Ijumaa, 8 Februari 2019

Watu Ambao Wamepatwa na Mungu Watafurahia Baraka za Milele

I
Kazi ya Mungu huendelea kwa miaka elfu sita,
na Aliahidi kwamba udhibiti wa yule muovu kwa wanadamu wote
pia haungekuwa kwa zaidi ya miaka elfu sita.
Na hivyo, wakati umekwisha. Mungu hataendelea wala kukawisha tena:
Katika siku za mwisho Atamshinda Shetani, achukue utukufu Wake wote,
na kurejesha roho zote ambazo ni Zake duniani
ili roho hizi zilizodhikishwa ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso,
na hivyo kazi Yake nzima duniani itahitimishwa.
Wataishi milele na Mungu, hawatatiwa doa tena.
Mkutano wa wale wote ambao wamepatwa na Mungu
watabaki baada ya upotezaji wa Shetani.
II
Mungu hatawaangamiza wanadamu wote; Yeye hataimaliza dunia nzima.
Atawaweka watu theluthi moja ambao wameshindwa na wanaompenda.
Atawafanya kuwa wenye kuzaa duniani, kama Waisraeli kabla.
Atatoa chakula na utajiri wote duniani.
Huru kutoka kwa madhara ya Shetani,
sehemu hii ya wanadamu wa dunia itapata yale Aliyowaahidi kabla.
Wanadamu walioshindwa watabaki; watafurahia baraka duniani.
Wao ni ushahidi wa ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani.
Wataishi milele na Mungu, hawatatiwa doa tena.
Mkutano wa wale wote ambao wamepatwa na Mungu
watabaki baada ya upotezaji wa Shetani.
III
Wanatoka kila nchi, kila dhehebu,
makabila tofauti yenye lugha tofauti,
wenye desturi tofauti na rangi tofauti za ngozi.
Wao ni tunda, ni tunda la wokovu wa Mungu.
Wao ni tunda, ni tunda la wokovu wa Mungu.
Mali iliyoibiwa ya vita itakombolewa na Mungu kutoka kwa mshiko wa Shetani.
Wao ndio matunda pekee kutoka kwa mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita.
Wameenea duniani kote. Watu walioungana tena.
Jumuiya ya wanadamu wasiofikiwa na nguvu mbaya ya Shetani.
Wao ni tunda, ni tunda la wokovu wa Mungu.
kutoka katika "Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Sikiliza zaidi nyimbo za injili

0 意見:

Chapisha Maoni