I
Hapo mwanzo Mungu aliumba binadamu.
Yaani, Aliumba baba wa binadamu Adamu,
aliyegusika na kuumbwa kikamilifu, aliyejaa uzima.
Adamu aliamka na utukufu wa Mungu ukimzunguka.
Alimuumba kutoka katika ubavu wa Adamu.
Yeye pia ni mzazi wa binadamu wote.
Hivyo watu ambao Mungu aliwaumba walijazwa kwa pumzi Yake na utukufu Wake.
Oo ni siku ya utukufu iliyoje, siku ya utukufu, wakati Mungu alipomuumba Adamu.
Oo ni siku ya utukufu iliyoje, siku ya utukufu, wakati Mungu alipomuumba Hawa.
Walikuwa wazazi wa binadamu, hazina Yake safi na ya thamani.
Walikuwa mume na mke, viumbe waishio wenye roho.
II
Mungu alimuumba Adamu kwa mikono Yake aliyejawa na utukufu na uzima.
Alikuwa ukamilifu unaogusika, kiumbe aliyepewa roho,
kiumbe aliyepewa pumzi, uwakilishi wa sura ya Mungu.
Hawa alikuwa kiumbe wa pili mwenye pumzi iliyotolewa na Mungu,
aliyejaa uzima na aliyejaa utukufu wa Mungu,
aliyetengenezwa kutoka kwa Adamu na sura sawa na ya Mungu,
kiumbe anayeishi na aliye na mifupa, mwili na roho.
Oo ni siku ya utukufu iliyoje, siku ya utukufu, wakati Mungu alipomuumba Adamu.
Oo ni siku ya utukufu iliyoje, siku ya utukufu, wakati Mungu alipomuumba Hawa.
Walikuwa wazazi wa binadamu, hazina Yake safi na ya thamani.
Walikuwa mume na mke, viumbe waishio wenye roho.
Walikuwa mume na mke, viumbe waishio wenye roho.
kutoka katika "Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza nyimbo nyimbo za injili
0 意見:
Chapisha Maoni