Jumapili, 23 Septemba 2018

ushuhuda wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza(II)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mateso

Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza(II)

Mo Zhijian Mkoa wa Guangdong
Tulipofika kwa kikosi cha SWAT, wale polisi waovu walitulazimisha kuvua nguo zetu zote na kisha wakafunga mikono yetu pingu na kuzungusha silisili kwa miguu yetu. Halafu walitulazimisha kurukaruka mizunguko mitatu kuzunguka uga ili kutufedhehesha. Baadaye, walitutenganisha ndani ya seli za gereza. Watu waliofungiwa katika seli za gereza wote walikuwa wauaji, wote walikuwa kama pepo na madubwana. Wale polisi waovu wakawaagiza wafungwa kunitesa, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, hao wafungwa hawakukosa tu kunidhulumu, lakini kwa kweli walinitunza. Baada ya siku nne, hao polisi waovu walijaribu kunilazimisha kumsaliti Mungu na kuwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini singezungumza. Walinichukua pamoja na ndugu mwingine na wakatuvuta ndani ya uga ambako walitufunga pingu mikononi na kuizungusha minyororo kwa miguu yetu. Mifuko myeusi iliwekwa juu ya vichwa vyetu na wakatuning'iniza kutoka kwa mti katikati ya uga. Kwa kichaa cha ukatili, waliweka siafu kote mtini, ambao kwa uendelevu walitambaa juu ya miili yetu wakituuma. Mateso ya elfu kadhaa za maumo ya siafu yalikuwa sawa na mateso ya elfu nyingi za mishale kupitia moyoni, jambo ambalo lilifanya kifo kionekane cha kuvutia zaidi kuliko kuishi. Niliweza tu kumwomba Mungu kwa uwezo wangu wote kuulinda moyo wangu na roho, ili Angenipa hiari na nguvu katika mateso yangu, akiniruhusu kupinga kumsaliti Mungu. Kwa wakati huu, maneno ya Mungu yalionekana katika mawazo yangu: “ili utukufu Wangu uweze kujaza ulimwengu, watu wote wanapitia taabu ya mwisho kwa ajili Yangu Mimi. Je unaelewa mapenzi Yangu? Haya ndiyo matakwa ya mwisho ambayo Nataka kutoka kwa mwanadamu, ambalo ni kusema, Natumai kwamba watu wote wanaweza kutoa ushuhuda wenye nguvu, unaovuma Kwangu mbele ya joka kubwa jekundu, kwamba waweze kujitolea wenyewe Kwangu kwa mara ya mwisho, na kutimiza matakwa Yangu kwa mara nyingine ya mwisho. Je, nyinyi mnaweza kufanya hili kweli? Nyinyi hamkuweza kuuridhisha moyo Wangu katika siku zilizopita—je, mnaweza kuvunja mpangilio huu katika mara ya mwisho?” (“Tamko la Thelathini na Nne” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalisababisha moyo wangu kujazwa na nguvu. Mungu aliteseka kufuatiliwa kwa kila njia zilizowezekana na serikali ya CCP ili kutuokoa. Alikuwa hana mto na hakuwa na mahali pa kuita nyumbani. Leo ninaweza kuteseka na Kristo; huu ni upendo wa Mungu na ni kuinuliwa kwangu na Mungu. Alimradi ninaweza kumtukuza Mungu, nitakuwa na furaha na niko tayari kufa. Nililitegemea neno la Mungu ili kupitia kila dakika na sekunde ya maumivu hayo. Tulining'inizwa juu ya mti huo kwa siku mbili usiku na mchana. Siku ya tatu, sikuweza kustahimili tena. Ilikuwa mapema msimu wa baridi wakati huo na mvua ilikuwa inanyesha na yote niliyovaa ilikuwa ni vazi moja bila bitana. Nilikuwa nimening'inizwa kutoka kwa mti huo kwa miguu yangu mitupu na sikuwa nimepata chochote cha kula au kunywa. Mateso ya njaa na baridi pamoja na maumivu yasiyovumilika yalinifanya nitake kufa; yote niliyoweza kufanya ni kuomba kwa kila njia. Niliogopa kwa kina kwamba kwa sababu ya udhaifu wa mwili, singeweza kuvumilia mateso na ningemsaliti Mungu. Katikati ya maumivu yangu, nikakumbuka mtume Stefano kutoka kwa Enzi ya Neema. Alipigwa kwa mawe hadi kufa na umati kwa sababu alikuwa akieneza injili ya Bwana Yesu. Kabla ya kufa, alimwomba Mungu aikubali roho yake. Kwa hiyo, nikamwomba Mungu: "Ee Mungu, mwili wangu ni dhaifu mno na sasa nimechukua maumivu zaidi ya ninavyoweza kuvumilia. Ninapenda kwamba ungechukua roho yangu, kwa maana afadhali nife kuliko kukusaliti Wewe." Baada ya kuomba, muujiza usiotarajiwa mno ulifanyika: nilikuwa na uzoefu wa kuwa nje ya mwili na nikaletwa kwa uwanja wa nyasi. Kulikuwa na nyasi ya kusitawi sana, ya kijani kila mahali na ng'ombe na kondoo wakiuzunguka. Hali yangu ya muda ya akili lilikuwa na utulivu hasa na sikuweza kujizuia kumsifu Mungu kwa sauti: "Msifu Mwenyezi Mungu kwa sauti, vitu vyote mbinguni na duniani hukusifu Wewe, hukukusifu Wewe, vyote vitakusifu Wewe. Acha malaika Wako wote wainuke na kukusifu, acha majeshi Yako yote ya mbinguni ikusifu Wewe, mtanuko wa ulimwengu hukusifu Wewe—Mwenyezi Mungu! Nyota zinazoangaza hukusifu Wewe, mbingu na ardhi na maji hukusifu Wewe, vyote hukusifu. Acha milima na vilima vimsifu Mwenyezi Mungu, Acha mawimbi na mawimbi makubwa yakusifu Wewe, yakusifu Wewe katika mahali pa juu mno—Mwenyezi Mungu! Msifu Mwenyezi Mungu katika mahali patakatifu sana, yakusifu Wewe kwa kigoma na ngoma, yakusifu Wewe kwa sauti! Msifu Mwenyezi Mungu kwa vyombo vya muziki na sauti ya tarumbeta, acha watu watakatifu Sayuni wakusifu, acha watu wote wakusifu Wewe—Mwenyezi Mungu! Ee Mwenyezi Mungu, wakusifu Wewe kwa sauti! Ngurumo kubwa za radi hukusifu Wewe, hukukusifu Wewe kwa sauti! Eneo kubwa pana na wazi humsifu Mwenyezi Mungu, acha kila kitu kilicho na pumzi kikusifu Wewe, kuimba kwa sifa hutetemesha miisho ya dunia, Mungu asifiwe!" ("Msifuni Mwenyezi Mungu kwa Sauti Kuu" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipojitosa kabisa katika furaha hii isiyo kifani na kuishi katika mipaka ya uhuru, maumivu, njaa na baridi ya kuning'inizwa kutoka kwa mti na vilevile maumivu ya kuumwa na siafu yote yalitoweka. Nilipoamka, ilikuwa tayari usiku wa tatu na wale polisi waovu walinishusha kutoka kwa mti. Niliangikwa kwa siku tatu na sikukosa tu kufa, pia nilikuwa nimejaa uchangamfu. Hii kwa kweli ilikuwa ni nguvu yenye enzi na ulinzi wa miujiza wa Mungu! Nilitoa shukrani za dhati na sifa kwa Mungu.
Mnamo siku ya nne, wale polisi waovu walinihoji tena na wakajaribu kunilazimisha niwasaliti ndugu zangu wa kiume na wa kike; pia walinilazimisha kukubali kwamba niliamini katika dhehebu, kunifanya nimsaliti Mungu na kuiacha njia ya kweli. Nuru ya Mungu ilinifanya nifikirie neno la Mungu: “Wakati wanapitia katika majaribu, ni kawaida kwa watu kuwa dhaifu, au kuwa na uhasi ndani yao, au kukosa uwazi juu ya mapenzi ya Mungu au njia yao ya kutenda. Lakini katika hali yoyote, lazima uwe na imani katika kazi ya Mungu, na usimkane Mungu, kama Ayubu” (“Ni Lazima Wale Wanaofaa Kufanywa Wakamilifu Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili. Maneno ya Mungu yalinipa ujasiri wa kuweka ukweli katika matendo na kutoa ushahidi juu ya Mungu. Bila kujali ni nini, sikuweza kumpinga Mungu au kumkufuru Mungu. Kwa hiyo, kwa ujasiri na kwa imani nilisema: "Naamini katika Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Mungu wa pekee wa kweli anayevitawala vitu vyote! Siamini katika dhehebu la uovu, mnageuza ukweli na kunizulia uongo!" Baada ya polisi mmoja muovu kusikia jambo hili, alikasirika sana na kunyakua stuli moja ndefu ya mbao na akaanza kunipiga nayo kwa mda mrefu kikatili. Alinipiga kiasi kwamba nilikuwa nikitema damu. Nililala nikiwa nimeduwazwa na nimezimishwa sakafuni. Walipoona kwamba nilikuwa nimepoteza fahamu, walinirashia maji baridi ili kuniamsha na kuendelea kunipiga. Wakati wa kupigwa huku kishetani na kinyama, upande wa mbele wa kifua changu na mgongo wangu zilikuwa nyeusi na bluu kabisa na nilipitia madhara mengi ya ndani. Wiki moja baadaye, mkojo wangu ulikuwa wote ni damu na figo yangu ya kulia iliharibiwa kwa sana (hata leo bado ina uchungu sana). Mwezi mmoja baadaye, hao polisi waovu hawakuweza kupata ushahidi wowote, kwa hiyo walibuni vitu vya uongo na kunilazimisha kutia sahihi. Kisha wakanifunga ndani ya kituo cha kizuizi cha jiji. Miezi mitatu baadaye, walinishtaki na "kuharibu utekelezaji wa sheria za kijamii" na kunihukumu mwaka mmoja wa marekebisho kupitia kazi. Kwa kambi ya kazi, niliishi maisha ya kinyama. Kila siku nilikuwa na njaa na nilipaswa kufanya kazi takribani saa kumi na mbili kwa siku. Nilidhulumiwa na kufedheheshwa mara kwa mara na polisi wa gereza; ama walikuwa wanatumia virungu vya umeme au kunifungia ndani ya chumba kidogo, cha giza. Isingekuwa Mungu kunitunza na kunilinda, ningekuwa nimeteswa na hao polisi waovu hadi kifo. Mnamo Novemba 7, mwaka wa 2003, hukumu yangu ilitimizwa na niliachiliwa kutoka kwa hiyo jahannamu ya duniani.
Baada ya kupitia mateso hayo ya ukatili, hatimaye niliona kwa dhahiri kwamba matangazo ya serikali ya CCP "chama cha Kikomunisti ni kizuri, cha utukufu na sahihi" na "China ina uhuru wa dini" kati ya misemo mengine, kwa kweli ni maonyesho tu katika njama mbovu ya kuidanganya umma na kuwapumbaza wananchi. Kwa kweli ninamchukia huyu shetani mzee kwa dhati. Yeye huzungumza maneno ya kujipendekeza na hufanya mambo maovu mno. Ili kupiga marufuku kazi ya Mungu ya siku za mwisho na kufanya China kuwa mahali pa wamkanao Mungu, huwa inafuatilia na kuwaua waumini bila kizuizi. Kiwango chake cha ukatili tayari kimefikia vimo vikubwa na imewafanya watu wapandwe na mori! Ninafikiria nyuma kuhusu jinsi nilivyokuwa nikiteswa kwa ukatili na kulazimishwa kufanya ungamo na kuteswa kwa ukatili na pepo wakati wa mchakato wangu wa kuhojiwa. Niliduwazwa mara kadhaa na kama haingekuwa ulinzi wa Mungu, ningekuwa nimemezwa na pepo hao. Wakati wa udhaifu wangu mkuu, neno la Mwenyezi Mungu lilinitumainisha kwa mfululizo: “Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, hamtapoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, na hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu” (“Tamko la Kumi na Tisa” la Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinipa kitu imara cha kutegemea! Kiliniruhusu kufurahia nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu wakati wa maumivu yangu ya kuzidi kiasi na udhaifu, ambayo ndiyo iliyokuwa njia ya pekee ambayo ningeweza kupita kipindi hiki cha giza na kilichorefuka kupita kiasi Ingawa nimepata uzoefu wa kukamatwa na kuteswa mara nyingi na serikali ya CCP, na mwili wangu umepitia ukatili usio na huruma na mateso, kwa kweli naelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na ninaona kwa dhahiri tabia ya kishetani ya uovu unaopinga maendeleo wa serikali China. Nimepata uzoefu pia wa upendo wa kweli wa Mwenyezi Mungu kwangu na nimeonja hekima inayoweza ya Mwenyezi Mungu na matendo ya ajabu. Huniamsha kutafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu. Leo, bado ninatimiza wajibu wangu katika kanisa kama nilivyofanya zamani; mimi humfuata Mungu katika njia sahihi ya uzima, mimi hutafuta ukweli na hutafuta kuishi maisha ya maana.
Tanbihi:
a. "Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi" inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.
b. "Inalindwa isivyo kawaida" inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: ushuhuda wa Kanisa la Mwenyezi Mungu

0 意見:

Chapisha Maoni