Jumamosi, 5 Januari 2019

Mmempa Mungu Nini Kama Malipo?

I
Mungu amekuwa kati yenu
kwa majira kadhaa ya kupuputika na ya kuchipua.
Ameishi nanyi kwa muda mrefu.
Mbele Yake ni matendo yenu mangapi maovu yamenyiririka?
Maneno ya dhati mnayoyasema, yanarudisha mwangwi katika masikio ya Mungu.
Mamilioni ya matakwa yenu hayawezi kuhesabiwa,
juu ya madhabahu Yake yamewekelewa.
Na bado hakuna kujitolea, hakuna chembe ya uaminifu
Madhabahu yake mnayalalia.
Matunda ya imani yenu yako wapi?
Mmepokea neema ya Mungu isiyo na mwisho,
mkaona siri Zake za mbinguni.
Mungu amewaonyesha moto wa mbinguni,
lakini hataki kuwachoma.
Ni kiasi gani mmerudisha kwa Mungu?
Ni kiasi gani mmempa kwa hiari?
II
Kama mmeshikilia chakula alichowapa Mungu, mnamtolea hicho,
mkisema ni malipo yenu kwa kazi ngumu,
mmempa yote mliyo nayo.
Imekuwaje hamjui
kwamba vyote mnavyompa Mungu, michango yenu yote
ni vitu vyote mlivyoiba kutoka kwa madhabahu Yake.
Sasa mnavitoa kwa Mungu.
Si mnamdanganya?
Yeye hufurahia kile kilicho juu ya madhabahu Yake
na sio faida ya kazi ya bidii mnayoitoa.
Mmepokea neema ya Mungu isiyo na mwisho,
mkaona siri Zake za mbinguni.
Mungu amewaonyesha moto wa mbinguni,
lakini hataki kuwachoma.
Ni kiasi gani mmerudisha kwa Mungu?
Ni kiasi gani mmempa kwa hiari?
III
Kweli mnathubutu kumdanganya Mungu,
hivyo basi Anawezaje kuwasamehe?
Mungu anawezaje kuvumilia hili kwa muda mrefu zaidi?
Amewatolea kila kitu.
Amefungua kila kitu kwenu.
Ameyakimu mahitaji yenu,
na Amefungua macho yenu.
Lakini mnapuuza dhamiri yenu na kumdanganya.
Mmepokea neema ya Mungu isiyo na mwisho,
mkaona siri Zake za mbinguni.
Mungu amewaonyesha moto wa mbinguni,
lakini hataki kuwachoma.
Ni kiasi gani mmerudisha kwa Mungu?
Ni kiasi gani mmempa kwa hiari?
kutoka kwa "Tabia Yako Ni Duni Sana!" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

0 意見:

Chapisha Maoni