Nyimbo za dini | Unajua Chanzo cha Uzima wa Milele?
I
Mungu ndiye chanzo cha uzima wa mwanadamu; mbingu na nchi vinaishi kwa mamlaka Yake.
Hakuna kitu kilicho hai kinachoweza kujitoa kutoka kwa utawala na mamlaka ya Mungu.
Haijalishi wewe ni nani, kila mtu lazima amtii Mungu,
atii utawala Wake, udhibiti Wake na amri Zake!
Pengine una hamu ya kupata uzima na ukweli,
mtafute Mungu ambaye unaweza kumwamini ili kupokea uzima wa milele.
Kama unataka kupata uzima wa milele, tafuta chanzo chake na kule Mungu aliko.
Mungu ni uzima usiobadilika, Yeye pekee ndiye aliye na njia ya uzima.
Kwani Mungu ni njia ya uzima, Mungu ni njia ya uzima wa milele.
II
Yeye ni mkuu katika ulimwengu.
Yeye ni uti wa mgongo katika kila moyo, na Anaishi na kupumua kati ya mwanadamu.
Hapo tu ndipo Ataweza kuleta maisha mapya na kumwongoza mwandamu katika njia ya uzima.
Mungu anakuja duniani kuishi kati ya mwanadamu, ili mwanadamu aweze kupata uzima na uwepo.
Mungu anaamuru ulimwengu kutumikia kazi Yake ya usimamizi.
Sio mbinguni tu ama katika moyo wa mwanadamu, Mungu anaishi katika dunia hii.
Kukataa ukweli huu hakutakuletea njia ya ukweli wala uzima.
Kama unataka kupata uzima wa milele, tafuta chanzo chake na kule Mungu aliko.
Mungu ni uzima usiobadilika, Yeye pekee ndiye aliye na njia ya uzima.
Kwani Mungu ni njia ya uzima, Mungu ni njia ya uzima wa milele.
Kama unataka kupata uzima wa milele, tafuta chanzo chake na kule Mungu aliko.
Mungu ni uzima usiobadilika, Yeye pekee ndiye aliye na njia ya uzima.
Kwani Mungu ni njia ya uzima, Mungu ni njia ya uzima wa milele.
Mungu anaamuru ulimwengu, Yeye ndiye njia pekee ya uzima.
Mungu ni njia ya uzima wa milele.
kutoka katika "Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Tufuate: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
0 意見:
Chapisha Maoni