Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushuhuda. Onyesha machapisho yote
Jumamosi, 13 Julai 2019
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 102
Julai 13, 2019neno-la-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Roho-Mtakatifu, Ushuhuda, VitabuNo comments
Nimeongea hadi kwa kiwango fulani na kufanya kazi hadi kwa kiwango fulani; ninyi nyote mnapaswa kuelewa mapenzi Yangu na kwa viwango tofauti muweze kuzingatia mzigo Wangu. Sasa ndicho kipindi muhimu kutoka katika mwili kuingia katika dunia ya roho, na ninyi ndio watangulizi kwa kutagaa enzi, wanadamu wa ulimwengu wanaovuka miisho ya ulimwengu. Ninyi ni wapendwa Wangu zaidi; ninyi ndio Ninaowapenda.
Jumamosi, 29 Juni 2019
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 110
Juni 29, 2019Kazi-ya-Mungu, maneno-ya-Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ushuhuda, VitabuNo comments
Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 110
Kila kitu kitakapofichuliwa utakuwa wakati ambapo Nitapumzika, na hata zaidi, utakuwa wakati ambapo kila kitu kitakuwa sawa. Mimi hufanya kazi Yangu binafsi; Mimi hupanga kila kitu na kusafidi kila kitu Mwenyewe. Nitakapotoka Sayuni na Nitakaporejea, wazaliwa Wangu wa kwanza watakapokuwa wamekamilishwa na Mimi, Nitakuwa Nimemaliza kazi Yangu kubwa. Katika mawazo ya watu kitu ambacho kinafanywa ni sharti kiweze kuonekana na kuguswa, lakini jinsi Ninavyoona, kila kitu ni kikamilifu wakati ambapo Ninafanya mpango Wangu.
Jumamosi, 22 Juni 2019
neno la Mungu | Sura ya 115
Juni 22, 2019hukumu-ya-Mungu, Kazi-ya-Mungu, Mungu-katika-Mwili, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Ushuhuda, VitabuNo comments
Neno la Mungu | Sura ya 115
Moyo Wangu utakufurahia mno, Nitacheza kwa furaha juu yako, na Nitakupa baraka zisizo na mwisho, kwa kuwa kabla ya uumbaji, ulitoka Kwangu, na leo lazima urejee upande Wangu, kwa kuwa wewe si wa dunia ama ulimwengu bali, badala yake, wewe ni Wangu. Nitakupenda milele, Nitakubariki milele na Nitakulinda milele. Ni wale tu ambao wametoka Kwangu wanaoyajua mapenzi Yangu, na ni wao tu wataudhukuru mzigo Wangu na kufanya kile ambacho Ninataka kukifanya. Sasa, kila kitu tayari kimekwisha kutimizwa. Moyo Wangu ni kama mpira wa moto, ukiwaonea shauku wana Wangu wapendwa kuunganishwa tena nami hivi punde, ukitamani sana nafsi Yangu kurejea Sayuni kikamilifu hivi karibuni. Una ufahamu kiasi juu ya hili.
Jumamosi, 15 Juni 2019
Kuzaliwa Upya Kupitia Neno la Mungu
Wang Gang Mkoa wa Shandong
Mimi ni mkulima na kwa sababu familia yangu ni maskini, daima ilinibidi nisafiri kwenda kote kutafuta kazi za muda ili kupata pesa; nilidhani kuwa ningeweza kujipatia maisha mazuri kupitia kazi yangu ya kimwili. Hata hivyo, kwa uhalisi, niliona kuwa hapakuwa na hakikisho la haki za kisheria za wafanyakazi wahamiaji kama mimi; mshahara wangu mara nyingi ulizuiliwa bila sababu yoyote. Mara kwa mara nilidanganywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao. Baada ya kazi ngumu ya mwaka mmoja, sikupokea kile nilichopaswa kupokea. Nilihisi kwamba ulimwengu huu kwa kweli ulikuwa wa giza! Watu hutendeana kama wanyama ambapo wenye nguvu huwawinda walio dhaifu; wao hushindana wenyewe kwa wenyewe, kupigana kwa kukaribiana sana, na sikuwa na mahali pa usalama kwendelea kuishi jinsi hii. Katika maumivu mno na mfadhaiko wa roho yangu, na wakati nilipokuwa nimepoteza imani katika maisha, rafiki yangu alishirikiana wokovu wa Mwenyezi Mungu nami. Tangu wakati huo, nilikutana mara kwa mara, kusali na kuimba pamoja na ndugu wa kiume na wa kike; tuliwasiliana ukweli, na tulitumia uwezo wetu ili kufidia udhaifu wa mwingine. Nilijihisi mwenye furaha sana na aliyekombolewa. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, niliona kwamba ndugu wa kiume na wa kike hawakujaribu kushindana kwa akili au kufanya utofautishaji wa kijamii; wote walikuwa wazi kabisa na walipatana wenyewe kwa wenyewe. Kila mtu alikuwa hapo kutafuta ukweli kwa bidii ili kuziacha tabia zao potovu, na kuishi kama wanadamu na kupata wokovu. Hili liliniwezesha kupitia furaha katika maisha na kuelewa umuhimu na thamani ya maisha. Kwa hiyo, niliamua kuwa ni lazima nieneze injili na kuwaruhusu watu zaidi wanaoishi gizani kuja kwa Mungu ili kupokea wokovu Wake na kuona mwanga tena. Kwa hiyo, nilijiunga na wale wa kutangaza injili na kumshuhudia Mungu. Lakini bila kutarajia, nilikamatwa na serikali ya CCP kwa kuhubiri injili na kupitia unyama mno wa mateso, utendewaji wa kikatili na kifungo cha jela.
Ilikuwa wakati wa alasiri katika majira ya baridi ya mwaka wa 2008, wakati dada wawili na mimi tulipokuwa tukiishuhudia kazi ya Mungu katika siku za mwisho kwa mlengwa wa injili, tuliripotiwa na watu waovu. Maafisa sita wa polisi walitumia udhuru wa haja ya kuangalia vibali vya makazi yetu ili kuingia kwa nguvu katika nyumba ya mlengwa wa injili. Walipokuwa wakiingia mlangoni, walisema kwa sauti kubwa: “Msisonge!” Wawili wa wale polisi waovu walionekana kuwa wazimu kabisa waliponirukia; mmoja wao alikamata kwa nguvu nguo juu ya kifua changu na mwingine akamata mikono yangu kwa nguvu na kutumia nguvu zake zote ili kuikaza nyuma yangu, kisha akaniuliza kwa ukali: “Unafanya nini? Unatoka wapi? Jina lako ni nani?” Nikauliza kwa kujibu: “Unafanya nini? Unanikamatia nini?” Waliposikia nikisema hivi, walikasirika kweli na wakasema kwa ukali: “Haijalishi sababu ni nini, wewe ndiwe tunayetafuta na unakuja nasi!” Baadaye, wale polisi waovu wakanichukua pamoja na wale dada wawili, wakatusukuma ndani ya gari la polisi na kutupeleka kwa kituo cha polisi cha mahali pale pale.
Baada ya kufika kwa kituo cha polisi, wale polisi waovu walinichukua na kunifungia ndani ya chumba kidogo; waliniamuru nichutame sakafuni na kunipangia watu wanne wanichunge. Kwa sababu nilikuwa nimechuchumaa kwa muda mrefu, nikawa nimechoka sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili. Papo hapo nilijaribu kusimama, wale polisi waovu walinijia mbio mbio na kugandamiza kichwa changu chini ili kunizuia kusimama. Ilikuwa tu hadi wakati wa usiku walipokuja kunipekua na kuniruhusu kusimama; walipokosa kupata chochote katika utafutaji wao, wote waliondoka. Muda mfupi baadaye, nikasikia mayowe yenye kutia hofu ya mtu aliyekuwa akiteswa katika chumba cha pili, na wakati huo, niliogopa sana: Sijui ni mateso gani na matendo katili watakayotumia kwangu baadaye! Nilianza kumwomba Mungu kwa moyo wangu kwa dharura: “Ee Mwenyezi Mungu, ninaogopa sana hivi sasa, naomba Unipe imani na nguvu, nifanye imara na jasiri ili niweze kuwa shahidi Kwako. Kama siwezi kuvumilia mateso yao na matendo ya ukatili, kama itanilazimu kujiua kwa kuuma ulimi wangu, sitawahi kukusaliti Wewe kama Yuda!” Baada ya kuomba, niliyafikiria maneno ya Mungu, “Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu” (“Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Naam, Mwenyezi Mungu ndiye tegemeo langu na Yeye yu pamoja nami; ni nini kingine cha kuogopwa? Ninahitaji kumtegemea Mungu ili kupigana na Shetani. Maneno ya Mungu yaliondoa woga kutoka moyoni mwangu, na moyo wangu uliwekwa huru.
Usiku huo, polisi wanne wa kishetani walinijia na mmoja wao akanielekeza na kuguta: “Bila shaka tulishika samaki mkubwa! Ninyi waumini wa Mwenyezi Mungu mnavuruga utaratibu wa jamii, na mnavunja sheria za kitaifa….” Aliguta alipokuwa akinisukuma ndani ya chumba cha mateso kwa ghorofa ya pili, akiniamuru nichuchumae. Chumba cha mateso kiliandaliwa na aina zote za vyombo vya mateso kama vile kamba, vijiti vya mbao, virungu, mijeledi, bunduki, nk. Vilikuwa vimepangwa kwa machafuko. Akiwa na uso uliojikunja na macho yaliyowaka kwa hasira, polisi mmoja mwovu alizishika nywele zangu kwa mkono mmoja, na kirungu cha umeme, ambacho kilitoa sauti za dhoruba za “kushambulia na kuzibua” kwa ule mkono mwingine, na akafanya madai ya kuitishia habari: “Ni watu wangapi walio katika kanisa lenu? Eneo la mkutano wenu liko wapi? Ni nani anayesimamia? Ni watu wangapi walio katika sehemu hiyo wakihubiri Injili? Ongea! Vinginevyo, utapata kinachokuja!” Nikaangalia hatari iliyotisha ya kirungu cha umeme na nikaangalia tena kwa chumba kilichojaa vyombo vya mateso; sikuweza kujizuia kuhisi fadhaa na kuogopa. Sikujua kama ningeweza kuyashinda mateso haya. Katika tu wakati huu muhimu, nilifikiria maneno ya Mwenyezi Mungu yakisema: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima wewe pia utembee njia niliyotembea Mimi …” (“Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilitambua kwamba hiki kilikuwa kitu ambacho Mungu alituaminia na ilikuwa ni njia ya maisha ambayo Mungu binafsi alituanzishia. Katika kuitembea njia ya kumwamini Mungu na kutafuta ukweli, bila shaka ni lazima mtu apitie mateso na kuvunjika moyo. Hili ni jambo lisiloepukika, na mwishowe, shida hizi huleta baraka kutoka kwa Mungu. Ni kwa njia ya mateso tu watu wanapoweza kupokea njia ya ukweli iliyotolewa na Mungu, na ukweli huu ni uzima wa milele, ambao hutolewa na Mungu. Napaswa kutembea katika nyayo za Mungu na kukabiliana na jambo hili kwa ujasiri; sipaswi kuwa na woga au hofu. Katika kufikiria jambo hili, moyo wangu mara moja ulizalisha aina fulani ya nguvu na nikasema kwa sauti kubwa: “Ninaamini tu katika Mwenyezi Mungu, sijui chochote kingine!” Wakati polisi muovu aliposikia jambo hili, alivurugika na kunidukua kwa nguvu kwa upande wa kushoto wa kifua changu na kirungu hicho cha umeme. Alinishtua kwa karibu dakika moja. Mara moja nilisikia kama damu katika mwili wangu ilikuwa imechemshwa; nilikuwa na maumivu yasiyovumilika kutoka kwa kichwa hadi kwa mguu na nikabiringika nikipiga mayowe sakafuni. Bado hakutaka kuniacha na ghafla akaanza kunivuta na akatumia kirungu kuniinua kwa kidevu changu, akiguta: “Sema! Hutakiri chochote?” Aliguta na kunidukua upande wa kulia wa kifua changu na kirungu cha umeme, nilichomwa na umeme vibaya sana kiasi kwamba nilikuwa nikitetemeka kutoka kichwa hadi mguu. Baadaye mwili uliuma vibaya sana kiasi kwamba nilizirai kama nimelala sakafuni bila kujongea. Sikujua ni muda gani uliokuwa umepita, lakini niliamka yule polisi muovu akisema: “Je! Unajifanya kuwa mfu? Unajifanya! Endelea kujifanya!” Walinidukua tena na kirungu kwa uso na kunipiga teke kwa paja. Baadaye, waliniburuta na kuniuliza kwa ukali: “Je, utaniambia!?” Bado sikujibu. Kisha hao polisi waovu walinipiga kikatili kwa uso wangu kwa ngumi zao na jino langu moja liling’olewa, jino jingine liligongwa hadi likalegea. Mara moja mdomo wangu ulianza kuvuja damu. Katika kukabiliwa na mateso ya kichaa ya pepo hawa, niliogopa tu kwamba ningemsaliti Mungu kwa sababu ya kutoweza kuyahimili mateso yao. Wakati huu, nilifikiri tena juu ya maneno ya Mungu, “Kutoka kwa nje, wale walio na mamlaka wanaweza kuonekana kuwa waovu, lakini msiogope, kwa kuwa hii ni kwa sababu mna imani kidogo. Almuradi imani yenu ikue, hakuna kitu kitakachokuwa kigumu mno” (“Sura ya 75” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa imani na nguvu tena, na niligundua kuwa ingawa hawa polisi waovu mbele yangu walikuwa na kichaa na bila nidhamu, walipangwa na mkono wa Mungu. Wakati huo, Mungu alikuwa akiwatumia kupima imani yangu. Alimradi niliegemea imani na kumtegemea Mungu na sikukubali kushindwa nao, bila kuzuilika wangeshindwa kwa aibu. Katika kufikiri juu ya hili, nilikusanya nguvu zangu zote za mwili wangu na nikajibu kwa sauti kuu: “Kwa nini mmenileta hapa? Kwa nini mnanishtua kwa umeme kwa kirungu cha umeme? Ni kosa gani nimelifanya?” Yule polisi muovu kwa ghafla akawa mtu aliyeshtuka kiasi cha kutowaza na kukandamizwa sana na dhamiri ya hatia. Alianza kugugumiza: “Mimi … mimi … Sikupaswa kukuletea hapa?” Kisha akaondoka kwa aibu. Katika kuona hali ya aibu ya mtanziko wa Shetani, niliguswa hadi nikalia. Katika mashaka haya, kwa kweli nilipitia nguvu na mamlaka ya maneno ya Mwenyezi Mungu. Alimradi neno la Mungu linawekwa katika vitendo na kufuatwa, basi Mungu atakutunza na kukukinga na nguvu za Mungu zitaandamana nawe. Wakati huo huo, nilijihisi ninawiwa na Mungu kwa sababu ya jinsi nilivyokuwa na imani kidogo. Baadaye, afisa mmoja mrefu wa polisi aliingia na kunijia na akasema: “Unapaswa tu kutuambia ni wapi familia yako huishi na ni watu wangapi walio katika familia yako, na tutakuachilia mara moja.” Alipoona kwamba singesema chochote, alivurugika na kukamata mkono wangu kwa nguvu na kuulazimisha mkono wangu kutia alama kwa ungamo la mdomo walilokuwa wameandika. Niliona kwamba huo ungamo la mdomo halikuwa vile niliyowaambia, lilikuwa ni ushahidi ghushi na wa bandia. Nilijawa na hasira ya haki na kulishika na kulirarua vipande vipande. Yule polisi muovu mara moja aliingiwa na hasira na kunipiga na ngumi yake upande wa kushoto wa uso wangu. Kisha akanipiga makofi mara mbili katika uso kwa nguvu sana kiasi kwamba nilishikwa na kizunguzungu. Baadaye, walinipeleka kwa chumba kidogo nilichokuwemo awali.
Baada ya kurudi kwa kile chumba kidogo, nilichubuliwa na kugongwagongwa sana, maumivu yalikuwa yasiyovumilika. Moyo wangu haukuweza kujizuia kuzalisha hisia ya huzuni na udhaifu: Kwa nini waumini wanapaswa kuteseka jinsi hii? Nilihubiri Injili na nia njema za kuwaruhusu watu kuutafuta ukweli na kuokolewa, na bila kutarajia nimepitia mateso haya. Katika kufikiri juu ya hili, nilihisi zaidi kuwa nilikuwa nimekosewa. Katika maumivu yangu, nilifikiria maneno ya Mungu: “Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. … Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?” (“Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mwenyezi Mungu yalivutia hisia kubwa kutoka kwa wangu. Ndio, Mungu alininyunyizia na kunipa maneno Yake makarimu ya uzima, Ameniruhusu kufurahia neema Yake nyingi bure na kuniruhusu kujua siri za ukweli ambazo hakuna mtu yeyote tangu vizazi vya zamani amezielewa. Hii ni baraka maalum ambayo Mungu amenipa. Napaswa kushuhudia kwa Mungu na kuvumilia maumivu yote kwa ajili ya Mungu. Kiasi chochote cha maumivu ni cha kufaa, kwa sababu ni jambo la thamani na la maana sana! Leo, ninateswa kwa kuhubiri injili na siko tayari kupitia maumivu yoyote ya kimwili kwa ajili ya injili; ninahisi kukosewa na kutokuwa tayari. Si nimemhuzunisha Mungu kwa kufanya hivi? Si nimekosa dhamiri? Ningewezaje kustahili baraka za huruma za Mungu na utolewaji wa maisha? Vizazi vya watakatifu wamebeba ushuhuda wa nguvu na mkubwa kwa Mungu kwa sababu walifuata njia ya Mungu; waliishi maisha yenye maana. Leo nina maneno haya yote kutoka kwa Mungu, kwa hiyo mimi si ni lazima hata zaidi nitoe ushuhuda mzuri kwa ajili ya Mungu? Kwa kutafakari jambo hili, mwili wangu haukujihisi kama mchungu, nilijua sana kuwa ni neno la Mwenyezi Mungu ambalo lilinipa uwezo wa uzima, likiniruhusu kuushinda udhaifu wa mwili.
Siku iliyofuata, hao polisi waovu hawakuwa na mkakati mwingine ulioachwa kujaribu. Walinitishia wakisema: “Hutasema chochote? Basi tutakufunga gerezani!” Baadaye, walinipeleka kwa kituo cha kizuizi. Katika kituo cha kizuizi, hao polisi waovu waliendelea kutumia njia zote za mateso kwangu na mara nyingi waliwahimiza wafungwa kunipiga. Katika baridi kali ya majira ya baridi, waliwaagiza wafungwa kunimwagilia ndoo za maji baridi na kunilazimisha kuoga na maji baridi. Nilikuwa nikitetemeka kwa baridi kutoka utosini hadi kidoleni. Hapa, wafungwa walikuwa mashine ya kutengeneza pesa kwa serikali na hawakuwa na haki yoyote ya kisheria. Hawakuwa na chaguo jingine ila kuvumilia kuminywa na kutumiwa na wengine kwa faida yao kama watumwa. Gereza lilinilazimisha kuchapisha pesa za karatasi zilizotumika kama sadaka za kuteketezwa kwa wafu mchana kutwa na kunilazimisha nifanye kazi ya ziada usiku. Kama ningesimama ili kupumzika, basi mtu fulani angekuja na kunipiga sana. Mara ya kwanza, waliweka sheria kwamba nilipaswa kuchapisha vipande 2,000 vya karatasi kwa siku, kisha wakaongeza viwe vipande 2,800 kwa siku, na hatimaye hadi vipande 3,000. Kiasi hiki kilikuwa hakiwezekani kwa mtu mwenye ujuzi kukamilisha sembuse mtu asiye na ujuzi kama mimi kukamilisha. Kwa kweli, walipanga hivyo kwa makusudi ili nisiweze kukamilisha yote ili waweze kuwa na udhuru wa kunitesa na kunidhuru. Alimradi sikuweza kufikia kiasi hicho, hao polisi waovu wangeniwekea pingu za miguu kwa miguu yangu ambazo zilikuwa na uzito wa zaidi ya kilo 5, na kuifunga mikono na miguu pamoja kwa pingu. Yote niliyoweza kufanya ni kuketi pale, kuinamisha kichwa changu na kugeuza kiuno changu, vinginevyo sikuweza kusonga. Aidha, hawa polisi wakatili na wasio na hisia hawakuuliza au kujali kuhusu mahitaji yangu ya msingi. Ingawa choo kilikuwa ndani ya seli ya gereza, sikuweza kabisa kutembea na kukitumia; niliweza tu kuwaomba wenzangu katika seli kuniinua na kuniwekelea kwa choo. Kama walikuwa wafungwa bora zaidi kidogo, basi wangeweza kuniinua; kama hakuna mtu aliyenisaidia, basi singekuwa na chaguo jingine ila kujinyia katika suruali yangu. Wakati wa maumivu mno ulikuwa wakati wa chakula, kwa sababu mikono na miguu yangu ilikuwa imefungwa pamoja. Niliweza tu kuteremsha kichwa changu kwa nguvu zangu zote na kuinua mikono na miguu yangu. Ni kwa njia hii tu nilivyoweza kuiweka skonsi kinywani mwangu. Nilitumia nguvu nyingi sana kwa kila umo. Pingu zilisugua mikono na miguu yangu na zikisababisha maumivu makubwa. Baada ya muda mrefu, vifundo vya mikono yangu na vya miguu vilikuwa vimekuza sagamba nyeusi na ngumu zilizong’aa. Mara nyingi sikuweza kula wakati nilipokuwa nimefungiwa, na mara chache, wafungwa wangenipa skonsi mbili ndogo. Mara nyingi wangekula sehemu yangu na yote niliyopata ilikuwa tumbo tupu. Nilipokea hata kinywaji kidogo zaidi; awali, kila mmoja alipewa tu bakuli mbili za maji kwa siku, lakini nilikuwa nimefungiwa na sikuweza kusogea, hivyo ni kwa nadra sana niliweza kunywa maji yoyote. Mateso hayo ya kinyama yalikuwa yasiyosemeka. Kwa ujumla, niliteseka hivi mara nne na kila mara nilikuwa nimefungiwa kwa siku zisizopungua tatu na zisizozidi nane. Kila wakati ambapo njaa haikuvumilika, ningefikiria maneno ambayo Mungu aliyasema zamani: “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu” (Mathayo 4:4). Hatua kwa hatua nilianza kutambua kwamba Mungu anataka kutimiliza ukweli kwamba “Neno Lake lakuwa uhai wa mwanadamu” kwangu kupitia mateso ya Shetani. Katika kuelewa mapenzi ya Mungu, moyo wangu uliokolewa na nikamwomba Mungu kwa amani na kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu. Pasipo kujua, sikuhisi uchungu sana tena au njaa. Hili kwa hakika lilinifanya nisihisi kuwa neno la Mungu ni ukweli, njia, na uzima na bila shaka ni msingi ambao napaswa kutegemea ili kuishi. Kwa hiyo, imani yangu kwa Mungu iliongezeka bila kujua. Nakumbuka wakati mmoja polisi wa gerezani kwa makusudi walinitesa na kunifunga pingu. Kwa siku tatu mchana na usiku sikunywa hata tone la maji. Mfungwa aliyekuwa amefungwa pingu karibu na mimi akasema: “Kulikuwa na mtu fulani wa umri mdogo kabla ambaye alifungwa pingu na kunyimwa chakula jinsi hii hadi kufa. Naona kuwa hujala chochote kwa siku kadhaa na bado una uchangamfu.” Katika kusikia maneno yake, nilifikiri kwamba ingawa sikuwa nimekula au kunywa chochote kwa siku tatu mchana na usiku, sikuhisi kero ya njaa. Nilihisi sana kwamba hii ilikuwa ni nguvu ya uzima katika maneno ya Mungu ikinisaidia na kunisababisha kwa hakika kuona Mungu akionekana kwangu katika maneno Yake. Moyo wangu ulikuwa na msisimko daima; katika mazingira haya ya mateso niliweza kwa kweli kupitia uhalisi wa ukweli kwamba “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.” Huu kwa kweli ni utajiri wa thamani zaidi wa maisha ambao Mungu ameniridhia, na pia ni zawadi yangu ya pekee. Aidha, singeweza kamwe kuupata katika mazingira ambayo sikuhitaji kuwa na wasiwasi juu ya chakula au nguo. Sasa, mateso yangu yalikuwa na maana nyingi sana na thamani! Wakati huu, sikuweza kujizuia kufikiria maneno ya Mungu: “Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la Mungu la mwisho, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili” (“Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kujaribu kuyaelewa maneno ya Mungu, nilitambua kwamba baada ya mateso na majaribu baraka huja kutoka kwa Mungu, na huu ndio ugavi wa mahitaji na umwagiliwaji wa maji kwangu kutoka kwa Mungu. Sasa, ingawa maneno ambayo Mungu amenipa yamepita vizazi vya watakatifu, bado nahitaji kuwa na imani na uvumilivu ili kuwa na uwezo wa kutokukubali kushindwa wakati wa majaribu na mateso yangu, kuitii mipango ya Mungu, na kupokea wokovu wa Mungu. Kisha nitaweza kuuingia uhalisi wa neno la Mungu na kuweza kuona matendo ya ajabu ya Mungu. Kama haingekuwa kwa gharama ya shida hii, singestahili kupokea ahadi na baraka za Mungu. Kupokea nuru ya Mungu kulinielekeza kuwa na udhabiti na nguvu zaidi ndani; niliweka azimio: Shirikiana na Mungu kwa bidii na kuyaridhisha mahitaji ya Mungu katikati ya mazingira haya machungu, kumshuhudia Mungu ili niweze kuwa na mavuno makubwa mno.
Mwezi mmoja baadaye, polisi wa CCP walinishtaki na “kushukiwa kuvuruga utaratibu wa jamii na kuharibu utekelezaji wa sheria”; nilihukumiwa mwaka mmoja wa mageuzi kupitia kazi. Nilipoingia kambi ya kazi, wale polisi waovu walieneza uvumi na upuuzi miongoni mwa wafungwa, wakisema kuwa nilikuwa muumini katika Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni baya kuliko mauaji na wizi, na waliwachochea wafungwa kunitesa. Kwa hiyo mara nyingi nilipigwa na kuwekwa katika hali ngumu na wafungwa bila sababu yoyote. Hili lilinifanya nione kweli kwamba China ni nchi ya mateso na maumivu inayoongozwa kwa uthabiti na Shetani, pepo. Kuna giza kutoka kila pembe, na hakuna mwanga unaoruhusiwa kuwepo; hakuna mahali kabisa pa waumini wa Mwenyezi Mungu kuishi. Wakati wa mchana, hao polisi waovu walinilazimisha kufanya kazi katika karakana. Kama sikufikia kiasi nilichopaswa kufikia, wangewaacha wafungwa wanipige wakati niliporudi kwa seli yangu gerezani na kutangaza “mfanyeni mfano ili kuwaogofya wengine.” Nilipokuwa katika karakana nikihesabu mifuko, ningehesabu mifuko 100 na kisha kuifunga pamoja. Wafungwa wangekuja daima na kutoa mfuko moja au kadhaa kutoka kwa ile niliyokuwa nimehesabu, kisha wangesema kwamba sikuhesabu vizuri na kuchukua hiyo kama fursa ya kunipiga ngumi na mateke. Wakati msimamizi huyo aliponiona nikipigwa, angekuja na kuniuliza kwa unafiki kilichokuwa kikiendelea na wafungwa wangewasilisha ushahidi wa uongo kwamba sikuwa nimehesabu mifuko ya kutosha. Kisha ningelazimika kustahimili mfululizo wa ukosoaji mkali kutoka kwa msimamizi. Aidha, wangeniamuru nikariri “amri za maadili mema” kila asubuhi, na kama sikuzikariri, ningepigwa; pia wangenilazimisha kuimba nyimbo zilizokisifu chama cha Kikomunisti. Kama waliona kwamba sikuwa nikiimba au kwamba midomo yangu haikuwa ikisonga, basi usiku bila shaka ningepigwa. Pia waliniadhibu kwa kunifanya nipanguse sakafu, na kama sikupangusa kwa matarajio yao, basi ningepigwa kwa nguvu nyingi. Wakati mmoja, kwa ghafla wafungwa fulani walianza kunigonga na kunipiga mateke. Baada ya kunipiga, waliniuliza: “Kijana, unajua kwa nini unapigwa? Ni kwa sababu hukusimama na kumsalimu msimamizi wakati alipokuja!” Baada ya kila wakati nilipopigwa, nilikuwa na hasira lakini sikuthubutu kusema chochote; niliweza kulia tu na kumwomba Mungu kimyakimya, nikimwambia Yeye juu ya chuki na malalamiko moyoni mwangu kwa sababu ya mahali hapa palipo na utovu wa sheria, na kukosa mantiki. Hapakuwa na busara hapa, palikuwa na vurugu tu. Kulikuwa hakuna watu hapa, kulikuwa na pepo wenye wazimu na nge tu! Nilihisi maumivu mengi sana na shinikizo nikiishi katika shida hii; sikuwa tayari kukaa hata dakika moja zaidi. Kila wakati nilipotumbukia katika hali ya udhaifu na maumivu, ningefikiri juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” (“Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinitia moyo. Bila kujali kama kile Mungu alichokuwa akinifanyia kilikuwa neema na baraka au majaribu na usafishwaji, yote ilikuwa ili kunikimu na kuniokoa; ilikuwa ni kuweka ukweli ndani yangu na kufanya ukweli kuwa maisha yangu. Leo, Mungu aliruhusu mateso haya na taabu zinijie. Ingawa jambo hili lilisababishia mateso mengi, liliniruhusu kuweza kwa kweli kuwa na uzoefu kwamba Mungu yu pamoja nami; lilinifanya kwa kweli nifurahie maneno ya Mungu kuwa mkate wa maisha yangu na taa ya miguu yangu na mwanga kwa njia yangu, likiniongoza hatua kwa hatua kupitia mahali hapa padhalimu na pasipovumilika. Huu ndio upendo na ulinzi wa Mungu ambao nilifurahia na kupata wakati wa mchakato wa mateso yangu. Wakati huu, niliweza kuona kwamba nilikuwa kipofu sana na wa ubinafsi na nilikuwa mwenye uroho mno. Katika kumwamini Mungu, nilijua tu jinsi ya kufurahia neema na baraka za Mungu na sikutafuta ukweli na uhai kwa kiwango hata kidogo. Mara mwili wangu uliopitia shida kidogo, ningenung’unika bila kukoma; sikuelewa kabisa mapenzi ya Mungu na sikutafuta kuielewa kazi ya Mungu. Daima ningemfanya Mungu ahisi huzuni na maumivu juu yangu. Kwa kweli nilikuwa bila dhamiri! Kwa majuto na kujilaumu, niliomba kimya kimya kwa Mungu: “Ewe Mwenyezi Mungu, naweza kuona kwamba kila kitu unachokifanya ni kuniokoa na kunipata. Ninachukia tu kwamba mimi ni mkaidi sana, ni kipofu na sina ubinadamu. Daima nimekuelewa visivyo na sijakuwa wa kufikiria mapenzi Yako. Ee Mungu, leo neno Lako limeuamsha moyo wangu wenye ganzi na roho yangu na limenisababisha kuyaelewa mapenzi Yako. Siko tayari tena kuwa na tamaa na mahitaji yangu mwenyewe; nitatii tu mipango Yako. Hata kama ni lazima nipitie matatizo yote, bado nitaendelea kushirikiana na Wewe kwa bidii na nitatoa ushahidi mkubwa sana Kwako muda wote wa mateso ya Shetani. Nitatafuta kujitenga na ushawishi wa Shetani na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu halisi ili kukuridhisha.” Baada ya kuomba, nilielewa nia njema za Mungu, na nilijua kwamba kila mazingira ambayo Mungu aliniruhusu kupitia yalikuwa ni upendo na wokovu mkubwa wa Mungu kwangu. Kwa hiyo, singefikiria tena kujikunyata au kumwelewa Mungu visivyo. Ingawa hali ilikuwa bado ni ile ile, moyo wangu kwa kweli ulijaa furaha na ridhaa; nilihisi kuwa ni heshima na fahari kuweza kupitia shida na mateso kwa sababu ya imani yangu kwa Mwenyezi Mungu, na ilikuwa ni zawadi ya pekee kwangu, mtu mpotovu; ilikuwa baraka maalumu na neema za Mungu kwangu.
Baada ya kuwa na uzoefu wa mwaka mmoja wa shida katika jela, naona kwamba mimi ni mdogo sana wa kimo na kwamba nakosa ukweli mwingi sana. Mwenyezi Mungu kwa kweli amefidia upungufu wangu kupitia mazingira haya ya kipekee na ameniruhusu kukua. Katika dhiki yangu, Amenifanya kupata utajiri wa thamani mno katika maisha na kuelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na kuona kwa dhahiri sura mbaya kwa Shetani, pepo, na kiini cha kupinga maendeleo cha upinzani wake kwa Mungu. Nilitambua uhalifu wake muovu wa kumtesa Mwenyezi Mungu na kuwaua Wakristo. Nilipitia kwa dhati wokovu na huruma kubwa Mwenyezi Mungu aliyokuwa nayo kwangu, mtu mpotovu, na nimehisi kwamba nguvu na maisha katika maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kunipa mwanga na kuwa maisha yangu na kunielekeza kumshinda Shetani na kwa ushupavu kutoka nje ya bonde la uvuli wa mauti. Vivyo hivyo, pia niligundua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeniongoza kwenye njia sahihi ya uzima. Ni njia ng’avu ya kupata ukweli na uzima! Kuanzia sasa na kwendelea, bila kujali ni mateso yapi, dhiki au majaribu hatari yanayonikabili, niko tayari kutafuta ukweli kwa bidii na kupata njia ya uzima wa milele ambayo Mwenyezi Mungu amenipa.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Ijumaa, 14 Juni 2019
Kuahidi Maisha Yangu kwa Moyo wa Ibada
Zhou Xuan Mkoa wa Shandong
Mnamo Aprili 3, mwaka wa 2003, niliambatana na dada mmoja kumtembelea muumini mpya. Muumini huyu mpya hakuwa na uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika siku za mwisho na aliishia kuturipoti. Kwa sababu hiyo, askari wanne waovu wenye nguo za raia walikuja na kwa ugomvi kutuingiza sisi wawili katika gari lao na kutupeleka kwa kituo cha polisi. Njiani, moyo wangu ulikuwa na wasiwasi mno, kwa sababu mwilini mwangu nilikuwa na peja ya mawasiliano, orodha isiyo kamili ya majina ya wanajumuiya wa kanisa letu, na daftari dogo. Niliogopa kwamba wale askari waovu wangeweza kugundua vitu hivi na niliogopa zaidi kwamba ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniita kupitia peja yangu ya mawasiliano, kwa hiyo mimi kwa mfululizo nilimwomba Mungu kwa haraka moyoni mwangu: “Mungu, ninapaswa kufanya nini? Ninakuomba Unipe suluhisho na usiruhusu vitu hivi viingie mikononi mwa askari hawa waovu.” Baada ya hili, nilichukua vitu hivi kutoka kwa mkoba wangu na kwa kimya kuviweka kiunoni mwangu na kusema kwamba tumbo langu liliuma na nilihitaji kutumia msala. Wale askari waovu wakaniapizia wakisema: “Wewe umejaa upuuzi!” Baada ya maombi yangu ya mara kwa mara, walimtaka askari mmoja wa kike anichunge nilipokwenda msalani. Nilipouondoa mshipi wangu, kifaa changu cha mawasiliano kilianguka na kwa urahisi nikakiokota na kukitupa katika bomba la maji taka. Kwa sababu niliogopa wakati huo kwamba huyo afisa wa kike angegundua mkoba kiunoni mwangu, sikuutupa katika bomba, lakini badala yake niliutia katika pipa la taka; nilidhani kwamba ningetumia msala tena usiku na kisha kuutupa ndani ya choo. Ilivyotukia, sikurudi kwa msala huo kamwe. Ilitukia kuwa wale askari waovu waliupata ule mkoba niliokuwa nimeutupa katika jaa la taka.
Wale askari waovu wakatufungia yule dada na mimi katika chumba kimoja na kutulazimisha tuvue nguo zetu zote ili waweze kutupekua. Walipekua hata kwa nywele zetu kuona kama tulificha chochote. Baada ya kumaliza kutafuta, walitutia pingu na kutufungia katika kile chumba. Ilipofika usiku, wale askari waovu walitutenganisha ili tuhojiwe kwa makini; waliniuliza: “Unatoka wapi? Jina lako ni nani? Ulikuja hapa lini? Unafanya nini hapa? Unaishi wapi? Unaamini nini? Jina la mtu uliye naye ni nani?” Kwa sababu hawakuridhishwa na majibu yangu, wale askari waovu walisema hivi kwa hasira: “Sisi huonyesha upole kwa wale wanaokiri na ukali kwa wale wanaobisha. Usiposema ukweli, utajilaumu mwenyewe! Sema! Ni nani anayekusimamia? Unafanya nini? Sema na tutakutendea kwa upole.” Nilivyoona jinsi walivyoonekana wakali kishetani, nilifanya uamuzi kwa kimya: kabisa sitakuwa Yuda, sitawasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike na sitazisaliti nia za familia ya Mungu. Walipoona kwamba hawakuweza kupata chochote kutoka kwangu, waliingiwa na wasiwasi na kuanza kunigonga na kunipiga mateke kwa ukali wakisema: “Kwa kuwa husemi chochote, tutakuadhibu kwa kukunyosha mikono na miguu!” Kisha ghafla kulikuwa na mlipuko mwingine wa kupigwa ngumi na mateke kwa ukali sana. Baadaye, mmoja wao akaniamuru niketi chini, na akanitia pingu na kuipinda mikono yangu kwelekea nyuma yangu kwa kukaza alivyoweza. Kisha akaweka kiti nyuma yangu na kutumia kamba kuifunga mikono yangu nyuma ya kiti. Alitumia mikono yake na akawekea nguvu zake zote kwelekea chini, akiweka shinikizo juu ya mikono yangu. Mara moja, mikono yangu ikahisi kama ingevunjika; iliumia vibaya sana hivi kwamba nilitoa yowe kali. Walikwenda mbele na nyuma jinsi hii kwa mikono yangu wakiniumiza bila kukoma kwa muda wa saa kadhaa. Baadaye, sikuweza kuvumilia na nilitikisika kutoka utosini hadi kidoleni. Walipoona hayo, wakasema: “Usijifanye kana kwamba wewe ni wazimu, tumeona hili mara nyingi kabla. Je, unadhani unamshtua nani? Je, unadhani kuwa kufanya hivi kutakuondoa kwa tatizo hili?” Waliona kwamba bado nilikuwa nikitikisika na askari mmoja mwovu akasema: “Nenda naye msalani na kumtia kinyesi kiasi kinywani mwake, angalia kama atakila au la.” Walitumia kijiti kuchotea kinyesi kiasi na kukifikicha ndani ya kinywa changu na kunifanya nikile; nilikuwa bado nikitoa pofu kwa kinywa na waliona kwamba bado nilikuwa nikitikisika, kwa hiyo waliniacha nishuke kutoka kwa kiti. Mwili wangu mzima uliumia bila kuvumilika kama kwamba nilikuwa na mito kutoka utosini hadi kidoleni na nilitoa yowe kwa maumivu nilipolala sakafuni nikiwa nimeduwaa. Baada ya muda mrefu, viganja vyangu na mikono viliaanza kusogea tena. Polisi hao waovu waliogopa kwamba ningegonga kichwa changu kwa ukuta na kujiua, kwa hiyo walinipa helmeti. Baadaye, waliniburuta na kunirudisha kwa kile chumba kidogo cha chuma. Nililia na kumwomba Mungu: “Ewe Mungu, mwili wangu ni dhaifu sana. Natamani kuwa Unilinde. Bila kujali jinsi Shetani anavyonitesa, ningependelea kufa kuliko kukusaliti Wewe kama Yuda. Sitawasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike au maslahi ya familia ya Mungu. Niko tayari kuwa shahidi Kwako ili kumuaibisha yule Shetani mzee.”
Siku ya tatu, wale askari waovu walichukua ile daftari dogo na orodha ya majina ya wanajumuiya wa kanisa niliyokuwa nimeitupa katika jaa la taka na kunihoji. Nilipoona vitu hivi, nilihisi hasa kutokuwa na raha na kujaa kujilaumu na majuto. Nilichukia kwamba nilikuwa na hofu sana na mwoga na kwamba sikuwa na ujasiri wa kutosha wakati huo wa kutupa mkoba ndani ya bomba la maji taka, jambo lililosababisha matokeo haya ya hatari. Nilichukia hata zaidi kwamba sikusikiliza mipango ya familia ya Mungu na kuleta vitu hivi wakati wa kutimiza wajibu wangu, jambo ambalo limelisababishia kanisa tatizo hili kubwa. Nilijua kwa kina kwamba nilistahili mateso niliyokuwa nikiyapitia siku hii na kwamba ilikuwa ni kuadibu kwa Mungu na hukumu vikinijia, na nilikuwa radhi kuvikubali. Nilikuwa radhi pia kumtegemea Mungu ili kumshinda Shetani. Wakati huu nilifikiri juu ya wimbo: “Sijali kuhusu njia iliyo mbele; ni kutenda tu mapenzi ya Mungu kama wito wangu. Wala sijali juu ya mustakabali wangu. Kwa kuwa nimechagua kumpenda Mungu, nitakuwa mwaminifu mpaka mwisho. Bila kujali jinsi hatari na shida zilivyo kubwa, au jinsi njia iliyo mbele ilivyo na mashimoshimo na ya kuparuza, kwa kuwa ninalenga siku ambayo Mungu atapata utukufu, nitatelekeza kila kitu na kujitahidi kwenda mbele” (“Kutembea Kama Askari kwa Njia ya Kumpenda Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Niliuimba wimbo huu kimya kimya na moyo wangu ulikuwa na imani na nguvu tena. Wale askari waovu wakaniuliza: “Je, vitu hivi ni vyako? Sema ukweli nasi, hatutakutendea bila haki. Wewe ni mwathirika na umedanganywa. Dini yenu ni Xie Jiao; Mungu mnayemwamini ni Mungu asiye dhahiri na yu mbali, ni ndoto za mchana. Chama cha Kikomunisti ni kizuri, na unapaswa kutegemea hicho chama na serikali. Ukiwa na shida yoyote, unaweza kuja kwetu na tutakusaidia kuitatua. Ukihitaji usaidizi kupata kazi, tunaweza kukusaidia pia. Kiri tu kila kitu juu ya kanisa lako; tuambie kile watu hawa walio kwa orodha yako wanachofanya. Wanaishi wapi? Ni nani mkuu wenu?” Nilitambua hila zao za uwongo na kusema: “Vitu hivi si vyangu, sijui.” Walipoona kwamba singefichua chochote, basi ilifichuka ni watu wa aina gani kamili na walinipiga kikatili na kuniangusha chini na kuendelea kunipiga kwa ukali sana na kutumia nguvu zao zote kuniburuta huku na huko wakitumia pingu zangu. Jinsi walivyozidi kuniburuta, ndivyo pingu zilivyozidi kujikaza na kuukata mwili wangu. Niliumia vibaya sana kiasi cha kulia kwa sauti kubwa na wale askari waovu wakasema kwa ukali: “Tutakufanya uonge, tutakuminya kidogo kidogo kama dawa ya meno ili kukufanya uzungumze!” Hatimaye, walichukua mikono yangu miwili na kuifunga ikielekea nyuma kwa kiti na kunifanya nikalie sakafu. Walinigonga na kuwekea nguvu zao na kugandamiza kwelekea chini juu ya mikono yangu; nilihisi maumivu yasiyovumilika na uchungu uliochoma kana kwamba mikono yangu ingevunjika. Wale askari waovu walinitesa na kunikemea: “Sema wazi!” Bila kusita nikasema: “Sijui!” “Usiposema wazi tutakuua; usiposema wazi basi usitarajie kuishi; tutakufunga jela kwa miaka kumi, miaka ishirini, maisha yako yote; usitarajie kutoka jela kamwe!” Niliposikia hivi, wazo fulani likanijia akilini mwangu ghafla: ni lazima niamue kuwa tayari kwenda jela maisha. Baadaye nilifikiri juu ya wimbo wa uzoefu: “Toa sadaka ya kupendeza mno kwa Mungu, nijidunduizie ile chungu zaidi. Simama na kwa uthabiti ushuhudie kwa Mungu, usikubali kushindwa na Shetani. Aa! Huenda vichwa vikavunjika na damu kuvuja, lakini hadhi ya watu wa Mungu haiwezi kupotea. Imani ya Mungu hupumzika kwa moyo, ni lazima niamue kumdhalilisha Shetani mzee” (“Ninataka Kuona Siku Ambapo Mungu Atapata Utukufu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Mungu alinipa nuru, akinifanya niwe imara na kuwa na ujasiri na akinipa imani na uamuzi kupitia kila kitu na kuwa shahidi kwa Mungu. Kwa sababu hiyo, hila za hao askari waovu hazikushinda; walinitesa mpaka wakachoka, kisha wakanirudisha kwa chumba cha chuma.
Siku chache baadaye, niliteswa na hao askari waovu mpaka nikawa sina nguvu. Nilikuwa katika mpagao wa usahaulifu kabisa na mikono yangu ilikuwa na ganzi. Katika kukabiliana na mateso haya katili na ya kinyama, niliogopa hasa kwamba hao askari waovu wangerudi na kunihoji. Mara tu nilivyofikiria hili, moyo wangu haukuweza kujizuia kutetemeka kwa hofu. Kwa kweli sikujua ni nini kingine wangetumia kunitesa, na sikujua ni lini masaili haya yangeisha. Niliweza tu kuendelea kuomba ndani ya moyo wangu kwa Mungu na kumwomba Mungu kuulinda moyo wangu na kunipa hiari na nguvu za kuvumilia mateso ili ningeweza kuwa shahidi kwa Mungu na kumfanya Shetani ashindwe kwa fedheha kamili.
Wakati wale askari waovu walipoona kuwa singekiri, waliungana na Brigedi ya Usalama wa Taifa na Shirika la Usalama wa Umma ili kunihoji. Kulikuwa na watu zaidi ya ishirini huko wakishika zamu kunihoji mchana na usiku wakijaribu kunilazimisha kukiri. Siku hiyo, askari wawili waovu kutoka kwa Brigedi ya Usalama wa Taifa ambao tayari walikuwa wamenihoji mara moja kabla walinijia na mwanzoni walizungumza kwa huruma wakisema: “Ukikiri ukweli, basi tutakuacha uende na tutahakikisha usalama wako. … Ni chama cha Kikomunisti tu kinachoweza kukuokoa, na Mungu hawezi kukuokoa ….” Wakati mmoja wao alipoona kwamba singetamka neno, aliingiwa na wasiwasi na kuanza kunipigia yowe kwa maneno machafu, akinilazimisha niketi sakafuni. Alinipiga teke kwa miguuni kwa nguvu alivyoweza akitumia viatu vya ngozi akisababisha maumivu yasiyoweza kustahimilika. Askari mwingine muovu akamwuliza: “Kunaendaje, anazungumza?” Alisema: “Yeye ni mkaidi sana, bila kujali unampiga kiasi gani na hatazungumza.” Huyo mtu akasema kwa ukali: “Kama hazungumzi, basi mpige hadi afe!” Yule askari muovu akanitishia akisema: “Hutazungumza? Basi tutakuua!” Nikasema: “Nimesema kila kitu ambacho nilihitaji kusema, sijui!” Alikasirika sana kiasi kwamba alionekana kuwa wazimu kabisa, kisha akanguruma kama mnyama wa mwitu na kuanza kunichapa na kunipiga mateke. Hatimaye alipata uchovu kwa kunipiga na kupata kamba kiasi cha unene wa kidole na kuiviringishia mkononi mwake mara chache. Kwa ukatili aliupiga uso wangu mijeledi tena na tena akisema: “Je, wewe humwamini Mungu? Wewe unateseka, kwa nini Mungu wako haji na kukuokoa? Kwa nini Yeye haji na kukufungua pingu? Mungu wako yuko wapi?” Niliyakereza meno yangu na kuvumilia maumivu. Niliomba kwa utulivu moyoni mwangu kwa Mungu: “Ee Mungu, ninapitia shida hii kwa sababu ya uasi wangu; ni kile ninachostahili. Mungu. Wakinipiga hadi kufa leo, kamwe sitakuwa kama Yuda. Nataka Uwe pamoja nami na kuulinda moyo wangu. Niko tayari kutoa maisha yangu ili kuwa shahidi Kwako na kumfedhehesha Shetani mzee.” Nilifikiria kuhusu wimbo: “Hakuna huruma katika kifo, na hakuna mshangao kwa hilo. Mapenzi ya Mungu huzidi yote. … Mungu aliniokoa na ameniwasilisha kwa Shetani, haya ndiyo mapenzi mazuri ya Mungu; moyo wangu utampenda Mungu wangu milele” (“Rudisha Upendo kwa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilifunga macho yangu na kuvumilia mateso ya Shetani na kupigwa. Wakati huo, ilikuwa ni kama nilisahau kuhusu maumivu yangu. Sikujua ni wakati upi mateso hayo yangeisha. Sikuthubutu kulifikiria, na sikuweza hata kutafakari juu ya hilo. Kitu pekee ambacho niliweza kufanya ni kusali bila kukoma na kumlilia Mungu. Maneno ya Mungu pia yalinipa imani ya mfululizo: “Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu” (“Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Msiwe na hofu ya wao wanaoua mwili, lakini hawana uwezo wa kuifisha roho: ila heri uwe na hofu ya yeye anayeweza kuiangamiza roho pamoja na mwili katika kuzimu” (Mathayo 10:28). Nilifikiri kuhusu jinsi joka kubwa jekundu lilikuwa tishio la bure tu lililoandikiwa kushindwa na mikono ya Mungu. Kama Mungu hakuyaruhusu, mauti hayangenijia; bila ruhusa ya Mungu, hakuna hata unywele wangu mmoja ungepotea. Pia nilifikiria kuhusu maneno haya ya Mungu: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” (“Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Nguvu ya neno la Mungu haina mipaka na imesababisha imani yangu kuongezeka; nilikuwa na azimio la kupambana na Shetani hadi mwisho. Yule askari muovu alipochoka kunipiga, aliniuliza tena: “Je, utasema?” Nilisema kikiki: “Hata ukinipiga hadi nife, bado sitajua!” Yule askari muovu aliposikia hayo, hakuweza kufanya chochote. Akatupa kamba na kusema: “Wewe ni mkaidi kweli, kama nyumbu. Kwa kweli wewe ni mzuri, huwezi kusema chochote hata ukifa. Ulipata kutoka wapi nguvu na imani nyingi jinsi hii? Wewe kwa kweli ni Liu Hulan zaidi ya Liu Hulan” Nilipomsikia akisema haya, ilikuwa ni kama nilimwona Mungu ameketi kwenye kiti Chake cha enzi kwa ushindi, akimwangalia Shetani akifedheheshwa. Nililia nusu na kumtukuza Mungu nusu: Ee Mungu, kwa kuitegemea nguvu Yako, ninaweza kumshinda Shetani, yule pepo! Kwa sababu ya ukweli huo, naona kwamba Wewe ni mwenye kudura na Shetani hana nguvu; Shetani daima atashindwa chini ya udhibiti Wako. Usipomruhusu, Shetani hataweza kunitesa hadi nife. Wakati huu, maneno ya Mungu yalinipa nuru tena: “Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa wale walio hai miongoni mwa vitu vyote, kwa Bwana wa viumbe vyote…. Tabia yake ni ishara ya mamlaka … ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui …” (“Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kupitia mateso katili ya joka kubwa jekundu, kwa kweli niliona upendo wa Mungu na wokovu kwangu na nilipitia nguvu na mamlaka ya neno la Mungu. Bila neno la Mungu kuniongoza kila hatua ya njia na kwa kutegemea tu nguvu yangu mwenyewe, haingewezekana kwangu kuyashinda mateso na kupigwa kwa joka kubwa jekundu. Vivyo hivyo, lilinifanya nione taswira yenyekuweza kudhuruiwa na iliyopondwapondwa ya joka kubwa jekundu. Nilikielewa kiini cha pepo cha unyama walo na kutojali kwalo kwa uhai na nililichukia na kulilaani ndani ya moyo wangu. Nilipenda kuvunja kabisa uhusiano wote nalo na kumfuata Kristo na kumtumikia Kristo milele.
Siku iliyofuata, askari waovu walikuja na kunihoji tena, kwa kweli walishangaa na kusema: “Ni nini kibaya na uso wako?” Nilipotazama katika kioo, sikuweza kujitambua; askari muovu alikuwa ameupiga uso wangu mijeledi kwa kamba siku iliyopita na ulikuwa umevimba sana na kuwa mweusi na bluu na kuwa kama panda. Nilipoona kuwa uso wangu ulikuwa umebadilika kabisa mpaka kutotambulika, nilihisi chuki kali kwa joka kubwa jekundu na nikafanya azimio langu kuwa shahidi. Sikuweza kabisa kuruhusu njama yake ishinde! Miguu yangu ilikuwa imepigwa vibaya sana kiasi kwamba sikuweza kutembea na wakati nilipokwenda msalani, niliweza kuona kwamba miguu yangu yote haikuwa na hali ya kawaida iliyobaki, kila kitu kilikuwa cheusi na bluu. Mmoja wa askari waovu akasema: “Hakuna haja ya wewe kuteswa hivi; ukiongea basi hutahitaji kuteseka; unajifanyia hivi mwenyewe! Lifikirie; kiri na tutakutuma nyumbani kwa mumeo na binti yako.” Baada ya kumsikia akisema haya, nilimchukia kabisa. Baadaye, walibadilisha mbinu zao na wakaanza kushika zamu kwa kutoniruhusu nilale mchana kutwa na usiku kucha. Nilipoanza kulala, wangepiga yowe na kupiga kelele kubwa ili kuniamsha; walijaribu kuivunja dhamira yangu kwa kutoniruhusu kulala ili nizungumze kwa usahaulifu, katika hali ya akili isiyobainika. Nilimshukuru Mungu kwa kunilinda. Ingawa wale askari waovu waliniweka kwa muda wa siku nne mchana na usiku, haikujalisha jinsi walivyonihoji, nilimtegemea Mungu kwa ustahimilivu na imani, na sio tu kwamba sikuwa na usahaulifu, lakini nilikuwa macho mno. Askari waovu waliponihoji tena na tena, wakasononeka zaidi na zaidi na wakawa wenye kukata tamaa. Walianza kutekeleza masaili ya shingo upande; walitoa matusi na kulalamika, walikasirikia kwamba nilikuwa nimewasababisha kupoteza hamu yao ya kula, kutopata mapumziko mazuri, na kuteswa na mimi, walihisi kuwa walikuwa na bahati mbaya sana. Hatimaye, yote waliyofanya yalikuwa kuniuliza maswali ya kawaida na hawakuwa tena na utashi wa kunihoji. Katika duru hii ya vita Shetani aliishia kushindwa tena.
Askari waovu hawakuachia hapo, walijaribu kunitongoza. Askari mmoja muovu alikuja na kuweka vidole chini ya kidevu changu, akachukua mkono wangu na kusema jina langu. Kwa sauti ya “upendo” akasema: “Wewe ni mzuri sana; haina thamani kuteseka sana hapa. Matatizo yoyote uliyo nayo, naweza kukusaidia kuyatatua. Imani yako kwa Mungu haijakupatia kitu. Nina nyumba mbili, siku moja, nitakuleta huko ili uwe na burudani; sisi wawili tunaweza kutengeneza ubia. Ukikiri, basi utakuwa huru. Chochote unachotaka, naweza kukusaidia. Sitakutendea bila haki….” Niliposikia uongo wake mbaya, mchafu sana, nilijihisi kuchafuka moyo na kwa nguvu zote nilimkataa. Hakuwa na chaguo jingine bali kuondoka kwa aibu. Hili lilinifanya niwaelewe kabisa hawa watu waliolaaniwa na wasio na aibu wanaodaiwa kuwa “polisi wa watu.” Ili kupata malengo yao wenyewe, wao hutumia mbinu zilizolaaniwa na za kishenzi bila aibu yoyote; hawana heshima yoyote au uadilifu; kwa kweli wao ni pepo wabaya na wachafu!
Hao askari waovu walikuwa na njama moja ya ujanja baada ya nyingine na waliitumia vibaya watu wa familia yangu kujaribu kunishurutisha, wakisema: “Unamwamini Mungu tu, hufikirii juu ya mume wako, binti, wazazi, na watu wengine wa familia; binti yako atakwenda shuleni siku fulani na kutafuta kazi. Unaamini katika Xie Jiao na hili litaathiri moja kwa moja matarajio yake ya mustakabali. Je, utaruhusu hili lifanyike kwake? Wewe humfikirii; Je, una moyo mgumu wa kumruhusu ahusike katika hili?” Kufuatia hili, walimleta mume wangu, binti, na shangazi ndani ili kuwaacha wajaribu kunishawishi. Nilipomwona binti yangu ambaye sikuwa nimemwona kwa miaka kadhaa, machozi yangu yalitiririka bila kuzuilika. Wakati huu, niliomba kwa nguvu zangu zote kwa Mungu: “Ee Mungu, nakuomba Uulinde moyo wangu, kwa sababu mwili wangu ni dhaifu mno. Wakati huu, siwezi kukamatwa na hila za Shetani na siwezi kujaribiwa na Shetani kuanguka katika hisia zangu; Siwezi kumsaliti Mungu au kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike; namwomba tu Mungu awe pamoja nami na kunipa imani na nguvu.” Shangazi akaniambia: “Fanya haraka na uzungumze, kwa nini wewe ni mjinga hivi? Ina thamani yoyote kupitia hili kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Ni nani atakayekushughulikia iwapo chochote kitatokea? Mama yako na baba yako wanahangaika juu yako, wana wasiwasi kila siku kukuhusu, hawawezi kula au kulala vizuri. Ni lazima utufikirie na urudi na kuishi maisha na sisi. Usimwamini Mungu. Angalia ni shida gani ulizopitia kwa sababu ya imani yako kwa Mungu; kwa nini unajisumbua?” Ingawa nilikuwa dhaifu, nililindwa na Mungu na nilitambua kuwa hili lilikuwa pambano la kiroho na niliweza kugundua hila za Shetani; maneno ya Mungu yalinikumbusha moyoni mwangu kwamba: “… lazima umridhishe Mungu licha ya kutotaka kuacha kitu chochote unachopenda, au kilio cha uchungu” (“Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, nilimwambia: “Shangazi, usijaribu kunishawishi, nimesema kila kitu ninachopaswa kuwaambia. Sijui nini kingine ninachopaswa kuwaambia. Wanaweza kunitendea kwa hali yoyote wanayotaka, ni juu yao. Hupaswi kujali kunihusu. Unapaswa kurudi!” Wakati wale askari waovu walipoona mwelekeo wangu imara, hawakuwa na uchaguzi mwingine bali kuiruhusu familia yangu irudi. Njama na mipango ya hao polisi waovu zilikuwa zimeshindwa, na walikuwa na hasira sana kwambawalisaga meno yao na kusema: “Kwa kweli wewe ni mkatili! Wewe una ubinafsi sana. Kwa hakika huna asili ya binadamu. Mungu wako yuko wapi? Kama Yeye ni mwenyezi sana, basi kwa nini Anaruhusu uteswe hapa? Kwa nini Mungu wako haji na kukuokoa? Kama kwa kweli kuna Mungu, basi kwa nini Yeye haji na kufungua pingu zako na kukuokoa? Mungu yuko wapi? Usidanganywe na uongo huu, usiwe mjinga. Hujachelewa mno kuamka na kuuona ukweli. Usipokiri, basi tutakupeleka gerezani kwa miaka mingi!” Uongo wa askari hawa waovu ulinifanya nifikirie kuonekana kwa Bwana Yesu akisulubishwa msalabani. Mungu mwenyewe alikuja na kuwa mwili ili kuwakomboa wanadamu wote; kila kitu Alichokifanya kilikuwa ni kwa manufaa ya mwanadamu; hata hivyo, alidhihakiwa, kukashifiwa, kushtakiwa, kukufuriwa, kutukanwa, na kuuawa na Mafarisayo na wale waliokuwa na mamlaka. Mungu alipitia fedheha mno ili kuwaokoa wanadamu, na hatimaye alitundikwa msalabani kwa ajili ya wanadamu. Maumivu yote ambayo Mungu alipitia ni kwa ajili ya wanadamu na leo maumivu ninayoyapitia ni maumivu ninayohitaji kuyapitia. Kwa sababu nina sumu ya joka kubwa jekundu, Mungu anatumia mazingira haya kwa upande mmoja ili kunipima, na kwa upande mwingine ili kuniruhusu kuelewa kwa hakika asili mbaya ya joka kubwa jekundu na, kulidharau na kulisaliti joka kubwa jekundu, na kumfuata Mungu kikamilifu. Kama vile tu neno la Mungu linavyosema: “Mungu anakusudia kutumia sehemu ya kazi ya pepo wachafu ili kuikamilisha sehemu ya mwanadamu, ili watu hawa waweze kufahamu matendo ya mapepo, na kuwawezesha watu wote wawafahamu kwa kweli mababu zao. Ni wakati huo tu ndipo wanadamu wanaweza kujinasua, sio tu kuwatoroka watoto wa mapepo, lakini hata zaidi mababu zao. Hili ndilo kusudi la asili la Mungu kulishinda kabisa joka kubwa jekundu, kufanya hivyo ili wanadamu wote wajue umbo halisi la joka kubwa jekundu, Aambue kinyago chake kabisa, na kuona umbo lake halisi. Hili ndilo Mungu anataka kutimiza, nalo ni lengo Lake la mwisho duniani ambalo Amefanyia kazi nyingi sana; Ananuia kulifanikisha hili ndani ya watu wote. Hili linajulikana kama ushawishi wa vitu vyote kwa ajili ya kusudi la Mungu” (“Sura ya 41” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili).
Hatimaye, wale askari waovu walinipeleka kwa kituo cha kizuizi na kunizuia kama mhalifu kwa mwezi mmoja. Katika mwezi huu, walinihoji mara moja zaidi. Kwa siku mbili mchana na usiku, hawakuniacha nilale na hawakunipa chakula cha kutosha. Wakati mwingine hawakunipa chakula chochote, lakini bado ilikuwa bure. Joka kubwa jekundu huwatesa na kuwaumiza watu jinsi hii bila kikomo! Wakati kuzuiliwa kwangu kulipofikia kikomo, walinihukumu miaka miwili ya marekebisho kupitia kwa kazi kwa “kuamini katika Xie Jiao na kuvuruga utaratibu wa jamii” bila ushahidi wowote. Kabla ya kwenda kambi ya kazi, familia yangu ilinitumia yuan 2,000 kwa ajili ya gharama za maisha, lakini zote zilibadhiriwa nao. Pepo hawa walikuwa kweli Shetani na pepo wabaya ambao walikuwa na kiu ya damu na uhai wa binadamu. Ulikuwa ni uovu kabisa! Katika nchi ya joka kubwa jekundu, hakuna sheria; chochote linachopinga, linaweza kuchinja na kunyonya lipendavyo; linaweza kuanzisha mashtaka ya jinai linavyotaka ili kuwadhibiti watu na kuwatesa watu. Joka kubwa jekundu huwasingizia na kuwanasa watu, huwaua watu wasio na hatia, hufanya kitu duni kuwa muhimu, na bila haki huwapachika watu sifa. Wao ni dhehebu halisi na la kweli, wao ni kikundi cha wahalifu wenye utaratibu na majambazi ambao huleta majanga na maafa kwa wanadamu. Kwa miaka miwili katika kambi ya kazi, niliona askari waovu wa serikali ya Kichina kimsingi huwadhulumu vibaya na kuwaamrishaamrisha wafanya kazi kama watumwa. Waliwalazimisha watu kula skonzi zilizookwa kwa mvuke na mchuzi wa mboga kila siku; mchana na usiku, walitulazimisha tufanye kazi ya ziada. Nilichoka kwa namna isiyovumilika kila siku na sikupokea fidia yoyote. Nilipokosa kufanya kazi nzuri, ningepata ukosoaji mkali na adhabu (vifungo virefu, kunyimwa chakula, kulazimishwa kusimama kimya). Wakati huu, hao askari waovu bado hawangeniruhusu niende, walinihoji wakijaribu kunilazimisha kukiri mazingira ya kanisa. Nililichukia vikali, nikitegemea imani na nguvu kutoka kwa Mungu, nikasema kwa hasira: “Mmenipiga na kuniadhibu; mnataka nini kingine? Nimesema kila kitu ninachopaswa kusema; mnaweza kunihoji kwa miaka kumi, miaka ishirini, na bado sitajua chochote. Mnaweza kusahau kuhusu hilo!” Waliposikia hili, wakasema kwa ghadhabu: “Huwezi kuponyeka, unaweza kusubiri hapa tu!” Hatimaye, hao askari waovu waliondoka kwa aibu na kushindwa.
Baada ya kupitia mateso ya kinyama ya joka kubwa jekundu na matendo ya kikatili pamoja na kuishi bila haki gerezani kwa miaka miwili, niliona kwa dhahiri kwamba tabia ya joka kubwa jekundu ni uongo, uovu, kiburi, na ukali. Ni chini ya mifugo. Wao hufikia kiwango cha kuweka mabango yakisema “uhuru wa kidini,” kisha wanakwenda huku na huko wakiwafuatilia na kuwatesa wateule wa Mungu kwa kila njia iwezekanayo. Wao kwa wayowayo huivuruga na kuivunja kazi ya Mungu. Wao ni wauaji ambao huua bila kupepesa jicho, wao ni majambazi ambao hupora kwa kisingizio cha “sadaka, haki, amani, na uadilifu.” Mwishowe, barakoa zao zimeambuliwa kabisa kupitia hekima ya kazi ya Mungu, na nyuso zao mbaya za pepo zimefunuliwa katika mwanga ili niweze kufungua mawanda yangu ya maono na kuamka kutoka katika ndoto yangu. Kama vile tu neno la Mungu linavyosema: “Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila kona, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi[b] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida[c]. Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi!” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Mwenyezi Mungu milele ni mwenye hekima, mwenye kudura na wa ajabu, na Shetani, joka kubwa jekundu, milele ni wa kusikitisha, mchafu na asiyeweza. Bila kujali jinsi alivyo mshenzi na mkosa nidhamu, na bila kujali jinsi hujitahidi na kuasi, daima atakuwa chombo cha Mungu kuwafundishia watu Wake wateule. Aidha, limehukumiwa kubagwa kuzimu na Mungu kama adhabu ya milele. Linajaribu kuvunja dhamira ya watu kupitia mateso yake ya kinyama ili watu waweze kujitenga na Mungu na kumtelekeza Mungu. Lakini limekosea! Mateso yake hutufanya tuone kwa usahihi kiini cha pepo. Ni jambo linalotuamsha kabisa kulisaliti kabisa na kuwa na imani na ujasiri kumfuata Mungu kwenye njia sahihi ya uzima. Daima nitamtegemea Mungu mwenye busara na mwenyezi. Kuanzia sasa kwendelea, bila kujali ni hatari zipi kemkem na shida zilizo kwa njia iliyo mbele, nitamfuata Mungu kwa uthabiti mpaka mwisho na kuwa na ushuhuda wa nguvu Kwake ili kuliaibisha joka kuu jekundu.
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “kutoweza kuwa.”
b. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo shetani hutumia huwadhuru watu.
c. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo shetani hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Alhamisi, 6 Juni 2019
Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu
Xiaoyan Jiji la Xinyang, Mkoa wa Henan
Nilikuwa na ubia wa kazi wa karibu na dada mmoja mzee katika masuala ya jumla. Baada ya kufanya kazi naye kwa muda fulani, nikamwona kuwa mzembe katika kazi yake na kwamba hakukubali ukweli. Kikwelikweli, nilikata kauli kumhusu. Hatua kwa hatua, uhusiano wa kawaida kati yetu ulipotea, hatukuweza kupatana vizuri, na hatukuweza kuwa mbia katika kazi. Nilihisi kuwa lilikuwa ni kosa lake hasa kwamba uhusiano wetu ulifikia kiwango hiki, na hivyo nilijaribu kufikiria njia za aina zote za kuzungumza naye ili apate kujijua. Lakini majaribu yangu yote ya kuzungumza naye yalikuwa bure au hata kuwa na athari za mkabala. Hatimaye tukaachana, kama masuala yetu hayajatatuliwa. Hili lilinifanya kuamini hata zaidi kuwa hakuwa mtu ambaye hukubali ukweli. Baada ya hapo, kanisa lilinipangia kukaa na familia mwenyeji tofauti. Baada ya muda mfupi, niligundua matatizo mengi pia yalikuwa na ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji, na mimi tena “nikajitahidi” kuwasiliana nao, lakini jitihada zangu zote hazikufaa, na wakaanza kuwa na chuki dhidi yangu. Nikiwa nimekabiliwa na hali hizi, nilikuwa na wasiwasi sana na kukanganyika: Mbona watu ninaokutana nao hawakubali ukweli? Mpaka siku moja, nikapata chanzo cha tatizo wakati nilipotatizika kazini.
Siku moja, kiongozi huyo akanipangia nimtumie mpango wa kazi, na nikamuaminisha huyo dada mzee kumpelekea. Nani angejua kwamba wiki moja baadaye, hicho kifurushi kingerejeshwa kwangu kama hakijafunguliwa. Nikiwa nimekabiliwa na hali hii, nilishtuka na kumlaumu yule dada mzee kwa sababu ya kushughulikia vibaya jambo hilo, jambo lililosababisha kifurushi kutopelekwa kwa kiongozi. Hakukuwa pia na mawasiliano yoyote kutoka kwa kiongozi kwa siku chache baada ya hili, na nilikuwa ninaanza kuwa na wasiwasi: Kwa kawaida ikiwa kitu kinakosa kutumwa au kinatumwa kama kimechelewa, kiongozi atapiga simu kuuliza kuhusu hali hiyo. Kwa nini hajawasiliana nami wakati huu? Anajaribu kunizuia kutekeleza wajibu wangu? Nikaanza kuwa na hofu zaidi na zaidi—mawazo yangu yalijaa wasiwasi na majuto. Sikuweza kujizuia kuanguka mbele ya Mungu, “Mungu, najihisi mgonjwa sana na kuwa na mgongano moyoni mwangu. Mpango wa kazi umerudishwa kwangu kama haujafunguliwa. Sijui kinachoendelea, na sijui ni kipengele gani changu kitakachokamilishwa katika kukumbwa na hali hii. Tafadhali niongoze na kunipa nuru na kunisaidia kuelewa mapenzi Yako.” Mara baada ya sala, mojawapo ya virai vya Mungu kiliendelea kunijia kichwani mwangu, “Wakati wowote unapofanya kitu kinaenda mrama au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu” (“Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili). Niligundua kwa ghafla kuwa masuala niliyokuwa nimeyakabili wakati wa kazi, kuwa mbia kubaya na dada mzee, na maoni ya ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji; si hizi zilikuwa ni njia za Mungu za kunishughulikia kupitia hali zangu? Nilimwita Mungu kwa ukimya, “Mungu, najua kwamba unanishughulikia na kunipa nidhamu kwa sababu Unanipenda, lakini sielewi ni vipengele vipi vyangu ambavyo Ulipenda kuvishughulikia katika kusababisha hali hizi. Ninakuomba Uniongoze na kunipa nuru.” Baadaye, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona vifungu hivi viwili, “Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwako kutojijua. Kwanza ponya ugonjwa wako mwenyewe, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako” (“Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Unapokabiliwa na mambo, unafaa kufanya uchaguzi, unafaa kuyaendea kwa usahihi, unahitaji kutulia na unahitaji kuutumia ukweli kutatua shida ile. Kuna maana gani ya wewe kuelewa ukweli fulani kwa kawaida? Hauko hapo tu ili kujaza tumbo lako na hauko hapo kunenwa tu na si chochote zaidi, wala hauko kwa ajili ya kutatua shida za wengine; badala yake uko ili kutatua ugumu wako mwenyewe, na ni baada tu ya kutatua shida zako binafsi ndipo utaweza kutatua shida za wengine” (“Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Maneno ya Mungu yalikuwa kama mwako wa umeme. Ndiyo, wakati mambo yanapotokea tunapaswa kwanza kujijua, na kutumia ukweli kutatua matatizo ndani yetu. Kwa kuboresha hali yetu, sisi hutatua matatizo yetu, na hivyo kufanya iwezekane kutatua matatizo ya watu wengine. Lakini sikujijua wakati mambo yalipotokea, na niliwakazia macho wengine, nikiwalalamikia wakati wowote ilipowezekana. Wakati uratibu haukuwa sawa, nilimuona mtu mwingine kuwa sababu, na nilijaribu kutafuta njia za kuwasiliana naye, kumfanya ajifunze mafundisho yao na kujijua. Wakati ndugu wa kiume na wa kike wa familia mwenyeji hawakuwa tayari kunisikiliza nikiwasiliana, niliamini ni kwa sababu hawakuwa wakifuatilia ukweli, na hawakuweza kuukubali ukweli. Wakati utaratibu wa kazi ulirejeshwa kwangu bila kufunguliwa, nilibadilisha lawama na wajibu kwa wengine. Haya yote yalipotokea, nilishindwa kuchunguza ni upotovu upi nilioufichua, na ni ukweli upi nilipaswa kuuingia. Ilikuwa ni kama sikuwa na upotovu, na nilifanya kila kitu sawa. Badala yake, nilitoa madai kwa wengine kulingana na viwango vyangu, na kama mtu hakuweza kufikia kiwango changu au alikataa kuyakubali mawasiliano yangu, basi nilifikia uamuzi kwamba huyo mtu ni lazima hakuwa akitafutilia ukweli na kuukubali ukweli. Kwa kweli nilikuwa mwenye kiburi mno na sikuwa na maarifa yangu mwenyewe. Sikuwa na maarifa kuhusu upotovu nilioufichua, wala sikutafuta ukweli ili kutatua matatizo yangu mwenyewe, lakini daima niliwapata wengine na kosa. Ningewezaje kuwa mbia kwa upatanifu na kuelewana na wengine? Ni hapo nilipogundua: Sababu yangu kutoelewana na yeyote si kwa sababu hawatafuti ukweli, au kukubali ukweli, lakini kwa sababu mimi sina maarifa yangu mwenyewe, na huwa sisisitizi matumizi ya ukweli kutatua matatizo yangu mwenyewe.
Baada ya kutambua yote haya, nilianza kuzingatia kuingia kwangu mwenyewe na kutatua matatizo yangu mwenyewe kwanza wakati mambo yalipotokea. Wakati wa kuwasiliana na ndugu wa kiume na wa kike hatimaye, kulikuwa na vijenzi vya maarifa yangu mwenyewe katika mawasiliano yangu. Huu ndio wakati nilipopata ndugu zangu wa kiume na wa kike kuwa wamebadilika. Walianza kuonyesha maarifa kiasi ya upotovu wao wenyewe, na hatua kwa hatua tulikuza ubia kwa upatanifu. Kama nimekabiliwa na ukweli huu, hatimaye niliweza kuona kwamba wakati masuala yanapotokea, ni muhimu mno kujijua na kutatua matatizo ya mtu mwenyewe kwanza. Ni hapo tu tunapoweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wetu wa kawaida, kuwa na ubia kwa upatanifu na wengine, na kufaidi kutokana na uzoefu wetu wa maisha.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Jumanne, 4 Juni 2019
Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ufuatiliaji
Li Li Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilichaguliwa kama kiongozi wa ngazi ya katikati na ndugu zangu wa kiume na kike. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje? Matokeo yake yalikuwa, tulipozungumzia mada fulani pamoja, almuradi nilikuwa na ufahamu kidogo wa mada hiyo, basi ningejaribu kuwa wa kwanza kusema kitu, hata hivyo wakati sikuwa na ufahamu wa mada iliyojadiliwa na sikuweza kusema chochote, nilijipata nikiwa na wasiwasi. Katika siku hizo chache za mikutano, nilihisi nimechoka sana na kuwa na wasiwasi hasa, kana kwamba nilikuwa katika uwanja fulani wa kupambana. Baadaye, nilitafakari juu ya kile nilichofichua na nilitambua kuwa hali ya aina hii ilikuwa ilisababishwa hasa na majisifu yangu na hakukuwa na matatizo halisi.
Halafu siku moja, viongozi waliniarifu juu ya mkutano, nilihisi msisimko hasa nilipoambiwa kwamba viongozi wa ngazi za juu wangeitisha mkutano huo, na nikafikiri: Inaonekana kama nitafunzwa ili kupanda cheo, nikifanya vizuri na kuacha picha nzuri basi labda nitapandishwa cheo, na wakati uwajibikaji wangu unapoongezeka, basi sio wafanyakazi wenzangu tu watakaonipenda lakini pia ndugu zangu wa kiume na wa kike. Kwa hiyo katika mkutano huo, nilizungumza kwa majaribio sana, kwa kuogopa kwamba maneno yoyote yasiyofaa yangeacha picha mbaya kwa viongozi wangu. Wakati mkutano ulipomalizika hatimaye, nilihisi furaha ingawa nilikuwa na wasiwasi na kuchoka siku zilizopita, na nilihisi kuwa wakati ujao ulikuwa na ahadi nyingi. Kuanzia hapo kuendelea, “ukimbizaji” wangu ulikuwa umeongezeka sana kwa nguvu.
Siku moja, nilisoma kifungu kifuatacho kutoka kwa mahubiri: “Zamani watu walipojaribu kupata kujijua, walitilia maanani tu makosa ambayo walikuwa wametenda au upotovu waliokuwa wamefichua, lakini walitelekeza kuchangua kila neno na tendo lao ili kuona yepi yalikuwa tabia za upotovu za shetani, yepi yalikuwa sumu za joka kubwa jekundu, yepi yalikuwa mawazo na dhana za watu, na yepi yalikuwa uwongo na mikengeuko. Kando na mambo haya, watu lazima pia wachangue mitazamo yao wenyewe na hali zao za ndani, ili kuelewa mambo yaliyofichika katika kina cha mioyo yao, na waje mbele ya Mungu na kuyang’amua mambo haya kutumia ukweli. Hapo tu ndipo mtu anaweza kujua uhalisi wa upotovu wake mwenyewe na kuona tatizo la kiini chake potovu. Kwa maana mtu hajafanya makosa makuu hakumaanishi kuwa hakuna matatizo katika kina cha moyo wake. Uovu fulani uliofichika, tabia, tatizo katika asili ya mtu ni hata ngumu zaidi kutatua. Magonjwa madogo hayawezi kuwaua watu; ni magonjwa makubwa tu ambayo huua” (“Ni kwa Kujua Kiini Chake Potovu tu Ndio Mtu Anaweza Kuingia Katika Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Ukusanyaji wa Mahubiri—Ruzuku ya Uzima). Baada ya kusoma hili, sikuweza kujizuia kufikiria saikolojia yangu mwenyewe kutoka mikutano miwili iliyopita, na kwa ndani nilifikiria: Ni asili gani iliyoitawala? Wakati huo, nilianza kutafuta ukweli uliotangamana kwa hali yangu mwenyewe ili nipate kuichunguza na kuichangua.
Chini ya mwongozo wa Mungu, niliona neno la Mungu: “Watu wengine hususan humpenda Paulo sana: Wanapenda kuhutubu na kufanya kazi nje. Wanapenda kukutana pamoja; wanapenda watu wanapowasikiliza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya watu wengine na kufurahia wakati wengine wanathamini mfano wao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, mtu wa aina hii aliye na tabia hiziana asili ya aina gani? Kama kweli anatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa yeye ni fidhuli na mwenye majivuno. Yeye hamwabudu Mungu kamwe; yeye hutafuta hadhi ya juu, na anataka kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwakalia, kuwa na hadhi akilini mwao. Kinachojitokeza kuhusu tabia yake ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuwaabudu wengine. Huu ni mfano bora wa Shetani. Unaweza kuelewa wazi asili yake kutoka kwa mienendo hii” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilijaribu tena na tena kulielewa kila neno la Mungu, na kuyalinganisha na mawazo yangu mwenyewe, maneno na matendo, ni hapo tu nilipoona ukweli. Sababu yangu hasa ya kuwa na wasiwasi na wa kupaswa kutii mamlaka ya kuongoza kwa mkutano haikuwa ni kuwaacha watu wengine wanisikilize au kunitilia thamani? Si ilikuwa tu ni kupata hadhi ya juu na kuwa na watu zaidi kuniheshimu sana? Nilipohisi kwamba viongozi waliniheshimu, nilifikiri kwamba maisha yangu ya baadaye yalijaa matumaini, na nilijihisi kuridhika nafsi zaidi na mwenye nguvu. Kutoka kwa hilo niliona hali ya kiburi changu mwenyewe, daima nilitaka kupanda ngazi, kuwatawala watu, kuwa na nafasi katika mioyo ya watu, nilitafuta sawa na Paulo aliyotafuta. Kimsingi, kile nilichofuatilia hakikuwa kumwabudu au kumridhisha Mungu, bali kutumia hadhi iliyotolewa na Mungu ili kuridhisha tamaa na malengo yangu mwenyewe. Si hivi ndivyo hasa jinsi malaika mkuu alivyofichua kiburi chake? Si nilishika njia ya mpinga Kristo?
Awali nilipohudhuria mikutano nilikuwa nikizuiwa kwa urahisi, lakini nilifikiri tu kwamba nilikuwa ovyo mno, na sikuvichangua vitu vilivyokuwa nyuma. Sasa baada ya uchambuzi nilitambua kwamba hili lilikuwa linaendeshwa na asili ya kiburi na ya majivuno, ambamo nyuma yake kulikuwa mipango ya kibinafsi na malengo ya kiburi. Nilitawaliwa na kiburi changu mwenyewe, na nilifanya mengi dhidi ya Mungu: Niliharakisha nikitekeleza wajibu wangu na nilikuwa na hamu ya kujionyesha mwenyewe ili kupata hadhi ya juu na kupata upendezwaji wa ndugu zangu wa kiume na wa kike; nilipojiweka wazi mbele ya ndugu wa kiume na wa kike, kwa kweli sikuwahi kamwe kuchambua mambo yaliyofichika ndani kwa kina, badala yake nilizungumza juu ya vitendo vyangu vya nje ili kujipandisha cheo na kujishuhudia mwenyewe; nilipokula na kunywa neno la Mungu, haikuwa kuinua ufahamu wangu au kupokea ukweli, bali kujionyesha kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike. … Wakati nilifikiria jambo hili nilijikunyata: Sikuwa nikimtumikia Mungu, nilikuwa nimejihusisha kabisa na mambo yangu mwenyewe na kumpinga Mungu. Sasa, kama Mungu hakuwa ameniruhusu kuitambua asili yangu ya kiburi, na kuona lengo na uchafu uliosababisha ufuatiliaji wangu wa shauku na kwamba nilikuwa katika njia mbaya, basi ningeendelea na njia zangu za kiburi, na huenda nikafanya mambo maovu ambayo humpinga na kumsaliti Mungu na hivyo kuwa na uelekeo wa adhabu ya Mungu.
Ninamshukuru Mungu kwa kunipatia nuru Kwake kwa wakati wa kufaa na mwongozo ambao uliniongoza kutambua kiini cha asili yangu ya kiburi, na kuniruhusu nione kwamba nilikuwa ninashika njia ya mpinga Kristo; uzoefu huu umenifanya hasa kutambua kwamba, katika uzoefu wangu sipaswi kutambua ufunuo wangu mwenyewe na makosa tu lakini kuyalinganisha na ukweli na kuchunguza mambo yaliyofichika ndani sana ili kupata ufahamu bora wa asili yangu mwenyewe na kufanya mabadiliko katika tabia yangu. Katika siku zijazo, ningependa kuchangua kwa makini hali yangu ya akili na hali ya ndani, na kuielewa asili yangu potovu, kutafuta na kupata njia sahihi kwa wokovu wa Mungu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Jumatatu, 3 Juni 2019
Uso halisi wa Mtu Anayedaiwa Kuwa Mtu Mzuri
Kemu Jiji la Zhumadian, Mkoa wa Henan
Katika mawazo yangu mwenyewe, daima nimejifikiria kuwa na ubinadamu mzuri. Nimefikiria hivi kwa sababu, majirani zangu mara nyingi walinisifu mbele ya wazazi wangu kwa kuwa mwenye busara na wa kuijali familia yetu; wakisema kuwa mimi nilikuwa kipenzi cha wazazi wangu. Baada ya kuolewa, wakwe zangu walinishukuru mbele ya majirani kwa kuwa wema na mtoto wao. Katika mahali pangu pa kazi, kiongozi wangu alinisifu kwa kuwa mwaminifu na mwenye ustadi. Na tangu nikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, nimekuwa mtii kwa chochote kanisa huniomba kufanya. Huwa sipingani kamwe na kiongozi hata nikikemewa na kiongozi huyu kwa kutofanya kazi nzuri, na mara nyingi mimi huwasaidia ndugu wa kiume na wa kike walio na mahitaji. Kwa hivyo, ninaamini kuwa mimi ni wa maana, mwenye huruma, na mtu mwema mwenye ubinadamu. Sijawahi kujifikiria mwenyewe kwa njia ya maneno ambamo Mungu hufichua kuwa mwanadamu hana ubinadamu au kwamba mtu ana ubinadamu dhaifu. Wakati wa kuwasiliana maneno ya Mungu na ndugu wa kiume na wa kike, ingawa najua nahitaji kuwa na ufahamu wa asili yangu mwenyewe, bado mimi hudumisha mtazamo wangu mwenyewe, nikifikiria moyoni mwangu: Hata kama mimi si mtu wa ubinadamu mzuri, bado nina ubinadamu bora kiasi ukilinganisha na wengine. Aidha, bila kujali neno la Mungu linavyosema au kile ndugu wa kiume na wa kike wanavyosema, siko tayari kujitenga na wazo la kuwa mtu wa ubinadamu mzuri.
Siku moja, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, kifungu kimoja kilivuta nadhari yangu. Mungu anasema, “Watu wengine ni wazuri kiasili; wana uwezo wa kutenda ukweli. Ubinadamu wa watu wengine ni mnyonge, hivyo ni vigumu kwao kutenda ukweli … Je, mnaweza kusema kuwa yule ambaye hatendi ukweli amewahi kuutafuta ukweli katika matendo yake? Hajautafuta kabisa. Fikira zake binafsi hutokea: ‘Njia hii ni nzuri, ni kwa faida yangu.’ Mwishowe, anatenda kulingana na mawazo yake binafsi. Hatafuti ukweli kwa sababu kuna kitu kisicho sawa na moyo wake, moyo wake hauko sawa. Hatafuti, hachunguzi, wala haombi mbele za Mungu; anatenda tu kwa ukaidi kulingana na matakwa yake. Mtu wa aina hii hana upendo wa ukweli kabisa. … Wale wasio na upendo kwa ukweli hawatautafuta katika wakati huo, wala hawatajichunguza baadaye. Kamwe hawachunguzi kama mambo wanayoyatenda ni sawa ama yenye makosa hatimaye, hivyo wanakiuka kanuni kila wakati, wanakiuka ukweli. … Mtu aliye na moyo anaweza kufanya makosa mara moja tu anapofuata utendaji, mara mbili kwa kiwango cha juu zaidi—mara moja ama mbili, sio mara tatu ama nne, hii ni akili ya kawaida. Kama anaweza kutenda makosa hayo sawa mara tatu ama nne, hii inathibitisha kuwa hana upendo wa ukweli, wala hautafuti ukweli. Mtu wa aina hii kwa waziwazi sio mtu mwenye utu” (“Kutenda Ukweli na Kutatua Asili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Baada ya kusoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu, nilikuwa na ufunuo wa ghafla. Inavyoelekea, ubinadamu mzuri au mbaya unahusiana kwa karibu na utekelezaji wa ukweli. Mtu wa ubinadamu mzuri atatafuta ukweli na kutenda ukweli katika kila kitu, na kujichunguza mwenyewe baadaye. Nimemejiona daima kuwa na ubinadamu mzuri, hivyo mimi ni mtu ambaye hutafuta na kutenda ukweli katika kila kitu? Nikifikiria nyuma, sikuomba au kutafuta ukweli kuhusu vitu vingi vilivyonikabili. Sikujichunguza au kujifahamu baadaye. Ingawa nilikuwa nimeonyesha tabia yangu potovu, sikutatua masuala yangu kwa kutafuta ukweli, lakini niliendelea kufanya kosa hilo hilo tena na tena. Wakati mwingine hata kama nilielewa kipengele kimoja cha ukweli, sikuonekana kutaka kukitenda. Nakumbuka mifano mingi ya jambo hili kwa dhahiri. Wakati mmoja, nakumbuka nikihisi hisi ya utengano na mtu niliyeshirikishwa naye. Nilikuwa na ufahamivu kuwa lingeathiri moja kwa moja matokeo yatakikanayo ya kazi ikiwa tatizo halikutatuliwa, lakini kwa sababu ya kiburi na majivuno yangu, nilikataa kuacha ubinafsi wangu na kuwa na mawasiliano ya wazi naye. Badala yake, nilistahimili jambo chungu lakini lisiloepukika na kuendelea kufanya kazi, na kusababisha kazi isiyofanikiwa sana. Wakati mwingine nilipoona ndugu wa kiume na wa kike wakifichua kipengele fulani cha hali yao potovu, sikujaribu kuwasiliana nao katika ukweli ili kuwasaidia kujijua, lakini badala yake niliwahukumu bila wao kujua. Sikutubu au kujaribu kubadilisha njia zangu hata baada ya kushughulikiwa mara chache, lakini badala yake niliendelea katika njia zangu za zamani. Sikujitahidi kupata matokeo mazuri mno katika kufanya kazi yangu, lakini daima nilikuwa mvivu na mjanja, nikishughulika na mambo kihobelahobela, daima nikimdanganya Mungu ili kudumisha nafasi yangu mwenyewe, bahati na hadhi. Sikuyapa umuhimu au kuwa na hisia ya hatia. Sikutafuta au kuchunguza mambo yalipotokea kazini mwangu, lakini nilifanya tu kama nilivyotaka. Hata kama ilileta hasara kubwa kwa kanisa, sikuhisi kama nilikuwa na deni kwa Mungu, wala sikuaibishwa na matendo yangu maovu. Hata kama Mungu alinikumbusha kupitia maneno Yake na kufichua upotovu wangu kwa njia ya kuwashughulikia na kuwapogoa ndugu, niliendelea kumpuuza Yeye, na kufanya makosa yale yale zaidi ya mara tatu au nne. Si vitendo hivi vinathibitisha kwamba nina ukosefu wa ubinadamu na mimi si mpenzi wa ukweli machoni pa Mungu? Bila kujali, sijajaribu kujijua kwa msingi wa asili yangu, lakini naendelea kuvaa laurusi ya “ubinadamu mzuri” juu ya kichwa changu. Nimekuwa mtovu wa haya jinsi gani!
Hivi sasa, moyo wangu umejaa hatia, na wakati huo huo umejaa shukrani kwa Mungu. Siwezi kujizuia kujimwaga mbele ya Mungu, “Mungu, asante kwa nuru Yako, kuniruhusu nijue kuwa mimi si mtu mwenye ubinadamu mzuri, kunisaidia kuelewa kuwa mtu mwenye ubinadamu wa kweli ni yule anayependa ukweli, ni mtu ambaye humsikiliza Mungu na kumtii Mungu, ni mtu ambaye yuko tayari kutenda ukweli na kufuatilia upendo wa Mungu. Mimi pia natambua ufahamu wangu juu yangu hautegemezwi kwa ukweli wa maneno ya Mungu, lakini umetegemezwa fikra zangu na dhana zangu, na vilevile maoni yangu ya kidunia. Ni upumbavu kabisa. Mungu, tangu sasa kuendelea, sitaki kujipima kulingana na mtazamo wa Shetani au mawazo yangu mwenyewe. Ninataka kujijua kwa msingi wa maneno Yako, na kufanya kila linalowezekana kufuatilia ukweli, ili hivi punde niweze kuwa mtu aliye na ukweli na ubinadamu ili kuufariji moyo Wako.”
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo