Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | Miaka Elfu Mbili ya Kungoja
I
Kwamba Mungu amekuwa mwili hutikisa ulimwengu wa kidini,
inavuruga utaratibu wa kidini,
na inakoroga roho za wale wanaongoja kuonekana kwa Mungu.
Nani asiyeshangazwa na haya? Ni nani asiye na hamu ya kumwona Mungu?
Mungu ameishi kwa miaka mingi kati ya binadamu, lakini binadamu hafahamu.
Leo, Mungu Mwenyewe ametokea na kuonyesha utambulisho Wake kwa halaiki.
Hili lingekosaje kuleta furaha katika moyo wa mwanadamu?
Mungu wakati mmoja alishiriki furaha na dhiki na mwanadamu,
na leo Amepatanishwa tena na binadamu kufanya upya upendo Wake wa zamani na wao.
II
Baada ya Yeye kuondoka Uyahudi, Mungu alipotea bila kuonekana.
Watu wana hamu ya kumwona tena, lakini kwamwe hawajawahi kutarajia
kuungana na Yeye hapa na leo.
Hii itakosa vipi kuleta kumbukumbu za kitambo?
Miaka elfu mbili iliyopita,
Simoni mwana wa Yohana alikutana na Bwana Yesu, na akala na Bwana katika meza moja.
Miaka ya kufuatia iliongeza upendo wake Kwake.
Alimpenda Yesu kwa dhati.
Mungu ameishi kwa miaka mingi kati ya binadamu, lakini binadamu hafahamu.
Leo, Mungu Mwenyewe ameonekana ili kufanya upya upendo Wake wa kitambo na mwanadamu,
kufanya upya upendo Wake wa kitambo na mwanadamu.
kufanya upya upendo Wake wa kitambo na mwanadamu.
kutoka katika "Kazi na Kuingia (10)" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Sikiliza nyimbo: nyimbo za kuabudu
0 意見:
Chapisha Maoni