Sura ya 4 Lazima Mjue Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho
3. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu.
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.
Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.
kutoka kwa "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kinachohukumiwa ni dutu ya mwanadamu iliyopotoka, dutu ya mwanadamu iliyopotoshwa na Shetani, na dhambi zote za mwanadamu. Mungu hahukumu makosa madogo madogo ya mwanadamu na yasiyokuwa na umuhimu. Kazi ya hukumu ni ya uwakilishi, na haifanywi mahususi kwa ajili ya mtu fulani. Badala yake, ni kazi ambayo kwayo kundi la watu wanahukumiwa ili kuiwakilisha hukumu ya wanadamu wote. Kwa Yeye mwenyewe kufanya kazi Yake katika kundi la watu, Mungu mwenye mwili anatumia kazi Yake ili kuwakilisha kazi ya wanadamu wote, ambayo inaenea taratibu. Kazi ya hukumu pia ipo hivyo. Mungu hahukumu aina fulani ya mtu au kundi fulani la watu, bali anawahukumu wasio na haki wote miongoni mwa wanadamu—upinzani wa mwanadamu kwa Mungu, kwa mfano, au mwanadamu kutomcha Yeye, au kusababisha usumbufu katika kazi ya Mungu, na kadhalika. Kile kinachohukumiwa ni hulka ya mwanadamu ya kumpinga Mungu, na kazi hii ni kazi ya mashindano ya siku za mwisho. Kazi na neno la Mungu mwenye mwili lililoshuhudiwa na mwanadamu ni kazi ya hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi wakati wa siku za mwisho, ambacho kilibuniwa na mwanadamu katika kipindi cha siku za nyuma. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu mwenye mwili ni hukumu yenyewe mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi.
kutoka kwa "Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufunua kiini cha mwanadamu, na kuchunguza maneno na matendo ya mwanadamu huyo. Maneno haya yanajumuisha kweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yanalenga nafsi na tabia potovu ya mwanadamu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu anavyomkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu za adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kufaidi ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka kwa "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki. Kazi Yake itakapoisha, wale watu watakaobaki watatakaswa na kufurahia maisha ya pili ya binadamu ya ajabu zaidi duniani waingiapo ulimwengu wa juu wa binadamu; kwa maneno mengine, wataingia katika siku ya binadamu ya raha na kuishi pamoja na Mungu. Baada ya wasioweza kubaki kupitia kuadibu na hukumu, umbo zao halisi zitafichuliwa kabisa; baada ya haya wote wataangamizwa na, kama Shetani, hawatakubaliwa tena kuishi duniani. Binadamu wa baadaye hawatakuwa tena na aina yoyote ya watu hawa; watu hawa hawafai kuingia eneo la raha ya mwisho, wala hawafai kuingia siku ya raha ambayo Mungu na mwanadamu watashiriki, kwani ni mashabaha ya adhabu na ni waovu, na si watu wenye haki.
kutoka kwa "Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja" katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi yake ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ile ya kuadibu na hukumu, ambayo inafichua yote ambayo si ya haki, na kuhukumu wanadamu hadharani, na kukamilisha wale ambao wanampenda kwa ukweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Kila kitu kitabainishwa kulingana na aina, na kitagawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yake. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua hatima ya wanadamu na kikomo cha safari yao. Kama mwanadamu hatashuhudia kuadibu na hukumu yake, basi hakutakuwepo na mbinu ya kufichua uasi na udhalimu wa mwanadamu. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mzuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi zote zinahitaji kuadibu kwa haki na hukumu kutimizwa. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu.
kutoka kwa "Maono ya Kazi ya Mungu (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo Mungu anawahukumu, na kuwaadibu, na kuwashutumu, lakini jueni kwamba shutuma yako ni ili kukufanya kuweza kujijua. Shutuma, laana, hukumu, kuadibu—haya yote ni ili kwamba uweze kujijua, ili tabia yako iweze kubadilika, na, zaidi ya hayo, ili uweze kujua thamani yako, na kutambua kwamba vitendo vyote vya Mungu ni vyenye haki, na kulingana na tabia Yake na mahitaji ya kazi Yake, kwamba Anafanya kazi kulingana na mpango Wake kwa wokovu wa mwanadamu, na kwamba Yeye ndiye Mungu mwenye haki anayempenda mwanadamu, na kumwokoa mwanadamu, na Anayemhukumu na kumwadibu mwanadamu. Kama utajua tu kwamba wewe ni mwenye hadhi ya chini, na kwamba umepotoka na hutii, lakini hujui kwamba Mungu angependa kuweka wazi wokovu Wake kupitia kwa hukumu na kuadibu ambako Anafanya ndani yako leo, basi huna njia yoyote ya kupitia haya, isitoshe huwezi kuendelea mbele. Mungu hajaja kuua, au kuangamiza, lakini kuhukumu, kulaani, kuadibu, na kuokoa. Kabla ya hitimisho ya mpango Wake wa usimamizi wa miaka 6,000—kabla ya Yeye kuweka wazi mwisho wa kila aina ya binadamu—kazi ya Mungu ulimwenguni ni kwa ajili ya wokovu, yote haya ni ili kuwafanya wale wanaompenda Yeye kukamilika kabisa, na kuwarejesha katika utawala Wake. … Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa yeye na kumfanya yeye kuutoa moyo wake na kumpa Yeye kupitia kwa baraka na neema Zake. Hivyo ni kusema, Anapomgusa mwanadamu Anamwokoa yeye. Wokovu kama huu ni wokovu ambao shughuli ya biashara inafanywa. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu anaponyenyekea kwa jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Leo, wokovu wako unatokea kwenye wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? Nyote mmeona Mungu mwenye mwili na kutambua kudura na hekima Yake; zaidi ya hayo, umepitia hali ya kupigwa na kufundishwa nidhamu mara kwa mara. Lakini je, hujapokea pia neema kubwa? Je, baraka zako si kubwa zaidi kuliko za mtu yeyote mwengine? Neema zako ni nyingi zaidi kuliko utukufu na utajiri ulioofurahiwa na Sulemani! Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, lisingekuwa neno moja tu ambalo Ningetumia kuwaadhibu nyinyi viumbe wenye kufa tu? Ningekuwa bado na akili ya kukuangamiza baada ya kukushutumu? Je, bado husadiki maneno haya Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
kutoka kwa "Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutoka kwa Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu Mambo Muhimu ya Muumini Mpya
Yaliyopendekezwa: Tazama zaidi Matamshi ya Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Neno la Mungu Vitabu.
0 意見:
Chapisha Maoni