Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za -mwisho. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo siku-za -mwisho. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 24 Juni 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 113

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 113

Kila kitendo Ninachokifanya kina hekima Yangu ndani yake, lakini mwanadamu hawezi kukielewa kamwe; mwanadamu anaweza tu kuona matendo Yangu na maneno Yangu, lakini hawezi kuuona utukufu Wangu, au kuonekana kwa nafsi Yangu, kwa sababu mwanadamu hasa anakosa uwezo huu. Chini ya hali ya kutombadilisha mwanadamu, wazaliwa Wangu wa kwanza nami tutarejea Sayuni na kubadili sura, ili mwanadamu aweze kuiona hekima Yangu na kudura Yangu. Hekima Yangu na kudura Yangu ambayo mwanadamu anaiona sasa ni sehemu moja ndogo tu ya utukufu Wangu, na haistahili kutajwa kamwe. Inavyoonyeshwa kutoka hapo, hekima Yangu na utukufu Wangu hauna kikomo na una kina kupita kiasi, na akili ya mwanadamu hasa haina namna ya kuuzingatia au kuufahamu. Kuujenga ufalme ni wajibu wa wazaliwa wa kwanza, nayo ni kazi Yangu pia, yaani ni kipengee cha mpango Wangu wa usimamizi. Ujenzi wa ufalme si sawa na ujenzi wa kanisa; kwa kuwa wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi ni nafsi Yangu na ufalme, basi wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi tutakapoingia katika Mlima Sayuni, ujenzi wa ufalme utatimizwa. Kuweka kwa namna nyingine, ujenzi wa ufalme ni hatua ya kazi: hatua ya kuingia katika ulimwengu wa kiroho. (Hata hivyo, yote ambayo Nimefanya tangu kuiumba dunia yamefanyika kwa ajili ya hatua hii. Ingawa Nasema ni hatua, kwa kweli siyo hatua kamwe.) Hivyo Nawatumia watendaji huduma wote kuihudumia hatua hii, na kwa hivyo katika siku za mwisho idadi kubwa za watu zitajiondoa; wote wanatoa huduma kwa wazaliwa wa kwanza. Yeyote anayetoa wema kwa watendaji huduma hawa atakufa kwa laana Zangu. (Watendaji huduma wote wanawakilisha njama za joka kubwa jekundu, na wote ni vikaragosi wa Shetani, kwa hiyo wale ambao wanatoa wema kwa watu hawa ni washirika wa joka kubwa jekundu nao ni wa Shetani.) Napenda yote ambayo Ninapenda na kudharau malengo yote ya laana Zangu na kuteketezwa. Je, ninyi pia mnaweza kufanya hivi? Yeyote anayesimama dhidi Yangu, bila shaka Sitamsamehe, wala kumwachilia huru! Ninapofanya kila tendo, Ninapanga idadi kubwa za watendaji huduma kunihudumia Mimi. Hivyo inaweza kuonekana kwamba katika historia yote, imekuwa kwa ajili ya hatua hii ambapo manabii na mitume wote wametoa huduma, na hawaupendezi moyo Wangu, hawatoki Kwangu. (Ingawa wengi wao ni waaminifu Kwangu, hakuna aliye Wangu. Hivyo, kukimbia kwao huku na kule ni kufanya msingi wa hatua hii ya mwisho kwa ajili Yangu, lakini hii yote ni jitihada bure kwao.) Kwa hiyo, katika siku za mwisho hata zaidi kutakuwa na idadi kubwa za watu wa kujiondoa. (Sababu Ninasema idadi kubwa ni kwa sababu mpango Wangu wa usimamizi umefikia mwisho wake, ujenzi wa ufalme Wangu umefanikiwa, na wazaliwa wa kwanza wameketi katika kiti cha enzi.) Yote ni kwa sababu ya kuonekana kwa wazaliwa wa kwanza. Kwa sababu ya kuonekana kwa wazaliwa wa kwanza, joka kubwa jekundu hujaribu kila namna iwezekanayo na hutumia njia zote kufanya uharibifu: likiwatuma kila aina ya pepo wabaya ambao huja kufanya huduma kwa ajili Yangu, ambao wamebainisha tabia zao halisi zilivyo katika wakati wa sasa, na ambao wameukatiza usimamizi Wangu. Haya hayawezi kuonekana kwa macho, na yote ni mambo ya ulimwengu wa kiroho. Hivyo watu hawaamini kwamba kutakuwa na idadi kubwa za watu wa kujiondoa, lakini Najua hatua Zangu, Nauelewa usimamizi Wangu, na hii ndiyo sababu ya kutomruhusu mwanadamu kuingilia kati. (Kutakuja siku ambapo kila aina ya pepo mbaya asiyefaa atafichua nafsi yake ya kweli, na watu wote wataridhika kwa dhati.)
Nawapenda wazaliwa Wangu wa kwanza, lakini ule ukoo wa joka kubwa jekundu unaonipenda kwa uaminifu mkubwa, Siupendi kabisa; kwa kweli Naudharau hata zaidi. (Watu hawa si Wangu, na ingawa wanaonyesha nia nzuri, na kusema maneno ya kufurahisha, kwa kweli hiyo ni njama ya joka kubwa jekundu, hivyo Nawachukia hadi kwenye kiini Changu.) Hii ni tabia Yangu, na huu ni ukamilifu wa haki Yangu. Mwanadamu hawezi kuelewa kabisa. Kwa nini ukamilifu wa haki Yangu inafichuliwa hapa? Kutokana na hili mtu anaweza kutambua tabia Yangu takatifu na isiyokosewa. Naweza kuwapenda wazaliwa Wangu wa kwanza na kuwadharau wale wote ambao si wazaliwa Wangu wa kwanza (hata kama wao ni watu waaminifu). Hii ni tabia Yangu. Je, hamwezi kuona? Katika dhana za watu, Mimi daima ni Mungu mwenye huruma, nami Nawapenda wote wanaonipenda; je, huku si kukufuru dhidi Yangu Mimi? Naweza kuwapenda ng'ombe na farasi? Naweza kumchukua Shetani kama mzaliwa Wangu wa kwanza na kufurahia hilo? Upuuzi! kazi Yangu ni kuwahusu wazaliwa Wangu wa kwanza, na mbali na wazaliwa Wangu wa kwanza, Sina kitu kingine cha kupenda. (Wana na watu ni zaidi, lakini wao si muhimu hata kidogo.) Watu wanasema kwamba kabla, Nilifanya kazi nyingi sana isiyo na maana, lakini kwa maoni Yangu kwa kweli hili ni jambo la thamani sana, la maana sana. (Hii ni yote iliyofanyika wakati wa kuupata mwili kuwili; kwa sababu Nataka kufichua nguvu Zangu, lazima Niwe mwili ili Niikamilishe kazi Yangu.) Sababu ambayo Nasema Roho Wangu huja kufanya kazi binafsi, ni kwa sababu kazi Yangu inakamilishwa katika mwili, hiyo ni kusema, wazaliwa Wangu wa kwanza na Mimi sasa tunaanza kuingia katika mapumziko. Vita na Shetani katika mwili ni vikali zaidi kuliko vita na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na vinaweza kuonekana na watu wote, hivyo hata ukoo wa Shetani pia unaweza kuwa na ushuhuda mzuri kwa ajili Yangu, na huna nia ya kuondoka; hii ndiyo maana yenyewe ya kufanya Kwangu kazi katika mwili. Ni hasa ili kuufanya ukoo wa ibilisi umuaibishe ibilisi mwenyewe; hii ni aibu yenye nguvu zaidi kumletea ibilisi Shetani, na kumfanya aone haya sana kiasi cha kukosa kupata mahali pa kujificha, na kuomba rehema mbele Zangu mara kwa mara. Nimeshinda, Nimeshinda juu ya kila kitu, Nimeipenya mbingu ya tatu kuufikia Mlima Sayuni, kufurahia furaha ya kifamilia pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza, kuhusika milele katika karamu kubwa ya ufalme wa mbinguni!
Kuhusu wazaliwa wa kwanza, Nimelipa gharama zote na kutumia nguvu zote. (Mwanadamu hajui kabisa kwamba yote ambayo Nimefanya, yote ambayo Nimesema, kwamba Nabaini kila aina ya pepo mbaya, na kwamba Nimemuondoa kila aina ya mtendaji huduma, yote imekuwa kwa sababu ya wazaliwa wa kwanza.) Lakini ndani ya kazi nyingi, mpango Wangu ni wenye utaratibu; haufanywi ovyo ovyo hata kidogo. Katika matamshi Yangu ya kila siku, mnapaswa kuweza kuona mbinu na hatua za kazi Yangu; katika matendo Yangu ya kila siku mnapaswa kuona hekima Yangu na kanuni Zangu katika kukabiliana na mambo. Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetani haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu. Kwa sababu Nimesema awali kwamba asili ya mwanadamu haibadiliki, ngano siku zote itakuwa ngano. Basi wazaliwa wa kwanza ni nini? Wazaliwa wa kwanza wanatoka Kwangu, hawaumbwi nami, hivyo hawawezi kuitwa ngano (kwa sababu mara tu mtu anapotaja ngano, inahusiana na neno “kupanda,” na “kupanda” maana yake ni “kuumba”; magugu yote yamepandwa na Shetani kisiri, ili kutenda kama watendaji huduma). Mtu anaweza tu kusema kwamba wazaliwa wa kwanza ni onyesho kamili na karimu la nafsi Yangu, wanapaswa kuwakilishwa na dhahabu na fedha, na vito vya thamani; hili linagusia ukweli kwamba kuja Kwangu ni kama kule kwa mwizi, nami Nimekuja kuiba dhahabu na fedha na vito vya thamani (kwa sababu hizi dhahabu na fedha na vito vya thamani vyote ni mali Yangu ya awali, nami Nataka kuvirudisha nyumbani Kwangu). Wakati ambapo wazaliwa wa kwanza nami tutarudi Sayuni pamoja, hizi dhahabu, fedha na vito vya thamani vitaibwa nami; katika wakati huu, kutakuwa na vizuizi na vurugu ya Shetani, na hivyo Nitazichukua dhahabu, fedha na vito vya thamani na kuzindua vita vya maamuzi na Shetani. (Hii haswa si hadithi, lakini ni jambo ambalo hutokea katika ulimwengu wa kiroho, hivyo kuhusu hili watu hawaelewi kabisa, na wanaweza tu kulisikia kama hadithi. Lakini lazima muone kutokana na lile Ninalosema kile mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita kilicho, na mnapaswa kutolifikiria kabisa kama utani, vinginevyo Roho Wangu Ataondoka kutoka ndani ya wanadamu wote.) Leo, vita hivi vimekamilika kabisa, nami Nitawaleta wazaliwa Wangu wa kwanza (Nikizileta dhahabu, fedha na vito vya thamani ambavyo ni Vyangu) pamoja nami Mlimani Kwangu Sayuni. Kutokana na uhaba wa dhahabu, fedha na vito vya thamani, na kwa sababu ni vya thamani, Shetani hujaribu kila namna iwezekanayo kuvipokonya, lakini Nasema tena na tena kwamba kile kitokacho Kwangu lazima kinirudie, maana yake ambayo imetajwa hapo juu. Maneno Yangu kwamba wazaliwa wa kwanza wanatoka Kwangu na ni Wangu ni tangazo kwa Shetani, hakuna mtu anaelewa hili, na yote ni jambo ambalo hutokea katika ulimwengu wa kiroho. Hivyo mwanadamu haelewi kwa nini Narudia kusisitiza kwamba wazaliwa wa kwanza ni Wangu, leo mnapaswa kuelewa! Nimesema kwamba matamshi Yangu yana kusudi na hekima, lakini mnaelewa hili tu kutoka nje, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuona hili wazi katika roho.
Nasema zaidi na zaidi, na zaidi Ninavyosema ndivyo maneno Yangu yanavyokuwa makali zaidi. Inapofika kiwango fulani, Nitayatumia maneno Yangu kuwafinyanga watu kwa kiwango fulani, si tu kuwafanya watu kuridhishwa moyoni na kwa neno, lakini hata zaidi ili kuwafanya kukaribia kifo; hii ni mbinu Yangu ya kazi, hii ni hatua Yangu ya kazi; lazima iwe hivi, hapo tu ndipo inaweza kumuaibisha Shetani na kuwafanya wazaliwa wa kwanza kamili (kuyatumia maneno Yangu ili hatimaye kuwafanya wazaliwa wa kwanza kamili, ili kuwaruhusu kujitenga na mwili na kuingia katika ulimwengu wa kiroho). Mwanadamu haelewi mbinu ya matamshi Yangu, sauti ya matamshi Yangu. Kutokana na maelezo Yangu nyote mnapaswa kuwa na umaizi kiasi, na nyote mnapaswa kuyafuata matamshi Yangu ili muikamilishe kazi ambayo mnapaswa kuifanya. Hiki ndicho Nilichowaaminia. Lazima muwe na ufahamu wa hili, si tu kutoka ulimwengu ya nje, lakini muhimu zaidi kutoka ulimwengu ya kiroho.

Jumapili, 5 Novemba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.