Jumatano, 23 Januari 2019

Tafuta Kumpenda Mungu Bila Kujali Mateso Yako Ni Makubwa Vipi

I
Lazima uelewe ilivyo ya thamani kazi ya Mungu leo.
Watu walio wengi hawana ufahamu huo,
wakifikiria mateso hayana thamani:
Wanateswa kwa ajili ya imani yao,
wamekataliwa na dunia, nyumba zao pia zina shida,
siku zao za usoni hazina matumaini, hazina matumaini.
Mateso ya wengine yanakuwa mengi zaidi,
sana hadi wanataka kufa.
Hii inaonyeshaje moyo unaompenda Mungu?
Watu kama hawa hawana thamani!
Hawawezi kuvumilia, hawana ushupavu.
Ni wanyonge na dhaifu pia, na hawana nguvu.
Lazima uone wazi kuwa
Mungu anakutakasa kwa kukusafisha.
Hivyo lazima utoe ushuhuda wako kila wakati
Haijalishi unavyoteseka,
mradi tu bado unapumua,
ubaki mwaminifu kwa Mungu, uusujudie mkono Wake.
Huu ni upendo wa kweli kwa Mungu, ushuhuda wa kweli.
II
Mungu ana hamu ya binadamu kumpenda Yeye,
lakini wanapompenda, mateso yao yanaongezeka.
Upendo wao kwa Mungu unapoongezeka,
nao watapitia katika majaribu makubwa zaidi.
Kama unampenda Yeye kweli, mateso makubwa yatakuja.
Lakini usipompenda, pengine kila kitu
katika maisha kitaonekana sawa, sawa katika maisha.
Moyo wako utakapoanza kutenda kumpenda Mungu,
utakuta vitu vingi vikiwa ngumu.
Wewe ni mdogo kwa kimo na hivyo unasafishwa,
na huwezi kumridhisha Mungu.
Na unyonge ndani zaidi, huwezi kutimiza mapenzi ya Mungu.
Unahisi yako mbali, hivyo utasafishwa, utasafishwa.
Lazima uone wazi kuwa
Mungu anakutakasa kwa kukusafisha.
Hivyo lazima utoe ushuhuda wako kila wakati
katika siku za mwisho.
Haijalishi unavyoteseka,
mradi tu bado unapumua,
ubaki mwaminifu kwa Mungu, uusujudie mkono Wake.
Huu ni upendo wa kweli kwa Mungu,
ushuhuda wenye nguvu, ushuhuda wenye nguvu, ndio.
Eh, kuwa wa kweli kwa Mungu.
kutoka katika "Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

 kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza zaidi Nyimbo za injili

0 意見:

Chapisha Maoni