Majonzi Yalivutia Upendo Wangu kwa Mungu(I)
Meng Yong Mkoa wa Shanxi
Mimi kwa asili ni mtu mwaminifu, ikiwa ndiyo maana nimekuwa nikidhulumiwa daima na watu wengine. Kwa sababu hiyo, nimeonja dharau ya ulimwengu wa mwanadamu na nilihisi maisha yangu yakiwa matupu na bila maana. Baada ya mimi kuanza kumwamini Mwenyezi Mungu, kupitia kusoma maneno ya Mungu na kuishi maisha ya kanisa, nilifurahia ari na shangwe katika moyo wangu ambazo sikuwahi kamwe kuzihisi kabla.
Kuona ndugu wa kiume na wa kike wa Kanisa la Mwenyezi Mungu wakipendana wenyewe kwa wenyewe kama familia kulinifanya nitambue kwamba Mungu peke yake ndiye mwenye haki, na kwamba ni katika Kanisa la Mwenyezi Mungu tu kuliko na mwanga. Kupitia miaka kadhaa ya kupata binafsi uzoefu wa kazi ya Mwenyezi Mungu, nimekuja kufahamu kwa kweli kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kuwabadilisha watu na kuwaokoa watu. Mwenyezi Mungu ni upendo, na ni wokovu. Ili watu wengi waweze kufurahia upendo wa Mungu na kutafuta na kupokea wokovu wa Mungu, ndugu zangu wa kiume na wa kike na mimi wote tulijitahidi kadri tulivyoweza kueneza injili, lakini hatukutazamia kukamatwa na kuteswa na Chama cha Kikomunisti.
Mnamo Januari 12, mwaka wa 2011, ndugu kadhaa wa kiume na wa kike nami tulifululiza kwa gari hadi mahali fulani ili kueneza injili, na tukaishia kuripotiwa na watu waovu. Muda mfupi baadaye, serikali ya wilaya iliwaagiza maafisa kutoka idara mbalimbali za kutekeleza sheria, kama vile kikosi cha kupambana na uovu, vikosi vya usalama wa kitaifa, kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya, vikosi vya polisi wa silaha, na idara ya polisi ya mahali palepale, kuja hapo kwa magari zaidi ya 10ya polisi kutukamata. Wakati ndugu mmoja na mimi tulipokuwa tukiandaa kuondoka kwa gari, tuliona polisi saba au wanane wakitumia virungu kumpiga ndugu mwingine kwa ghadhabu. Wakati huo, maafisa wanne wa polisi walikimbia haraka na kulizuia gari letu. Mmoja wale maafisa waovu akachomoa vifunguo vya gari bila maelezo yoyote, na kutuamuru tuekae ndani ya gari bila kutoka. Wakati huo, niliona kuwa yule ndugu alikuwa tayari amepigwa kiasi kwamba alikuwa ameketi sakafuni, bila kusogea. Sikuweza kujizuia kujaa hasira za kudhulumiwa na kukimbia nje ya gari ili kuzuia vurugu yao, lakini wale polisi mabaya waliupinda mkono wangu na kunisukuma kando. Nilijaribu kutoa hoja nao: "Chochote kilicho, tunaweza kukizungumzia. Mnawezaje kuanza tu kuwapiga watu?" Walijibu kwa kupiga ukelele kwa ukali: "Fanya haraka na kurudi kwa gari lako, utapata yako hivi punde!" Baadaye, walitupeleka kwa kituo cha polisi, na gari letu pia lilikamatwa kwa nguvu.
Baada ya saa tatu usiku huo, maafisa wawili wa polisi walikuja kunihoji. Walipoona kwamba hawakuweza kupata taarifa yoyote muhimu kutoka kwangu, walishikwa na wasiwasi na kughadhabika, walisaga meno yao kwa hasira wakiapiza: "Potelea mbali, tutakushughulikia baadaye!" Kisha wakanifungia katika chumba cha kusubiri. Saa tano u nusu usiku, maofisa wawili walinipeleka katika chumba kisichokuwa na kamera za upelelezi. Nilihisi kuwa wangetumia nguvu dhidi yangu, hivyo nikaanza kumwomba Mungu mara kwa mara moyoni mwangu, nikimwomba Mungu kunilinda. Wakati huu, afisa mmoja mwovu wa polisi aliyeitwa Jia kwa jina la ukoo alinijia kunihoji: "Je, umekuwa katika gari la Volkswagen Jetta katika siku kadhaa zilizopita?" Nikajibu hapana, na akapiga ukelele kwa ghadhabu: "Watu wengine tayari wamekuona, na bado unalikana?" Baada ya kusema hivyo, alinipiga kofi kwa ukali kwa uso. Yote niliyohisi yalikuwa ni maumivu makali kwa shavu langu. Kisha akanguruma kwa sauti kubwa: "Hebu tuone jinsi ulivyo mjeuri!" Alichukua ukanda mpana hali akiongea na kunichapa nao kwa uso wangu, sijui ni mara ngapi nilichapwa, lakini sikuweza kujizuia kupiga kelele kwa maumivu mara kwa mara. Walipoona jambo hili, waliuvuta ukanda kuziba kinywa changu. Maafisa wachache waovu wakati huo wakaufunika mwili wangu kwa blanketi kabla ya kunipiga kwa ghadhabu na virungu vyao, wakiacha tu walipochoka mno ili kupumua. Nilikuwa nimepigwa vibaya sana kiasi kwamba kichwa changu kilikuwa kikizunguka na mwili wangu uliumia kana kwamba kila mfupa ulikuwa umetawanywa. Wakati huo sikujua ni kwa nini walikuwa wakinitendea jinsi hii, lakini baadaye niligundua kwamba walinifunika kwa blanketi ili kuzuia pigo hilo kuacha alama mwilini mwangu. Kuniweka ndani ya chumba bila upelelezi, kukitia kinywa changu kifaa cha kuninyamazisha, na kunifunika kwa blanketi—yote ni kwa sababu waliogopa kwamba matendo yao maovu yangefichuka. Sikuwahi kufikiria kamwe kwamba "polisi wa watu" wenye heshima wangeweza kuwa wadanganyifu sana na waovu! Wale wanne walipochoka kutokana na kunipiga, walibadilisha utaratibu wa kunitesa: Maofisa wawili wa waovu waliupinda mkono mmoja wangu na kuuvuta juu kwa nguvu, wakati maafisa wengine wawili waovu waliuinua ule mkono wangu mwingine juu ya bega kwa nyuma na kuuvuta chini kwa nguvu. Lakini mikono yangu miwili haikuweza kuvutwa pamoja kwa vyovyote, kwa hiyo walidunga goti la nguvu kwa mkono wangu. Yote niliyosikia ilikuwa ni "klik," na mikono yangu miwili ikahisi kama imeambuliwa. Liliumiza sana kiasi kwamba nilikaribia kufa. Waliita aina hii ya mateso "Kubeba Upanga Mgongoni," ambayo watu wa kawaida hawangeweza kuvumilia kabisa. Haikunichukua muda mrefu kupoteza hisia katika mikono yangu yote miwili. Hili bado halikutosha kwao kuacha, kwa hiyo waliniamuru nipige magoti ili kuongeza maumivu yangu. Nilikuwa na maumivu mengi kiasi kwamba mwili wangu wote ulikuwa katika hali ya woga na wasiwasi, kichwa changu kilikuwa kinavuma, na fahamu zangu zilianza kuwa na kiwi kidogo. Niliwaza: Nimeishi kwa miaka mingi sana; ingawa nimekuwa na magonjwa daima, sijawahi kuwa na hisia ya kutoweza kudhibiti fahamu zangu mwenyewe. Je, niko karibu kufa? Baadaye, kweli sikuweza kuvumilia tena, hivyo nilifikiria kutafuta faraja kwa njia ya kifo. Wakati huo, neno la Mungu lilinipa nuru kutoka ndani: “Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani…. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu!” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu kwa ghafla yanifanya kuchangamka na kutambua kuwa njia yangu ya kufikiri haikulingana na nia za Mungu na ingeweza tu kumfanya Mungu ahuzunike na kusikitika. Kwa sababu katikati ya maumivu haya na mateso, kile ambacho Mungu anataka kuona siyo mimi kutafuta kifo, lakini kwamba naweza kuvumilia aibu na kuubeba mzigo mzito, na kwamba ninaweza kuutegemea mwongozo wa Mungu ili kupambana na Shetani, kumshuhudia Mungu, na kumfanya Shetani aaibike na kushindwa. Kutafuta kifo kungekua kuanguka ndani ya mpango wa Shetani, kumaanisha nisingeweza kushuhudia na badala yake ningekuwa mfano wa aibu. Baada ya kuelewa nia za Mungu, nikamwomba Mungu kimya kimya: Ee Mungu! Uhalisi umeonyesha kuwa asili yangu ni dhaifu mno. Sina hiari na ujasiri wa kuteswa kwa ajili Yako na nilitaka kufa kutokana na maumivu kidogo ya kimwili tu. Sasa najua kwamba siwezi kufanya chochote kuaibisha jina Lako na ni lazima niwe shahidi na kukuridhisha Wewe bila kujali ni shida gani ninayostahiki. Lakini wakati huu, mwili wangu wa kimwili una maumivu makubwa mno na ni dhaifu, na ninajua kuwa ni vigumu sana kushinda mapigo ya pepo hawa peke yangu. Tafadhali nipe ujasiri na nguvu zaidi ili niweze kukutegemea Wewe kumshinda Shetani. Naapa kwa maisha yangu kwamba sitakusaliti au kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike. Nilipomwomba Mungu mara kwa mara, moyo wangu polepole ukawa mtulivu. Wale polisi waovu wakaona kwamba nilikuwa napumua kwa shida na waliogopa kwamba wangelazimika kuwajibika kama ningekufa, kwa hiyo walikuja kuzifungua pingu zangu. Lakini mikono yangu ilikuwa tayari imekauka, na pingu zilikuwa zimejikaza sana hivi kwamba zilikuwa ngumu sana kufungua. Ikiwa wangetumia nguvu zaidi mikono yangu ingevunjika. Wale polisi waovu wanne walichukua dakika kadhaa kufungua pingu kabla ya kuniburuta na kunirudisha kwa chumba cha kusubiri masaili.
Alasiri iliyofuata, wale polisi walinisingizia "kosa la jinai" kunirudisha kwa nyumba yangu ili kuivamia, na kisha wakanipeleka kwa kituo cha kizuizi. Mara tu nilipoingia kituo cha kizuizi, maafisa wanne wa magereza wakaninyang'anya jaketi langu la pamba, suruali, viatu, na saa, ikiwa ni pamoja na yuan1,300 taslimu nilizokuwa nimebeba. Wanilazimisha nivae sare ya gerezani ya kawaida na kunilazimisha kutumia yuan 200 kununulia blanketi kutoka kwao. Baadaye, hao maafisa wa magereza walinifungia pamoja na wanyang’anyi wenye silaha, wauaji, wabakanaji, na walanguzi wa madawa ya kulevya. Nilipoingia katika seli yangu, nikaona wafungwa kumi na wawili wenye vipara wakiniangalia kwa chuki. Mazingira yalikuwa mazito na ya kuogofya, na nikahisi wasiwasi kwa ghafla. Wawili wa viongozi wa seli wakanijia na kuniuliza: "Je, uko hapa kwa nini?" Nikasema: "Kueneza injili." Bila neno jingine, mmoja wao akanichapa kofi kwa uso mara mbili, na kusema: "Wewe ni 'Askofu,' sivyo?" Wafungwa wengine wote wakaanza kucheka kishenzi na kunitania kwa kuuliza: "Kwa nini usimruhusu Mungu wako akuokoe kutoka hapa?" Katikati ya kuzomewa na kudhihakiwa, kiongozi wa seli akanichapa kofi kwa uso mara chache zaidi. Kutoka wakati huo kwendelea, wakanipa jina la utani "Askofu" na mara nyingi walinifedhehesha na kunidhihaki. Kiongozi mwingine wa seli akaona sapatu nilizokuwa nimevaa na akapiga ukelele kwa kujigamba: "Hujui thamani yako kabisa. Je, unastahili kuvaa viatu hivi? Vivue! "Alipokuwa akilisema, alinilazimisha kuvivua na kuvaa jozi ya sapatu zao kuukuu. Pia walipeana blanketi yangu kwa wafungwa wengine kutumia. Wale wafungwa walipigania blanketi yangu kwa fujo, na hatimaye nilisalia na blanketi kuukuu ambayo ilikuwa nyembamba, iliyopasuka, chafu, na yenye kunuka. Wakichochewa na hao maafisa wa magereza, wafungwa hawa walinipa shida za aina zote na mateso. Taa iliwaka daima katika seli usiku, lakini kiongozi mmoja wa seli kwa ghafula akaniambia kwa tabasamu la uovu: "Nizimie hiyo taa." Kawa kuwa sikuweza kufanya hivyo (hata hakukuwa na swichi), walianza kunicheka na kunidhihaki tena. Siku iliyofuata, wafungwa vijana wachache walinilazimisha kusimama kwa kona moja na kukariri amri za gerezani, wakitishia: "Utakiona cha mtema kuni kama hutazikariri kwa siku mbili." Sikuweza kujizuia kutishika, na nilivyozidi kufikiria yale niliyoyapitia siku chache zilizopita, ndivyo nilivyozidi kuogopa. Jambo nililoweza kufanya tu lilikuwa kuendelea kumwita Mungu na kumwomba Mungu anilinde ili niweze kulishinda jambo hili. Wakati huu, wimbo wa neno la Mungu ulinipa nuru: "Kama bado unaweza kumpenda Mungu bila kujali kama wewe uko gerezani au u mgonjwa, kama wengine wanakucheka kwa dharau au kukukashifu, au kama umefikia mwisho wa matumaini, hili linamaanisha kwamba moyo wako umemgeukia Mungu" ("Je, Moyo Wako Umemgeukia Mungu" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Neno la Mungu lilinipa nguvu na kunionyesha njia kwangu kuitenda—kutafuta kumpenda Mungu na kutoa moyo wangu kwa Mungu! Katika wakati huo, ghafla ikawa dhahiri kabisa moyoni mwangu: Kwa Mungu kuruhusu mateso haya kunifika hakukuwa ni kunitia uchungu au kwa makusudi kunifanya kuteseka, lakini kunifundisha kuugeuza moyo wangu kwa Mungu katika mazingira kama hayo, ili niweze kuupinga udhibiti wa mvuto wa giza wa Shetani na hivyo moyo wangu bado unaweza kuwa karibu na Mungu na kumpenda Mungu, kamwe kutolalamika na daima kutii mipango na matayarisho ya Mungu. Nikiwa na hili katika akili yangu, sikuogopa tena. Bila kujali ni jinsi gani Shetani hunitendea, yote nitakayoshughulikia ni kuhusu kuipa nafsi yangu kwa Mungu na kutenda kadiri niwezavyo kutafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, kamwe kutomwinamia Shetani.
Maisha gerezani kwa kweli ni ya kuchukiza mno. Hawa walinzi wa gerezani waliendelea kuja na njia za kuwatesa watu: Nilibanwa katikati ya wafungwa wengine kadhaa wakati wa kulala usiku. Hata kugeuka kitandani kulikuwa kugumu. Kwa kuwa nilikuwa wa mwisho kufika, hata nililazimika kulala karibu na choo. Baada ya kukamatwa, sikulala kwa siku kadhaa na nikawa mwenye usingizi kiasi kwamba sikuweza kuvumilia na ningesinzia. Wafungwa waliokuwa kwenye zamu ambao walikuwa wakilinda wangekuja kunibughudhi, kwa makusudi wakinipiga kidogo kichwani mpaka ningeamka kabla wao wangeondoka. Wakati mmoja, takriban saa tisa usiku, mfungwa mmoja aliniamsha kwa makusudi kwa sababu alitaka kuangalia ukubwa wa chupi yangu ndefu ili kuona kama ingemtosha. Alileta chupi yake ndefu iliyokuwa chafu na kuukuu ili kubadilishana na yangu. Hizi zilikuwa siku za baridi zaidi za mwaka, lakini hawa wafungwa bado walitaka kuchukua chupi yangu ndefu ya pekee niliyokuwa nayo. Watu waliokuwa huko ndani walikuwa wakatili kama wanyama. Walikuwa na tabia kali na mioyo miovu, bila hata chembe ya ubinadamu, kama pepo ambao huwatesa watu jahanamu ili kujifurahisha. Aidha, chakula huko kilikuwa hata kibaya zaidi kuliko kile kilichopewa mbwa na nguruwe. Mara ya kwanza, nilipokea nusu bakuli ya uji wa mchele, na niliona kwamba kulikuwa na mawaa mengi meusi ndani yake. Sikujua yalikuwa nini, na rangi ya uji huo pia ilikuwa nyeusi. Ilikuwa vigumu sana kuumeza. kwa kweli nilitaka kufunga kula wakati huo, lakini maneno ya Mungu yalinipa nuru: “…katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana” (“Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalijaa upendo na huba kama faraja ya mama, yakiamsha ujasiri wangu wa kukabiliana na mateso. Mungu hutaka niendelee kuishi, lakini nilikuwa dhaifu mno, daima nikitaka tulizo kupitia kifo. Hata sikujihifadhi kwa upendo mkubwa; bado ni Mungu ambaye hunipenda mno. Joto fulani kwa ghafla lilitapakaa moyoni mwangu, likinifanya kuwa na mhemko sana kiasi kwamba machozi yalinitoka machoni mwangu na kutiririka ndani ya uji wangu wa mchele. Kuguswa na upendo wa Mungu mara nyingine tena kulinipa nguvu. Lazima nile chakula hiki bila kujali jinsi kinavyoonja. Nilimaliza ule uji kwa pumzi moja. Baada ya kifungua kinywa, mkuu wa seli alifanya nisugue sakafu. Hizi ndizo zilizokuwa siku za baridi sana za mwaka na hakukuwa na maji moto, hivyo niliweza kutumia maji baridi tu kwa kitambaa cha kusafisha. Mkuu wa seli pia aliniamuru nisugue jinsi hii kila siku. Kisha, wanyang'anyi kadhaa wenye silaha walinilazimisha kukariri amri za gerezani. Kama sikuweza kuzikariri, wangenipiga ngumi na mateke; kupigwa makofi kwa uso kulikuwa hata kwa kawaida zaidi. Kukabiliana na mazingira kama hayo, mara nyingi nilishangaa ni nini ningepaswa kufanya ili kuziridhisha nia za Mungu. Usiku, nilivuta blanketi yangu juu ya kichwa changu na kuomba kimya kimya: Ee Mungu, Uliyaruhusu mazingira haya kunifika, hivyo nia Zako njema zinapaswa kuwa ndani ya mazingira haya. Tafadhali nifichulie nia Zako. Wakati huo, maneno ya Mungu yalinipa nuru: “Maua na nyasi zinanyooka toka upande mmoja hadi upande mwingine wa miteremko, lakini mayungiyungi yanaongeza mng’aro kwa utukufu Wangu duniani kabla ya kufika kwa majira ya kuchipua—je, mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki? Je, angeweza kunishuhudia duniani kabla ya kurudi Kwangu? Je, angeweza kujitolea kwa ajili ya jina Langu katika nchi ya joka kubwa jekundu?” (“Tamko la Thelathini na Nne” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndio, nyasi na mimi vyote ni viumbe vya Mungu. Mungu alituumba ili tumdhihirishe Yeye, kumtukuza Yeye. Nyasi inaweza kuongeza mng'aro kwa utukufu wa Mungu duniani kabla ya majira ya kuchipua kufika, kumaanisha imetimiza wajibu wake kama kiumbe cha Mungu. Kazi yangu leo ni kuyatii matayarisho ya Mungu na kumshuhudia Mungu mbele ya Shetani, kuacha kila mtu aone kwamba Shetani ni pepo aliye hai ambaye humdhuru na kumwangamiza mwanadamu, ilhali Mungu ni Mungu mmoja wa kweli ambaye humpenda na kumwokoa mwanadamu. Kuvumilia mateso haya yote na fedheha sasa si kwa sababu nimefanya kosa, lakini ni kwa ajili ya jina la Mungu. Kuvumilia mateso haya kunaleta sifa kuu. Jinsi Shetani anavyozidi kunifedhehesha, ndivyo ninavyopaswa kuzidi kusimama upande wa Mungu na kumpenda Mungu. Njia hiyo, Mungu anaweza kupata utukufu, na ningekuwa nimetimiza wajibu niliopaswa kuutimiza. Alimradi Mungu ana furaha na radhi, moyo wangu pia utapokea faraja. Niko tayari kuvumilia mateso ya mwisho ili kumridhisha Mungu na kuyaruhusu yote yatayarishwe na Mungu. Nilipoanza kufikiria jinsi hii, nilihisi kuguswa hasa moyoni mwangu, na kwa mara nyingine tena sikuweza kuyadhibiti machozi yangu: "Ee Mungu, Wewe unapendeza mno! Nimekufuata kwa miaka mingi sana, lakini sijawahi kamwe kuuhisi upendo wako wa huruma kama nilivyouhisi leo, au kuhisi kuwa karibu na Wewe kama nilivyohisi leo." Nilisahau kabisa mateso yangu na nikazama katika hisia hii ya kusisimua kwa muda mrefu, muda mrefu …
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
0 意見:
Chapisha Maoni