I
Kumwogopa Mungu hakumaanishi
hofu isiyo na jina, kuepuka, kuabudu kama mungu au ushirikina.
Badala yake, kumcha Mungu kunamaanisha
Ni kuweka wakfu, upendo, ibada kamili,
kurudisha fadhila, kujisalimisha bila malalamiko.
II
Bila maarifa halisi ya Mungu,
mtu hawezi kustahi au kuamini, kuelewa,
wala hawezi kweli kujali au kutii,
lakini anaweza kujazwa na hofu na wasiwasi,
kujaa shaka, kuelewa visivyo,
kuelekea kuepa na kutaka kuepuka.
Bila maarifa halisi ya Mungu,
kuweka wakfu na kurudisha fadhila haviwezi kuwa,
na wanadamu hawangekuwa na ibada
na kujisalimisha ambako ni halisi,
kuabudu kama mungu kwa ujinga tu,
ni ushirikina usio na hisia tu.
III
Bila maarifa halisi ya Mungu,
mtu hawezi kutembea katika njia Zake, kumuogopa Mungu, kujitenga na uovu.
Badala yake, yote wanayofanya yatajaa
uasi na kwa kutojali,
kujaa mashtaka yaliyojaa kashfa,
hukumu zisizo sahihi juu Yake,
na kwa mienendo miovu waliupinga ukweli
na kile maneno ya Mungu kweli humaanisha.
Lakini kwa imani halisi katika Mungu,
wanaweza kujua jinsi ya kumfuata na kumtegemea Yeye.
Ni hapo tu ndipo mtu angeweza kufahamu,
kuelewa Mungu, kuanza kumtunza.
IV
Ni kwa utunzaji halisi tu kwa ajili ya Mungu
ndipo mtu anaweza kuwa na utii halisi.
Na kutoka kwa utii kutatiririka
uwekaji wakfu halisi kwa Mungu,
na kutoka kwa uwekaji wakfu halisi kama huu,
kurudisha fadhila bila sharti.
Ni hivyo tu ndivyo mtu anaweza kujua kiini cha Mungu,
tabia, na Yeye ni nani.
Wanapomjua Muumba,
basi ibada ya kweli na kujisalimisha kunaweza kuchochea.
Ni wakati tu mambo haya yapo
ndipo mtu anaweza kweli kuweka kando njia yake mbovu.
V
Na mambo haya yote yanafanyiza mchakato mzima
wa "kumcha Mungu na kujitenga na maovu"
na kutoa maudhui pia kwa ukamilifu wa
"kumcha Mungu na kujitenga na maovu."
Pia ni njia ambayo inahitaji kusafiriwa
ili kuwa mtu anayemcha Mungu na kujitenga na maovu.
kutoka kwa "Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tufuate: Umeme wa Mashariki, nyimbo za dini
0 意見:
Chapisha Maoni