I
Mungu aliwaumba binadamu;
ikiwa mwanadamu amepotoshwa
au kama anamfuata,
Mungu huwachukulia binadamu kama wapendwa,
Mwanadamu sio kitu Chake cha kuchezea.
II
Yeye ni Muumba na binadamu uumbaji Wake.
Inaonekana kuwa cheo ni tofauti,
lakini kile ambacho Mungu anamfanyia mwanadamu huenda zaidi ya uhusiano wao.
Mungu anawapenda wanadamu na anawajali, na humwonyesha mwanadamu kujali anakostahili.
Bila kuchoka Yeye huwatolea wanadamu,
hahisi kamwe kuwa ni kazi ya ziada,
wala Hahisi kwamba anahitaji sifa hapo.
III
Hahisi kwamba kuwaokoa wanadamu,
kuwaruzuku na kuwapa vyote
ni sifa kubwa kwao.
Ni kwamba tu kwa njia Yake mwenyewe,
kiini Chake, kile anacho na kile Alicho,
Anawaruzuku wanadamu kwa utulivu na kimya.
Haijalishi ni kiasi gani ambacho mwanadamu anapata kutoka Kwake,
Mungu haulizi sifa.
Inaamuliwa na asili Yake;
ni ya kufuatana na tabia Yake.
kutoka katika "Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I" katika Neno Laonekana katika Mwili
kutoka kwa Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Sikiliza zaidi nyimbo za injili
0 意見:
Chapisha Maoni