Jumatano, 6 Februari 2019

Ni Wale tu Wenye Imani ya Kweli Hupata Kibali cha Mungu

I
Musa alipogonga mwamba na maji yakatoka,
zawadi kutoka Yehova, ilikuwa ni kwa imani.
Daudi alipocheza muziki kumsifu Yehova,
kama moyo wake ukijaa furaha, ilikuwa ni kwa imani.
Ayubu alipopoteza mifugo wake na mali yake yote,
na akafunikwa na majipu, ilikuwa ni kwa imani.
Na wakati bado aliweza kusikia sauti ya Yehova,
na bado kuhisi utukufu Wake, ilikuwa ni kwa imani.
Ilikuwa ni kwa imani, kwa imani. Ilikuwa ni kwa imani na si chochote kingine, hasa imani tu!
Ilikuwa ni kwa imani, kwa imani. Ilikuwa ni kwa imani na si chochote kingine, hasa imani tu!
II
Petro alipomfuata Yesu na kutoa ushuhuda mtukufu
akiwa ametundikwa msalabani, ilikuwa ni kwa imani.
Yohana alipoona mfano mtukufu wa Mwana wa Adamu
na maono ya siku za mwisho, ilikuwa ni kwa imani yake.
Mataifa wanapogundua Mungu amerejea katika mwili
kufanya kazi Yake, pia ni kwa imani.
Wengi wamegongwa na neno la Mungu, kufarijiwa na kuokolewa,
ilikuwa pia ni kwa sababu ya imani.
Ilikuwa ni kwa imani, kwa imani. Ilikuwa ni kwa imani na si chochote kingine, hasa imani tu!
Ilikuwa ni kwa imani, kwa imani. Ilikuwa ni kwa imani na si chochote kingine, hasa imani tu!
kutoka katika "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza nyimbo nyimbo za kuabudu

0 意見:

Chapisha Maoni