Jumamosi, 9 Februari 2019

Nyimbo za dini | Kizazi cha Siku za Mwisho Kimebarikiwa

Nyimbo za dini | Kizazi cha Siku za Mwisho Kimebarikiwa
              I
Yote ni neema ya Mungu kwamba tunaweza kuona uzuri wa Mungu,
kwamba leo tunatafuta kumpenda,
kwamba tunataka kukubali
mafunzo ya ufalme wa wakati wetu.
Hii yote ni neema ya Mungu,
na kwa hili Anatuinua.
Na ninapofikiria jambo hili, ninahisi uzuri wa Mungu.
Mungu anatupenda kweli, la sivyo hatungehisi jinsi tunavyohisi.
Tumebarikiwa
zaidi ya watakatifu, zaidi ya wengine.
Kwa hiyo Mungu daima anasema watu wa enzi ya mwisho wamebarikiwa.
II
Ni kutokana na hili tu ndiyo naona kwamba kazi hii yote
inafanywa binafsi na Mungu Mwenyewe,
na watu wanaongozwa na kuelekezwa na Mungu.
Namshukuru Mungu kwa hili,
na Ningependa ndugu Zangu wajiunge na Mimi kumsifu Mungu:
"Utukufu wote uwe Kwako, Mungu mkuu Mwenyewe!
Acha utukufu Wako uongezeke na ufichuliwe katika wale kati yetu
waliochaguliwa na kupatwa na Wewe."
Tumebarikiwa
zaidi ya watakatifu, zaidi ya wengine.
Kwa hiyo Mungu daima anasema watu wa enzi ya mwisho wamebarikiwa.
III
Mungu alitupangia kabla muda mrefu uliopita kutupata katika siku za mwisho,
hivyo ulimwengu wote uweze kuona utukufu wote wa Mungu ndani yetu.
Sisi ni matunda ya mpango wa Mungu, kilele cha kazi Yake.
Hadi sasa, Niligundua kiasi cha upendo Alio nao Mungu kwetu.
Neno la Mungu na kazi anayofanya juu yetu
yote inapita mara milioni ile ya miaka iliyopita.
Si katika Israeli, si hata na Petro,
kwamba Mungu alifanya kazi nyingi sana, Mungu aliwahi kusema mengi hivi.
Tumebarikiwa
zaidi ya watakatifu, zaidi ya wengine.
Kwa hiyo Mungu daima anasema watu wa enzi ya mwisho wamebarikiwa.
kutoka katika "Njia … (4)" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 意見:

Chapisha Maoni