Wu Wen Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Nilikuwa mtu dhaifu na mwenye tabia nyepesi kuhisi. Wakati sikumwamini Mungu, mara kwa mara ningejihisi mwenye huzuni na masikitiko kutokana na mambo yaliyokuja katika maisha. Kulikuwa na nyakati nyingi kama hizi, na siku zote nilihisi kwamba maisha yangu yalikuwa magumu; hapakuwa na furaha, hamkuwa na ridhisho moyoni mwangu ya kuzungumzia. Uchungu huu ulikuwa tu kama pingu zilizonifunga kabisa kila mara, zikinifanya niwe mwenye huzuni. Ilikuwa tu baada kumwamini Mwenyezi Mungu ndipo nilipata kiini cha matatizo ndani ya maneno ya Mungu na nikapata uhuru polepole.
Nilisoma haya katika maneno ya Mwenyezi Mungu: “Kwa kuwa watu wanajipenda kupita kiasi, maisha yao yote ni ya uchungu na matupu” (“Sura ya 46” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, ilionekana nilijua sababu ya huzuni yangu–nilikuwa mwenye majivuno zaidi. Mara kwa mara ningehisi masikitiko na maumivu kutoka kwa maneno machache yasiyopendeza au kutoka kwa tazamo la kitongotongo kutoka kwa mtu mwingine. Niliposhughulikiwa na kupogolewa nilihisi kuumizwa na mwenye huzuni, kwa sababu heshima yangu iliumizwa na nilihisi nilikuwa nimepoteza hadhi. Nilikuwa na wasiwasi juu ya njia yangu ya baadaye katika maisha. ... Je, haya yote si ni kwa sababu nilijali sana juu ya sifa yangu mwenyewe, hadhi, majivuno, tamaa, na kudura ya baadaye? Kuhusu ufunuo huu, siku za nyuma, nilifikiri tu kwamba hili lilikuwa ni kwa sababu kulikuwa na mambo mengi katika moyo wangu na akili, kwamba mawazo yangu yalikuwa mazito, kwamba kujiepusha na aibu kulikuwa muhimu kwangu, na kwamba nilikuwa mtu asiye makini, lakini sikuwa nimetatua tatizo la njia ya kuingilia . Inawezekana kuwa ni kwa sababu nilikuwa na majivuno zaidi, niliishi katikati ya mateso ya Shetani, katika utumwa naye? Nilitafuta kimyakimya ndani ya moyo wangu. Baadaye, nilipokuwa nikisomasoma maneno ya Mungu katika “Wale Ambao Hutupia Ushawishi wa Giza Wanaweza Kuchumwa na Mungu,” Niliona maneno haya kutoka kwa Mungu: “Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani, ambao hawawezi kutoa moyo wao kwa Mungu, hawa ndio watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaishi chini ya anga ya kifo.” Nikafikiri: Je, si hii ndiyo hali yangu kabisa? Nikawa na uhakika hata zaidi. Kisha, Nikaona zaidi ya maneno ya Mungu: “Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kutafuta ukweli, basi ni hapo tu utakuwa na hali ya sahihi. Kuishi katika hali ya haki ni muhimu kwa ajili ya kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali ya haki ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli, basi uwezekano wa kuepuka ushawishi wa giza haupo. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, mtu hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali ya haki ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika ukweli wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua, wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi ya Mungu, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu” (“Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nikisoma hili, nilihisi moyo wangu ukichangamka. Wakati watu wanapojipenda, hawawezi labda kuwa na uhusiano sahihi na Mungu, na moyo wao wa kutafutilia ukweli hauwezi kuwa mkubwa hivyo. Mwishoni, kwa sababu ya majivuno yao, watajiangamiza kwa kuishi wakimilikiwa na Shetani. Asante kwa kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu ambako kuliniwezesha kuona hali yangu ya hatari na kwamba kuna njia ya kutupia ushawishi wa giza—kuwa na moyo wa kutafuta ukweli, kumtegemea na kumtazamia Mungu kwa kweli ninapokabiliwa na mambo, kusoma maneno ya Mungu zaidi, kutafuta kanuni za utendaji katika maneno ya Mungu, na kuwa mwaminifu kwa Mungu daima. Wakati wa kupata kazi ya Roho Mtakatifu, upotovu ulio ndani ya binadamu unaweza kupitia mabadaliko pamoja na kuingia kwao ndani ya ukweli. Hii ndiyo njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini nilikuwa nimepuuza kipengele hiki, kwa baridi tu nikijaribu kushughulikia upotovu wangu peke yangu, si kutegemea kwa kupanga kazi ya Roho Mtakatifu ili kujibadilisha. Si ajabu kwamba nilifaulu tu kujihini kwa muda; sikuwa nimetatua hali hii kutoka kwa mizizi yake. Kama tu inavyosema katika maneno ya Mungu: “Kadiri watu wanavyozidi kuwa mbele ya Mungu, ndivyo inavyokuwa rahisi zaidi kwao kukamilishwa na Mungu. Hii ndiyo njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi Yake. Usipoelewa hili, haitawezekana wewe kuingia kwenye njia sahihi, na kukamilishwa na Mungu hakutawezekana. … utakuwa tu na bidii yako na bila kazi yoyote ya Mungu. Je, si hili ni kosa katika uzoefu wako?” (“Kuhusu Uzoefu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kuelewa hili, ninajiweka kwenye njia hii kwa utambuzi hata sana, kujinyima mwenyewe, nikipuuza hisia na mawazo yangu; badala yake, ninaweka moyo wangu mintarafu ya kutafuta ukweli, kwa kutekeleza wajibu wangu kwa dhati, kufanya mazoezi ya kufikiria zaidi juu ya maneno ya Mungu, kutegemea maneno ya Mungu katika matendo yangu, kujiruhusu kuishi katika hali nzuri. Ingawa kuna nyakati katika matendo yangu mahususi ambapo sijatenda kwa usahihi kikamilifu, nimehisi ufunguliwaji na uhuru wa kuishi katika nuru na nimefurahia kazi ya Roho Mtakatifu. Sio tu kuwa nimeweza kuona upotovu wangu na upungufu wangu, lakini nimekuwa na nia ya kutamani kubadilisha hivi karibuni na motisha ya kutenda ukweli. Msimamo wangu umebadilika pia; Mimi tena si mwenye huzuni, sikitiko, mwenye kuchusha, lakini kuna uchangamfu na nguvu katika moyo wangu. Nimekuwa pia na furaha zaidi, na ninafurahia sana kuishi katika kanisa!
Bila shaka, kipengele hiki cha upotovu ndani yangu ni cha kina zaidi na haiwezekani kabisa kutupia ushawishi wa Shetani kutoka kwa kuweka mambo haya katika vitendo mara kadhaa. Hata hivyo, Mungu ameniruhusu kuonja utamu wa “kutupia ushawishi wa giza, nikiishi katika nuru,” ambacho kimenipa motisha na matumaini katika ufuatiliaji wangu. Ninaamini kwamba almradi ninaendelea kustahimili katika kushirikiana na Mungu na kutembea njia ambayo Mungu ameonyesha, kutafuta ukweli katika vitu vyote, na kuishi kwa maneno ya Mungu, kutupia minyororo ya roho, nitatupia ushawishi wa giza, na kuchumwa na Mungu.
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
0 意見:
Chapisha Maoni