Alhamisi, 10 Januari 2019

Mahitaji ya Mwisho ya Mungu kwa Mwanadamu

I
Ikiwa wewe ni mtendaji huduma, unaweza kumhudumia Mungu kwa uaminifu,
bila kuwa mwenye kukaa tuau kutenda tu bila kuwa na dhati?
Ukigundua kuwa Mungu huwa hakushukuru,
bado utaweza kukaa na kufanya huduma maisha yote?
Kama ungetumia juhudi nyingi lakini Mungu bado hakuthamini,
bado ungeendelea kumfanyia kazi katika giza?
Ukitumia vitu fulani kwa ajili ya Mungu
lakini matakwa yako madogo hayajakidhiwa,
basi utakata tamaa na kwa hasira kumlaumu Mungu?
Kama daima u mwaminifu sana na una upendo kwa Mungu
na bado unapitia uchungu wa ugonjwa, kufukarishwa kwa maisha,
hata marafiki wanakuacha na familia yako inaondoka,
au misiba mingine inatokea, uaminifu wako, upendo, vitadumu?
II
Kama hakuna chochote ulichokiwaza kinacholingana na kile Mungu hufanya,
utaitembeaje njia yako ya baadaye?
Usipopata chochote kamwe
ambacho wakati mmoja ulitarajia kupokea kutoka kwa Mungu,
basi unaweza kuendelea kama mfuasi wa Mungu?
Ikiwa hujawahi kamwe kuona kusudi
na umuhimu wa kazi ya Mungu,
unaweza kumtii bila kutoa hukumu?
Unaweza kuyathamini maneno yote ya Mungu, mambo Aliyoyasema,
kazi yote ambayo Amekuwa akifanya Akiwa na mwanadamu?
Unaweza kuwa mfuasi mwaminifu wa Mungu,
kuwa tayari kuteseka kwa ajili Yake kwa maisha yako yote,
hata kama hutapata chochote?
Unaweza kwenda bila kufikiria, kufanya mipango
au kuandaa njia yako ya baadaye ya kusalia?
Unaweza kufanya hivi kwa ajili ya Mungu?
kutoka kwa "Tatizo Kubwa Sana: Usaliti (2)" katika Neno Laonekana katika Mwili

kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

0 意見:

Chapisha Maoni