Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I
Mamlaka ya Mungu (I)
Sehemu ya Pili
Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Mwenyezi Mungu alisema, Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu.
Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kujitokeza kwa kila kiumbe kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Wakati huu, moyo Wake ulifaidi sehemu ndogo ya kutosheka, lakini mpango Wake ulikuwa ndio tu umeanza. Punde si punde, siku mpya ilikuwa imewadia—na ukurasa unaofuata ulikuwa upi kwenye mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, kuangaza kwetu kwa macho kunatufikisha kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mpya. Bila shaka, kwa Muumba, bila tashwishi ilikuwa ni siku nyingine nzuri, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa mwanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Ilikuwaje nzuri, ilikuwaje muhimu, na ilikuwaje yenye thamani isiyopimika? Hebu na tuweze kusikiliza matamshi yaliyotamkwa na Muumba….
“Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo ishara, na majira, na siku na miaka: Na tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu ipeane nuru juu ya nchi” (Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa ardhi kavu na mimea iliyokuwa ndani yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa rahisi kwa kiasi fulani, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mzuri kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litaweza kutimizwa. Mungu aliamuru nuru kujitokeza mbinguni, na nuru hizi hazikuangaza tu kwenye mbingu lakini pia kwenye ardhi, lakini pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na maana ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.
Nuru kwenye mbingu ni viumbe vilivyo kwenye mbingu vinavyoweza kuonyesha nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mpigo na mara ngapi ambapo vimeamriwa na Mungu, na vinaangaza sehemu mbalimbali zenye vipindi tofauti vya muda kwenye ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya kuzunguka kwa nuru hizi husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa ardhi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia karamu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo nyongeza na saidizi timilifu kwa misimu minne—mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo nuru hizi huhudumu kwa mpangilio maalum kama alama za mara kwa mara na sahihi kwa minajili ya vipimo mbalimbali, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawaje ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishi wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.
Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha “jioni na asubuhi,” “ile anga,” “ardhi na bahari,” “nyasi, miti isiyozaa na aina mbalimbali za miti,” na “nuru, misimu, siku, na miaka” kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu vitendo vya Muumba vimechangamsha moyo wako na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.
Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza na huvutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kukwepa haya ila kuyaangazia tu macho matendo haya ya kipekee yaliyozaliwa kutokana na utekelezwaji wa mamlaka husika. Nguvu zake za kipekee zafurahisha baada ya kufurahisha, na binadamu anabaki akishangaa na akijawa na furaha, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; nini kingine tena, binadamu amefurahishwa kwa kumtazama alivyo, na kilichozaliwa ndani yake ni heshima, kustahi, na mtagusano wa karibu. Mamlaka na vitendo vya Muumba vinayo athari kwa roho ya binadamu na hutakasa roho ya binadamu na zaidi, kutosheleza roho ya binadamu. Kila mojawapo ya fikira Zake, kila mojawapo ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kiungo muhimu miongoni mwa viumbe vyote, na ni utekelezaji mkuu wenye thamani zaidi wa kuunda ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote.
Hebu tuendelee kusoma Maandiko fungu hadi fungu, tunapoangalia vitendo vingi zaidi vya Muumba.
Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti
Maandiko yanasema, “Mungu akasema, Maji na yalete kwa wingi kiumbe kiendacho chenye uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga la mbingu. Na Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kinachoenda, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi, kila kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye kwa jinsi yake: Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri” (Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa hewani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu….
Kama vile maneno ya Mungu yalivyotamkwa, maisha mapya mazuri, kila mojawapo ikiwa na umbo tofauti, kwa ghafla vilipata uhai miongoni mwa matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikijitikisatikisa kwa minajili ya kupata nafasi, kuruka, kurukaruka kwa furaha…. Samaki wa maumbo na ukubwa wote waliweza kuogelea majini, samakigamba wa kila aina waliweza kukua kwenye michanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za mwani kuanza kukua kwa haraka, ikiyumbayumba kutokana na msongo wa maisha mbalimbali ya majini, yasiyosita, na yanayosihi yale maji tulivu, ni kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki wako! Kwani hutawahi kuwa pekee tena! Kuanzia muda ule ambao viumbe mbalimbali vilivyo na uhai viliumbwa na Mungu na kuonekana majini, kila maisha mapya yalileta nguvu kwenye maji yaliyokuwa tulivu kwa muda mrefu, na kuweza kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia hapo kwenda mbele, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kutangamana pamoja, na wala havikujiona tofauti. Yale maji yalikuwepo kwa minajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakipatia uhai kila maisha yaliyokuwa karibu na kumbatio lake, na kila maisha yalikuwepo kwa minajili ya maji kwa sababu ya uhai wake. Kila moja ilipatia uhai mwenzake, na wakati uo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitolea ushuhuda wa miujiza na ukubwa wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizoshindwa za mamlaka ya Muumba….
Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia maisha yalivyoanza kujaza mbingu. Mmoja baada ya mwengine, ndege, wakubwa na wadogo, walipaa kwenye mbingu kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye neema. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na mbinu walizopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa mbinu walizokuwa nazo wakapaa katikati ya mbingu na ardhi, kotekote kwenye mbuga na misitu…. Walikuwa ndio wapenzi wa hewani, walikuwa ndio wapenzi wa viumbe vyote. Hivi punde ndio wangekuwa kiunganishi kati ya mbingu na ardhi, na wangepitisha ujumbe kwa viumbe vyote…. Waliimba, wakawa wanapaapaa kwa furaha kotekote, walileta vifijo, vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia kuimba kwao kwa uwazi, kuvutia, na kutumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kusifu Muumba kwa maisha aliyowapa. Walicheza kwa uchangamfu ili kuonyesha utimilifu na miujiza ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia agano la mamlaka ya Muumba kupitia kwenye maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa….
Licha ya kama vilikuwa majini, au mbinguni, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hivi hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishika na viumbe vyovyote. Havikuwahi kuthubutu kwenda nje ya mipaka viliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaana, na kutii kwa umakinifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa kufahamu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na matamshi na maelekezi ya kimbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao wenyewe maalum, na wakashukuru maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti viumbe vyote kwa kimya ambacho hakikumiliki matumizi yoyote ya lugha, na iliyokuwa tofauti na mwanadamu. Utiliaji mkazo wa mamlaka Yake kwa njia hii maalum ulimshawishi binadamu kupata maarifa mapya, na kuufanya ufasiri mpya wa mamlaka ya kipekee ya Mungu. Hapa, lazima Niwaambie kwamba kwenye siku hii mpya, ule utiliaji mkazo wa mamlaka ya Muumba ulionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.
Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya fungu hili la maandiko:
“Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.” Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama viumbe vyote Alivyokuwa ameumba vikiumbika na kusimama wima kwa sababu ya matamshi Yake, na kwa utaratibu vikianza kubadilika. Wakati huu, Mungu alikuwa ametosheka na mambo mbalimbali Aliyoyaumba kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.” Wewe unaona nini hapa? Kinawakilisha nini kwamba “Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri ”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepangilia na kushauri, kukamilisha shabaha Alizokuwa ameweka wazi ili kuzikamilisha. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.” Kwa maneno mengine, Hakujutia chochote, lakini Alitosheka. Ni nini maana ya Yeye kutojutia chochote? Tunaelezewa kwamba Mpango wa Mungu ni mtimilifu, kwamba nguvu na hekima Zake ni timilifu, na hiyo ni kutokana tu na mamlaka Yake kwamba utimilifu kama huo unaweza kukamilishwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kukamilika na kuwa timilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho timilifu, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia utimilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa kizuri, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri ,” kila kitu Alichoumba kikachukua mfumo wa kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa mahali maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu. Vilevile, wajibu wao miongoni mwa viumbe vyote na safari ambayo lazima waabiri kwenye usimamizi wa Mungu wa viumbe vyote, ulikuwa tayari umeamriwa na Mungu, na usingebadilishwa. Hii ilikuwa sheria ya kimbinguni iliyotolewa na Muumba kwa viumbe vyote.
“Na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri,” matamshi haya mepesi, yasiyopongezwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ndiyo matamshi ya sheria ya kimbinguni na maelekezo ya kimbinguni kwa viumbe vyote kutoka kwa Mungu. Ni mfano mwingine halisi wa mamlaka ya Muumba, mfano ambao ni wa kimatendo zaidi na unaojitokeza zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote viliishi na kufa pia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itabatilishwa na Muumba! Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!
Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….
“Mungu akasema, Na nchi izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, na kile kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake: na ikawa hivyo. Na Mungu akaunda mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake: na Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.” (Mwa 1:24-25). Viumbe hai gani ndivyo vinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: ng'ombe, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai kwenye nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.”
Kama tu kwenye siku zile tano za awali, na kwa sauti sawa, kwenye siku ya sita Muumba akashurutisha kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na vikajitokeza kwenye nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anapotekeleza mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure bilashi, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kikajitokeza wakati ule Aliochagua. Muumba aliposema “Na nchi izae kiumbe hai kwa jinsi zake,” nchi ilijawa mara moja na maisha, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Kwenye jangwa lenye nyasi za kijani, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwengine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kurukaruka…. Mara moja, nchi pana tambarare yenye utulivu ikajaa uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali kulikuwa mandhari ya kupendeza kwenye nchi ile tambarare iliyotulia, na kujitokeza huko kukaleta nguvu zisizo na mipaka …. Wangekuwa wenza wa nchi ile tambarare, na wenyeji wakuu wa nchi ile tambarare, kila mmoja akitegemea mwengine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha ukuzwaji wa milele kwa minajili ya kuwepo kwao….
Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwengine. Hata ingawaje ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka juu kwa juu, wengine wakapepesuka; wengine walichimba wakienda mbele, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine wakaruka juu na chini…. Wote walishughulika kwa kujaribu kujitafutia makao: Baadhi walisukumana na kujipata kwenye nyasi, baadhi walianza kuyachimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, wakiwa wamejificha kwenye msitu…. Ingawaje walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusita kupumzika, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kolevu cha kumetameta yaliwapa mlo wenye utomvu mwingi…. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakusita kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walimilikiwa na nishati ya ajabu pamoja na uchangamfu usio na mipaka, na kwa viumbe vyote wao ndio walikuwa amilifu zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya kazi na wakafanyiza miili yao bidii kwa minajili ya siku zao za usoni, wakiwa wamejishughulisha na kukimbia hapa na pale kwa minajili ya kesho yao ili waweze kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila inchi ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na wakitumia mkondo wao binafsi maalum wa maisha, waliweka alama katika viumbe vyote, na baadaye wakaacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchanga, nyasi, na misitu, na walipatia mchanga nguvu na uthabiti, vivyo hivyo kwenye nyasi, na misitu na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote….
Mtazamo wa Muumba ulienea kotekote kwenye viumbe vyote ambavyo Alikuwa ameumba na wakati huu kwa muda huo macho Yake yalitulizia misitu na milima, akili Yake ikigeuka. Huku matamshi Yake yakitamkwa wazi kwenye misitu mingi, na juu ya milima, kulionekana aina ya viumbe fulani vilivyokuwa tofauti na vyovyote vile vilivyokuwa vimekuja hapo awali: Walikuwa “wanyama wa mwitu” waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Walikuwa wamepitiliza muda mrefu ajabu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, huku kila mmoja wao akiwa na uso wake pekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa wamejikinga, baadhi yao walikuwa na meno ya sumu, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo-ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho— mapana, baadhi walikuwa na mtazamo wa woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakidundadunda kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakirukaruka kwa kwato nne, baadhi walikuwa wakiangalia mbele juu ya mti, baadhi walikuwa wamejilalia tu wakisubiria misituni, baadhi walikuwa wakitafuta vyumba vya chini kwa chini ili kupumzika, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kuonyesha furaha ya kipekee kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi walikuwa wakibweka, baadhi walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti nyororo, baadhi walikuwa na sauti ya kati, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti safi na yenye mdundo wa kimuziki…; baadhi walikuwa wa kuogofya, na baadhi walikuwa warembo, na baadhi walikuwa wakitisha, baadhi walikuwa wa kuvutia, baadhi walikuwa wa kutishia, baadhi walikuwa wasio na hatia ila wachangamfu…. Mmoja baada ya mwengine, wote walikuja. Tazama namna walivyotembea, kwenye uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda kutazamana…. Kila mmoja akiwa na maisha fulani waliyopewa na Muumba, na umwitu wao binafsi, na ukatili, walionekana kwenye misitu na pia juu ya milima. Viumbe vya kudharauliwa kati ya vyote, na vyenye kuamrisha kabisa—ni nani aliyewafanya kuwa mabingwa wa kweli wa milimani na misituni? Kutoka muda ambao Kuonekna kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kuweka madai” hayo katika misitu, na “kuweka madai” kwenye milima, kwani Muumba alikuwa tayari amepangilia mipaka yao na Akaamua upana wa uwepo wao. Hawa ndio waliokuwa mabwana wa kweli wa milimani na misitu, na ndiyo maana walikuwa na umwitu mwingi na kwa hivyo wenye dharau. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wasiowezekana, wenye unyama, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Na ilikuwa kwa sababu waliishi umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na mwanadamu ndiposa waliweza kutimiza wajibu wao waliopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule umwitu wao uliilinda milima na kulinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la uwepo wao na utekelezaji wao. Wakati uo huo, umwitu wao uliendeleza na kuhakikisha usawazisho miongoni mwa viumbe vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na ukitaji mizizi kwenye milima na misitu; kuingia kwao kuliweza kuingiza nguvu na uthabiti zaidi kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia hapa kwenda mbele, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu kule kusihiwa na Muumba ili waweze kushikilia eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kuendeleza usawazisho wa viumbe vyote vilivyoanzishwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!
Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu
Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule ni sura mbaya kweli, hakuna vile ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kijinga ulioje! Kile wanachofaa kusema ni, “ingawaje mdudu huyu ana sura mbaya sana, aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Kwenye fikira za Mungu, Alinuia kupatia kila mojawapo ya sura, na kazi na matumizi aina zote, katika viumbe mbalimbali vilivyo na uhai Alivyoumba, na hivyo basi hamna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia sura yao ya nje hadi mkusanyiko wao wa ndani, kuanzia katika mazoea yao ya kuishi hadi mahali pa kuishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana sura ya ng’ombe, punda wana sura ya punda, paa ana sura ya paa, na ndovu wana sura ya ndovu. Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi kinachovutia zaidi na ni kipi kinachotisha zaidi kwa sura? Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi chenye manufaa zaidi na uwepo wa kile ambacho hakihitajiki sana? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu hufanana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui mkubwa mwenye milia walivyo, kwani sura inavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na viumbe vyote, binadamu anafaa kurejelea mamlaka ya Muumba, hivi ni kusema kwamba, rejelea mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika viumbe vyote; huu ndio mtazamo wenye hekima zaidi. Mtazamo tu wa kutafutiza, na wa kuwa mtiifu, kwa nia ama makusudio ya mwanzo ya Muumba ndio ukubalifu wa kweli na hakika wa mamlaka ya Muumba. Ni vyema kwa Muumba, kwa hivyo ni sababu gani ambayo binadamu atakuwa nayo ya kusema kwamba si vyema?
Hivyo basi, viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba....
Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba
Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, ingawaje vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawaje wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!
Kupitia ushirika uliotajwa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Kiongozi wa viumbe vyote tu, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung'amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu kutazama vitendo halisi vya dhana nyingi za mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kushukuru, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
0 意見:
Chapisha Maoni