Majonzi Yalivutia Upendo Wangu kwa Mungu(II)
Meng Yong Mkoa wa Shanxi
Maisha gerezani kwa kweli ni ya kuchukiza mno. Hawa walinzi wa gerezani waliendelea kuja na njia za kuwatesa watu: Nilibanwa katikati ya wafungwa wengine kadhaa wakati wa kulala usiku. Hata kugeuka kitandani kulikuwa kugumu. Kwa kuwa nilikuwa wa mwisho kufika, hata nililazimika kulala karibu na choo. Baada ya kukamatwa, sikulala kwa siku kadhaa na nikawa mwenye usingizi kiasi kwamba sikuweza kuvumilia na ningesinzia.
Wafungwa waliokuwa kwenye zamu ambao walikuwa wakilinda wangekuja kunibughudhi, kwa makusudi wakinipiga kidogo kichwani mpaka ningeamka kabla wao wangeondoka. Wakati mmoja, takriban saa tisa usiku, mfungwa mmoja aliniamsha kwa makusudi kwa sababu alitaka kuangalia ukubwa wa chupi yangu ndefu ili kuona kama ingemtosha. Alileta chupi yake ndefu iliyokuwa chafu na kuukuu ili kubadilishana na yangu. Hizi zilikuwa siku za baridi zaidi za mwaka, lakini hawa wafungwa bado walitaka kuchukua chupi yangu ndefu ya pekee niliyokuwa nayo. Watu waliokuwa huko ndani walikuwa wakatili kama wanyama. Walikuwa na tabia kali na mioyo miovu, bila hata chembe ya ubinadamu, kama pepo ambao huwatesa watu jahanamu ili kujifurahisha. Aidha, chakula huko kilikuwa hata kibaya zaidi kuliko kile kilichopewa mbwa na nguruwe. Mara ya kwanza, nilipokea nusu bakuli ya uji wa mchele, na niliona kwamba kulikuwa na mawaa mengi meusi ndani yake. Sikujua yalikuwa nini, na rangi ya uji huo pia ilikuwa nyeusi. Ilikuwa vigumu sana kuumeza. kwa kweli nilitaka kufunga kula wakati huo, lakini maneno ya Mungu yalinipa nuru: “…katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalijaa upendo na huba kama faraja ya mama, yakiamsha ujasiri wangu wa kukabiliana na mateso. Mungu hutaka niendelee kuishi, lakini nilikuwa dhaifu mno, daima nikitaka tulizo kupitia kifo. Hata sikujihifadhi kwa upendo mkubwa; bado ni Mungu ambaye hunipenda mno. Joto fulani kwa ghafla lilitapakaa moyoni mwangu, likinifanya kuwa na mhemko sana kiasi kwamba machozi yalinitoka machoni mwangu na kutiririka ndani ya uji wangu wa mchele. Kuguswa na upendo wa Mungu mara nyingine tena kulinipa nguvu. Lazima nile chakula hiki bila kujali jinsi kinavyoonja. Nilimaliza ule uji kwa pumzi moja. Baada ya kifungua kinywa, mkuu wa seli alifanya nisugue sakafu. Hizi ndizo zilizokuwa siku za baridi sana za mwaka na hakukuwa na maji moto, hivyo niliweza kutumia maji baridi tu kwa kitambaa cha kusafisha. Mkuu wa seli pia aliniamuru nisugue jinsi hii kila siku. Kisha, wanyang'anyi kadhaa wenye silaha walinilazimisha kukariri amri za gerezani. Kama sikuweza kuzikariri, wangenipiga ngumi na mateke; kupigwa makofi kwa uso kulikuwa hata kwa kawaida zaidi. Kukabiliana na mazingira kama hayo, mara nyingi nilishangaa ni nini ningepaswa kufanya ili kuziridhisha nia za Mungu. Usiku, nilivuta blanketi yangu juu ya kichwa changu na kuomba kimya kimya: Ee Mungu, Uliyaruhusu mazingira haya kunifika, hivyo nia Zako njema zinapaswa kuwa ndani ya mazingira haya. Tafadhali nifichulie nia Zako. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Maua na nyasi zinanyooka toka upande mmoja hadi upande mwingine wa miteremko, lakini mayungiyungi yanaongeza mng’aro kwa utukufu Wangu duniani kabla ya kufika kwa majira ya kuchipua—je, mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki? Je, angeweza kunishuhudia duniani kabla ya kurudi Kwangu? Je, angeweza kujitolea kwa ajili ya jina Langu katika nchi ya joka kubwa jekundu?” (“Tamko la Thelathini na Nne” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndio, nyasi na mimi vyote ni viumbe vya Mungu. Mungu alituumba ili tumdhihirishe Yeye, kumtukuza Yeye. Nyasi inaweza kuongeza mng'aro kwa utukufu wa Mungu duniani kabla ya majira ya kuchipua kufika, kumaanisha imetimiza wajibu wake kama kiumbe cha Mungu. Kazi yangu leo ni kuyatii matayarisho ya Mungu na kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani, kuacha kila mtu aone kwamba Shetani ni pepo aliye hai ambaye humdhuru na kumwangamiza mwanadamu, ilhali Mungu ni Mungu mmoja wa kweli ambaye humpenda na kumwokoa mwanadamu. Kuvumilia mateso haya yote na fedheha sasa si kwa sababu nimefanya kosa, lakini ni kwa ajili ya jina la Mungu. Kuvumilia mateso haya kunaleta sifa kuu. Jinsi Shetani anavyozidi kunifedhehesha, ndivyo ninavyopaswa kuzidi kusimama upande wa Mungu na kumpenda Mungu. Njia hiyo, Mungu anaweza kupata utukufu, na ningekuwa nimetimiza wajibu niliopaswa kuutimiza. Alimradi Mungu ana furaha na radhi, moyo wangu pia utapokea faraja. Niko tayari kuvumilia mateso ya mwisho ili kumridhisha Mungu na kuyaruhusu yote yatayarishwe na Mungu. Nilipoanza kufikiria jinsi hii, nilihisi kuguswa hasa moyoni mwangu, na kwa mara nyingine tena sikuweza kuyadhibiti machozi yangu: "Ee Mungu, Wewe unapendeza mno! Nimekufuata kwa miaka mingi sana, lakini sijawahi kamwe kuuhisi upendo wako wa huruma kama nilivyouhisi leo, au kuhisi kuwa karibu na Wewe kama nilivyohisi leo." Nilisahau kabisa mateso yangu na nikazama katika hisia hii ya kusisimua kwa muda mrefu, muda mrefu …
Siku yangu ya tatu katika kituo cha kizuizi, afisa mmoja wa magereza alinipeleka kwa ofisi yake. Nilipofika huko, nikaona zaidi ya watu kumi na wawili wakinitazama kwa macho ya pekee. Mmoja wao alishikilia kamera ya video mbele yangu upande wangu wa kushoto, huku mwingine akinijia na mikrofoni, akiuliza: "Kwa nini unamwamini Mwenyezi Mungu?" Hapo ndipo nilipogundua kwamba haya yalikuwa ni mahojiano ya vyombo vya habari, kwa hiyo nilijibu kwa unyenyekevu wa kujivunia: "Tangu nilipokuwa mdogo, daima nimekuwa chini ya dhuluma ya watu na kutothaminiwa, na nimewaona watu wakidanganyana na kutumiana kwa manufaa ya wao kwa wao. Nilihisi kwamba jamii hii ilikuwa ya uovu mno, yenye hatari mno; watu walikuwa wakiishi maisha matupu na ya kutojiweza, bila matumaini na bila malengo ya maisha. Baadaye, wakati mtu fulani aliponihubiria injili ya Mwenyezi Mungu, nilianza kuiamini. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, nimehisi waumini wengine wakinitendea kama familia. Hakuna mtu katika Kanisa la Mwenyezi Mungu anayenilia njama. Kila mtu anaelewana na mwenzake na ni wa upendo. Huwa wanatunzana, na hawana hofu ya kuzungumza kile kilicho akilini mwao. Katika neno la Mwenyezi Mungu nimepata kusudi na thamani ya maisha. Nadhani kumwamini Mungu ni kuzuri sana." Mwandishi huyo kisha akauliza: "Unajua ni kwa nini uko hapa?" Nikajibu: "Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, sijali tena juu ya faida na hasara za kibinafsi au heshima na aibu. Moyo wangu unageuka zaidi na zaidi kuelekea wema, na niko tayari zaidi na zaidi kuwa mtu mzuri. Kuona jinsi neno la Mwenyezi Mungu linaweza kwa hakika kuwageuza watu na kuwageuza kuwa watu wema, nilifikiria kuwa kama watu wote wanaweza kumwamini Mungu, basi nchi yetu pia ingekuwa ya utaratibu zaidi na kiwango cha uhalifu pia kingeshuka. Kwa hivyo, niliamua kuwaambia watu wengine habari hii njema, lakini sikujua kamwe kwamba kazi nzuri kama hiyo ingekuwa kinyume cha sheria nchini China. Na hivyo nilikamatwa na kuletwa hapa." Mwandishi huyo aliona kwamba majibu yangu hayakuwa na manufaa kwao, kwa hiyo mara moja akaacha mahojiano na akageuka na kwenda. Wakati huo, naibu mkuu wa Brigedi ya Usalama wa Taifa alikuwa na hasira kiasi kwamba alishinda akikanyaga kanyaga kwa nguvu. Alinitazama kwa ukali, akisaga meno na kunong'ona: "Wewe ngoja tu na uone!" Lakini sikuogopa maonyo yake au vitisho. Kinyume chake, nilihisi kuheshimiwa sana kwa kuweza kumshuhudia Mungu wakati kama huo, na aidha nilimpa Mungu utukufu kwa ajili ya kutukuzwa kwa jina la Mungu na kushindwa kwa Shetani.
Halijoto lilikuwa ya chini sana mnamo siku ya Januari 17. Kwa kuwa wale polisi waovu walikuwa wameninyang'anya koti langu la pamba, nilikuwa nimevaa chupi yangu ndefu tu na kuishia kushikwa na mafua. Nilishikwa na homa kali na pia sikuweza kuacha kukohoa. Usiku, nilijifunikia blanketi chakavu, nikivumilia maumivu ya ugonjwa huku pia nikifikiri juu ya uteswaji usio na mwisho wa wafungwa kwangu. Nilijihisi kuwa mwenye ukiwa sana na asiyejiweza. Taabu yangu ilipofikia kiwango fulani tu, wimbo wa neno la Mungu ulirudia katika sikio langu: "Kama ukinipa ugonjwa, na kuuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini kama kuadibu Kwako na hukumu vingeniacha, singekuwa na njia ya kwendelea kuishi. Kama singekuwa na kuadibu Kwako na hukumu, ningekuwa nimepoteza upendo Wako, upendo ambao ni wa kina sana kwangu kuuweka katika maneno. Bila upendo Wako, ningeishi chini ya utawala wa Shetani …" ("Ujuzi wa Petro wa Kuadibu na Hukumu" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Hii ilikuwa sala halisi na ya kweli ya Petro mbele ya Mungu. Petro kamwe hakuongozwa na mwili. Alichokipenda sana na kukithamini kilikuwa ni kuadibu na hukumu za Mungu. Alimradi kuadibu na hukumu za Mungu hazikumwacha, moyo wake ungepata faraja kubwa mno. Sasa napaswa pia kufuata mfano wa kufuatilia na ufahamu wa Petro. Mwili umepotoshwa na bila kuepuka utaoza. Hata kama nikikabiliwa na ugonjwa na kupoteza uhuru wangu, ni mateso ninayostahili kuvumilia. Lakini nikipoteza kuadibu na hukumu za Mungu, hiyo ni sawa na kupoteza uwepo wa Mungu na upendo, na pia ina maana ya kupoteza fursa ya kutakaswa. Hicho ndicho kichungu mno. Chini ya nuru ya Mungu, kwa mara nyingine tena nilipitia upendo wa Mungu. Mimi pia nilichukia udhaifu wangu na kutokuwa na thamani, na niliona kuwa asili yangu ni ya ubinafsi sana, bila kuonyesha nadhari yoyote kamwe kwa hisia za huzuni za Mungu. Siku iliyofuata, wafungwa wengine kadhaa katika seli hiyo hiyo waliugua, lakini homa yangu kali ilipungua kimiujiza. Nilihisi utunzaji na ulinzi wa Mungu kwangu na pia niliona maajabu ya kazi ya Mungu. Kwa siku chache zilizofuata, skonsi ndogo za kuokwa kwa mvuke tulizokuwa tukipata zikawa hata ndogo zaidi, hivyo baadhi ya wafungwa wakanza kulalamika: "Tangu kufika kwa 'Askofu,' kwanza tulipata baa na sasa tuna njaa." Walisema lote lilikuwa ni kosa langu na kwamba lingekuwa la maana tu kama ningepata hukumu ya kifo. Usiku mmoja, mchuuzi mmoja alikuja kwa dirisha na mkuu wa seli akanunua hemu nyingi sana, nyama ya mbwa, mapaja ya kuku, na kadhalika. Hatimaye, akaniamuru nilipe. Nilimwambia sikuwa na pesa, kwa hiyo akasema kwa ukali: "Ikiwa huna fedha nitakutesa polepole!" Siku iliyofuata, alinilazimisha nioshe shuka za kitanda, nguo, na soksi. Maafisa wa magereza katika kituo hicho cha kizuizi pia walinilazimisha niwaoshee soksi zao. Katika kituo hicho cha kizuizi, ilinibidi kuvumilia mapigo yao karibu kila siku. Wakati wowote ambapo sikuweza kuvumilia tena, daima ningeongozwa ndani na maneno ya Mungu: “Lazima umfanyie Mungu wajibu wako wa mwisho wakati wa muda wako hapa duniani. Zamani, Petro alisulubiwa juu chini kwa ajili ya Mungu; hata hivyo, unapaswa kumridhisha Mungu mwishowe, na utumie nguvu zako zote kwa ajili ya Mungu. Kiumbe anaweza kumfanyia Mungu nini? Kwa hiyo unapaswa kujitolea kwa rehema ya Mungu mapema iwezekanavyo. Maadamu Mungu anafurahia na Anapendezwa, basi mwache Afanye chochote Atakacho. Wanadamu wana haki gani ya kulalamika?” (“Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Moja” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa nguvu isiyopimika. Ingawa mara kwa mara ningekuwa mwenye uelekeo wa mashambulizi, aibu, shutuma, na mapigo ya wafungwa, nafsi yangu iliweza kufanikisha faraja na furaha. Kama mtiririko wa joto wenye nguvu, upendo wa Mungu ulinisukuma kuendelea, ukiniwezesha kwa kweli kuhisi kwamba upendo wa Mungu ni mkubwa mno.
Asubuhi moja, afisa mmoja wa magereza aliwasilisha hasa karatasi moja ya gazeti. Wafungwa walitoa tabasamu la uovu na sura mbaya kwa sauti ya kudhihaki kusoma maneno kutoka kwa gazeti na kumkashifu na kumkufuru Mwenyezi Mungu. Nilikuwa na hasira sana ndani kiasi kwamba nilianza kusaga meno yangu. Wafungwa walikuja kuniuliza yote hayo yalikuwa ni nini, na nikasema kwa sauti kubwa: "Hii ni kampeni ya kuharibu jina na Chama cha Kikomunisti!" Kuwasikilizwa wafungwa hawa wote wakifuata tu umati na kufifisha ukweli na kumkufuru Mungu kwa kuzungumza lugha moja na shetani, ilivyoonekana niliona kuja kwa mwisho wao. Kwa kuwa dhambi ya kumkufuru Mungu haitasamehewa kamwe, yeyote anayeikosea tabia ya Mungu atapata adhabu kali zaidi na malipo! Kwa kufanya hivi, Chama cha Kikomunisti kinawapeleka watu wote wa China kwa adhabu yao ya mwisho, kikiufichua kabisa tabia yake ya kweli kama pepo mla roho! Baadaye polisi aliyehusika na kesi yangu alinihoji tena. Wakati huu, hakutumia mateso ili kujaribu kulazimisha ungamo, na badala yake akabadilika kwa kutumia uso "wenye huruma" kuniuliza: "Ni nani kiongozi wako? Nitakupa fursa nyingine. Ukituambia, utakuwa sawa. Nitakuonyesha huruma kubwa. Ulikuwa hauna hatia mwanzoni, lakini watu wengine walikusaliti. Kwa hiyo ni kwa nini unawaficha? Unaonekana kama mtu mwenye tabia nzuri. Kwa nini utoe maisha yako kwa ajili yao? Ukituambia, unaweza kwenda nyumbani. Kwa nini ukae hapa na kuteseka?" Hawa wanafiki waliona kwamba njia ya kuwa wagumu haikufua dafu, kwa hiyo waliamua kujaribu njia ya kuwa wapole. Wao kwa kweli wamejaa hila za ujanja na ni stadi wa zamani wa njama na hila! Kuona huo uso wake wa unafiki kuliujaza moyo wangu na chuki kwa kundi hili la pepo. Nikamwambia: "Nimekuambia kila kitu ninachokijua. Sijui chochote kingine." Baada ya kuona mtazamo wangu thabiti, alijua kwamba hangeweza kupata chochote kutoka kwangu, kwa hiyo akaondoka kwa huzuni.
Baada ya kuzuiliwa kwa kituo cha kizuizi kwa nusu mwezi, niliachiliwa tu baada ya polisi kuiuliza familia yangu kulipa yuan 8,000 kama fedha za dhamana. Lakini walinionya nisiende mahali popote na kuwa ni lazima nikae nyumbani na kuhakikisha kuwa ningepatikana wakati wowote. Siku niliyoachiliwa, maafisa wa magereza hawakunipa chakula chochote cha kula kwa makusudi, huku wafungwa wakisema: "Mungu wako ni wa ajabu. Hatukukuwa wagonjwa, lakini sisi sote tukawa wagonjwa hapa. Ulikuja hapa kama umejaa magonjwa, lakini sasa unaondoka bila ugonjwa wowote. Hongera! "Katika wakati huu, moyo wangu ukawa na shukurani hata zaidi na kujaa sifa kwa Mungu! Mjomba wangu ni mlinzi wa jela. Aliendelea kushuku kuwa nimeachiliwa kwa sababu baba yangu alikuwa na uhusiano maalum na mtu fulani mwenye nguvu, ama sivyo hakuna jinsi ambavyo ningeweza kuachiliwa kutoka gereza la usalama wa juu katika kipindi cha nusu mwezi—angalau sana ingekuwa miezi mitatu. Familia yangu nzima ilijua vizuri sana kwamba hii ilikuwa imedhamiriwa na kudura ya Mungu na kwamba alikuwa ni Mungu akifichua kazi Yake nzuri kwangu. Niliona wazi kwamba haya yalikuwa mashindano kati ya Mungu na Shetani. Bila kujali jinsi Shetani alivyo katili na muovu, daima atashindwa na Mungu. Kuanzia wakati huo kwendelea, nikaamini kuwa kila kitu nilichokabiliwa nacho kilikuwa sehemu ya matayarisho ya Mungu. Mwishoni mwa mwezi Mei, mwaka wa 2011, chini ya uhalifu wa "kuvuruga utaratibu wa jamii," polisi wa Kikomunisti walifanya nihukumiwe kifungo cha mwaka mmoja wa kuelimishwa tena kupitia kazi, cha kutumikiwa nje ya gereza chini ya uchunguzi, na kifungo hicho kikiwekwa kando kwa miaka miwili.
Baada ya kupitia mateso haya na taabu, nilikuwa na ufahamu na niliweza kutambua asili ya uovu ya Chama cha kukana Mungu cha Kikomunisti cha China, na nikakuza chuki kubwa kwake. Yote kinayofanya ni kutumia mbinu za nguvu nyingi ili kudumisha hali yake ya kutawala, kushambulia na kukandamiza matendo yote ya haki na kuchukia sana ukweli kwa kuvuka mpaka. Ni adui mkuu mno wa Mungu. Ili kiweze kufanikisha lengo lake la kuwadhibiti watu kwa kudumu, huwa kiko tayari kufanya chochote kuizuia na kuivuruga kazi ya Mungu duniani, kwa ukali kikiwakandamiza na kuwatesa waumini wa Mungu, kikitumia tuzo na adhabu, kikiwafanya wengine kufanya kinavyotaka, kikisema kitu kimoja huku kikifanya kingine, na kuficha udanganyifu na hila daima. Utofautishaji kinaoutoa huniruhusu kuona hata zaidi kwamba ni neno la Mungu pekee linaloweza kuwaletea watu maisha wakati wa mateso. Wakati watu wako katika hali ya kukata tamaa kabisa au wako karibu kufa, neno la Mungu ni kama maji ya uzima, likistawisha mioyo mikavu ya watu. Pia ni kama kiowevu cha miujiza ambacho kinaweza kuponya majeraha ya roho za watu, kikiwaokoa kutoka kwa hatari, kuyachochea maisha yao kwa imani na ujasiri, na kikiwaletea nguvu isiyo na kikomo, kikiwawezesha kufurahia utamu wa neno la Mungu katikati ya mateso yao, ambacho kinaweza kutoa faraja kwa roho zao, na kuwafanya wahisi kwamba nguvu ya neno la Mungu ni nyingi mno na haina mwisho. Katika kipindi hiki cha mwezi nusu cha maisha katika jela, kama Mungu hangekuwa na mimi, akitumia maneno Yake kunikumbusha, kunipa nuru, na kunitumainisha, hakuna jinsi ambavyo asili yangu dhaifu ingeweza kuhimili mateso kama hayo. Kama si kwa Mungu kunitunza na kunilinda, hakukuwa na jinsi yoyote ambavyo mwili wangu hafifu na dhaifu ungekuwa umehimili mateso na ukatili wa wale polisi waovu, ambayo, hata kama hayakuwa yamenitesa hadi kufa, yangekuwa yameacha mwili wangu ukiwa mgonjwa na uliojeruhiwa. Lakini Mungu kwa ajabu alinilinda katika siku hizo za giza sana, ngumu mno, na hata aliuponya ugonjwa wangu wa awali. Mungu kwa kweli ni mwenye uweza mno! Kwa kweli upendo Wake kwangu ni wa kina mno, mkubwa mno! Kwa kweli sijui jinsi ya kuonyesha shukrani yangu kwa Mungu, na ninaweza tu kusema kwa dhati: Ee Mungu, natumaini kukupenda Wewe zaidi milele! Bila kujali ni jinsi gani njia mbele ilivyo ya kuparuza na ya matuta au ni kiasi gani cha mateso ni lazima nivumilie, nitaitii matayarisho Yako na kudhamiria kukufuata Wewe hadi mwisho!
Ingawa mwili wangu wa kimwili umeteseka kidogo kupitia uzoefu huu, faida nilizopata kutoka kwao ni ya umuhimu. Hili ni jambo kuu katika njia yangu ya kumwamini Mungu, na vilevile mwanzo mpya katika njia yangu ya kumwamini Mungu. Ninahisi kwa kina kwamba, katika miaka kumi ambayo nimemwamini Mungu, sijawahi kamwe kuutambua vyema upendo wa Mungu kwa kina kama ninavyoutambua leo, na kwa kweli nilihisi kuwa thamani na maana ya kumwamini Mungu, kumfuata Mungu, na kumwabudu Mungu ni kubwa mno; na zaidi ya hayo, sijawahi kamwe kuwa tayari kutafuta kumpenda Mungu na kutoa maisha yangu yaliyobaki ili kufidia upendo wa Mungu kwa kiwango nifanyavyo leo. Ningependa kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati na sifa. Utukufu wote na sifa kwa Mwenyezi Mungu!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: ushuhuda wa Umeme wa Mashariki
0 意見:
Chapisha Maoni