Jaweni na Upendo kwa Ajili ya Mungu | Muziki wa Akapela "Yasifu Maisha Mapya"

Haleluya! Twakushukuru na kukusifu Wewe, Mwenyezi Mungu! Kristo wa siku za mwisho ameonekana, akifanya kazi na kuzungumza miongini mwa wanadamu. Neno lake hutuhukumu, kutuadibu na kututakasa, likituongoza kwenye njia sahihi ya maisha ya binadamu.

Ukaribisheni Urejeaji wa Bwana Yesu | Sifa na Ibada “Mungu Ameleta Utukufu Wake Mashariki”

Mungu aliipa Israeli utukufu Wake kisha Akauhamisha mbali na pale, na kuwaleta Waisraeli na kuwaleta watu wote Mashariki. Mungu amewaelekeza wote kwenye mwanga ili waweze kuungana tena na kuwa pamoja na mwanga, wasilazimike kuutafuta tena, kuutafuta mwanga.

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | “Bwana Wangu Ni Nani” ( Filamu za Injili )

Liu Zhizhong ni mzee katika kanisa moja la mtaani la nyumba nchini China. Amekuwa muumini kwa zaidi ya miaka 30, na amesisitiza bila kukoma kwamba “Biblia ni ufunuo wa Mungu,” “Biblia inamwakilisha Mungu, kuamini katika Mungu ni kuamini katika Biblia, kuamini katika Biblia ni kuamini katika Mungu.”

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya

Mungu ametutunza daima–Yeye amesikiliza maombi yetu! Anajua tumekuwa tukitamani kurejea Kwake! Sasa kwa hakika Amerejea! Tunasubiri nini bado? Tafadhali endelea kutazama drama yenye muziki ya Kanisa la Mwenyezi Mungu—Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo!

NYENDO ZA MATESO YA KIDINI NCHINI CHINA (Christian Videos) swahili

Wakristo wanaoteswa katika filamu hii ni watu kutoka kwa vikundi vya kidini na madhehebu tofauti ambao walitafuta ukweli, na ambao waliisikia sauti ya Mungu na hivyo wakarudi kwa Mwenyezi Mungu.

Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano hukumu. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho ya hoja yaliyopangwa kwa uhusiano hukumu. Panga kwa tarehe Onyesha machapisho yote

Jumatano, 3 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.)Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi.

Jumapili, 5 Novemba 2017

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Mwenyezi Mungu alisema, Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.

Jumatatu, 6 Mei 2019

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

2. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni hukumu ya kiti cha enzi kikubwa, cheupe, kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).
Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao.

Ijumaa, 14 Septemba 2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu

Sura ya 4 Lazima Mjue Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

3. Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Hukumu na Kuadibu.

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi.

Jumanne, 7 Mei 2019

3. Ni vipi kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa wanadamu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

3. Ni vipi kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho 

humtakasa na kumwokoa wanadamu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).

Alhamisi, 9 Mei 2019

4. Umuhimu wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho unaweza kuonekana katika matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho

III. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho
4. Umuhimu wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho unaweza kuonekana katika matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho
(1) Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho inafanywa kumtakasa, kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu, na kukiunda kikundi cha washindi
Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa sababu umelihifadhi neno la uvumilivu wangu, pia mimi nitakuhifadhi dhidi ya saa ya majaribu, ambayo itajia dunia yote, kuwajaribu wale waishio duniani.

Jumatatu, 26 Machi 2018

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki.

Jumatatu, 19 Februari 2018

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

22. Maneno ya Mungu Yameniamsha

Miao Xiao Mji wa Jinan, Mkoa wa Shandong
Katika siku zilizopita, nilikuwa daima nikifikiri kuwa Mungu aliposema “ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi” Alikuwa anaashiria wale wanaoikubali hatua hii ya kazi lakini wanaishia kurudi nyuma kwa sababu hawako radhi kustahimili mateso ya kuadibu na hukumu Yake.

Jumatano, 2 Mei 2018

60. Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu

60. Chochote Mungu Asemacho Ndiyo Hukumu Hasa ya Mwanadamu

Xunqiu    Mji wa Nanyang, Mkoa wa Henan
Nilikuwa nikidhani kwamba Mungu alimhukumu na kumuadibu mwanadamu wakati tu Alipoufichua upotovu wa asili wa mwanadamu au alipoeleza maneno mkali ambayo yaliuhukumu mwisho wa mwanadamu. Ilikuwa ni baadaye kabisa tu ambapo tukio moja liliponiongoza kutambua kwamba hata maneno mapole ya Mungu pia yalikuwa ni hukumu na kuadibu Kwake. Niligundua kuwa kila neno Alilolisema Mungu ni hukumu Yake kwa mwanadamu.

Jumapili, 18 Februari 2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)

Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo.

Jumatano, 10 Julai 2019

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Maneno ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 103

Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami.

Jumatatu, 20 Mei 2019

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?

IV. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Hatua Tatu za Kazi ya Mungu na Majina Yake

2. Kuna tofauti ipi kati ya jinsi ambavyo Bwana Yesu alifanya kazi katika Enzi ya Neema na jinsi Mwenyezi Mungu anavyofanya katika Enzi ya Ufalme?


Maneno Husika ya Mungu:
Wakati wa kupata mwili Kwake mara ya kwanza, ilikuwa muhimu kwa Mungu kuponya wagonjwa na kufukuza mapepo kwa sababu kazi Yake ilikuwa ni kukomboa. Ili kulikomboa kabila lote la mwanadamu, Alipaswa kuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe. Kazi Aliyoifanya kabla ya kusulubiwa ilikuwa kuponya watu na kufukuza mapepo, ambayo iliashiria wokovu Wake wa mwanadamu kutoka katika dhambi na uchafu. Kwa sababu ilikuwa ni Enzi ya Neema, ilikuwa muhimu Kwake kuponya wagonjwa, na kwa njia hiyo Alionyesha ishara na miujiza, mambo ambayo yalikuwa kiwakilishi cha neema katika hiyo enzi; kwani Enzi ya Neema ilikitwa katika kutolewa kwa neema, ikiashiriwa na amani, furaha, na baraka ya vitu, vyote vikiwa zawadi za imani ya watu kwa Yesu. Hii ni kusema kuwa, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kutoa neema ulikuwa uwezo asilia wa mwili wa Yesu katika Enzi ya Neema, mambo haya yalikuwa ni kazi ya Roho iliyopatikana katika mwili.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ambayo Yesu alifanyika ililingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, ustahamilivu, huruma na wema. Aliwabariki wanadamu kwa wingi na kuwaletea neema nyingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu Wake na upendo, huruma Yake na wema. Katika siku hizo, chote alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, roho yake ilifarijika, na alikuwa anaruzukiwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa tayari na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji neema nyingi, ustahimili na uvumilivu usio na mwisho, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu walichoona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya kulipia dhambi za binadamu, yaani, Yesu. Yote waliyojua ni kwamba Mungu angeweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na yote waliyoona ni huruma ya Yesu na wema Wake. Hii yote ilikuwa ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Na hivyo, kabla ya kuweza kukombolewa, walilazimika kufurahia neema za aina nyingi ambazo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na pia wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu pekee ndio walipata haki ya wa kupokea msamaha na kufurahia neema nyingi kutoka kwa Yesu—kama vile Yesu alivyosema: Sijakuja kuwakomboa wenye haki, ila wenye dhambi, kukubali dhambi zao zisamehewe. … Jinsi Yesu alivyowapenda wanadamu zaidi, Akisamehe dhambi zao na kuwapa huruma na wema wa kutosha, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, wa kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa gharama kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anavyotunza mtoto mchanga aliye kifuani pake. Yeye hakuwa na hasira nao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na ghadhabu miongoni mwao, lakini alistahimili dhambi zao na Akapuuza upumbavu wao na kutofahamu, hata kusema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine. Ilikuwa ni kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha wa dhambi kupitia uvumilivu Wake.
kutoka katika “Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Roho Mtakatifu Anafanya kazi kulingana na enzi, sio tu katika mapenzi Yake ama kulingana na masharti. Enzi zimebadilika, na enzi mpya lazima ilete kazi mpya. Huu ni ukweli wa kila hatua ya kazi, na hivyo kazi Yake haiwezi kurudiwa. Katika Enzi ya Neema, Yesu Alifanya nyingi ya kazi hiyo, kama kuponya magonjwa, kukemea mapepo, kuwekelea mikono Yake juu ya wanadamu, na kumbariki mwanadamu. Hata hivyo, kuendelea kufanya hivyo hakutasaidia chochote katika wakati huu. Roho Mtakatifu Alifanya kazi hivyo katika huo wakati, kwani ilikuwa Enzi ya Neema, na mwanadamu alipewa neema ya kutosha ili afurahie. Mwanadamu hakuhitajika kulipa gharama yoyote na angepokea neema mradi tu angekuwa na imani. Kila mtu alitendewa kwa neema kubwa. Sasa, enzi imebadilika, na kazi ya Mungu imeendelea zaidi; kupitia kuadibu na hukumu Yake, uasi wa mwanadamu na vitu vichafu katika mwanadamu vitatupiliwa mbali. Jinsi ilivyokuwa hatua ya wokovu, ilimbidi Mungu kufanya kazi hiyo, Akimwonyesha mwanadamu neema ya kutosha ili mwanadamu afurahie, ili Amkomboe mwanadamu kutoka kwa dhambi, na kwa neema amsamehe mwanadamu dhambi zake. Hatua hii ya sasa ni ya kufichua udhalimu ulio ndani ya mwanadamu kwa njia ya kuadibu, hukumu, kupigwa na maneno, na vile vile nidhamu na ufunuo wa maneno, ili baadaye binadamu waweze kuokolewa. Hii ni kazi ya undani zaidi kuliko ukombozi. Katika Enzi ya Neema, mwanadamu alifurahia neema ya kutosha na amezoea neema hii, kwa hivyo sio ya kufurahiwa na mwanadamu tena. Kazi kama hii imepitwa na wakati sasa na haitafanyika tena. Sasa, mwanadamu anaokolewa kupitia hukumu ya neno. Baada ya mwanadamu kuhukumiwa, kuadibiwa na kusafishwa, tabia yake basi inabadilika. Je sio kwa sababu ya maneno ambayo Nimenena?
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.
Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.
kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu sasa ameanza rasmi kuwakamilisha watu. Ili kufanywa kuwa kamili, watu lazima wapitie ufunuo, hukumu, na kuadibu kwa maneno ya Mungu, na kupitia majaribio na usafishaji wa maneno Yake (kama vile jaribio la watendaji huduma). Kuongezea, watu lazima waweze kustahimili jaribio la kifo. Yaani, mtu ambaye kweli anafanya mapenzi ya Mungu anaweza kutoa sifa kutoka ndani ya kina cha moyo wake katikati ya hukumu ya Mungu, kuadibu, na majaribio, na anaweza kutii Mungu kwa ukamilifu na kujitelekeza mwenyewe, hivyo kumpenda Mungu kwa moyo wa uaminifu, nia moja, na utakatifu; huyo ndiye mtu kamili, na pia ni kazi ambayo Mungu anataka kufanya, na kile ambacho Mungu anataka kutimiza.
kutoka katika “Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake yenye haki. Tabia ya Mungu hasa huwa na haki, ghadhabu, uadhama, hukumu, na laana, na ukamilishaji Wake wa mwanadamu hasa ni kupitia hukumu. Watu wengine hawaelewi, na huuliza ni kwa nini Mungu anaweza tu kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu kupitia hukumu na laana. Wao husema kwamba kama Mungu angemlaani mwanadamu, si mwanadamu angekufa? Kama Mungu angemhukumu mwanadamu, si mwanadamu angelaaniwa? Basi anawezaje hata hivyo kufanywa mkamilifu? Hayo ndiyo maneno ya watu wasioijua kazi ya Mungu. Kile ambacho Mungu hulaani ni uasi wa mwanadamu, na kile Anachohukumu ni dhambi za mwanadamu. Ingawa Yeye hunena kwa ukali, na bila kiwango cha hisi hata kidogo, Yeye hufichua yote yaliyo ndani ya mwanadamu, na kupitia maneno haya makali Yeye hufichua kile kilicho muhimu ndani ya mwanadamu, lakini kupitia hukumu kama hiyo, Yeye humpa mwanadamu ufahamu mkubwa wa kiini cha mwili, na hivyo mwanadamu hujitiisha chini ya utii mbele za Mungu. Mwili wa mwanadamu ni wa dhambi, na wa Shetani, ni wa kutotii, na chombo cha kuadibu kwa Mungu—na kwa hiyo, ili kumruhusu mwanadamu kujijua, maneno ya hukumu ya Mungu lazima yamfike na lazima kila aina ya usafishaji itumike; ni wakati huo tu ndiyo kazi ya Mungu inaweza kuwa ya kufaa.
kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwenye macho ya mwanadamu, wokovu ni upendo wa Mungu, na upendo wa Mungu hauwezi kuwa kuadibu, kuhukumu, na kulaani; wokovu lazima uwe na upendo, huruma, na, zaidi ya hayo, maneno ya faraja, na lazima wokovu uwe na baraka zisizo na mipaka kutoka kwa Mungu. Watu husadiki kwamba wakati Mungu anapomwokoa mwanadamu Anafanya hivyo kwa kumgusa yeye na kumfanya yeye kuutoa moyo wake na kumpa Yeye kupitia kwa baraka na neema Zake. Hivyo ni kusema, Anapomgusa mwanadamu Anamwokoa yeye. Wokovu kama huu ni wokovu ambao shughuli ya biashara inafanywa. Pale tu ambapo Mungu atampa yeye mara mia ndipo mwanadamu anaponyenyekea kwa jina la Mungu, na kulenga kuwa na mienendo mizuri mbele ya Mungu na kumletea Yeye utukufu. Haya si mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu. Mungu amekuja kufanya kazi ulimwenguni ili kumwokoa mwanadamu aliyepotoka—hakuna uongo katika haya; kama upo, Asingefanya kazi Yake yeye Mwenyewe. Kitambo, mbinu Zake za wokovu zilikuwa kuonyesha upendo na huruma mkuu, kiasi cha kwamba Alijitolea Yake yote kwa Shetani ili naye aweze kuwapata wanadamu wote. Leo haifanani kamwe na kitambo: Leo, wokovu wako unatokea kwenye wakati wa siku za mwisho, wakati wa uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake; mbinu za wokovu wako si upendo wala huruma, lakini kuadibu na hukumu ili mwanadamu aweze kuokolewa kabisa. Hivyo basi, kila kitu unachopokea ni kuadibu, hukumu, na kupiga bila huruma, lakini jua kwamba katika kupiga huku kusiko na huruma hakuna hata adhabu ndogo zaidi, jua kwamba licha ya namna ambavyo maneno haya yanavyoweza kuwa makali, kile kinachokupata ni maneno machache yanayoonekana kutokuwa na huruma kabisa kwako, na jua kwamba, licha ya namna ambavyo hasira Yangu itakavyokuwa, kile kitakachokujia bado ni maneno ya mafunzo, na sinuii kukudhuru, au kukuua. Je, haya yote ni ukweli, sivyo? Jua kwamba leo, haijalishi kama kutakuwa na kuhukumu kwa haki au utakasaji usio na huruma na kuadibu, yote haya ni kwa minajili ya wokovu. Haijalishi kama leo kunao uainishaji wa kila mmoja kulingana na aina yake, au uwekaji wazi wa aina za mwanadamu, matamko yote ya Mungu na kazi ni kwa ajili ya kuwaokoa wale wanaompenda Mungu kwa dhati. Kuhukumu kwa haki ni kwa ajili ya kumtakasa mwanadamu, utakasaji usio na huruma ni kwa ajili ya kumsafisha mwanadamu, maneno makali au kuadibu yote ni kwa ajili ya kutakasa, na kwa minajili ya wokovu. Na hivyo, mbinu ya leo ya wokovu haifanani na ya kitambo. Leo, kuhukumu kwa haki kunakuokoa wewe, na ni zana nzuri pia ya kumuainisha kila mmoja wenu kulingana na aina, na kuadibu kusiko na huruma kunawaletea wokovu mkubwa—na ni kipi ambacho unahitajika kusema mbele ya kuadibu na kuhukumu huku? Je, hujafurahia wokovu kutoka mwanzo hadi mwisho? … Hebu fikiria: Kama nia Yangu ya kuja ulimwenguni ingekuwa ni kushutumu na kukuadhibu wewe, na wala si kukuokoa, je, siku zako zingedumu kwa muda mrefu? Mngeweza, enyi viumbe wenye dhambi wa mwili na damu, kuishi hadi leo? Kama ingekuwa tu ni kwa ajili ya kuwaadhibu nyinyi, kwa nini Nikawa mwili na kuanza kushughulikia shughuli kubwa kama hiyo? Je, lisingekuwa neno moja tu ambalo Ningetumia kuwaadhibu nyinyi viumbe wenye kufa tu? Ningekuwa bado na akili ya kukuangamiza baada ya kukushutumu? Je, bado husadiki maneno haya Yangu? Ningeweza kumwokoa mwanadamu kupitia tu kwa upendo na huruma? Au Ningetumia tu kusulubishwa kwa minajili ya kumwokoa mwanadamu? Je, tabia Yangu yenye haki si nzuri zaidi ya kumfanya mwanadamu kuwa mtiifu kabisa? Je, haiwezi kabisa kumwokoa mwanadamu zaidi?
Ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa makali, yote yanasemwa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, kwa kuwa Ninazungumza tu maneno na sio kuuadhibu mwili wa mwanadamu. Maneno haya humsababisha mwanadamu kuishi katika nuru, kujua kwamba mwanga upo, kujua kwamba mwanga ni wa thamani, hata zaidi kujua jinsi maneno haya yalivyo na manufaa kwa mtu, na kujua kwamba Mungu ni wokovu. Ingawa Nimesema maneno mengi ya kuadibu na hukumu, hayajafanywa kwako katika vitendo. Nimekuja kufanya kazi Yangu, kuzungumza maneno Yangu na, ingawa maneno Yangu yanaweza kuwa magumu, yanasemwa kwa hukumu ya upotovu na uasi wako. Madhumuni Yangu ya kufanya hili yanabaki kumwokoa mtu kutoka kwa utawala wa Shetani, kutumia maneno Yangu ili kumwokoa mwanadamu; Kusudi Langu sio kumdhuru mwanadamu kwa maneno Yangu. Maneno Yangu ni makali ili matokeo yaweze kupatikana kutoka katika Kazi Yangu. Ni katika kufanya kazi kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kujijua na anaweza kujitenga mbali na tabia yake ya uasi.
kutoka katika “Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Jumatatu, 15 Oktoba 2018

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Tatu

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Tamko la Mia Moja na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosema kile Ninachosema na kufanya Ninachokifanya wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu.

Jumamosi, 17 Februari 2018

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asili yake na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani.

Jumatatu, 1 Januari 2018

Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Kwa nini Umeme wa Mashariki Hutapakaa Kwenda Mbele na Maendeleo Yasiyozuilika?

Kristo wa siku za mwisho amekuwa akifanya kazi Yake nchini China kwa zaidi ya miaka 20, kazi ambayo imetetemesha makundi mbalimbali ya kidini kwa kina. Swali la kufadhaisha zaidi kwa jumuiya za kidini wakati huu limekuwa: Wachungaji wengi na wazee wa kanisa katika jumuiya ya kidini wamefanya liwezekanalo kuuhukumu na kuushambulia Umeme wa Mashariki kupitia njia mbalimbali kama vile kueneza uvumi kuhusu na kuukashifu Umeme wa Mashariki.

Jumamosi, 13 Januari 2018

Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kikristo,

Ni Tofauti Gani Iliyopo Kati Ya Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Ukristo na Kanisa la Mwenyezi Mungu huamini katika Mungu huyo huyo. Watu wanaoelewa historia ya dini wanajua kwamba Uyahudi wa Israeli ulizaliwa na kazi ambayo Yehova Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria. Ukristo, Ukatoliki, na Othodoksi ya Mashariki yote yalikuwa makanisa yaliyoibuka baada ya Bwana Yesu mwenye mwili kufanya kazi ya ukombozi.

Alhamisi, 22 Februari 2018

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa,

Imani za Kimsingi za Kanisa la Mwenyezi Mungu

(1) Mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mafundisho ya Ukristo yanatoka kwa Biblia, na mafundisho ya Kanisa la Mwenyezi Mungu yanatoka kwa ukweli wote ulioonyeshwa na Mungu tangu wakati wa uumbaji wakati wa kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme.

Jumapili, 19 Mei 2019

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?

V. Ni Lazima Mtu Ashuhudie Kipengele cha Ukweli Kuhusu Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu ya Hukumu Katika Siku za Mwisho na Kazi Yake ya Ukombozi Katika Enzi ya Neema

1. Kuna tofauti ipi kati ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme?


Aya za Biblia za Kurejelea:
Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).
Na kwamba toba na msamaha wa dhambi vinapaswa kuhubiriwa katika jina lake miongoni mwa mataifa yote, kuanzia Yerusalemu” (Luka 24:47).
Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).
Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).
Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Yesu ilikuwa kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu na kusulubiwa tu. Kwa hivyo, hakukuwa na haja Kwake kusema maneno zaidi ili kumshinda mtu yeyote. Mengi ya yale Aliyomfundisha mwanadamu yalitolewa kutoka kwa Maandiko, na hata kama kazi yake haikuzidi Maandiko, bado Aliweza kutimiza kazi ya kusulubiwa. Yake haikuwa kazi ya neno, wala kwa ajili ya kumshinda mwanadamu, lakini kwa minajili ya kumkomboa mwanadamu. Yeye Alihusika kama dhabihu ya dhambi tu kwa mwanadamu, na hakuhusika kama chanzo cha Neno kwa mwanadamu.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alizungumza tu na wanafunzi Wake mfululizo wa mahubiri kwa Enzi ya Neema, kama jinsi ya kuweka vitendoni, jinsi ya kukusanyika pamoja, jinsi ya kuuliza kwa maombi, jinsi ya kuwatendea wengine, na mengineyo. Kazi Aliyoifanya ilikuwa hiyo ya Enzi ya Neema, na alielezea tu juu ya jinsi wanafunzi na waliomfuata wanapaswa kuweka vitendoni. Alifanya tu kazi ya Enzi ya Neema na hakuna hata moja ya siku za mwisho. Wakati Yehova aliandika sheria ya Agano la Kale kwa Enzi ya Sheria, mbona basi hakufanya kazi ya Enzi ya Neema? Mbona hakueleza wazi mapema kazi ya Enzi ya Neema? Hii haingekuwa ya manufaa kwa kukubali kwa mwanadamu? Alitabiri tu kwamba mtoto mchanga wa kiume angezaliwa na kuja mamlakani, lakini Hakutekeleza mapema kazi ya Enzi ya Neema. Kazi ya Mungu katika kila enzi ina mipaka ya wazi; Anafanya tu kazi ya enzi ya sasa na Hatekelezi hatua ifuatayo ya kazi mapema. Kwa njia hii tu kazi Yake ya kuwakilisha ya kila enzi inaweza kuletwa mbele. Yesu alizungumzia tu ishara za siku za mwisho, kuhusu jinsi ya kuwa mtulivu na jinsi ya kuokolewa, jinsi ya kutubu na kukiri, na pia jinsi ya kubeba msalaba na kuvumilia mateso; Kamwe hakuzungumza kuhusu jinsi mwanadamu katika siku za mwisho anapaswa kuingia ndani, ama jinsi ya kutafuta kukidhi matakwa ya Mungu.
kutoka katika “Ni Jinsi Gani Mwanadamu Ambaye Amemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.
Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka, n.k? Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Maneno ambayo Mungu Alizungumza katika enzi hii ni tofauti na yale yaliyozungumzwa katika Enzi ya Sheria, na kwa hivyo, pia yako tofauti na maneno yaliyonenwa katika Enzi ya Neema. Katika Enzi ya Neema, Mungu hakufanya kazi ya neno, lakini Alieleza tu usulubisho ili kuwakomboa binadamu wote. Biblia inaelezea tu ni kwa nini Yesu alikuwa Asulubiwe, na mateso ambayo Alipitia kwenye msalaba, na jinsi mwanadamu anapaswa kusulubiwa kwa ajili ya Mungu. Katika enzi hiyo, kazi yote iliyofanywa na Mungu ilikuwa kuhusu usulubisho. Katika Enzi ya Ufalme, Mungu katika mwili Anazungumza maneno ili kushinda wale wote wanaomwamini. Huu ni, “Neno kuonekana katika mwili”; Mungu amekuja katika siku za mwisho ili kufanya kazi hii, ambayo ni kusema, Amekuja kutimiza umuhimu wenyewe wa Neno kuonekana katika mwili. Ananena tu maneno, na majilio ya ukweli ni chache. Hii ndiyo dutu kamili ya Neno kuonekana katika mwili, na wakati Mungu katika mwili Anaponena maneno Yake, huku ndiko kuonekana kwa Neno katika Mwili, na ni Neno kuja katika mwili. “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu, na Neno likawa mwili.” Hii (kazi ya kuonekana kwa Neno katika mwili) ni kazi ambayo Mungu atatimiza katika siku za mwisho, na ni sura ya mwisho ya mpango Wake mzima wa uongozi, kwa hivyo Mungu lazima Aje duniani na kudhihirisha maneno Yake katika mwili. Yale yanayofanywa leo, yale yatakayofanywa baadaye, yale yatakayotimizwa na Mungu, hatima ya mwisho mwanadamu, wale watakaookolewa, wale watakaoangamizwa, na mengine mengi—kazi hii ambayo lazima itimizwe mwishowe imesemwa wazi, na yote ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu halisi wa Neno kuonekana kwa mwili. Amri za utawala na katiba ambayo ilipeanwa hapo awali, wale ambao wataangamizwa, wale watakaoingia katika mapumziko—maneno haya lazima yatimizwe. Hii ni kazi iliyotimizwa kimsingi na Mungu katika mwili katika siku za mwisho. Anawafanya watu waelewe kule ambako wale waliopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa na wale wasiopangiwa na Mungu wanapaswa kuwa, jinsi ambavyo watu Wake na wana Wake watawekwa kwenye vikundi, ni nini kitaifanyikia Uyahudi, ni nini kitaufanyikia Misri—katika siku za usoni, kila mojawapo ya maneno haya yatatimizwa. Hatua za kazi za Mungu zinaharakishwa. Mungu hutumia neno kama mbinu ya kumfichulia mwanadamu kinachopaswa kufanyika katika kila enzi, kinachopaswa kufanywa na Mungu katika mwili wa siku za mwisho, na huduma Yake ambayo inapaswa kufanywa, na maneno haya ni kwa ajili ya kutimiza umuhimu hasa wa Neno kuonekana kwa mwili.
kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kile ambacho Nasema leo ni kuhukumu dhambi za watu na maovu yao; ni kulaani uasi wa watu. Udanganyifu na upotovu wao, na maneno na matendo yao, mambo yote ambayo hayako sambamba na mapenzi Yake yatapitia hukumu, na uasi wa watu unaamuliwa kuwa wenye dhambi. Ananena kulingana na kanuni za hukumu, naye anadhihirisha tabia Yake yenye haki kwa kuhukumu maovu yao, kulaani uasi wao, na kufichua nyuso zao zote mbaya.
kutoka katika “Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi inayofanywa na Mungu katika enzi hii ni hasa ya kutoa maneno kwa ajili ya uzima wa mwanadamu, kuweka wazi hulka ya asili ya mwanadamu na tabia ya mwanadamu iliyoharibika, uondoaji wa dhana za kidini, fikra za kinjozi, mitazamo iliyopitwa na wakati, vilevile maarifa na utamaduni wa mwanadamu. Hii ni lazima iwekwe wazi na kusafishwa kupitia maneno ya Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu Anatumia maneno na siyo ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Anatumia maneno Yake kumweka wazi mwanadamu, kumhukumu mwanadamu, kumwadibu mwanadamu, na kumkamilisha mwanadamu, ili katika maneno ya Mungu, mwanadamu aje kuona hekima na wema wa Mungu, na aje kuelewa tabia ya Mungu, ili kupitia maneno ya Mungu, mwanadamu aone matendo ya Mungu.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anaifunua, na kuishughulikia na kuipogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.
kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ingawa neno “neno” ni rahisi na la kawaida, neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa dunia nzima; neno Lake hubadilisha moyo wa binadamu, fikira na tabia zee za binadamu, na sura nzee ya ulimwengu mzima. Kupitia enzi nyingi, Mungu pekee wa leo ndiye anayefanya kazi katika njia kama hiyo, na ni Yeye tu Anayeongea na kumwokoa binadamu hivyo. Kuanzia wakati huu kuendelea, binadamu huishi katika mwongozo wa neno, wakichungwa na kuruzukiwa na neno. Binadamu wote wanaishi katika ulimwengu wa neno, wanaishi katika laana na baraka za neno la Mungu, na hata kuna binadamu zaidi wanaoishi chini ya hukumu na kuadibu kwa neno. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa minajili ya wokovu wa binadamu, kwa minajili ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa minajili ya kubadilisha sura asilia ya ulimwengu wa uumbaji wa kale. Mungu aliuumba ulimwengu kwa neno, huwaongoza wanadamu kote ulimwenguni kwa neno, na pia hushinda na kuwaokoa binadamu kwa neno. Hatimaye, Yeye atatumia neno ili kuutamatisha ulimwengu mzima wa kale. Ni hapo tu ndipo mpango wa usimamizi unapokuwa mkamilifu kabisa.
kutoka katika “Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huo, Yesu alifanya kazi kubwa ambayo haikueleweka kwa wanafunzi Wake, na kusema mengi kwamba watu hawakuelewa. Hii ni kwa sababu, wakati huo, Hakutoa maelezo. … Yesu hakuja kumkamilisha na kumpata mwanadamu, lakini kufanya awamu moja ya kazi: kuleta injili ya ufalme wa mbinguni na kukamilisha kazi ya kusulubiwa—na punde tu Yesu Aliposulubishwa, kazi Yake ilifika mwisho kamili. Lakini kwa awamu iliyoko sasa—kazi ya ushindi—maneno mengi zaidi lazima yasemwe, kazi nyingi zaidi lazima ifanywe, na lazima kuwe na hatua nyingi. Hivyo pia ni lazima siri za kazi ya Yesu na Yehova zitafichuliwa, ili wanadamu wote waweze kuwa na ufahamu na uwazi wa imani yao, kwa kuwa hii ni kazi ya siku za mwisho, na siku za mwisho ni mwisho wa kazi ya Mungu, wakati wa kuhitimisha kazi hii. Hii awamu ya kazi itakufafanulia sheria ya Yehova na ukombozi wa Yesu, na ni hasa ili uweze kuelewa kazi nzima ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita, na kuelewa kusudi la kazi zote Alizozifanya Yesu na maneno Aliyoyasema, na hata upofu wako wa imani kwenye na katika ibada ya Biblia. Yote haya yatakuwezesha kujua. Wewe utakuja kufahamu kazi anayoifanya Yesu na kazi ya Mungu leo; utaelewa na kushuhudia ukweli wote, uzima, na njia. Katika awamu ya kazi Aliyoifanya Yesu, kwa nini Yesu Aliondoka bila kumaliza kazi ya Mungu? Kwa sababu awamu ya kazi ya Yesu haikuwa kazi ya kumalizia. Wakati Yeye Alisulubishwa msalabani, maneno Yake pia yalifika mwisho; baada ya kusulubiwa kwake, kazi Yake kwa hivyo ilimalizika. Awamu ya sasa ni tofauti. Ni baada tu ya maneno hayo kusemwa hadi mwisho na kazi nzima ya Mungu iwe imehitimika ndipo kazi yake itakapokuwa imemalizika. Wakati wa awamu ya kazi ya Yesu, kulikuwa na maneno mengi yaliyobakia bila kusemwa, au ambayo hayakuwa yameelezwa kikamilifu kwa ufasaha. Waama, Yesu hakujali Alichosema au kile ambacho hakusema, kwa kuwa huduma yake haikuwa huduma ya maneno; na hivyo baada ya Yeye kusulubishwa msalabani Aliondoka. Awamu hiyo ilikuwa hasa kwa ajili ya kusulubiwa, na ni tofauti na awamu ya sasa. Awamu ya kazi hii ni hasa kwa ajili ya kukamilisha, kufumbua, na kuleta kazi yote kwenye hitimisho. Kama maneno hayasemwi hadi tamati yake kabisa, hakutakuwa na mbinu ya kuhitimisha kazi hii, kwa kuwa awamu hii ya kazi yote inafikishwa mwisho na kukamilika kwa kutumia maneno. Wakati huo, Yesu Alifanya kazi kubwa isiyoeleweka na mwanadamu. Akaondoka kimyakimya, na leo bado kunao wengi wasioelewa maneno Yake, ambao ufahamu wao ni potofu lakini bado unaaminika nao kwamba ni sahihi, ambao hawajui kuwa wao si sahihi. Mwishoni, awamu hii ya sasa itafikisha kazi ya Mungu mwisho ulio kamilifu, na kutoa hitimisho Lake. Wote watakuja kufahamu na kujua mpango wa usimamizi wa Mungu. Dhana zilizo ndani ya mwanadamu, nia yake, fahamu yake potofu, dhana zake kuhusu kazi ya Yehova na Yesu, maoni yake kuhusu watu wa Mataifa mengine na michepuko yake ingine na makosa yake yatarekebishwa. Na mwanadamu ataelewa njia yote ya haki ya uzima, na kazi yote anayofanya Mungu, na ukweli wote. Wakati hayo yatafanyika, awamu hii ya kazi itafikia kikomo.
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli"

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika.

Jumanne, 17 Julai 2018

hukumu la Neno la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, hukumu,

hukumu la Neno la Mwenyezi Mungu | Nilifurahia karamu kubwa

Xinwei    Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo. Na baada ya karibu mwezi mmoja, mipango ilikuwa inakaribia kukamilika. Mwezi huo ulikuwa wa joto, na wakati tulikuwa tumeteseka kimwili mioyo yetu ilikuwa imeridhika yenye furaha, kazi yetu ikiwa imeendelea vizuri mbele ya joka kubwa jekundu.