Jumatano, 24 Aprili 2019

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

I. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kupata Mwili kwa Mungu

4. Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya 

hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima 

apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” (Yohana 5:22).
Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (Yohana 5:27).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa sababu yule anayehukumiwa ni mwanadamu, mwanadamu ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa, na sio roho ya Shetani ambayo inahukumiwa moja kwa moja, kazi ya hukumu haifanywi katika ulimwengu wa roho, bali miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayefaa zaidi na anayestahili, kuliko Mungu mwenye mwili kwa ajili ya kuhukumu upotovu wa mwili wa mwanadamu. … Shetani anaweza tu kushindwa kabisa ikiwa Mungu mwenye mwili anahukumu upotovu wa mwanadamu. Kuwa sawa na mwanadamu akiwa na ubinadamu wa kawaida, Mungu mwenye mwili anaweza kumhukumu mwanadamu asiye na haki; hii ni ishara ya utakatifu Wake wa ndani na hali Yake ya kutokuwa wa kawaida. Ni Mungu pekee ndiye anayestahili, na aliye katika nafasi ya kumhukumu mwanadamu, maana Ana ukweli, na mwenye haki, na kwa hivyo Ana uwezo wa kumhukumu mwanadamu. Wale ambao hawana ukweli na haki hawafai kuwahukumu wengine.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hukumu Yangu kwako leo ni kwa sababu ya uchafu wako; kuadibu Kwangu kwako leo ni kwa sababu ya upotovu na uasi wako. Si kwa ajili ya kupata mamlaka na ufahari kati yenu wala kuwadhulumu kimakusudi, lakini ni kwa sababu ninyi mnaoishi katika nchi ya uchafu mmepakwa matope na uchafu mwingi sana. Mmepoteza tu uadilifu wenu, ubinadamu wenu, na hamko tofauti na nguruwe wanaoishi katika maeneo maovu mno. Ni kwa sababu ya hukumu hizi ndiyo mmeweza kuona kwamba Mungu ni Mungu mwenye haki, kwamba Mungu ni Mungu mtakatifu. Ni kwa sababu ya utakatifu na haki yake ndiyo Amewahukumu kuwapatilizia hasira Zake juu yenu. Kwa sababu Yeye anaweza kudhihirisha tabia yake ya haki anapotazama uasi wa wanadamu, na kwa sababu Anaweza kudhihirisha utakatifu Wake anapotazama uchafu wa wanadamu, hii inatosha kuonyesha kuwa Yeye ni Mungu Mwenyewe ambaye ni mtakatifu na bila doa, lakini pia Anaishi katika nchi ya uchafu. Kama Yeye angekuwa mtu Anayejitia matope pamoja na watu na kama Asingekuwa na dalili zozote za utakatifu au tabia ya haki, Asingekuwa na sifa kuhukumu uovu wa wanadamu au kuwa hakimu wa wanadamu. Kama mwanadamu angemhukumu mwanadamu, isingekuwa kama kuzaba kofi uso wake wenyewe? Mtu anawezaje kuwa na haki ya kuhukumu aina sawa ya mtu, ambaye ni mchafu tu kama yeye? Yule tu ambaye anaweza kuwahukumu wanadamu wote wachafu ni Mungu mtakatifu Mwenyewe, na mwanadamu angewezaje kuzihukumu dhambi za mwanadamu? Mwanadamu angewezaje kuona dhambi za mwanadamu, na angewezaje kuwa na sifa zinazostahili kumshutumu mwanadamu? Kama Mungu hangekuwa na haki ya kuzihukumu dhambi za mwanadamu, basi Angewezaje kuwa Mungu mwenye haki mwenyewe? Wakati ambapo tabia potovu za watu zinadhihirishwa, Yeye ananena kuwahukumu, na ni wakati huo tu ndipo wanaweza kuona kwamba Yeye ni mtakatifu.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza inapaswa iondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanahitajika kutupilia mbali tabia yao iliyopotoka, kwanza wanapaswa kujua tabia yao iliyopotoka. Ikiwa mwanadamu anafanya kazi ili kuondoa taswira za Miungu wasio dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu wasio dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kuwekwa hadharani, kutupwa, au kufukuzwa kabisa kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu ndiyo inayoweza kuchukua nafasi ya vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza ili kuwaruhusu watu kuvielewa taratibu, na ni kwa njia hii pekee ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu zinakuwa wazi pale ambapo Mungu mwenye mwili atafanya kazi Yake rasmi, kwa sababu ukawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume na nadharia za Mungu asiye dhahiri na wa kufikirika katika fikra za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kudhihirishwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni pevu kiasi gani, hawezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu zaidi kwa utendaji, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwanadamu na anaonyesha kikamilifu sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kupatwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. … Kwa hiyo, mwanadamu aliyepotoka anahitaji zaidi wokovu wa Mungu mwenye mwili, na anahitaji zaidi kazi ya moja kwa moja ya Mungu mwenye mwili. Mwanadamu anamhitaji Mungu mwenye mwili ili kumchunga, kumsaidia, kumnywesha maji, kumlisha, kumhukumu na kumwadibu, na anahitaji neema zaidi na wokovu mkubwa kutoka kwa Mungu mwenye mwili. Ni Mungu katika mwili pekee ndiye anayeweza kuwa msiri wa mwanadamu, mchungaji wa mwanadamu, msaada wa mwanadamu uliopo kila mara, na hii yote ni ulazima wa kufanyika mwili leo na katika nyakati za nyuma.
kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni hasa kwa sababu Shetani amepotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu ndiye Mungu anakusudia kuokoa, ya kuwa Mungu ni sharti achukue mwili ili afanye vita na Shetani na amchunge mwanadamu binafsi. Hii pekee ndiyo yenye manufaa kwa kazi Yake. Miili hiyo miwili ya Mungu ya nyama imekuwepo ili kumshinda Shetani, na pia imekuwepo ili imuokoe mwanadamu kwa njia bora zaidi. Hilo ni kwa sababu yule anayefanya vita na Shetani anaweza tu kuwa Mungu, awe ni Roho wa Mungu au ni mwili wenye nyama wa Mungu. Kwa kifupi, yule anayefanya vita na Shetani hawezi kuwa ni malaika, sembuse kuwa mwanadamu, ambaye amepotoshwa na Shetani. Malaika hawana uwezo wa kuifanya, na mwanadamu ni dhaifu hata zaidi. Kwa hivyo, ikiwa Mungu anataka kufanyia kazi maisha ya mwanadamu, kama Yeye anataka kuja duniani binafsi kumfinyanga mwanadamu, basi ni lazima Yeye binafsi apate mwili, yaani, lazima Yeye binafsi avae mwili, na kwa utambulisho Wake wa asili na kazi ambayo ni lazima afanye, aje miongoni mwa wanadamu na kumwokoa mwanadamu binafsi. La sivyo, kama ingekuwa ni Roho wa Mungu au mwanadamu ndiye aliyefanya kazi hii, basi vita hivi daima vingeshindwa kutimiza matokeo yake, na kamwe havingekwisha. Wakati tu Mungu anapata mwili ili Yeye binafsi aende kwa vita dhidi ya Shetani miongoni mwa watu ndipo mwanadamu anapata nafasi ya wokovu. Aidha, hapo tu ndipo Shetani anaaibishwa, na kuwachwa bila nafasi zozote za kutumia au mipango yoyote ya kutekeleza. Kazi inayofanywa na Mungu aliyepata mwili haiwezi kutimizwa na Roho wa Mungu, na hata zaidi haiwezi kufanywa na mtu yeyote mwenye mwili kwa niaba ya Mungu, kwa kuwa kazi ambayo Yeye hufanya ni kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, na ili kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Kama mwanadamu angeshiriki katika vita hivi, yeye angekimbia tu kwa vurugu ya huzuni, na hangekuwa na uwezo kabisa wa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Angekuwa hana uwezo wa kumwokoa mwanadamu kutoka msalabani, ama wa kushinda wanadamu wote waasi, lakini angeweza tu kufanya kazi kidogo ya zamani kwa mujibu wa kanuni, au vinginevyo kazi ambayo haihusiani na kushindwa kwa Shetani. Kwa hivyo, mbona ujisumbue? Kuna umuhimu gani wa kazi ambayo haiwezi kuwapata wanadamu, sembuse kumshinda Shetani? Na kwa hivyo, vita dhidi ya Shetani vinaweza kufanywa tu na Mungu Mwenyewe, na haviwezi kufanywa na mwanadamu kabisa. Wajibu wa mwanadamu ni kutii na kufuata, kwa kuwa mwanadamu hana uwezo wa kufanya kazi ya kuanzisha kipindi kipya, wala, zaidi ya hayo, hawezi kutekeleza kazi ya kupigana na Shetani. Mwanadamu anaweza tu kumtosheleza Muumba chini ya uongozi wa Mungu Mwenyewe, ambapo Shetani hushindiwa; hili ndilo jambo pekee ambalo mwanadamu anaweza kulitenda. Na kwa hivyo, kila wakati vita vipya vinapoanza, kila wakati kazi ya enzi mpya inapoanza, kazi hii inafanywa na Mungu binafsi, ambapo kupitia kazi hiyo Yeye huongoza enzi nzima, na kufungua njia mpya kwa ajili ya wanadamu wote.
kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi mzima ya mpangilio wa usimamizi wa Mungu inafanywa binafsi na Mungu mwenyewe. Awamu ya kwanza, kazi ya Enzi ya Sheria baada ya uumbaji wa ulimwengu, ilifanywa binafsi na Mungu. Mungu alitumia Musa kueneza sheria. Awamu ya pili ya kukomboa wanadamu wote pia ilitekelezwa binafsi na Mungu mwenye mwili; kando na Mungu kupata mwili, hakuna yule ambaye angetosha kufanya hivyo. Awamu ya tatu inaenda bila kusemwa: Kuna haja kuu zaidi ya mwisho wa kazi ya Mungu kufanywa na Mungu Mwenyewe. Kazi ya ukombozi, ushindi, kumpata, na kumkamilisha wanadamu wote inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kama hangefanya kazi hii Yeye binafsi, basi utambulisho wake hauwezi kuwakilishwa na mwanadamu, au kazi kufanywa na mwanadamu. Ili kumshinda Shetani, ili kumpata mwanadamu, na ili kumpa mwanadamu maisha ya kawaida duniani, Yeye binafsi humwongoza mwanadamu na hufanya kazi binafsi miongoni mwa wanadamu; kwa ajili ya mpangilio mzima wa usimamizi, na kwa kazi yake yote, ni lazima Yeye binafsi afanye kazi hii. Kama mwanadamu anaamini tu kuwa Mungu alikuja kuonekana naye na kumfurahisha, basi imani kama hizo hazina thamani, na hazina umuhimu. Maarifa ya mwanadamu ni ya kijuujuu mno! Ni kwa Mungu kutekeleza kazi Yeye mwenyewe ndivyo Mungu anaweza kufanya kazi yake vizuri na kikamilifu. Mwanadamu hana uwezo wa kuifanya kwa niaba ya Mungu. Kwa kuwa yeye hana utambulisho wa Mungu ama kiini Chake, hana uwezo wa kufanya kazi hii, na hata kama mwanadamu angekuwa na uwezo, haingekuwa na matokeo yoyote. Wakati wa kwanza Mungu kuwa mwili kwa ajili ya ukombozi, ilikuwa ni ili kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, ili kufanya mwanadamu aweze kutakaswa na kusamehewa dhambi zake. Kazi ya ushindi pia inafanywa na Mungu binafsi miongoni mwa wanadamu. Kama, katika awamu hii, Mungu angekuwa wa kusema tu ya unabii, basi nabii au mtu ambaye ana kipawa angepatikana wa kuchukua nafasi Yake; kama unabii pekee ungesemwa, mwanadamu angechukua nafasi ya Mungu. Lakini ikiwa mwanadamu binafsi angefanya kazi ya Mungu Mwenyewe na angefanya kazi kwa maisha ya mwanadamu, haingewezekana kwake kufanya kazi hii. Ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi: Ni lazima Mungu binafsi awe mwili ili kufanya kazi hii. Katika Enzi ya Neno, kama unabii pekee ungesemwa, basi Isaya au nabii Eliya wangepatikana wakifanya kazi hii, na hakungekuwepo na haja ya Mungu Mwenyewe kuifanya kazi hii binafsi. Kwa sababu kazi ambayo inafanywa katika awamu hii si tu ya kuongea kuhusu unabii, na kwa sababu ni ya umuhimu mkubwa zaidi kuwa kazi ya maneno inatumiwa kumshinda mwanadamu na kumshinda Shetani, kazi hii haiwezi fanywa na mwanadamu, na ni lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe binafsi. Katika Enzi ya Sheria Yehova alifanya sehemu ya kazi ya Mungu, ambapo baadaye alinena baadhi ya maneno na kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa manabii. Hiyo ni kwa sababu mwanadamu angemwakilisha Yehova katika kazi yake, na waonaji wangeweza kutabiri mambo na kutafsiri baadhi ya ndoto kwa niaba Yake. Kazi iliyofanyika hapo mwanzo haikuwa kazi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu moja kwa moja, na ilikuwa bila uhusiano na dhambi ya mwanadamu, na mwanadamu alitakiwa tu atii sheria. Kwa hivyo, Yehova hakuwa wa kuwa na mwili na kujifichua Mwenyewe kwa mwanadamu; badala yake Yeye aliongea moja kwa moja na Musa na wengine, akawafanya wao kusema na kufanya kazi kwa niaba yake, na kusababisha wao wafanye kazi moja kwa moja miongoni mwa wanadamu. Awamu ya kwanza ya kazi ya Mungu ilikuwa uongozi wa mwanadamu. Ilikuwa ndio mwanzo wa vita dhidi ya Shetani, lakini vita hivi vilikuwa bado kuanza rasmi. Vita rasmi dhidi ya Shetani vilianza na kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya kwanza, na vimeendelea hadi leo. Tukio la kwanza la vita hivi ni wakati Mungu aliyepata mwili alisulubishwa msalabani. Kusulubiwa kwa Mungu aliyekuwa mwili kulimshinda Shetani, na ilikuwa mafanikio ya awamu ya kwanza katika vita. Wakati Mungu mwenye mwili huanza kufanya kazi kwa mwanadamu moja kwa moja, huu ni mwanzo rasmi wa kazi ya kumrejesha mwanadamu, na kwa sababu hii ni kazi ya kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ni kazi ya kufanya vita na Shetani. Awamu ya kazi iliyofanywa na Yehova hapo mwanzo ilikuwa tu ya uongozi wa maisha ya mwanadamu duniani. Ilikuwa ndio mwanzo wa kazi ya Mungu, na hata ingawa ilikuwa bado haijashirikisha vita vyovyote, au kazi kuu yeyote, ilikuwa imeweka msingi kwa ajili ya kazi ya vita vijavyo. Baadaye, awamu ya pili ya kazi wakati wa Enzi ya Neema ilihusisha kubadilisha tabia ya zamani ya mwanadamu, ambayo ina maana kuwa Mungu Mwenyewe alitengeneza kwa ustadi kazi ya mwanadamu. Hii ilikuwa ni lazima ifanywe na Mungu: ilihitaji kuwa Mungu binafsi awe mwili, na kama hangekuwa mwili, hakuna mwingine angeweza kuchukua nafasi yake katika awamu hii ya kazi, kwa kuwa iliwakilisha kazi ya kupambana dhidi ya Shetani moja kwa moja. Kama mtu angekuwa amefanya kazi hii kwa niaba ya Mungu, wakati mwanadamu alisimama mbele ya Shetani, Shetani hangeweza kutii na haingewezekana kumshinda yeye. Ilibidi iwe Mungu aliyepata mwili aliyekuja kumshinda, kwa kuwa kiini cha Mungu mwenye mwili bado ni uungu, mwili Anaouvaa unamiliki uhai wa kibinadamu na huku ndiko kuonekana kwa Muumba; chochote kitakachotokea, utambulisho Wake na kiini havitabadilika. Na kwa hivyo, Yeye alivaa mwili na alifanya kazi ili kusababisha kujisalimisha kwa Shetani. Katika awamu ya kazi ya siku za mwisho, kama mwanadamu angefanya kazi hii na angefanywa kusema maneno moja kwa moja, basi hangeweza kusema maneno hayo, na kama unabii ungesemwa, basi haungekuwa na uwezo wa kumshinda mwanadamu. Kwa kuchukua mwili, Mungu huja kumshinda Shetani na kusababisha kujisalimisha kwake kamili. Wakati Yeye atamshinda Shetani kabisa, kumshinda mwanadamu kikamilifu, na kumpata mwanadamu kabisa, awamu hii ya kazi itakamilika na mafanikio kutimizwa. Katika usimamizi wa Mungu, mwanadamu hawezi kuwa naibu wa Mungu na kuwa Mungu wakati hayupo. Hasa, kazi ya kuongoza enzi na kuzindua kazi mpya ina haja kubwa zaidi kufanywa binafsi na Mungu Mwenyewe. Kumpa mwanadamu ufunuo na kwa kumpa yeye unabii kunaweza kufanywa na mwanadamu, lakini kama ni kazi ambayo ni lazima ifanywe na Mungu binafsi, kazi ya vita kati ya Mungu Mwenyewe na Shetani, basi kazi hii haiwezi kufanywa na mwanadamu. Katika awamu ya kwanza, wakati hakukuwepo na vita dhidi ya Shetani, Yehova binafsi aliongoza wana wa Israeli kutumia unabii uliosemwa na manabii. Baadaye, awamu ya pili ya kazi ilikuwa vita na Shetani, na Mungu Mwenyewe binafsi akawa mwili, kuja katika mwili, ili kufanya kazi hii. Chochote ambacho kinahusisha vita na Shetani pia kinahusisha kupata mwili kwa Mungu, ambayo ina maana kuwa vita hivi haviwezi kufanywa na mwanadamu. Kama mwanadamu angekuwa wa kufanya vita, hangeweza kumshinda Shetani. Jinsi gani yeye angekuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya Shetani wakati bado yumo chini ya utawala wake? Mwanadamu yumo katikati: Kama wewe utaegemea kuelekea kwa Shetani wewe ni wa Shetani, lakini wewe ukimridhisha Mungu wewe ni wa Mungu. Kama mwanadamu angeweza kuwa mbadala wake Mungu katika kazi ya vita hivi, je, yeye angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo? Kama angekuwa na uwezo, je, hangeangamia kitambo sana? Je, yeye si angekuwa ameingia katika ulimwengu wa jahanamu muda mrefu uliopita? Na hivyo, mwanadamu hana uwezo wa kuchukua nafasi ya Mungu katika kazi yake, ambayo ni kusema kwamba mwanadamu hana kiini cha Mungu, na kama ungepambana na Shetani hungeweza kumshinda Shetani. Mwanadamu anaweza tu kufanya baadhi ya kazi; anaweza kushinda baadhi ya watu, lakini hawezi kuwa mbadala wa Mungu katika kazi ya Mungu Mwenyewe. Je, ni jinsi gani mwanadamu atafanya vita na Shetani? Shetani ataweza kukushika mateka kabla hata hujaanza. Ni wakati Mungu Mwenyewe hufanya vita dhidi ya Shetani na mwanadamu kufuata na kutii Mungu katika msingi huu tu ndipo mwanadamu anaweza kupatwa na Mungu na kutoroka kutokana na vifungo vya Shetani. Kile mwanadamu anaweza kufikia kwa hekima yake na uwezo wake mwenyewe ni kidogo sana; hana uwezo wa kufanya mwanadamu akamilike, kumwongoza mwanadamu, na, zaidi ya hayo, kumshinda Shetani. Akili na hekima ya mwanadamu haviwezi kuharibu miradi ya Shetani, hivyo je, ni jinsi gani mwanadamu awezavyo kufanya vita na Shetani?
kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili 

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 意見:

Chapisha Maoni