Alhamisi, 17 Januari 2019

Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Anakuwa Mwili Ndipo Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwandani Wake

I
Ni Wakati tu Mungu anapojinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani,
kumaanisha Anakuwa mwili ili kuishi kati ya wanadamu,
hapo ndipo wataweza kuwa wasiri Wake,
hapo ndipo wanaweza kuwa marafiki Zake wa karibu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
wakati ambapo Mungu ni wa Roho, ameinuliwa na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
ndipo mwanadamu ataweza kuelewa mapenzi Yake na kupatwa na Yeye.
II
Mungu hunena na kufanya kazi katika mwili,
Akishiriki furaha huzuni na dhiki ya mwanadamu,
Akiishi katika dunia yao, Akiwalinda na kuwaongoza,
hivyo Akiwatakasa ili wapate baraka Yake na wokovu.
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
wakati ambapo Mungu ni wa Roho, ameinuliwa na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
ndipo mwanadamu ataweza kuelewa mapenzi Yake na kupatwa na Yeye.
III
Kupitia kwa haya, mwanadamu anaweza kweli kuelewa mapenzi ya Mungu
na kuwa mwandani Wake; hili tu ndilo la utendaji.
Kama Mungu angekuwa asiyeonekana na asiyeguswa na mwanadamu,
mwanadamu angewezaje kuwa mwandani Wake? Je, fundisho hili ni bure?
Mwanadamu anawezaje kupata sifa ya kuwa mwandani wa Mungu
wakati ambapo Mungu ni wa Roho, ameinuliwa na mgumu kumwelewa?
Ni kwa kuwa tu mwili ulioumbwa sawa na mwanadamu
ndipo mwanadamu ataweza kuelewa mapenzi Yake na kupatwa na Yeye.
Ni Wakati tu Mungu anapokuwa mwili ndipo mwanadamu ataweza kuwa msiri Wake.
kutoka katika "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Sikiliza nyimbo nyimbo za injili

0 意見:

Chapisha Maoni