Jumanne, 25 Septemba 2018

Kuuonja Upendo wa Mungu Katikati ya Dhiki

Kuuonja Upendo wa Mungu Katikati ya Dhiki

Chen Lu Wilaya ya Tonglu, Mkoa wa Zhejiang
Baada ya mlo mkuu wa siku, polisi waliongeza mkazo wa masaili yao. Walinitisha vikali, wakisema: "Tuambie! Ni nani kiongozi wa kanisa lako? Kama hutuambii, tuna njia zingine, tunaweza kukufanya unywe juisi ya pilipili kali, maji ya sabuni, kukufanya ule kinyesi, kukuvua nguo zote, kukutupa sehemu ya chini ya ardhi, na kukufanya ugande hadi kufa! Usipozungumza leo, tutakuuliza tena kesho. Tuna muda kwa upande wetu!" Polisi waliposema hivi, kwa kweli niliona kuwa hawakuwa watu kamwe, lakini walikuwa kundi la pepo katika mwili wa binadamu. Jinsi walivyozidi kunitisha kwa njia hiyo, ndivyo nilivyozidi kuwachukia moyoni mwangu, na ndivyo nilivyozidi kudhamiria kutokubali kamwe kushindwa nao. Walipoona singekubali kushindwa, walitafuta kitambaa cha mfuko, wakakilowesha maji, na kunigubika nacho kichwani mwangu. Walikibonyeza kwa kichwa changu na hawangeniruhusu kusogea, kisha wakakikaza. Sikuweza kusogea kabisa kwa sababu mikono yangu ilikuwa imefungiwa pingu kwa kiti. Kabla ya muda mrefu mno, nilikuwa karibu kunyongwa; Nilihisi kwamba mwili wangu mzima ulikwisha kuwa mgumu. Lakini hilo bado halikuwa la kutosha kuondoa chuki yao. Walichukua chungu cha maji baridi na kuyamimina ndani ya pua langu, wakinitisha, wakisema kwamba kama singezungumza, wangeninyonga. Mfuko uliolowa maji wenyewe haukupitisha hewa, na zaidi ya hayo maji yalikuwa yakimwagwa ndani ya pua langu. Kupumua kulikuwa kugumu sana, na ilihisi kana kwamba kifo kilikuwa kinakaribia. Niliomba kimya kimya kwa Mungu: "Ee Mungu, pumzi hii yangu nilipewa na Wewe, na leo ninastahili kuishi kwa ajili Yako. Bila kujali ni jinsi gani polisi wananitesa, sitakusaliti. Kama ukinihitaji nijitolee maisha yangu, niko tayari kutii madhumuni na mipango Yako bila malalamiko hata kidogo….” Bado waliendelea kunitesa. Nilipoanza tu kupoteza fahamu na nilikuwa karibu kuacha kupumua, ghafla wakatoa mikono yao. Sikuweza kujizuia kuendelea kumshukuru Mungu moyoni mwangu. Niliona waziwazi kwamba Mungu ni Bwana wa kila kitu, kwamba Yeye daima Ananilinda na kunikinga, na hata kama nilianguka mikononi mwa polisi, Mungu aliwaruhusu tu kuutesa mwili wangu lakini hakuwaruhusu kuyashikilia maisha yangu. Baada ya hayo, imani yangu ilikua.
Siku iliyofuata takribani saa sita mchana, polisi kadhaa walinichukua na dada mwingine ndani ya gari la polisi na kutupeleka kwa nyumba ya kizuizi. Mmoja wao akaniambia kwa kuniogofya: "Wewe hujatoka hapa. Tutakufungia kwa miezi sita, kisha tutakuhukumu miaka 3 hadi 5, kwa vyovyote akuna atakayejua." "Kunihukumu?" Mara tu niliposikia kwamba ningehukumiwa, sikuweza kujizuia kuwa dhaifu. Nilihisi kwamba kama ningetumikia kifungo watu wengine wangeniangalia kwa dharau. Nilipokuwa tu na maumivu na dhaifu, Mungu alinionyesha tena neema Yake. Wale watu wengine katika seli nilimowekwa wote walikuwa dada ambao walimwamini Mwenyezi Mungu. Ingawa walikuwa katika hilo shimo la pepo, hawakuonyesha hofu hata kidogo. Walitiana moyo na kusaidiana, na walipoona kwamba nilikuwa hasi na dhaifu, walizungumza nami kuhusu uzoefu wao binafsi na kuwa na ushuhuda, wakinipa matumaini kwa Mungu. Pia waliniimbia wimbo wa uzoefu ili kunitia moyo: "Unajitumia kwa ajili ya Mungu, ninajitolea Kwake, kutelekezwa na familia, kukashifiwa na ulimwengu. Njia ya kumfuata Mungu si rahisi kabisa. Niliweka moyo wangu wote na nafsi yangu katika kupanua ufalme wa Mungu. Nimeona kugeuka kwa misimu. Nakaribisha furaha na huzuni zilizo mbele. Kuridhisha mahitaji ya Mungu, mimi huitii mipango Yake. … Kuitembea njia ya kumpenda Mungu, mimi huvumilia majaribio machungu. Hatari na dhiki havivuti malalamiko yoyote kutoka kwa kinywa changu. Ingawa mwili wangu huteseka sana, moyo wangu unampenda Mungu. Mimi huenda kila mahali kama shahidi wa matendo ya Mungu. … Majaribio na mateso hunisumbua kwa uzito sana. Mema na mabaya ya maisha ninayoishi. Hata hivyo niko tayari kufanya mapenzi ya Mungu, kutumia asili yangu nzima kwa ajili Yake. Nimeamua kwamba nitateseka maisha yangu yote. Ndiyo, nitateseka maisha yangu yote. Na nitaridhisha moyo wa Mungu!" ("Mfuateni Mungu kwa Njia Yenye Mashimoshimo" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nikifikiri kuhusu wimbo huu, nilihisi nguvu ya maisha kutoka kwa dada hawa, na nilitiwa moyo pakubwa. Ulikuwa ni ukweli, tulikuwa tukifuata Mungu wa kweli na kutembea njia sawa ya uzima katika nchi chini ya utawala wa chama kikanacho Mungu ambacho kilimwona Mungu kama adui. Tulikuwa tumekusudiwa kupitia shida nyingi, lakini yote haya yalikuwa na maana, na hata kukaa gerezani lilikuwa jambo la utukufu kwa sababu tulikuwa tukiteswa kwa ajili ya kufuatilia ukweli na kuifuata njia ya Mungu. Ilikuwa tofauti kabisa na watu wa dunia kufungwa kwa kutenda makosa mabaya ya jinai. Nilifikiria kizazi baada ya kizazi cha watakatifu wengi ambao walipitia mateso na fedheha kwa sababu ya kushikilia njia ya kweli. Lakini sasa, nilikuwa nimepewa mengi sana kwa ukarimu ya neno la Mungu—nilielewa ukweli ambao vizazi vya watu havikuweza kuuelewa, nilijua siri ambazo vizazi havikuwa vimejua, hivyo ni kwa nini sikuweza kuvumilia mateso kidogo ili kumshuhudia Mungu? Wakati nilifikiria jambo hilo, nilijikokota tena kutoka kwa hali yangu ya udhaifu, moyo wangu ulijaa imani na nguvu, na nikaamua kumtegemea Mungu na kuyakabili mateso ya kesho na matakwa ya ungamo nikijivunia.
Siku kumi baadaye, polisi walinipeleka kwa kituo cha kizuizi peke yangu. Niliona kuwa watu wengine wote huko walizuiliwa kwa ulaghai, wizi, na biashara haramu. Mara tu nilipoingia, waliniambia: "Yeyote anayeingia hapa kwa kawaida huwa haitoki. Sote tunasubiri hukumu zetu, na baadhi yetu tumekuwa tukisubiri kwa miezi." Nikiangalia watu hawa, nilikuwa na wasiwasi sana moyo wangu ulikaribia kupasuka. Niliogopa kwamba wangenitendea vibaya, na kisha nilipofikiri juu ya ukweli kwamba polisi wangenifungia nao, nilidhani kwamba huenda wangenipa hukumu ya mhalifu. Nilikuwa nimesikia kwamba baadhi ya ndugu wa kiume na wa kike walikuwa wamefungwa kwa muda mrefu kama miaka minane. Sikujua hukumu yangu ingekuwa urefu gani, na nilikuwa na umri wa miaka 29 tu! Haingewezekana ujana wangu kutumiwa kama nimefungiwa katika seli hii yenye giza? Siku zangu kutoka hapa kwendelea zingetumikaje? Wakati huo, ilionekana kwamba makazi yangu ya kudumu, wazazi, mume, na mtoto kwa ghafla walikuwa mbali sana na mimi. Ilikuwa ni kama kisu kikipinda ndani ya moyo wangu, na machozi yalijitunga machoni mwangu. Nilijua kwamba nilikuwa nimeanguka katika ulaghai wa Shetani, kwa hiyo nikamwita Mungu kwa hamasa, nikimtumainia Yeye aniongoze kuepuka mateso haya. Katikati ya sala yangu, nilihisi uongozi wazi ndani yangu: Unapokabiliana na hili, una ruhusa kutoka kwa Mungu. Kama vile tu Ayubu akijaribiwa, usilalamike. Mara moja, maneno ya Mungu yakaniletea nuru mara nyingine tena: “Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa?” (“Unajua Nini Kuhusu Imani?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Hukumu na kuadibu katika maneno ya Mungu kulinifanya niaibike. Niliona kwamba sikukaribia kuwa mwaminifu kwa Mungu, lakini nilisema kuwa nilitaka kuwa shahidi mzuri Kwake. Hata hivyo, nilipokabiliwa na hatari ya kufungwa, nilitaka tu kutoroka. Hakukuwa na uwezo wa utendaji wa kuteseka kwa ajili ya ukweli. Kufikiria nyuma wakati ule nilipokamatwa, Mungu alikuwa kwa upande wangu wakati wote. Yeye hakuniacha katika hatua yoyote ya njia kwa hofu kwamba ningepoteza njia yangu au kuanguka kwa njia. Upendo wa Mungu kwangu ulikuwa wa kweli kabisa na haukuwa mtupu kamwe. Lakini nilikuwa na ubinafsi na mchoyo, na wakati wote nilifikiria kuhusu faida na hasara zangu za kimwili. Sikuwa tayari kulipa gharama yoyote kwa ajili ya Mungu—ningewezaje kuwa na utu wowote? Dhamiri yoyote? Si mimi nilikuwa mnyama katili asiye na moyo, wala roho? Nilipofikiria jambo hilo, nilijihisi kujaa majuto na madeni. Niliomba kimya kimya kwa Mungu na kutubu: Ee Mungu! Nilikosa. Siwezi tena kukuhudumia kwa maneno matupu na kukudanganya Wewe. Niko tayari kuishi kwa kudhihirisha ukweli ili kukuridhisha. Bila kujali hukumu yangu itakuwa nini, bila shaka nitakuwa shahidi Kwako—nakuuliza tu kwamba Uulinde moyo wangu. Wakati huo huo, mkuu wa wafungwa alikuja na kuniambia: "Sijui ni kwa nini uko hapa, lakini tuna msemo: 'Kiri ili uwe na pumziko na utatumikia kifungo mpaka mwisho; pinga vikali na unaweza kwenda kuishi maisha yako upendavyo.' Kama hutaki kuzungumza, usizungumze." Namshukuru Mungu kwa mpango huu wa ajabu na hekima iliyotolewa kwangu na mkuu wa wafungwa. Nilishukuru pia kuwa wafungwa wengine hawakukosa kugombana nami tu, lakini kwa kweli walinitunza, wakinipa nguo, kunipa chakula cha ziada wakati wa chakula, na kugawana nami matunda na vitafunio walivyovinunua wenyewe, na pia walinisaidia na kazi yangu ya kila siku. Nilijua kwamba yote haya yalikuwa usanifu na mpango wa Mungu; ilikuwa huruma ya Mungu kwa asili yangu ya kama mtoto. Nikitazama upendo Wake na ulinzi Wake, niliweka azimio langu: Bila kujali jinsi hukumu yangu itakavyokuwa ndefu, nitakuwa shahidi kwa Mungu!
Katika kituo cha kizuizi, polisi wangenihoji mara moja kila siku mbili. Walipogundua kuwa kuchukua msimamo mkali hakungeniweza, walibadilisha na kuwa wapole. Polisi aliyekuwa akinihoji akawa na tabia za upole kwa makusudi na kuzungumza nami, akanipa chakula bora cha kula, na akasema angenisaidia kupata kazi nzuri. Nilijua kwamba huu ulikuwa ni udanganyifu wa Shetani, hivyo kila wakati aliponihoji niliomba tu kwa Mungu, nikimwomba Yeye kunilinda na kutoniruhusu niathiriwe na hila hizi. Wakati mmoja alipokuwa akinihoji, yule polisi hatimaye alifichua nia zao mbovu: "Hatuna neno nawe, tunataka tu kulichukulia hatua kali Kanisa la Mwenyezi Mungu. Tunatarajia unaweza kujiunga nasi." Niliposikia maneno haya maovu, nilikuwa na hasira kubwa. Niliwaza: Mungu aliumba mwanadamu na ameendelea kutukimu na kutuongoza njia yote hadi sasa. Na sasa Amekuja kuwaokoa wale Aliowaumba na kutusaidia kutoroka kutoka kwa lindi letu kuu la mateso. Ni nini tena kilicho na kosa na hilo? Kwa nini linachukiwa sana, kukashifiwa sana na pepo hawa? Sisi ni viumbe wa Mungu. Kumfuata Mungu na kumwabudu Yeye ni sawa na sahihi, basi kwa nini Shetani atuzuie kwa njia hii, aondoe hata uhuru wa kumfuata Mungu? Sasa wanajaribu kunifanya kuwa kibaraka katika jitihada zao za kumwandama Mungu. Serikali ya CCP kwa kweli ni kundi la pepo walioamua kumkataa Mungu katakata. Wao ni wapinga maendeleo waovu kweli! Nilikuwa na hisia zisizoelezeka za maumivu ndani ya moyo wangu wakati huo, na yote niliyotaka ilikuwa ni kushuhudia Mungu na kuufariji moyo Wake. Wakati polisi walipoona kwamba bado singezungumza, walianza kutumia mbinu za kisaikolojia dhidi yangu. Walimpata mume wangu kupitia China Mobile na wakamleta yeye na mtoto wangu ili kunishawishi. Mume wangu mwanzoni alikuwa sawa na imani yangu kwa Mungu, lakini baada ya kudanganywa na polisi, aliniambia mara kwa mara: "Ninakusihi kuiacha imani yako. Angalau fikiria mtoto wetu kama si mimi. Kuwa na mama aliye gerezani kutakuwa na athari mbaya sana kwake. …” Nilitambua kwamba mume wangu alikuwa anasema hivi kwa ujinga, hivyo nikamkatiza na kusema: "Bado hunifahamu? Tuliishi pamoja kwa miaka mingi sana, wakati upi uliponiona nikifanya chochote kiovu? Kama hufahamu kitu basi usipayuke tu." Wakati mume wangu alipoona kwamba maneno yake hayakuweza kugeuza mawazo yangu, alitupa maneno haya katili: "Wewe ni mkaidi na hautasikiliza—nitakutaliki tu, basi!" Neno hili, "taliki," liliuchoma moyo wangu kwa kina. Lilinifanya niichukie serikali ya CCP hata kwa kina zaidi. Kulikuwa kukashifu huku kwayo na kuchonganisha kulikomfanya mume wangu aichukie kazi ya Mungu kwa njia hiyo na kusema maneno hayo yasiyo na huruma kwangu. Serikali ya CCP kwa kweli ndiyo mhalifu ambaye huwaambia watu wa kawaida kuikosea Mbinguni! Pia ilikuwa mhalifu katika kudhoofisha hisia zetu kama mume na mke! Kwa kufikiria haya, sikutaka kusema kitu chochote zaidi kwa mume wangu. Nilisema tu kwa utulivu: "Basi fanya haraka umrudishe mtoto wetu nyumbani." Polisi walipoona kwamba mbinu hii haikuwa imefua dafu, walikuwa na hasira sana kiasi kwamba walienda dalji mbele na nyuma mbele ya dawati lao na kunipigia yowe, wakisema: "Tumefanya kazi kwa bidii sana na hatujapata jibu hata moja kutoka kwako! Kama utaendelea kukataa kuzungumza tutakupachika cheo cha mkuu wa mkoa huu, kama mfungwa wa kisiasa! Usipozungumza leo, hakutakuwa na fursa nyingine!" Lakini bila kujali jinsi walivyojitapa na kupayapaya, nilimwomba tu Mungu moyoni mwangu, nikimuuliza Yeye aimarishe imani yangu.
Wakati wa masaili yangu, kulikuwa na wimbo wa neno la Mungu ambao uliendelea kuniongoza kutoka ndani: “Katika hatua hii ya kazi sisi tunatakiwa kuwa na imani kuu na upendo mkuu. Huenda tukajikwaa kutokana na uzembe kidogo kabisa kwa. … Watu lazima wafikie kiwango ambacho wamestahimili mamia ya kusafisha na wawe na imani iliyo kuu zaidi kuliko ya Ayubu. Wanatakiwa kustahimili taabu ya ajabu sana na aina zote za mateso bila kuondoka kwa Mungu wakati wowote. Wanapokuwa watiifu hadi kufa, na wawe na imani kuu katika Mungu, basi hatua hii ya kazi ya Mungu imetimizwa” (“Kile ambacho Mungu anakamilisha ni imani ya wanadamu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Kwa sababu ya imani na nguvu nilizopokea kutoka kwa maneno ya Mungu, wakati nilipokuwa nikihojiwa nilionekana madhubuti sana. Lakini niliporudi kwa seli yangu, sikuweza kujizuia kuwa dhaifu kidogo na kusononeka. Ilionekana kuwa mume wangu kwa kweli angenitaliki na singekuwa na nyumba tena. Pia sikujua hukumu yangu ingekuwa na urefu gani. Katikati ya maumivu haya, nilifikiria maneno haya kutoka kwa Mungu: “Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali wowote au baraka zozote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani zaidi kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake” ("Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" katika Neno Laonekana katika Mwili). Niliguswa sana na matendo ya Petro, na hili pia liliyatikisa hiari yangu ya kukiacha kila kitu ili nimridhishe Mungu. Ilikuwa ni kweli. Petro alipofikia hatua yake ya kupatwa na majonzi, bado alikuwa anaweza kuhimili na kumridhisha Mungu. Haikuwa kwa matarajio yake mwenyewe au jaala, au faida yake mwenyewe, na mwishowe alipotundikwa juu chini kwa msalaba alitenda kama shahidi mzuri kwa Mungu. Lakini tena nilikuwa na bahati nzuri kumfuata Mungu mwenye mwili, kufurahia utoaji wa Mungu usio na mwisho kwa maisha yangu pamoja na neema na baraka Zake, lakini sikuwahi kulipa kamwe gharama yoyote halisi kwa Mungu. Halafu Aliponihitaji kuwa shahidi Kwake, sikuweza kumridhisha mara hiyo moja tu? Ukosaji wa fursa hii ungekuwa kitu ambacho ningejutia kwa maisha yote? Nilipofikiria hilo, niliamua hiari yangu mbele ya Mungu: Ee Mungu, niko tayari kufuata mfano wa Petro. Bila kujali matokeo yangu yatakuwa nini, hata kama ni lazima nitalikiwe au kutumikia kifungo jela, sitakusaliti Wewe! Baada ya kuomba, nilihisi wimbi la nguvu likiinuka ndani yangu. Singefikiria tena kama ningehukumiwa au la, au ni kwa muda gani hukumu hiyo ingekuwa, na singefikiria tena kama ningeweza kurudi nyumbani na kuungana tena na familia yangu au la. Ningefikiria tu kwamba siku nyingine katika pango hili la pepo ilikuwa siku nyingine ya kuwa shahidi kwa Mungu, na hata kama ningetumikia kifungo mpaka mwisho kabisa, singekubali kushindwa na Shetani. Nilipojitoa mwenyewe, kwa kweli nilikuwa na ladha ya upendo wa Mungu na huba. Siku chache baadaye wakati wa alasiri moja, mlinzi mmoja ghafla akaniambia: "Kusanya vitu vyako, unaweza kwenda nyumbani." Sikuthubutu kuamini masikio yangu kabisa! Kabla ya kuachiliwa polisi walinitaka nitie sahihi hati moja. Niliona maneno haya yameandikwa kwa dhahiri: "Hana hatia kutokana na ushahidi usiotosha, mwachilie." Kuona hili, nilikuwa na msisimko usiokadirika. Niliona tena kudura na uaminifu wa Mungu, kwamba “… wale ambao wako tayari kujitoa wenyewe wanaweza kuvuka bila wasiwasi.” Mapigano haya katika vita vya kiroho yamepotezwa na Shetani na Mungu alitukuzwa mwishowe!
Baada ya kupitia siku 36 kizuizini na mateso na polisi wa Kichina, nilikuwa na ufahamu wa kweli wa udhalimu wa ukatili, na kiini cha uasi na cha kupinga maendeleo cha serikali ya CCP. Kuanzia wakati huo kwendelea nikawa na chuki kubwa kwayo. Najua kwamba wakati wa shida hizo, Mungu alikuwa nami daima, akanipa nuru, akiniongoza, na kuniruhusu niushinde ukatili wa Shetani na majaribio kila hatua ya njia. Hili lilinipa uzoefu wa ukweli kwamba maneno ya Mungu kwa kweli ni maisha ya wanadamu na nguvu zetu. Pia nilifahamu kwa kweli kwamba Mungu ni Bwana wetu na hutawala kila kitu, na bila kujali ni hila ngapi Shetani anazo, daima atashindwa na Mungu. Alijaribu kuutesa mwili wangu kunilazimisha kumsaliti Mungu, kumtelekeza Yeye, lakini mateso yake ya ukatili hayakukosa tu kunivunja, lakini yaliuimarisha uamuzi wangu na kuniruhusu kuona kabisa uso wake muovu, kutambua upendo wa Mungu na wokovu. Ninamshukuru Mungu kwa dhati kwa kila kitu ambacho Amenitayarishia, akaniruhusu nipate utajiri wa thamani zaidi wa maisha! Azimio langu la kibinafsi ni: Bila kujali ukandamizaji au dhiki zilizo kwa njia iliyo mbele, niko tayari kumfuata Mungu kwa uthabiti na kuendelea kueneza injili kama awali ili kuufidia upendo Wake mkubwa!
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Tazama zaidi: ushuhuda wa Umeme wa Mashariki

0 意見:

Chapisha Maoni