Jumapili, 3 Februari 2019

Wale tu Walio Watulivu Mbele ya Mungu Ndio Wanaolenga Maisha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ukweli,

Wale tu Walio Watulivu Mbele ya Mungu Ndio Wanaolenga Maisha

I
Wale ambao wanaweza kuwa na utulivu kweli mbele ya Mungu
ni wale ambao wanaweza kuwa huru kutokana na mahusiano ya kidunia,
na wanaweza kumruhusu Mungu akae ndani mwao.
Yeyote asiyeweza kuwa mtulivu mbele ya Mungu
ni mtu ambaye ni mwasherati, hajizuii.
Eh, na ni mwovu kabisa.
Wote wawezao kuwa watulivu mbele ya Mungu
ni waliojitolea ambao wanamtamani Mungu.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio wanaojali kuhusu maisha
na kufanya ushirika katika roho.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio walio na kiu kwa maneno ya Mungu.
Ndio wanaofuatilia ukweli.
II
Wale wanaopuuza kuwa watulivu mbele ya Mungu,
ambao hawatendi hili, ni watu wa bure ambao
wameshikana kabisa na dunia.
Hawana uhai, hawana uhai.
Hata kama wanadai kumwamini Mungu, si kweli,
maneno matupu tu yazungumzwayo kwa urahisi.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, Mungu huwakamilisha, huwakamilisha.
Wao hupewa baraka za kushangaza.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio wanaojali kuhusu maisha
na kufanya ushirika katika roho.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio walio na kiu kwa maneno ya Mungu.
Ndio wanaofuatilia ukweli.
III
Wale ambao kwa nadra hula na kunywa maneno ya Mungu,
ambao hawajali uingiaji wa maisha lakini hulenga mambo,
ni wanafiki bila siku zijazo.
Watu wa Mungu ni wale wanaoweza kweli kuwasiliana
Na Yeye na kuwa watulivu mbele Yake.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio wanaojali kuhusu maisha
na kufanya ushirika katika roho.
Wale wanaoweza kuwa watulivu, watulivu mbele ya Mungu
ndio walio na kiu kwa maneno ya Mungu.
Ndio wanaofuatilia ukweli.
kutoka katika "Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza nyimbo nyimbo za dini

0 意見:

Chapisha Maoni