Jumanne, 8 Januari 2019

Enzi Tofauti, Kazi Tofauti ya Mungu

Katika siku za mwisho, hasa ni ukweli
kwamba "Neno linakuwa mwili"
ambalo limetimizwa na Mungu.
I
Kupitia kazi Yake halisi duniani,
Mungu humfanya mwanadamu kumjua,
humfanya mwanadamu kushiriki naye,
na humfanya mwanadamu aone matendo Yake halisi.
Humfanya mwanadamu aone kwa dhahiri
kwamba wakati mwingine Yeye huonyesha au
haonyeshi ishara na kutenda maajabu.
Hili linategemea enzi.
Hili laonyesha kwamba Mungu ana uwezo
wa kuonyesha ishara na maajabu,
lakini hubadilisha kufanya Kwake kazi
kutegemeza kwa kazi Yake na enzi.
'Sababu ni enzi tofauti
na hatua tofauti ya kazi ya Mungu,
matendo ambayo Mungu hufanya wazi ni tofauti.
Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio katika ishara, maajabu au miujiza,
lakini ni katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya, wakati wa enzi mpya.
II
Katika hatua ya sasa ya kazi,
Haonyeshi ishara au maajabu
Alionyesha katika enzi ya Yesu,
kwa sababu kazi Yake katika enzi hiyo ilikuwa tofauti.
Mungu hafanyi kazi hiyo sasa.
Na wengine hudhani kwamba Hawezi kuifanya
au si Mungu kwani Haifanyi.
Si huo ni uongo tu?
Mungu anaweza kuonyesha ishara na maajabu,
lakini Anafanya kazi katika enzi tofauti
na hivyo Hafanyi kazi hiyo.
'Sababu ni enzi tofauti
na hatua tofauti ya kazi ya Mungu,
matendo ambayo Mungu hufanya wazi ni tofauti.
Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio katika ishara, maajabu au miujiza,
lakini ni katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya, wakati wa enzi mpya.
III
Ee, mwanadamu huja kumjua Mungu
kwa njia ambayo Mungu hufanya kazi.
Maarifa haya huleta kwa mwanadamu
imani katika Mungu, katika kazi na vitendo Vyake.
'Sababu ni enzi tofauti
na hatua tofauti ya kazi ya Mungu,
matendo ambayo Mungu hufanya wazi ni tofauti.
Imani ya mwanadamu kwa Mungu sio katika ishara, maajabu au miujiza,
lakini ni katika kazi Yake halisi wakati wa enzi mpya,
wakati wa enzi mpya, wakati wa enzi mpya.
kutoka katika "Kuijua Kazi ya Mungu Leo" katika Neno Laonekana katika Mwili


 kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya


Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 意見:

Chapisha Maoni