Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwenyezi Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mwenyezi Mungu. Onyesha machapisho yote
Jumatatu, 9 Julai 2018
Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje
Julai 09, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Umeme-wa-Mashariki, VitabuNo comments
Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu. Una uwezo wa kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu kila unapofanya chochote; hata kama huelewi mapenzi ya Mungu, bado ni lazima utimize wajibu na majukumu yako kadri ya uwezo wako.
Jumamosi, 7 Julai 2018
Tamko la Arubaini na Mbili
Julai 07, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Mwenyezi Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, Umeme-wa-Mashariki, VitabuNo comments
Tamko la Arubaini na Mbili
Punde tu kazi mpya inapoanza, watu wote wanakuwa na kuingia kupya, na wanasonga mbele nami bega kwa bega, tunatembea pamoja kwenye barabara kubwa ya ufalme, na kuna urafiki mkubwa kati ya mwanadamu na Mimi. Ili kuonyesha hisia Zangu, ili kudhihirisha mtazamo Wangu kwa mwanadamu, Nimemzungumzia mwanadamu kila mara. Sehemu ya maneno haya, hata hivyo, yanaweza kuwaumiza watu, huku mengine yanaweza kuwa ya msaada mkubwa kwao, na kwa hiyo Nawashauri watu kusikiliza kwa makini sana kile kinachotoka kinywani Mwangu. Matamko Yangu huenda yasiwe sanifu na yenye ustarabu, lakini yote ni maneno kutoka kina cha moyo Wangu.
Jumatano, 4 Julai 2018
Tamko la Arubaini na Moja
Julai 04, 2018Mwenyezi Mungu, Neno-Laonekana-katika-Mwili, ukweli, Umeme-wa-Mashariki, VitabuNo comments
Tamko la Arubaini na Moja
Wakati mmoja Nilianza shughuli kubwa miongoni mwa wanadamu, lakini hawakutambua, kwa hivyo ilinibidi Nitumie neno Langu ili kuwafichulia. Na hata hivyo, mwanadamu bado hangeweza kuyaelewa maneno Yangu, na akasalia kutojua malengo ya mpango Wangu. Na hivyo kwa sababu ya kasoro na dosari za mwanadamu, alifanya mambo ili kukatiza mpango Wangu wa usimamizi, na pepo wachafu wakachukua nafasi ya kujidhihirisha, wakawafanya wanadamu kafara wao, mpaka wakateswa na pepo hao wachafu na wakachafuliwa kila mahali. Ulikuwa wakati huu ambapo Niliona nia ya mwanadamu na kusudi lake.