Jumamosi, 2 Februari 2019

Hakuna Ayejali Kumwelewa Mungu kwa Utendaji

I
Mungu akikasirika, Anamkabili mwanadamu
asiyemsikiliza kwa makini Yeye,
ambaye anamfuata, anayedai kumpenda,
bado hupuuza Anachohisi.
Moyo Wake utaachaje kuumia?
Hata wale wanaotaka kuwa
wandani wa Mungu,
hawataki kuja karibu na Yeye,
kumjua au kuujali moyo Wake.
Mungu ni mpweke!
Si tu kwa sababu binadamu wapotovu wanampinga Mungu,
lakini wanaotafuta kuwa wa kiroho,
wale wanaotafuta kumjua Mungu,
hata walio tayari kutoa maisha yao kwa Mungu
hawaelewi mawazo Yake.
Hawajui tabia Yake au hisia Zake kamwe.
Oh, Mungu ni mpweke, Mungu ni mpweke.
II
Katika kazi ya usimamizi ya Mungu,
japo Hutenda kazi na kusema kwa dhati,
na kumkabili mwanadamu kwa ukunjufu,
wafuasi Wake wamejitenga Naye.
Hakuna anayetaka kumsogelea,
kuujali moyo Wake au hisia Zake.
Hata wale wanaotaka kuwa
wandani wa Mungu,
hawataki kuja karibu na Yeye,
kumjua au kuujali moyo Wake.
Mungu ni mpweke!
Si tu kwa sababu binadamu wapotovu wanampinga Mungu,
lakini wanaotafuta kuwa wa kiroho,
wale wanaotafuta kumjua Mungu,
hata walio tayari kutoa maisha yao kwa Mungu
hawaelewi mawazo Yake.
Hawajui tabia Yake au hisia Zake kamwe.
Eh, Mungu ni mpweke, Mungu ni mpweke.
III
Mungu akiwa na furaha, hakuna anayeshiriki furaha Yake.
Anapoeleweka visivyo, moyo Wake haufarijiki.
Moyo Wake unapoumia ndani,
hakuna aliye tayari kumsikiliza Akimwambia siri.
Katika maelfu ya miaka ya kazi ya usimamizi,
hakuna anayeelewa hisia za Mungu,
hakuna anayezielewa au kusimama pamoja Naye
kushiriki machungu Yake na furaha.
Hata wale wanaotaka kuwa
wandani wa Mungu,
hawataki kuja karibu na Yeye,
kumjua au kuujali moyo Wake.
Mungu ni mpweke!
Si tu kwa sababu binadamu wapotovu wanampinga Mungu,
lakini wanaotafuta kuwa wa kiroho,
wale wanaotafuta kumjua Mungu,
hata walio tayari kutoa maisha yao kwa Mungu
hawaelewi mawazo Yake.
Hawajui tabia Yake au hisia Zake kamwe.
Eh, Mungu ni mpweke, Mungu ni mpweke.
kutoka katika "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kuhusu Sisi: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza nyimbo nyimbo za dini

0 意見:

Chapisha Maoni