Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neema. Onyesha machapisho yote
Jumapili, 19 Mei 2019
1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?
Mei 19, 2019Kazi-ya-Mungu, Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, neema, siku-za-mwisho, VitabuNo comments
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
“Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu.
kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Biblia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.
kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. … Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu
Jumapili, 5 Mei 2019
1. Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?
Mei 05, 2019Hukumu-na-Kuadibu, Kazi-ya-Mungu, Kumbukumbu-za-Maongezi-ya-Kristo, neema, VitabuNo comments
III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho
1. Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Kwa hivyo mtakuwa watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45).
“Utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14).
“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Jumatano, 20 Machi 2019
Wimbo wa dini | Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe
Machi 20, 2019Kumpenda-Mungu, Mfuateni-Mwanakondoo-na-Kuimba-Nyimbo-Mpya, neema, Ufalme, VitabuNo comments
Wimbo wa dini | Mwenyezi Mungu, Sasa Niko na Wewe
Ⅰ
Mwenyezi Mungu, sasa kwa sababu tuko na Wewe, masumbuko yanabadilika kuwa furaha.
Kula, kunywa, kufurahia maneno Yako, tuko na Wewe kila siku.
Maji Yako ya uzima yanatustawisha, tuna ukarimu kwa vyote.
Jua ukweli, ingia katika ukweli, yote yanakutegemea Wewe.
Jumamosi, 17 Novemba 2018
Tamko La Kumi Na Saba
Tamko la Kumi na Saba
Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni.... Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani[a] vinaanza.
Alhamisi, 15 Novemba 2018
Tamko la Tano
Tamko la Tano
Milima na mito huenda ikibadilika, vijito hutiririka mbele, na maisha ya mtu ni yenye uvumilivu mdogo kuliko ardhi na anga. Mwenyezi Mungu pekee ndiye maisha ya milele yaliyofufuka milele, katika vizazi hai milele! Vitu vyote na matukio viko katika mikono Yake, Shetani yuko chini ya miguu Yake.
Leo hii ni kwa sababu ya uteuzi wa Mungu ulioamuliwa kabla kwamba Ametuokoa kutoka kukamatwa na Shetani.
Jumatano, 14 Novemba 2018
Tamko la Pili
Novemba 14, 2018Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, maisha, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, ushahidi, VitabuNo comments
Tamko la Pili
Kanisa la Filadelfia limechukua umbo, na hili limesababishwa kabisa na neema na rehema za Mungu. Watakatifu wameleta upendo wao wa Mungu mbele na kamwe hawakuyumbayumba kutoka kwa njia yao ya kiroho. Kuwa imara katika imani kwamba Mungu mmoja wa kweli Amekuwa mwili, ya kwamba Yeye ndiye Mkuu wa ulimwengu Ambaye hutawala vitu vyote—hii imethibitishwa na Roho Mtakatifu na ni ushahidi thabiti! Kamwe hauwezi kubadilika!
Eh, Mwenyezi Mungu! Leo Umefungua macho yetu ya kiroho, kuwaruhusu vipofu kuona, viwete kutembea, wenye ukoma kuponywa. Umefungua dirisha la mbinguni na tumeona siri za dunia ya kiroho.
Jumamosi, 10 Novemba 2018
Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"
Matamshi ya Mungu | "Unajua Nini Kuhusu Imani?"
Mwenyezi Mungu anasema, "Ninasema kwamba binadamu ana imani Kwangu kwa sababu Nampa neema nyingi kupindukia, na mambo yapo mengi sana ya kupata. Wayahudi waliniamini Mimi kwa neema Yangu, na wakanifuata Mimi popote Nilipoenda. Binadamu hawa wasiojua wenye maarifa na uzoefu finyu walitafuta tu kuona ishara na maajabu ambayo nilionyesha. Walinichukulia Mimi kuwa mkuu wa nyumba ya Wayahudi ambaye angeweza kutekeleza miujiza mikubwa zaidi. Kwa hivyo, Nilipopunga mapepo kutoka kwa binadamu walijizungumzia miongoni mwao kwa mkanganyo mkubwa wakisema Mimi ni Eliya, kwamba Mimi ni Musa, kwamba Mimi ndimi nabii wa kale zaidi kati ya wote, kwamba Mimi ndimi daktari mkuu zaidi kuliko wote.
Ijumaa, 2 Novemba 2018
Tamko la Sabini na Tatu
Novemba 02, 2018baraka, Hukumu, Kanisa, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Tamko la Sabini na Tatu
Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu. Ni ya kutaka uangalifu mkubwa hasa. Maneno Yangu si matupu kamwe na yote ni ya kweli. Unapaswa kuamini kwamba kila neno ni la kweli na sahihi. Usiwe asiye mwangalifu; huu ni wakati muhimu! Baraka au bahati mbaya iko katika wakati huu. Tofauti ni kama mbingu na dunia.
Alhamisi, 1 Novemba 2018
Tamko la Sabini na Nne
Novemba 01, 2018Kanisa, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, ukweli, Umeme-wa-Mashariki, VitabuNo comments
Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija juu yako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa tena na huzuni na hakutakuwa na machozi? Ni kwa sababu ya hili. Ndani Yangu, kila kitu kinatimizwa, lakini ndani ya wanadamu, vitu vyote ni vipotovu na bure, na vyote ni vidanganyifu kwa wanadamu.
Jumatano, 31 Oktoba 2018
Tamko la Themanini na Sita
Oktoba 31, 2018baraka, huruma, Mwenyezi-Mungu, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. Kwa wale Ninaowapenda, Nitawapenda daima mpaka mwisho kabisa na upendo hautabadilika kamwe. Kwa wale Ninaowachukia, moyo Wangu hauguswi hata kidogo bila kujali ni wazuri kiasi gani. Hii ni kwa sababu wao sio Wangu na hawana sifa Zangu na hawana uzima Wangu.
Jumapili, 28 Oktoba 2018
Tamko la Tisini na Nne
Oktoba 28, 2018huruma, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni. Hili linamaanisha kwamba tutarudi kutoka kwa nyama hadi kwa mwili wa awali. Hii ndiyo maana ya kweli ya “kurudi Sayuni.” Hii pia ndiyo maana ya kweli na lengo la mpango Wangu mzima wa usimamizi, na hata zaidi sehemu muhimu zaidi ya mpango Wangu wa usimamizi, ambayo hakuna anayeweza kuizuia, na ambayo itatimizwa mara moja.
Ijumaa, 26 Oktoba 2018
Tamko la Tisini na Tisa
Oktoba 26, 2018Hukumu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, neema, Neno-Laonekana-katika-Mwili, VitabuNo comments
Tamko la Tisini na Tisa
Kwa sababu mwendo wa kazi Yangu unaongeza kasi, hakuna anayeweza kuenda mwendo sawa na nyayo Zangu, na hakuna anayeweza kupenya akili Yangu, lakini hii ndiyo njia tu ambayo lazima isafiriwe. Hii ni “wafu” yaani wakati Ninapoongea kuhusu kufufuliwa kutoka kwa wafu (inarejelea kukosa uwezo wa kufahamu mapenzi Yangu, kukosa uwezo wa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Yangu. Haya ni maelezo mengine ya “wafu”, na hayamaanishi kutelekezwa na Roho Wangu). Wakati nyinyi na Mimi tumebadilika kutoka kwa awamu hii hadi kwa mwili, basi maana ya awali ya kufufuliwa kutoka wafu itatimizwa (yaani, hii ni maana ya awali ya ufufuko kutoka kwa wafu). Sasa, hii ni hali yenu: Hamwezi kufahamu mapenzi Yangu na hamwezi kupata nyayo Zangu.
Jumatatu, 15 Oktoba 2018
Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Moja
Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Moja
Mwenyezi Mungu alisema, Sitakuwa mwenye huruma kwa yeyote anayeingilia usimamizi Wangu ama anayejaribu kuiharibu mipango Yangu. Kila mtu anapaswa kuelewa kile Ninachomaanisha kutoka kwa maneno Ninayosema na lazima aelewe vizuri kile Ninachozungumzia. Kwa kuzingatia hali iliyopo, kila mtu anapaswa kujichunguza: Ni wajibu gani unaotekeleza? Unaishi kwa ajili Yangu, au unamtumikia Shetani? Je, kila moja ya matendo yako hutoka Kwangu, au hutoka kwa Shetani? Haya yote yapaswa kuwa dhahiri ili kuepuka kukosea amri Zangu za utawala na hivyo kupata ghadhabu Yangu.
Jumamosi, 6 Oktoba 2018
Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Kumi na Tisa
Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Kumi na Tisa
Mwenyezi Mungu alisema, Ni lazima nyote muelewe nia Zangu, nyote mnapaswa kuelewa hali Yangu ya moyo. Sasa ni wakati wa kujiandaa kurudi Sayuni, sina mawazo ya lolote isipokuwa hili. Mimi Ninatumaini tu kwamba Ninaweza kukutana nanyi siku moja hivi karibuni, na kutumia kila dakika na kila sekunde pamoja nanyi katika Sayuni. Mimi Naichukia kabisa dunia, Nauchukia kabisa mwili, na Mimi Namchukia kabisa hata zaidi kila binadamu duniani;
Alhamisi, 30 Agosti 2018
Kanisa la Mwenyezi Mungu swahili worship songs | Njia Yote Pamoja na Wewe
Agosti 30, 2018Hukumu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, neema, Nyimbo, Wimbo-wa-Uzoefu-wa-MaishaNo comments
- Kanisa la Mwenyezi Mungu swahili worship songs | Njia Yote Pamoja na Wewe
-
🎬😇👍
- 🎼🎼 → → 🎙️🎙️ ↓↓ 😊😊
- I
- Nilikuwa kama mashua,
- ikielea baharini.
- Ulinichagua,
- na mahali pazuri Uliniongoza.
- Sasa katika familia Yako,
- nikipewa joto na upendo Wako,
- nina amani kabisa.
Jumatatu, 30 Julai 2018
Umeme wa Mashariki | Tamko la Arubaini na Saba
Ili kuwafanya wanadamu wawe wakomavu katika maisha na kuwafanya wanadamu na Mimi tuweze kutimiza matokeo katika udhanifu wetu wa pamoja, Nimewaendeka wanadamu kila mara, Nikiwakubalia kupata chakula na riziki kutoka kwa neno Langu na kupokea utele Wangu kutoka kwake. Sijawahi kuwapa wanadamu sababu ya kuaibika, lakini mwanadamu hafikirii hisia Zangu kamwe. Hii ni kwa sababu wanadamu hawana hisia na "hudharau" vitu vyote isipokuwa Mimi. Kutokana na dosari za wanadamu, Nawasikitikia sana na hivyo Nimefanya kila Niwezalo, ili waweze kufurahia utele wa dunia hadi kiasi cha kuiridhisha mioyo yao kwa wakati wao duniani. Simtendei mwanadamu bila haki na kwa kuzingatia watu walionifuata kwa miaka mingi, Nimekuwa na moyo wa huruma kwao.
Jumapili, 21 Januari 2018
Swahili Gospel Song | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo
Swahili Gospel Song | "Njia Yote Pamoja na Wewe" Mungu ni Upendo
Nilikuwa kama mashua, ikielea baharini.
Ulinichagua, na mahali pazuri Uliniongoza.
Sasa katika familia Yako, nikipewa joto na upendo Wako,
nina amani kabisa.
Unanibariki, Unatoa maneno Yako ya hukumu.
Bado sijui jinsi ninavyokosa kuithamini neema Yako.
Kila mara nikiasi, kwa namna fulani nikiuumiza moyo Wako.
Na bado Hunitendei kulingana na dhambi
zangu lakini Unafanya kazi kwa ajili ya wokovu wangu.
Ninapokuwa mbali, Unaniita nirudi kutoka hatarini.