Jumapili, 3 Machi 2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 12

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 12

Watu wote wanapotilia maanani, wakati vitu vyote vinafanywa upya na kuhuishwa, wakati kila mtu anamtii Mungu bila shaka, na yuko tayari kubeba jukumu zito la mzigo wa Mungu—hapa ndipo wakati umeme wa mashariki unatoka, ukiangaza yote kutoka Mashariki hadi Magharibi, ukiyatisha yote ya ulimwengu na ujaji wa mwanga huu; na wakati huu, Mungu tena huanza maisha Yake mapya. Ambayo ni kusema, wakati huu Mungu huanza kazi mpya duniani, akitangaza kwa watu wa ulimwengu wote kwamba “Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika.” Hivyo, ni wakati upi ambao umeme unatoka kutoka Mashariki? Wakati mbingu zinatiwa giza na dunia inapunguka mwanga pia ni wakati ambapo Mungu huuficha uso Wake kutoka kwa dunia, na wakati hasa ambapo yote chini ya mbingu yako karibu kuzongwa na dhoruba kuu. Wakati huu, watu wote wanaingiwa na hofu kubwa, wakiogopa radi, wakiogopa kung’aa kwa umeme, na hata kuogopa zaidi shambulio la gharika, kiasi kwamba wengi wao wanafumba macho na kusubiri Mungu aachilie huru ghadhabu Yake na kuwabwaga. Na hali mbalimbali zinapoendelea kupita, umeme wa mashariki unatoka ghafla. Ambayo ni kusema, katika Mashariki ya dunia, kutoka wakati ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe huanza, hadi wakati Yeye huanza kufanya kazi, mpaka wakati uungu huanza kushika madaraka makuu pande zote duniani—huu ni mwale unaong’aa wa umeme wa mashariki, ambao daima umemulika kwa ulimwengu mzima. Wakati ambapo nchi duniani zinakuwa ulimwengu wa Kristo ndio wakati ambapo ulimwengu mzima unatiwa nuru. Sasa ndio wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka: Mungu mwenye mwili Anaanza kufanya kazi, na, zaidi ya hayo, Anaongea moja kwa moja katika uungu. Inaweza kusemwa kwamba Mungu anapoanza kuongea duniani ni wakati ambapo umeme wa mashariki unatoka. Kwa usahihi zaidi, wakati ambapo maji ya uhai yanatiririka kutoka katika kiti cha enzi—wakati ambapo matamshi kutoka katika kiti cha enzi huanza—bila shaka ni wakati ambapo matamshi ya Roho wa mara saba huanza kirasmi. Wakati huu, umeme wa mashariki huanza kutoka, na kwa sababu ya tofauti katika wakati, kiwango cha mwangaza pia kinabadilika, na kunao, pia, mpaka kwa mawanda ya nuru. Lakini kadri kazi ya Mungu inavyoendelea, kadri mpango Wake unavyobadilika—kadri kazi kwa wana na watu wa Mungu inavyobadilika—umeme unazidi kutekeleza kazi yake ya asili, kiasi kwamba yote kotekote duniani yanaangazwa, na hakuna mashapo ama takataka zinazobaki. Huu ndio udhihirisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6000, na tunda hasa linalofurahiwa na Mungu. “Nyota” haihusu nyota zilizo angani, lakini wana na watu wote wa Mungu ambao hufanya kazi kwa ajili ya Mungu. Kwa sababu wana shuhudia kwa Mungu katika ufalme wa Mungu, na kumwakilisha Mungu katika ufalme wa Mungu, na kwa sababu wao ni viumbe, wanaitwa “nyota.” Mabadiliko yanayotokea yanahusu mabadiliko katika utambulisho na hadhi: Yanabadilika kutoka kwa watu duniani hadi kwa watu wa ufalme, na, zaidi ya hayo, Mungu yuko pamoja nao, na utukufu wa Mungu uko ndani yao.Kwa hiyo, wanashika mamlaka ya kifalme badala ya Mungu, na sumu na najisi ndani yao zinatakaswa kwa sababu ya kazi ya Mungu, hatimaye zikiwafanya kufaa kwa matumizi na Mungu na kuupendeza moyo wa Mungu—ambacho ni kipengele kimoja cha maana cha maneno haya. Wakati ambapo mwale wa mwanga kutoka kwa Mungu unaiangaza nchi yote, vitu vyote mbinguni na duniani vitabadilika kwa viwango mbalimbali, na nyota angani pia zitabadilika, jua na mwezi vitafanywa upya, na watu duniani watafanywa upya baadaye—ambayo yote ni kazi inayofanywa na Mungu katikati ya mbingu na dunia, na haishangazi.
Mungu anapowaokoa watu—ambayo, kwa kawaida, haijumuishi wale ambao si wateule—ni wakati hasa ambapo Mungu huwatakasa na kuwahukumu watu, na watu wote hulia kwa uchungu, ama kuanguka vitandani mwao, au wanabwagwa na kutumbukizwa katika jahanamu ya kifo kwa sababu ya maneno ya Mungu. Ni kwa sababu tu ya matamshi ya Mungu kwamba wanaanza kujijua. Kama sio, macho yao yangekuwa ya chura—yakiangalia juu, hakuna anayesadiki, hakuna kati yao akijijua, bila kujua uzito wao. Kwa kweli watu wamepotoshwa na Shetani kwa kiwango fulani. Ni kwa sababu hasa ya kudura ya Mungu kwamba uso mbaya wa mwanadamu unaelezwa waziwazi kabisa, ukimsababisha mwanadamu, baada ya kuuona, kuulinganisha na uso wake mwenyewe wa kweli. Watu wote wanajua kwamba idadi ya seli za ubongo walizo nazo vichwani mwao zinaonekana kuwa wazi kabisa kwa Mungu, sembuse nyuso zao mbaya au mawazo ya ndani kabisa. Kwa maneno ya “Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imetiishwa chini ya kusafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa” inaweza kuonekana kwamba siku moja, kazi ya Mungu iishapo, wanadamu wote watakuwa wamehukumiwa na Mungu. Hakuna atakayeweza kutoroka, Mungu atashughulika na watu wote mmoja mmoja, Asikose kutilia maanani hata mmoja wao, na hapo tu ndipo Moyo wa Mungu utaridhika. Na hivyo, Mungu anasema, “Tena, wao ni kama wanyama wakitoroka kutoka kwa mwangaza Wangu wakikimbilia usalama katika mapango ya milimani; ilhali, hakuna hata mmoja kati yao anayeweza kufutiliwa mbali kutoka katika mwanga Wangu.” Watu ni wanyama duni na wa hali ya chini. Wakiishi mikononi mwa Shetani, ni kana kwamba wamepata usalama katika misitu ya kale ndani sana ya milima—lakini kwa sababu vitu vyote haviwezi kutoroka uchomaji kwa mwako wa moto wa Mungu, hata vikiwa chini ya “ulinzi” wa nguvu za Shetani, vingewezaje kusahaulika na Mungu? Wanapokubali kuwasili kwa maneno ya Mungu, maumbo mbalimbali yasiyo ya kawaida na hali za ajabu za watu wote zinaonyeshwa kwa mchoro wa kalamu ya wino ya Mungu; Mungu huzungumza ifaavyo mahitaji na akili ya mwanadamu. Hivyo, kwa watu, Mungu anaonekana kuwa mjuzi mzuri katika saikolojia. Ni kana kwamba Mungu ni mwanasaikolojia, lakini pia kana kwamba Mungu ni daktari wa tiba ya sehemu za ndani za mwili—haishangazi kwamba Ana ufahamu kama huo wa mwanadamu, ambaye ni “mgumu kufahamika”. Kadri watu wanavyofikiria hili, ndivyo hisia yao ya thamani ya Mungu inavyokuwa kubwa zaidi, na ndivyo wanavyohisi zaidi kwamba Mungu ni mkubwa na asiyeeleweka. Ni kana kwamba, kati ya mwanadamu na Mungu, kuna mpaka usiovukika wa mbingu, lakini pia kana kwamba hao wawili wanaangaliana kutoka kila ukingo wa Mto Chu[a], kila mmoja asiweze kufanya kingine zaidi ya kumtazama mwingine. Ambayo ni kusema, watu wa dunia humtazama Mungu tu kwa macho yao, hawajawahi kuwa na fursa ya kumchunguza kwa karibu, na yote waliyo nayo ni hisia ya upendo. Katika mioyo yao, daima wana hisia kwamba Mungu anapendeza, lakini kwa sababu Mungu ni “mkatili mno na asiye na huruma”, hawajawahi kuwa na fursa ya kuzungumzia maumivu makali katika mioyo yao mbele Yake. Wao ni kama mke mzuri mchanga mbele ya mume wake—ambaye, kwa sababu ya uaminifu wa mume wake, hajawahi kuwa na nafasi ya kutoa wazi hisia zake za kweli. Watu ni mafidhuli wanaojidharau, na hivyo, kwa sababu ya udhaifu wao, kwa sababu ya kukosa kwao kujiheshimu, chuki Yangu ya mwanadamu kwa kiasi fulani inaongezeka bila kufahamu, na ghadhabu katika moyo Wangu inatoka nje kwa nguvu. Katika akili Yangu, ni kana kwamba nimepitia kiwewe. Nilipoteza matumaini kwa mwanadamu kitambo, lakini kwa sababu “Kwa mara nyingine, siku Yangu inaikaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ambayo kwayo inafaa kutengeneza mwanzo mpya,” mara nyingine Ninakusanya ujasiri kuwashinda wanadamu wote, kumteka na kumshinda joka kuu jekundu. Kusudi la asili la Mungu lilikuwa kama ifuatavyo: kutofanya chochote zaidi ya kuwashinda wazao wa joka kuu jekundu katika China; hili tu ndilo lingeweza kufikiriwa kuwa kuzidiwa nguvu kwa joka kuu jekundu, ushinde wa joka kuu jekundu, na hili tu ndilo lingetosha kudhibitisha kwamba Mungu hutawala kama Mfalme duniani kote, ikidhibitisha utimilifu wa shughuli kuu ya Mungu, na kwamba Mungu ana mwanzo mpya duniani, na Anatukuzwa duniani. Kwa sababu ya mandhari mazuri ya mwisho, Mungu hana budi kuonyesha uchu ulio ndani ya moyo Wake: “Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kueleza kile kilicho ndani ya moyo Wangu.” Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba kile kilichopangwa na Mungu ni kile ambacho Mungu ameshatimiza, kwamba kilijaaliwa na Mungu, na ni kile hasa Mungu huwafanya watu kupitia na kutazama. Mandhari ya ufalme ni mazuri, Mfalme wa ufalme ni mshindi, kutoka kichwani hadi kidoleni hakuna dalili yoyote ya mwili na damu, Yeye mzima ni mtakatifu. Mwili wake wote unang’aa kwa utukufu mtakatifu, haujatiwa doa na mawazo ya kibinadamu hata kidogo, mwili Wake wote, kutoka juu hadi chini, umejaa haki na uzuri wa mbingu, na unatoa harufu nzuri ya kupendeza mno. Kama wapenzi katika Wimbo wa Suleiman, Yeye bado ni mzuri kuliko watakatifu wote, wa juu zaidi kuliko watakatifu wa kale, Yeye ni mfano kati ya watu wote, na Asiyelinganishika na mwanadamu; watu hawafai kumtazama moja kwa moja. Hakuna awezaye kuufikia uso mtukufu wa Mungu, sura ya Mungu, au taswira ya Mungu, hakuna awezaye kushindana, na hakuna awezaye kuyasifu kwa urahisi kwa kinywa chake.
Maneno ya Mungu hayana mwisho, kama maji yabubujikayo kutoka kwa chemchemi hayatawahi kukauka, na hivyo hakuna awezaye kuelewa siri ya mpango wa Mungu wa usimamizi—lakini kwa Mungu, siri kama hizo haziishi. Akitumia njia na lugha tofauti, Mungu amezungumza mara kadhaa kuhusu kufanywa Kwake upya na kubadilishwa kwa ulimwengu mzima, kila wakati ukiwa wa kina zaidi kuliko wakati uliopita: “Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa jivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo.” Kwa nini Mungu husema mambo kama hayo tena na tena? Je, Haogopi watu watachoshwa nayo? Watu wanapapasa tu katikati ya maneno ya Mungu, wakitaka kumjua Mungu kwa njia hii, lakini kamwe hawakumbuki kujichunguza. Hivyo, Mungu hutumia njia hizi kuwakumbusha, kuwafanya wajijue, ili kutoka kwao wenyewe wanaweza kupata kujua uasi wa mwanadamu, na hivyo kufuta uasi wao mbele za Mungu. Wanaposoma kwamba Mungu anataka “kusafisha na kutatua,” hali yao ya moyo inakua na wasiwasi mara moja, na misuli yao, pia, inaonekana kuacha kusonga. Mara moja wanarudi mbele za Mungu kujikosoa, na hivyo wanakuja kumjua Mungu. Baada ya hili—baada ya wao kuamua—Mungu hutumia fursa hiyo kuwaonyesha kiini cha joka kuu jekundu; hivyo, watu hushiriki na ufalme wa kiroho moja kwa moja, na kwa sababu ya wajibu unaochukuliwa na uamuzi wao, akili zao zinaanza pia kuchukua wajibu fulani, ambalo linazidisha pendo kati ya mwanadamu na Mungu—ambalo ni la manufaa muhimu zaidi kwa kazi ya Mungu katika mwili. Kwa njia hii, watu hutaka kukumbuka nyakati zilizopita bila kufahamu: Katika wakati uliopita, kwa miaka watu walimwamini Mungu asiye yakini, kwa miaka, kamwe hawakuwekwa huru mioyoni mwao, hawakuwa na uwezo wa raha kuu, na ingawa walimwamini Mungu, hakukuwa na mpango katika maisha yao. Ilikuwa kana kwamba hakukuwa na tofauti na kabla ya wao kuwa waumini, maisha yao bado yalihisi kuwa matupu na yasiyo na matumaini, ilikuwa kana kwamba imani yao wakati huo ilikuwa aina ya mtego, na kana kwamba ingekuwa heri wasingeamini. Kwa sababu walimtazama Mungu Mwenyewwa vitendo wa leo, ni kana kwamba mbingu na dunia zimefanywa upya; maisha yao yameng’aa, hawako bila matumaini tena, na kwa sababu ya ujaji wa Mungu wa vitendo, wanahisi kuwa imara katika mioyo yao na watulivu ndani ya roho zao. Hawafuatilii upepo tena na kushikia yasiyo dhahiri katika yote wafanyayo, ufuatiliaji wao haukosi lengo maalum tena na hawatupi mikono huku na kule ovyo ovyo tena. Maisha ya leo ni mazuri hata zaidi, watu wameingia katika ufalme bila kutarajia na kuwa mmoja wa watu wa Mungu, na baadaye…. Katika mioyo yao, watu wanavyofikiria zaidi, ndivyo utamu unavyokuwa mkuu zaidi, wanavyofikiria zaidi, ndivyo wanavyokuwa na furaha zaidi, na ndivyo wanavyotiwa moyo zaidi kumpenda Mungu. Hivyo, bila wao kutambua, urafiki kati ya Mungu na mwanadamu unaimarishwa. Watu wanampenda Mungu zaidi, na kumjua Mungu zaidi, na kazi ya Mungu ndani ya mwanadamu inazidi kuwa rahisi, na haiwalazimishi au kuwashurutisha watu tena, lakini inafuata hali ya asili ya maisha, na mwanadamu hutekeleza kazi yake maalum—hapo tu ndipo wataweza kumjua Mungu polepole. Hii tu ndiyo hekima ya Mungu—haijumuishi juhudi hata kidogo, na inazalishwa kama ifaavyo asili ya mwanadamu. Hivyo, wakati huu Mungu anasema, “Katika wakati wa kupata mwili Kwangu katika dunia ya binadamu, binadamu walifika pasipo kujua katika siku hii na usaidizi wa uongozi wa mkono Wangu, pasipo kujua wakaja kunifahamu. Lakini, kuhusu jinsi ya kutembea katika njia iliyo mbele, hakuna aliye na fununu, hakuna anayejua, na bado hakuna aliye na kidokezo juu ya mwelekeo ambao hiyo njia itampeleka. Mwenyezi pekee akimwangalia ndipo yeyote ataweza kutembea njia hiyo hadi mwisho; akiongozwa tu na umeme kutoka Mashariki ndipo yeyote ataweza kuvuka kizingiti kinachoelekea katika ufalme Wangu.” Je, huu si muhtasari wa kile Nimeeleza katika moyo wa mwanadamu hapo juu? Hii ndiyo siri ya maneno ya Mungu. Mawazo katika moyo wa mwanadamu ni kile kinachozungumzwa kwa kinywa cha Mungu, na kile kinachozungumzwa kwa kinywa cha Mungu kinatamaniwa na mwanadamu, na hiki hasa ndicho Mungu ni bingwa zaidi kwacho katika kuufichua moyo wa mwanadamu; kama sivyo, wote wangetolewa shaka kwa dhati vipi? Je, haya si matokeo Mungu anataka kutimiza katika kumshinda joka kuu jekundu?
Kwa kweli, kama lilivyokuwa kusudi la asili la Mungu, maana ya maneno Yake mengi haiko katika maana yake ya juu juu. Katika maneno Yake mengi, Mungu anabadilisha dhana za watu kwa kusudi tu na kuvuta kwingine uangalifu wao. Mungu hashikizi umuhimu wowote kwa maneno haya, na hivyo maneno mengi hayastahili ufafanuzi. Wakati ushindi wa mwanadamu kwa maneno ya Mungu umefika mahali upo leo, nguvu ya watu imefika mahali fulani, na hivyo Mungu baadaye hutamka maneno zaidi ya onyo—katiba Atoayo kwa watu wa Mungu: —“Ingawa wanadamu ambao wanaijaza dunia ni wengi kama nyota, Nawajua wote wazi kama Ninavyotazama kiganja cha mkono Wangu mwenyewe. Na, ingawa wanadamu ambao ‘wananipenda’ ni wengi pia kama mchanga wa bahari, ni wachache tu ndio waliochaguliwa na Mimi: wale tu wanaoufuatilia mwanga unaong’aa, walio kando na wale ‘wanaonipenda’.” Kwa kweli, kunao wengi wasemao wanampenda Mungu, lakini kunao wachache wanaompenda katika mioyo yao—ambayo, ingeonekana, inaweza kujulikana wazi hata macho yakiwa yamefumbwa. Hii ndiyo hali halisi ya dunia nzima ya wale wamwaminio Mungu. Katika hili, tunaona kwamba sasa Mungu amegeukia kazi ya kuwafuta watu, ambayo inaonyesha kwamba kile Mungu hutaka, na kile kinachomridhisha Mungu, si kanisa la leo, lakini ni ufalme baada ya kufutwa. Kwa sasa, Anatoa onyo zaidi kwa “bidhaa hatari” zote: Isipokuwa Mungu asichukue hatua, punde tu Mungu anapoanza kuchukua hatua, watu hawa watafutwa kutoka katika ufalme. Mungu kamwe hafanyi mambo bila uangalifu, daima Yeye hutenda kulingana na kanuni ya “moja ni moja na mbili ni mbili,” na kama kuna wale ambao Hataki kuwatazama, Yeye hufanya kila Awezalo kuwafuta ili kuwakomesha kusababisha taabu baadaye. Hili linaitwa “kuondoa taka na kusafisha kabisa.” Wakati Mungu anatangaza amri za kiutawala kwa mwanadamu ndio wakati hasa ambapo Anaonyesha matendo yake ya muujiza na yote yaliyo ndani Yake, na hivyo baadaye Yeye anasema: “Kuna wanyama wa porini wasiohesabika milimani, lakini wote ni wapole kama kondoo mbele Zangu; mafumbo yasiyoeleweka yako chini ya bahari, lakini yanajiwakilisha Kwangu wazi kama vitu vyote vilivyo katika uso wa dunia; katika mbingu juu kuna milki ambayo mwanadamu hawezi kuifikia kamwe, ilhali Natembeatembea katika milki hizo zisizofikika.” Maana ya Mungu ni hii: Ingawa moyo wa mwanadamu ni wa kudanganya kushinda vitu vyote, na huonekana kuwa wa siri yasiyoisha kama jahanamu ya dhana za watu, Mungu hujua hali halisi za watu kama kiganja Chake. Kati ya vitu vyote, mwanadamu ni mnyama mkali na mkatili zaidi kuliko mnyama pori, lakini Mungu amemshinda mwanadamu hadi kiwango ambacho hakuna anayethubutu kuinuka na kupinga. Kwa kweli, kama ilivyo maana ya Mungu, kile watu hufikiria katika mioyo yao ni kigumu kufahamika zaidi kuliko vitu vyote kati ya vitu vyote, hakieleweki, lakini Mungu hauheshimu moyo wa mwanadamu, Anauchukulia tu kama mnyoo mdogo machoni Pake; kwa neno moja kutoka kwa kinywa Chake, Anaushinda, wakati wowote Anapotaka, Anaubwaga, kwa mtikiso kidogo zaidi wa mkono Wake, Anauadibu, na Anauhukumu apendapo.
Leo, watu wote wanaishi katikati ya giza, lakini kwa sababu ya ujaji wa Mungu, watu wanapata kujua kiini cha mwanga kutokana na kumwona Mungu, na kotekote katika dunia ni kana kwamba chungu kuu cheusi dunia umepinduliwa juu ya ulimwengu; hakuna awezaye kuvuta pumzi, wote wanataka kugeuza hali, ilhali hakuna ambaye amewahi kukiondoa chungu cheusi. Ni kwa sababu tu ya kupata mwili kwa Mungu ndipo macho ya watu yamefumbuliwa kwa ghafla, na wamemwona Mungu wa vitendo, na hivyo, Mungu anawauliza kwa sauti ya kuhoji: “Mwanadamu hajawahi kunitambua katika mwanga, lakini ameniona tu katika ulimwengu wa giza. Huko katika hali sawa kabisa na hiyo leo? Ilikuwa katika kilele cha ghasia ya joka kuu jekundu ndipo Nilivaa kirasmi mwili ili kufanya kazi Yangu.” Mungu hafichi kile kinachoendelea katika ufalme wa kiroho, wala Hafichi kile kinachofanyika katika moyo wa mwanadamu, na hivyo tena na tena Yeye huwakumbusha watu: “Nafanya hivi sio tu kuwawezesha watu Wangu kumjua Mungu mwenye mwili, bali pia ili kuwatakasa watu Wangu. Kwa sababu ya ukali wa amri Zangu za utawala, watu wengi bado wako katika hatari ya kuondolewa na Mimi. Isipokuwa ukifanya juhudi zote kujishughulikia, kuushinda mwili wako mwenyewe, isipokuwa ukifanya hivi, bila shaka utakuwa kitu Ninachodharau na kukataa, cha kutupwa chini kuzimu, jinsi tu Paulo alivyopokea adhabu moja kwa moja kutoka kwa mikono Yangu, ambapo kwayo hakukuwa na kutoroka.” Kadri Mungu anavyosema mambo kama hayo, ndivyo watu wanavyokuwa wenye hadhari na nyayo zao wenyewe zaidi, na ndivyo wanavyoogopa amri za kiutawala za Mungu zaidi, na hapo tu ndipo mamlaka ya Mungu yanaweza kuzalishwa na uadhama Wake kuwekwa wazi. Hapa, Paulo anatajwa mara nyingine ili kuwafanya watu kuelewa mapenzi ya Mungu: Hawapaswi kuwa wale wanaoadibiwa na Mungu, lakini wale wanaozingatia mapenzi ya Mungu. Hili tu ndilo linaloweza kuwafanya watu, katikati ya hofu yao, kukumbuka kutoweza kwa uamuzi wao wa wakati uliopita mbele ya Mungu kumridhisha Mungu kikamilifu, jambo ambalo linawapa majuto makuu hata zaidi, na kuwapa maarifa zaidi ya Mungu wa vitendo, na hivyo hapo tu ndipo wanaweza kuwa bila shaka kuhusu maneno ya Mungu.
“Sio tu kwamba mwanadamu hanifahamu Mimi katika mwili Wangu; jambo baya hata zaidi, ameshindwa kuielewa nafsi yake mwenyewe inayoishi katika mwili. Imekuwa miaka mingapi, na wakati huu wote wanadamu wamenidanganya, wakinichukua kama mgeni kutoka nje? Ni mara ngapi…?” Haya “Ni mara ngapi” yanaorodhesha uhalisi wa upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, yakionyesha watu mifano ya kweli ya kuadibu; hili ni thibitisho la dhambi, na hakuna awezaye kulikataa tena. Watu wote humtumia Mungu kama chombo cha kila siku, kana kwamba Yeye ni kitu fulani muhimu cha nyumbani ambacho wanaweza kukitumia wapendavyo. Hakuna anayemhifadhi Mungu kwa upendo mkubwa, hakuna ambaye amejaribu kuujua uzuri wa Mungu, na uso mtukufu wa Mungu, sembuse yeyote anayemtii Mungu kimakusudi. Wala hakuna ambaye amewahi kumtazama Mungu kama kitu kinachopendwa moyoni mwake, wote wanamkokota aje wanapomhitaji, na kumtupa pembeni na kutomjali wasipomhitaji. Ni kana kwamba, kwa mwanadamu, Mungu ni karagosi, ambayo mwanadamu anaweza kuitawala apendapo, na kutoa madai kwa vile apendavyo au atamanivyo. Lakini Mungu anasema, “Kama, katika wakati wa kupata mwili Kwangu, Singekuwa Nimejali kuhusu udhaifu wa mwanadamu, basi binadamu wote, kwa sababu ya kupata mwili Kwangu, wangetishwa kabisa, na kwa sababu hiyo, wameingia kuzimu,” ambayo inaonyesha tu jinsi umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu kulivyo kukuu: Katika mwili, Amekuja kuwashinda wanadamu, badala ya kuwaangamiza wanadamu wote kutoka katika ufalme wa kiroho. Hivyo, Neno lilipokuwa mwili, hakuna aliyejua. Ikiwa Mungu hangekuwa anajali udhaifu wa mwanadamu, wakati Alipokuwa mwili na mbingu na dunia zikageuzwa juu chini, watu wote wangekuwa wameangamizwa. Kwa sababu ni desturi ya watu kupenda kilicho kipya na kuchukia kilicho kizee, na mara nyingi wanasahau nyakati mbaya wakati mambo yanaendelea vizuri, na hakuna kati yao ajuaye alivyobarikiwa, hivyo Mungu huwakumbusha tena na tena kwamba wanapaswa kuthamini jinsi leo imepiganiwa kwa nguvu; kwa ajili ya kesho, wanapaswa kuthamini leo hata zaidi, na hawapaswi, kama mnyama, kupanda juu na kutomtambua bwana, na wasikose kujua kuhusu baraka wanazoishi kati yazo. Hivyo, wanakuwa wenye mwenendo mzuri, hawajigambi au kuwa wenye kiburi tena, na wanapata kujua kwamba sio ukweli kwamba asili ya mwanadamu ni nzuri, lakini kwamba huruma na upendo wa Mungu umemjia mwanadamu; wanaogopa kuadibu, na hivyo hawathubutu kufanya zaidi.
Tanbihi:
a. Katika Uchina, “Mto wa Chu” ni neno kutoka tukio la kihistoria linalotumika kutaja mipaka ya nchi au mipaka ya vita.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili 

Soma Zaidi: Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 13


0 意見:

Chapisha Maoni