangu. Wakati ananiona nikionekana mwenye kukata tamaa na kuwa na aibu sasa, atanicheka? Ndugu watanidharau? Je, kuhusu nini kuokoa heshima yangu? … Nilifikiri na kufikiri, na bado sikuweza kuachana na wazo langu la heshima na hadhi yangu, lakini mara tu nilipofikiri juu ya mapenzi ya dharura ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu na kuwa ndugu zangu hawakuwa na mwongozo na uongozi wa Roho Mtakatifu, niliadibiwa ndani ya moyo wangu. Wakati tu nilipokuwa nikiyumbayumba, maneno haya kutoka kwa Mungu yalinipa nuru: “Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani” (“Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Chini ya uongozi kutoka kwa maneno ya Mungu nilielewa dhamira Yake na nilipata ufahamu fulani wa jinsi ya kuongoza na kuwakamilisha watu katika kazi ya Roho Mtakatifu. Niligundua: Kazi ya Mungu na hekima ya Mungu ni ya ajabu na ya miujiza. Sijui ni kutumia aina gani ya mtu au kitu Yeye atanipatia nuru na kuniongoza kuelewa dhamira Yake, wala sijui ni kwa aina gani ya mazingira atashughulika na tabia yangu potovu. Ni lazima nijifunze kutii kazi ya Roho Mtakatifu, na haijalishi ni ukubwa au udogo jinsi hadhi ya mtu ilivyo, umri wake ni upi, ama kwa muda gani ameamini Mungu, almuradi ushirika wake unakubaliana na ukweli, ni mapenzi Yake Mungu ya sasa, na yanaweza kutuonyesha njia ya utendaji, inayotokana na kazi na nuru ya Roho Mtakatifu. Ni lazima nikubali, nitii, na kutenda–hii ndiyo mantiki ya binadamu ambayo lazima nimiliki. Nisipotii kazi ya Roho Mtakatifu, basi niko radhi kukubali kazi yangu kuwa hatarini ili kudumisha ubatili wangu mwenyewe. Niko radhi kukubali ndugu zangu kuishi katika giza ili niweze kudumisha taswira na hadhi yangu. Katika hali hiyo, mimi ni mtumishi mbaya kupindukia kweli na mpinga Kristo! Nilipogundua hayo, sikuweza kujizuia kuhisi uoga na sikuthubutu tena kwa mara nyingine kuwa mkaidi na kwenda kinyume na kupata nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Nilikuwa radhi kuacha asili yangu ya kishetani na kufariji moyo wa Mungu kupitia utendaji halisi. Kwa hivyo, nilimwita mfanyakazi mwenza huyo mara moja na kumsihi aje awasiliane nasi. Kilichonifanya nione haya ni kwamba baada ya kukutana uso kwa uso, ndugu huyo hakunidharau hata kidogo wala kunicheka. Alishirikiana kwa uhalisi kabisa katika ushirika jinsi walivyokuwa wamefanya kazi pamoja wakati Roho Mtakatifu alifanya kazi kati yao, na jinsi walivyomtegemea Mungu na kumwomba Mungu walipokutana na vipingamizi na ushinde, ni matendo gani waliyoyaona kutoka kwa Mungu baada ya hayo, ni aina gani ya mapatano ya kweli waliyoyapata kuhusu Mungu, na zaidi. Nikiona sura ya kaka yangu imetulia na kujawa na furaha, kisha nikiona kuwa ndugu zangu walionekana kusikiliza kwa makini na kwa kuvutiwa, kisha kuona tabasamu zikijitokeza asteaste kwenye nyuso zao, nilihisi maumivu makali kama kwamba nilikuwa nimevunjika moyo. Hata hivyo, wakati huu haikuwa kwa ajili ya kuukidhi heshima au hadhi yangu, ila ni kwa sababu nilikuwa nimekemewa moyoni mwangu kutokana na kuwiwa kwa Mungu. Kwa sababu ya haya, kwa kweli nilipitia ile jukumu na wajibu unaotekwa kiongozi mzuri. Ikiwa barabara ninayochukua binafsi si sahihi, itaudhuru na kuharibu maisha ya watu wengi sana. Italeta mateso ya kiroho kwa watu wengi sana. Kwa hivyo basi, mimi sijakuwa mhalifu mkuu wa kumpinga Mungu? Wakati kazi ya Mungu imekamilika, ninapaswa kutoa maelezo kwake vipi? Ilikuwa ni wakati huo ambapo hatimaye nilijichukia kabisa ndani ya moyo wangu. Nilijichukia kwamba hapo awali nilipokuwa nikitekeleza wajibu wangu sikujishughulisha kwa uaminifu katika kazi yangu lakini nilifikiri tu ufuatiliaji wa sifa na hadhi na kufurahia katika baraka za hadhi. Sio tu kwamba ilikatiza kuingia kwa ndugu na zangu katika maisha, lakini hata zaidi ilikatiza kutenda mapenzi ya Mungu. Nilikuwa pia nimepoteza mara nyingi mshiko wa kazi ya Roho Mtakatifu na kuanguka katika giza. Niliona kwamba ufuatiliaji wa sifa na hadhi ulifanya madhara mengi zaidi kuliko mema. Lakini wakati nilikuwa ninahisi hatia na huzuni, pia nilihisi kuwa na chembe cha faraja. Hii ilikuwa kwa sababu, chini ya uongozi wa Mungu, nilikuwa mwishowe nimeacha faida ya kibinafsi ili niweke ukweli katika vitendo wakati huu mmoja. Nilikuwa nimetenda jambo ambalo lilikuwa la manufaa kwa kazi, kwa ndugu zangu, na kwangu. Nilikuwa nimemwaibisha Shetani kupitia vitendo vya kiutendaji na nilisimama kama shahidi wa Mungu wakati huu.
Katika uzoefu wangu wa kazi ya Mungu na kwa sababu ya kufuatilia kwangu sifa na hadhi, nilikuwa nimepitia vipingamizi vingi na kushindwa. Nilikuwa nimechukua mizunguko mingi, na kwa sababu ya haya nilikuwa nimepitia kushughulikiwa na kutakaswa. Hatua kwa hatua, niliona hadhi kama kitu kisicho na umuhimu sana, na yale niliyoyaamini hapo awali—bila hadhi hakukuwa na mategemeo ya baadaye na hakuna mtu atakayekutazamia—mtazamo huu uliopotoka uligeuzwa. Nimemfuata Mungu sasa kwa miaka 15. Kila wakati ninapofikiri kazi ya Mungu kwangu, kuna hisia nzuri daima ambayo inayonijia. Sitawahi kamwe kusahau upendo wa Mungu na wokovu kwangu. Kama haingekuwa kwa ajili ya Mungu kubuni mazingira yangu na kushughulikia hamu zangu za umaarufu, faida na hadhi katika hatua za mwanzo za maisha yangu, ningewezaje kuwa radhi kuacha imani ambayo nimeishi nayo kwa miaka mingi na ambayo imekuwa maisha yangu? Kama haingekuwa kwa ajili ya wokovu wa Mungu kunijia kwa wakati, bado ningekuwa ninaendelea kuishi kulingana na sumu za Shetani, na kupoteza maisha yangu kwa ajili ya ndoto ambayo haingeweza kufikiwa. Na kama haingekuwa kwa ufunuo na usafishaji wa mara kwa mara kutoka kwa Mungu, ningekuwa bado ninaendelea kusonga mbele kwa njia yenye makosa na singeweza kamwe kufahamu jinsi kiburi changu kilivyokuwa cha hatari na jinsi tamaa yangu ya hadhi ilivyo na nguvu. Mimi hasa singetambua kwamba mimi ni adui wa Mungu. Ilikuwa kazi ya ajabu ya Mungu ambayo iliyoniwezesha kubaini asili na madhara mengi ya kufuatilia umaarufu, faida na hadhi. Iliruhusu maadili na mitazamo yangu yenye kasoro kuhusu maisha kupitia mabadiliko makubwa, na iliniruhusu kuelewa kwamba ni ufuatiliaji tu wa ukweli na kutekeleza wajibu wa kiumbe ndio uhai wa kweli wa binadamu, na kwamba ni kwa njia ya kuachana na ushawishi mbovu wa Shetani na kuishi kulingana na maneno ya Mungu tu ndio naweza kuishi na maana na kwa thamani. Ni kwa sababu ya matunda ya hukumu na adabu ya Mungu kabisa ndio ninaweza kuwa na uelewa na mabadiliko ninayo leo. Ingawa kupitia hukumu na adabu ya Mungu kulihitaji nipitie uchungu wa utakaso, nimepata ufahamu fulani wa kazi ya utendaji wa Mungu, ya nafsi Yake ya ukarimu, na tabia Yake ya haki na utakatifu. Sasa nina uwezo wa kuona wazi, kuchukia, na kuyatupa sumu za Shetani zilizonidhuru kwa miaka mingi, na nina uwezo wa kuwa na maisha ya kweli ya binadamu. Hakuna mojawapo ya haya yalifanyika bure. Kilikuwa kitu chenye cha maana mno, cha thamani zaidi. Nikiwa njiani kuanzia leo kuendelea, niko radhi kukubali zaidi ya hukumu na adabu, na majaribio na utakaso unaotoka kwa Mungu ili kila aina ya tabia yangu mbovu iweze kutakaswa hivi karibuni, na niweze kuwa mtu ambaye anaambatana na Mapenzi ya Mungu.
Tanbihi:
a. Nakala ya awali imetoa “tamaa ya.”
b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumapili, 26 Mei 2019

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuzing’uta Pingu za Roho

Wu Wen Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Nilikuwa mtu dhaifu na mwenye tabia nyepesi kuhisi. Wakati sikumwamini Mungu, mara kwa mara ningejihisi mwenye huzuni na masikitiko kutokana na mambo yaliyokuja katika maisha. Kulikuwa na nyakati nyingi kama hizi, na siku zote nilihisi kwamba maisha yangu yalikuwa magumu; hapakuwa na furaha, hamkuwa na ridhisho moyoni mwangu ya kuzungumzia. Uchungu huu ulikuwa tu kama pingu zilizonifunga kabisa kila mara, zikinifanya niwe mwenye huzuni. Ilikuwa tu baada kumwamini Mwenyezi Mungu ndipo nilipata kiini cha matatizo ndani ya maneno ya Mungu na nikapata uhuru polepole.
Nilisoma haya katika maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kwa kuwa watu wanajipenda kupita kiasi, maisha yao yote ni ya uchungu na matupu” (“Sura ya 46” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, ilionekana nilijua sababu ya huzuni yangu–nilikuwa mwenye majivuno zaidi. Mara kwa mara ningehisi masikitiko na maumivu kutoka kwa maneno machache yasiyopendeza au kutoka kwa tazamo la kitongotongo kutoka kwa mtu mwingine. Niliposhughulikiwa na kupogolewa nilihisi kuumizwa na mwenye huzuni, kwa sababu heshima yangu iliumizwa na nilihisi nilikuwa nimepoteza hadhi. Nilikuwa na wasiwasi juu ya njia yangu ya baadaye katika maisha. ... Je, haya yote si ni kwa sababu nilijali sana juu ya sifa yangu mwenyewe, hadhi, majivuno, tamaa, na kudura ya baadaye? Kuhusu ufunuo huu, siku za nyuma, nilifikiri tu kwamba hili lilikuwa ni kwa sababu kulikuwa na mambo mengi katika moyo wangu na akili, kwamba mawazo yangu yalikuwa mazito, kwamba kujiepusha na aibu kulikuwa muhimu kwangu, na kwamba nilikuwa mtu asiye makini, lakini sikuwa nimetatua tatizo la njia ya kuingilia . Inawezekana kuwa ni kwa sababu nilikuwa na majivuno zaidi, niliishi katikati ya mateso ya Shetani, katika utumwa naye? Nilitafuta kimyakimya ndani ya moyo wangu. Baadaye, nilipokuwa nikisomasoma maneno ya Mungu katika “Wale Ambao Hutupia Ushawishi wa Giza Wanaweza Kuchumwa na Mungu,” Niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani, ambao hawawezi kutoa moyo wao kwa Mungu, hawa ndio watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaishi chini ya anga ya kifo.” Nikafikiri: Je, si hii ndiyo hali yangu kabisa? Nikawa na uhakika hata zaidi. Kisha, Nikaona zaidi ya maneno ya Mungu: “Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kutafuta ukweli, basi ni hapo tu utakuwa na hali ya sahihi. Kuishi katika hali ya haki ni muhimu kwa ajili ya kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali ya haki ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli, basi uwezekano wa kuepuka ushawishi wa giza haupo. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, mtu hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali ya haki ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika ukweli wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua, wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi ya Mungu, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu” (“Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nikisoma hili, nilihisi moyo wangu ukichangamka. Wakati watu wanapojipenda, hawawezi labda kuwa na uhusiano sahihi na Mungu, na moyo wao wa kutafutilia ukweli hauwezi kuwa mkubwa hivyo. Mwishoni, kwa sababu ya majivuno yao, watajiangamiza kwa kuishi wakimilikiwa na Shetani. Asante kwa kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu ambako kuliniwezesha kuona hali yangu ya hatari na kwamba kuna njia ya kutupia ushawishi wa giza—kuwa na moyo wa kutafuta ukweli, kumtegemea na kumtazamia Mungu kwa kweli ninapokabiliwa na mambo, kusoma maneno ya Mungu zaidi, kutafuta kanuni za utendaji katika maneno ya Mungu, na kuwa mwaminifu kwa Mungu daima. Wakati wa kupata kazi ya Roho Mtakatifu, upotovu ulio ndani ya binadamu unaweza kupitia mabadaliko pamoja na kuingia kwao ndani ya ukweli. Hii ndiyo njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini nilikuwa nimepuuza kipengele hiki, kwa baridi tu nikijaribu kushughulikia upotovu wangu peke yangu, si kutegemea kwa kupanga kazi ya Roho Mtakatifu ili kujibadilisha. Si ajabu kwamba nilifaulu tu kujihini kwa muda; sikuwa nimetatua hali hii kutoka kwa mizizi yake. Kama tu inavyosema katika maneno ya Mungu: “Kadiri watu wanavyozidi kuwa mbele ya Mungu, ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kwao kukamilishwa na Mungu. Hii ndiyo njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake. Usipoelewa hili, haitawezekana wewe kuingia kwenye njia sahihi, na kukamilishwa na Mungu hakutawezekana. … utakuwa tu na bidii yako na bila kazi yoyote ya Mungu. Je, si hili ni kosa katika uzoefu wako?” (“Kuhusu Uzoefu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kuelewa hili, ninajiweka kwenye njia hii kwa utambuzi hata sana, kujinyima mwenyewe, nikipuuza hisia na mawazo yangu; badala yake, ninaweka moyo wangu mintarafu ya kutafuta ukweli, kwa kutekeleza wajibu wangu kwa dhati, kufanya mazoezi ya kufikiria zaidi juu ya maneno ya Mungu, kutegemea maneno ya Mungu katika matendo yangu, kujiruhusu kuishi katika hali nzuri. Ingawa kuna nyakati katika matendo yangu mahususi ambapo sijatenda kwa usahihi kikamilifu, nimehisi ufunguliwaji na uhuru wa kuishi katika nuru na nimefurahia kazi ya Roho Mtakatifu. Sio tu kuwa nimeweza kuona upotovu wangu na upungufu wangu, lakini nimekuwa na nia ya kutamani kubadilisha hivi karibuni na motisha ya kutenda ukweli. Msimamo wangu umebadilika pia; Mimi tena si mwenye huzuni, sikitiko, mwenye kuchusha, lakini kuna uchangamfu na nguvu katika moyo wangu. Nimekuwa pia na furaha zaidi, na ninafurahia sana kuishi katika kanisa!
Bila shaka, kipengele hiki cha upotovu ndani yangu ni cha kina zaidi na haiwezekani kabisa kutupia ushawishi wa Shetani kutoka kwa kuweka mambo haya katika vitendo mara kadhaa. Hata hivyo, Mungu ameniruhusu kuonja utamu wa “kutupia ushawishi wa giza, nikiishi katika nuru,” ambacho kimenipa motisha na matumaini katika ufuatiliaji wangu. Ninaamini kwamba almradi ninaendelea kustahimili katika kushirikiana na Mungu na kutembea njia ambayo Mungu ameonyesha, kutafuta ukweli katika vitu vyote, na kuishi kwa maneno ya Mungu, kutupia minyororo ya roho, nitatupia ushawishi wa giza, na kuchumwa na Mungu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Jumatano, 22 Mei 2019

26. Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

26. Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii kwa moyo wake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi inayofanywa na Mungu daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya vitendo kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. … Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Kwa kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kusalimisha na kuweka kando dhana zenu. Kila hatua inapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu. Kama nyinyi ni wazembe, hakika mtakuwa wamoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayevuruga kazi ya Mungu. … Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa kwa awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Wanadamu kama hawa tu ndio wanatii Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima kwa utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haijakubaliwa na Mungu.
kutoka katika "Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kufuata njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu ni kuingia katika njia sahihi ya kazi halisi ya Roho Mtakatifu; pia ni kufuata njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea. Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya maneno, na kila kitu kinanenwa kutoka kwa maneno Yake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya maneno Yake, maneno Yake halisi. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu.
kutoka katika "Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika Ndio Wanaoingia Katika Uhalisi wa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake.
kutoka katika "Kuhusu Desturi ya Sala" katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kuupata uridhisho wa Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanaongozwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. … Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi, sifa za kuhitimu, ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia mapungufu yako. Unapoutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kuingia kwa undani zaidi kwenye upande mzuri, na kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa yako mwenyewe na mapungufu, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na katika hali isiyo ya kukaa tu, utaingia kikamilifu, na hii itamaananisha kuwa wewe ni mtu sahihi.
kutoka katika "Ni muhimu sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.
kutoka katika "Jinsi ya Kuujua Uhalisi" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. … Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza.
kutoka katika "Ni muhimu sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Wewe ni usiye na hila na uko wazi, radhi kujijua, na radhi kuweka ukweli katika vitendo. Mungu anaona kuwa uko radhi kujijua na uko radhi kuweka ukweli katika vitendo, kwa hivyo unapokuwa mnyonge na hasi, Anakupa nuru mara mbili, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa radhi zaidi kujitubia mwenyewe, na kuwa na uwezo zaidi wa kutenda mambo ambayo unapaswa kutenda. Ni kwa njia hii tu ndipo moyo wako unakuwa na amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida anatilia maanani kumjua Mungu, ambaye anatilia maanani kujijua yeye mwenyewe, ambaye anayatilia maanani matendo yake atakuwa na uwezo wa kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, kupokea mara kwa mara ushauri na nuru kutoka kwa Mungu.
kutoka katika "Ni Wale tu Wanaolenga Vitendo Ndio Wanaweza Kufanywa kuwa Watimilifu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili ya mwanadamu, na kujielewa mwenyewe; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata utiifu wa makusudi. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. …
… Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Kitawaathiri vipi ndugu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu. Kwa njia hii mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri.
kutoka katika "Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje" katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa Mtu:
Roho Mtakatifu hufanya kazi kulingana na maneno ya Kristo, na hufanya kazi pia kulingana na watu kukubali na kumtii Kristo. Ni ikiwa tu watu watamkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo wanaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa watu humpinga Kristo au kuasi dhidi ya Kristo, basi hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama imani ya mtu kwa Mungu inaweza kuwaletea wokovu inaamuliwa na kama anaweza kweli kumkubali na kumtii Kristo au la. Kazi ya Roho Mtakatifu imejitegemeza kikamilifu kwa mtu kukubali na kumtii Kristo. Katika Enzi ya Neema, kazi ya Roho Mtakatifu ilifanywa kulingana na watu kukubali Bwana Yesu, kumtii Yeye, na kumwabudu Yeye. Katika Enzi ya Ufalme, kazi ya Roho Mtakatifu inafanywa kulingana na watu kukubali Mwenyezi Mungu, kumtii Mwenyezi Mungu, na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Roho Mtakatifu hufanya kazi pia kulingana na maneno ya Mwenyezi Mungu, ili kuwaleta waumini katika maneno ya Mungu na kuwafanya wafikie wokovu na ukamilifu. Huu ni msingi na kanuni ya kazi ya Roho Mtakatifu. Viongozi wengi wa dini wamekufa kama adhabu ya kumpinga au kumlaumu Kristo. Watu wengi wa kidini wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, wakianguka katika giza kupitia kukataa kwao kumkubali Kristo wa siku za mwisho. Katika nyumba ya Mungu, watu wengi wamechakaa katika maisha na kukata tamaa kwa sababu ya fikra zao za kudumu juu ya Kristo, na bado wengi wengine wameondolewa kwenye kazi ya Roho Mtakatifu kwa kumwamini tu Roho wa Mungu na si Kristo. Mambo haya yote yamesababishwa na watu kutomkubali au kumtii Kristo. Iwapo muumini ana kazi ya Roho Mtakatifu au la huamuliwa kikamilifu na mtazamo wake kwa Kristo. Ikiwa mtu anamwamini tu Mungu wa mbinguni, na hamtii Kristo, hatapokea kazi ya Roho Mtakatifu kamwe. Kwa sasa bado kuna watu wengi katika makanisa mbalimbali ambao humwamini tu Roho Mtakatifu lakini hawamwamini Kristo, na hivyo hupoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna wengi ambao huamini tu maneno ya Kristo, lakini hawamtii Kristo, na kwa hivyo wanachukiwa na Mungu. Kwa hivyo, kumkubali Kristo na kumtii Kristo ni ufunguo wa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ni iwapo tu mtu humkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo atafikia wokovu na kukamilishwa. Kwa uwazi, kazi za Roho Mtakatifu katika kila enzi zina misingi na kanuni zake. Nani ajuaye kuna watu wangapi bado hawaoni umuhimu wa kumtii Kristo. Roho Mtakatifu hufanya kazi kikamilifu kulingana na maneno ya Kristo. Ikiwa watu hawawezi kuyakubali maneno ya Kristo, na wanaendelea kushikilia fikra kuyahusu na wakayapinga, basi hawawezi kabisa kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengi huomba tu katika jina la Mwenyezi Mungu, lakini hawatii kazi ya Kristo, na hawakubali kabisa maneno ya Kristo. Watu kama hawa ni wapinga Kristo, na hawawezi kabisa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu.
kutoka katika "Matokeo Ambayo Yanaweza Kufanikishwa na Ufahamu Halisi wa Ukweli" katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha
Jinsi watu wanavyoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu pia ni suala muhimu. Hupaswi kufikiri kuwa utapata kazi ya Roho Mtakatifu kwa kusoma neno la mungu bila kujali. Mtu anapaswa kuwa na moyo unaotafuta ukweli. Moyo wa mtu unapaswa kuwa sahihi, anapaswa kutafuta ukweli, kusoma neno la Mungu, kuomba Mungu kwa uaminifu na hamu. Ni wakati huo tu ambapo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Mtu hawezi kuwa na msisimuko wa mara moja au kuwa na hamu, au shauku ya muda mfupi ya kusoma neno la Mungu na aweze kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Ni lazima awe mtu anayefaa, mtu anayetafuta ukweli, na makusudi yao yanapaswa kuwa sahihi. Kulingana na maneno ya Mungu, mtu wa aina hii huwa na njaa na kiu ya haki, na mtu tu wa aina hii anaweza kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Watu ambao hutenda maovu hawawezi kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Watu ambao huishi na mawazo kuhusu Mungu, ambao huishi na tabia ya kuasi, ambao huishi kwa njia mbaya, hawatapokea kwa njia rahisi kazi ya Roho Mtakatifu iwapo hawatafuta ukweli. Kuishi na tabia ya uasi kwa Mungu kunamaanisha nini? Inamaanisha kuwa kilindini cha moyo wao wako katika hali ya kumpinga Mungu. Moyo wao hauko sahihi, unampinga Mungu, una mgogoro na Mungu, unalalamika kuhusu Mungu, au haupendi ukweli. Katika hali hizi chache zisizo za kawaida, mtu hawezi kupokea kazi ya Roho mtakatifu kwa urahisi, na hiki ni kipengele muhimu. Yaani, iwapo kila wakati unaishi maisha yako katika hali ya kumuasi Mungu au kuishi katika hali ya kumpinga Mungu, hutapokea kazi ya Roho Mtakatifu kwa urahisi. Roho Mtakatifu huchunguza sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mtu. Tulikuwa tukisema, "Mungu huchunguza kilindini mwa moyo wa mtu," hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa Roho huchunguza kilindini mwa moyo wa mtu, si hiyo ni kweli? Hivyo Roho Mtakatifu huchunguza ndani ya moyo wa mtu yeyote katika hali zote, akitafuta kujua mtazamo wake ni wa aina gani na kuona iwapo anautafuta ukweli. Mungu anaweza kuona hili kwa wazi zaidi. Hivyo, ni lazima mtazamo wako uwe sahihi ili kutafuta ukweli. Akili yako inatafuta ukweli, inatamani ukweli na inatamani kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Iko tayari kutenda ukweli na ina hamu ya ukweli ili kusuluhisha matatizo. Wakati huu, Roho Mtakatifu atakupa nuru.
kutoka katika "Jinsi Mtu Anapaswa Kutafuta Ukweli" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (I)
Sasa, tunaweza kuona kwamba Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake hasa kuwaongoza watu kuingia katika neno la Mungu na kuuelewa ukweli. Ni vipengele vipi kuingia katika neno la Mungu kunavihusisha? Kuingia katika neno la Mungu hakumaanishi kwamba mtu anasoma sentensi moja mahsusi, anaizingatia kidogo na kisha ana uelewa kidogo. Hii si sawa na kuingia katika neno la Mungu. Ni jambo tofauti kabisa. Jambo muhimu zaidi ni kuingia katika neno la Mungu kupitia uzoefu. "Uzoefu" huu unahusisha tajriba anuwai. Sio kipengele kimoja tu cha uzoefu. Kuna vipengele vingi kwa uzoefu huu. Kutimiza wajibu wa mtu pia ni kupitia neno la Mungu. Kuweka ukweli katika matendo ni kupitia neno la Mungu. Hasa kupitia aina mbalimbali za majaribu na usafishwaji hata zaidi ni kupitia neno la Mungu. Bila kujali ni chini ya mazingira gani au hali, almradi unapitia neno la Mungu, utaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa mfano, tunapokabiliwa na majaribu, sisi humwomba Mungu ili kutafuta nia za Mungu. Matokeo yake, Roho Mtakatifu hutupa nuru ili tuweze kuyaelewa makusudi ya Mungu. Hivi ndivyo kwa sababu inahusiana na kuingia katika neno la Mungu. … Aidha, katika mfanyiko tendani wa kutimiza wajibu wetu, na katika uzoefu wa maisha yetu ya kila siku, bila kujali ni hali gani, almradi tutafute ukweli, tutafute nia za Mungu na kumwomba Mungu, tutaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu yuko hapo kutuongoza kuingia katika neno la Mungu na ukweli. Kuna baadhi ya watu ambao wana uzoefu mkubwa kuhusiana na kipengele hiki. Bila kujali ni hali gani inayowakumba, wao humwomba Mungu. Bila kujali ni watu wa aina gani wanaokutana nao, wao humwomba Mungu na kumuuliza Mungu awape nuru na kuwapa hekima na akili. Wao humwomba Mungu kuwaongoza. Almradi watu hupitia kazi ya Mungu kwa njia hii, wataelewa mambo mengi ya neno la Mungu. Watajua jinsi wanavyopaswa kutenda katika hali thabiti, dhahiri. Watajua jinsi ya kuliweka katika matumizi mazuri. Hii ndiyo njia ya kuingia katika neno la Mungu.
kutoka katika "Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (II)
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?