Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Enzi ya Ufalme. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Enzi ya Ufalme. Onyesha machapisho yote
Jumanne, 28 Novemba 2017
Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno | Kanisa la Mwenyezi Mungu
Novemba 28, 2017Enzi ya Ufalme, Matamshi ya Kristo, Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Matamshi-ya-Kristo-wa-Siku-za-Mwisho-Chaguzi, Mungu, neno la Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo Mungu hufanyia kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumfanya binadamu kuwa mtimilifu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwenye neno, binadamu anajua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha binadamu, na kile ambacho binadamu anastahili kuingia ndani chake. Kupitia neno, kazi yote ambayo Mungu hupenda kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa.