Jumanne, 29 Januari 2019

Kutenda Ukweli Kunahitaji Gharama ya Kweli

I
Taabu zinapokuja, anza kuomba:
"Ee Mungu! Ningependa kukuridhisha Wewe,
kustahimili taabu ili kuufurahisha moyo Wako,
bila kujali ukubwa wa taabu ninazokabili.
Hata kama ni lazima nitoe maisha yangu,
bado ninafanya kazi ili kukuridhisha Wewe."
Kwa uamuzi huu, unapoomba,
utasimama imara katika ushuhuda wako.
Kila wakati ukweli unapowekwa katika matendo,
kila usafishaji, kila wakati wanapojaribiwa,
kila wakati kazi ya Mungu iko kwao,
watu hustahimili maumivu makubwa.
Hili ni jaribio, vita vya ndani,
gharama ya kweli ya kulipwa.
II
Ikiwa kuna kitu unachotaka kusema,
lakini hakihisi kuwa sahihi ndani,
ikiwa hakiwafaidi ndugu zako,
ikiwa wanaweza kuumizwa, usiseme chochote,
ukiona afadhali kuwa na uchungu na kupambana ndani,
kwani maneno haya hayawezi kuridhisha mapenzi ya Mungu.
Kila wakati ukweli unapowekwa katika matendo,
kila usafishaji, kila wakati wanapojaribiwa,
kila wakati kazi ya Mungu iko kwao,
watu hustahimili maumivu makubwa.
Hili ni jaribio, vita vya ndani,
gharama ya kweli ya kulipwa.
III
Vita vya ndani vinaendelea,
lakini uko tayari kuumia,
kuacha kile unachopenda,
kustahimili taabu ili kumridhisha Mungu,
kuteseka lakini kutoridhisha mwili kamwe,
kuuridhisha moyo wa Mungu,
hivyo utafarijiwa pia.
Huku ni kulipa gharama inayotakiwa na Mungu.
Kila wakati ukweli unapowekwa katika matendo,
kila usafishaji, kila wakati wanapojaribiwa,
kila wakati kazi ya Mungu iko kwao,
watu hustahimili maumivu makubwa.
Hili ni jaribio, vita vya ndani,
gharama ya kweli ya kulipwa, eh~
gharama ya kweli ya kulipwa.
kutoka katika "Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tufuate: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Sikiliza nyimbo nyimbo za injili

0 意見:

Chapisha Maoni