Jumamosi, 26 Januari 2019

Nyimbo za dini | Ufuatiliaji Unaopaswa Kufuatwa na Waumini

 Nyimbo za dini | Ufuatiliaji Unaopaswa Kufuatwa na Waumini

I
Mungu amefanya kazi kiasi gani ndani yako?
Umepitia kiasi gani, na kuonja kiasi gani?
Anakujaribu, anakufunza nidhamu. Anatekeleza kazi Yake kwako.
Kama mmoja anayetafuta ukamilishaji wa Mungu, je, unaweza kuonyesha matendo Yake yote,
kuwaruzuku wengine kwa njia ya uzoefu na kujitumia mwenyewe kufanya kazi Yake?
Kufuatilia kuonyesha matendo ya Mungu.
Kuwa onyesho halisi na dhihirisho la Yeye.
Na ustahili kutumiwa na Yeye.
II
Ili kuwa na ushahidi kwa ajili ya matendo ya Mungu, kuwaonyesha wengine kupitia uzoefu wako,
na maarifa na mateso ambayo umestahimili.
Tafuta hili na Atakufanya uwe mkamilifu.
Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu ili upate tu baraka Zake mwishowe,
inathibitisha kuwa mtazamo wako wa imani katika Mungu si safi.
Kufuatilia kuonyesha matendo ya Mungu.
Kuwa onyesho halisi na dhihirisho la Yeye.
Na ustahili kutumiwa na Yeye.
III
Unapaswa daima kujaribu kutafuta jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha halisi
na jinsi ya kumridhisha Anapoonyesha mapenzi Yake kwako.
Unapaswa kutafuta kutoa ushahidi kwa maajabu Yake na hekima Yake,
jifunze jinsi ya kuonyesha nidhamu Yake na ushughulikiaji Wake kwako.
IV
Kama upendo wako ni ili tu uweze kushiriki utukufu Wake, hili haliwezi kufikia mahitaji Yake.
Shuhudia matendo Yake, tosheleza mahitaji Yake,
na upitie kazi Yake inayofanywa kwa watu.
Iwe ni maumivu, machozi, au huzuni, yapitie yote kwa vitendo.
Unahitaji kufanya hizi kazi zote ili uweze kuwa shahidi wa Mungu.
Kufuatilia kuonyesha matendo ya Mungu.
Kuwa onyesho halisi na dhihirisho la Yeye.
Na ustahili kutumiwa na Yeye.
Kufuatilia kuonyesha matendo ya Mungu.
Kuwa onyesho halisi na dhihirisho la Yeye.
Na ustahili kutumiwa na Yeye. Na ustahili kutumiwa na Yeye.
kutoka katika "Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 意見:

Chapisha Maoni