Ijumaa, 11 Januari 2019

Ufalme Wote Washangilia

I
Dunia nzima inaporudi kwa Mungu,
Kazi Yake ulimwenguni kote inafuata sauti Yake.
Watu watatumia njia nyingi kupokea maneno Yake.
Wote wakaribia na kumwabudu Mungu. Hizi zitakuwa kazi za Mungu.
Mungu hataanza tena kamwe mahali pengine.
Atawafanya watu wote waje mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani,
na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma,
na watu watalazimika kutafuta njia ya kweli.
Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.
Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu
watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.
II
Jumuiya nzima ya kidini inakabiliwa na njaa kali,
na ni Mungu wa leo pekee aliye chemchemi ya maji yaliyo hai,
Akimiliki chemchemi itiririkayo milele iliyotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu,
na watu watakuja na kumtegemea Yeye.
Wanaopata neno la Mungu wana njia ya kutembea.
Wanaoishi bila neno la Mungu wanapaswa kutafuta njia ya kweli.
Maneno ya Mungu yataenea kwa nyumba nyingi. Yatajulikana kwa wote.
Ni hapo tu ndipo kazi Yake itaenea ulimwenguni kote.
Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.
Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu
watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.
III
Kwa hivyo kama kazi ya Mungu itapanuka, maneno Yake ni lazima yaenee.
Maneno ya Mungu yanaonyesha mamlaka yayo mnamo siku ya utukufu Wake.
Maneno Yake yote, tangu kabla ya enzi hadi sasa yatatimia.
Utukufu wote utakuwa kwa Mungu. Maneno Yake yatatawala duniani.
Waovu wataadibiwa na maneno yaliyo katika kinywa cha Mungu,
na wenye haki watabarikiwa kwa maneno yaliyo katika kinywa Chake.
Wote wataasisiwa na kukamilishwa,
yote yatatimizwa na maneno Yake.
Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.
Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu
watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.
Ufalme wote unaposhangilia, ni siku ya utukufu wa Mungu.
Mataifa na watu wanaopata habari njema ya Mungu
watabarikiwa na kutunzwa na Yeye.
kutoka katika "Ufalme wa Milenia Umewasili" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Soma Zaidi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Sikiliza zaidi nyimbo za injili

0 意見:

Chapisha Maoni