Watu wengine wanaweza kuwa na utambuzi kidogo katika maneno ya Mungu, lakini hakuna yeyote kati yao ambaye huamini hisia zake; wao huogopa sana kuingia katika ukanaji. Hivyo, wao kila mara wamegeuka kati ya furaha na huzuni. Ni haki kusema kwamba maisha ya watu wote yamejaa huzuni; kusongeza hili katika hatua nyingine zaidi, kuna usafishaji katika maisha ya kila siku ya watu wote, lakini Naweza kusema kwamba hakuna anayepata ufunguliwaji wowote katika roho yake kila siku, na ni kana kwamba milima mitatu mikuu inakilemea kichwa chake.
Hakuna maisha yao yoyote yaliyo na furaha na shangwe kila wakati—na hata wakati ambapo wana furaha kidogo, wao wanajaribu tukujifanya kuwa wana furaha. Ndani ya mioyo yao, watu kila mara huwa na hisi ya kitu fulani kisichokwisha. Hivyo, hawako thabiti ndani ya mioyo yao; maishani, mambo huonekana kuwa matupu na yasiyo haki, na inapohusu kumwamini Mungu, wao wana shughuli nyingi na wanapungukiwa na wakati, ama sivyo hawana wakati wa kula na kunywa maneno ya Mungu, au hawawezi kula na kunywa maneno ya Mungu. Hakuna hata mmoja kati yao aliye na amani, na mwenye akili timamu, na thabiti ndani ya moyo wake. Ni kana kwamba daima wameishi chini ya anga lililotanda mawingu, kana kwamba wao huishi katika anga isiyo na hewa safi, na hili limesababisha kuchanganyikiwa katika maisha yao. Mungu daima hunena kuelekea udhaifu wa watu moja kwa moja, Yeye daima huwagonga katika udhaifu wao—hamjaona kwa dhahiri toni ambayo kwayo Amenena kote? Mungu kamwe hajawahi kuwapa watu nafasi ya kutubu, na Yeye huwafanya watu waishi katika "mwezi" bila hewa safi. Tangu mwanzo mpaka leo, umbo la nje la maneno ya Mungu limefichua asili ya mwanadamu, lakini hakuna ambaye ameona kwa dhahiri kiini cha maneno haya. Inaonekana kwamba kwa kufichua asili ya mwanadamu, watu huja kujijua na hivyo huja kumjua Mungu, lakini hii si njia katika kiini. Toni na kina kikuu zaidi cha maneno ya Mungu huonyesha tofauti wazi kati ya Mungu na mwanadamu. Katika hisia zao, jambo hili huwafanya watu kuamini bila kufahamu kwamba Mungu ni asiyefikika na asiyeingilika; Mungu huleta kila kitu hadharani, na inaonekana kwamba hakuna anayeweza kurudisha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu kwa namna ulivyokuwa. Si vigumu kuona kwamba lengo la matamshi yote ya Mungu ni kutumia maneno kuwapindua watu wote, na hivyo kutimiza kazi Yake. Hii ni hatua ya kazi ya Mungu. Lakini hiki sicho kile ambacho watu huamini katika mawazo yao. Wao huamini kwamba kazi ya Mungu inakaribia kilele chake, kwamba inakaribia athari yake ya kutambulika sana ili kushinda joka kuu jekundu, ambalo ni kusema, kuyafanya makanisa yasitawi, na hakuna anayekuwa na dhana kuhusu Mungu mwenye mwili, ama sivyo watu wote kumjua Mungu. Lakini hebu tusome kile ambacho Mungu anasema: Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na hawezi kushughulishwa kwa urahisi, ihali mwanadamu ni mwanadamu, na hapaswi kuwa mpotovu kwa urahisi ... na kutokana na hili, wao kila mara huwa wanyenyekevu na wavumilivu mbele Yangu; hawana uwezo wa kutangamana na Mimi, kwani wana dhana nyingi sana.” Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba, haijalishi kile asemacho Mungu au kile afanyacho mwanadamu, watu hawawezi kabisa kumjua Mungu; kwa sababu ya nafasi inayochukuliwa na kiini chao, lolote litokealo, wao, mwishowe, hawawezi kumjua Mungu. Hivyo, kazi ya Mungu itaisha wakati ambapo watu watajiona kama wana wa jehanamu. Hakuna haja ya Mungu kuachia huru ghadhabu Yake kwa watu, au kuwashutumu moja kwa moja, au hatimaye kuwahukumu kifo ili kuhitimisha usimamizi Wake wote. Yeye hupiga soga tu kwa mwendo Wake mwenyewe, kana kwamba ukamilishaji wa kazi Yake ni wa ziada, kitu fulani kinachotimizwa kwa wakati Wake wa ziada bila juhudi hata kidogo. Kutoka nje, inaonekana kuna haraka fulani kwa kazi ya Mungu—lakini Mungu hajafanya chochote, Yeye hafanyi chochote ila kunena. Kazi miongoni mwa makanisa siyo ya kiwango kikubwa kama ya nyakati zilizopita: Mungu hawaongezi watu, au kuwafukuza, au kuwafichua—kazi kama hiyo ni ya upuuzi sana. Inaonekana kama kwamba Mungu hafikirii kufanya kazi kama hiyo. Yeye husema tu kidogo ya kile Anachopaswa kusema, baadaye Yeye hugeuka na kutoweka bila kuonekana—ambalo, kwa kawaida, ni onyesho la kukamilika kwa matamshi Yake. Na kipindi hiki kitakapofika, watu wote wataamka kutoka katika usingizi wao. Wanadamu wamelala kwa maelfu ya miaka, wamekuwa katika usingizi kabisa. Na kwa miaka mingi, watu wamekuwa wakikimbia huku na kule katika ndoto zao, na hata wao hulia katika ndoto zao, wasiweze kuzungumza kuhusu udhalimu ulio ndani ya mioyo yao. Hivyo, wao "huhisi huzuni kidogo ndani ya mioyo yao"—lakini watakapoamka, watagundua ukweli wa kweli, na kutamka ghafula kwa mshangao: "Kwa hiyo hiki ndicho kinachoendelea!" Hivyo inasemekana kwamba, “Leo, watu wengi sana bado wamelala fofofo. Ni wakati tu ambapo wimbo wa ufalme husikika ndipo wao hufumbua macho yao yenye usingizi na kuhisi huzuni kidogo ndani ya mioyo yao."
Hakuna roho ya yeyote ambayo imewahi kufanywa huru, kamwe roho ya mtu yeyote haijawahi kuwa changamfu na yenye furaha. Wakati ambapo kazi ya Mungu itamalizika kabisa, roho za watu zitafanywa huru, kwani kila mmoja atakuwa ameainishwa kufuatana na aina, na hivyo wote watakuwa thabiti katika mioyo yao. Ni kana kwamba watu wako katika safari ya baharini iliyoenea sana na mioyo yao huwa thabiti wanaporudi nyumbani. Wafikapo nyumbani, watu hawatahisi tena kwamba dunia ni tupu na isiyo haki, lakini wataishi kwa amani katika nyumba zao. Hiyo ndiyo itakuwa hali miongoni mwa wanadamu wote. Hivyo, Mungu anasema kuwa watu “hawajawahi kamwe kuweza kujinasua kutoka kwa utumwa wa Shetani.” Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika hali hii huku akiwa katika mwili. Kwa sasa, hebu tuweke kando kile Mungu anasema kuhusu hali halisi mbalimbali za mtu, na tuzungumze tu juu ya siri ambazo Mungu bado hajamfunulia mwanadamu. “...mara nyingi mno watu wamenitazama Mimi na macho ya kudhihaki, kana kwamba mwili Wangu umefunikwa kwa miiba na ni wa kuchukiza sana kwao, na hivyo watu hunichukia Mimi sana, na huamini kwamba Sina thamani.” Kwa namna nyingine, kwa kiini, tabia halisi ya mwanadamu hufichuliwa katika maneno ya Mungu: Amefunikwa na manyoya, hakuna kinachopendeza kumhusu yeye, na hivyo chuki ya Mungu kwa mwanadamu huongezeka, maana mwanadamu ni nungunungu aliyejawa miiba tu asiye na chochote cha kufurahia. Kwa juujuu, maneno haya yanaonekana kufafanua dhana za mtu kwa Mungu[a]—lakini kwa kweli, Mungu anachora picha ya mwanadamu kulingana na “mfano” wake. Maneno haya ni jinsi Mungu anavyoeleza kinananaga kuhusu mwanadamu, na ni kama kwamba Mungu amenyunyizia dawa ya kutengeneza filamu juu ya mfano wa mwanadamu; hivyo, mfano wa mwanadamu unajulikana sana kote ulimwenguni, na hata huwashangaza watu. Tangu wakati ambapo Alianza kunena, Mungu amekuwa akipanga majeshi Yake kwa vita vikubwa na mwanadamu. Yeye ni kama profesa wa aljebra wa chuo kikuu anayeweka wazi ukweli kwa mwanadamu, na kile kinachothibitishwa na ukweli Anaoorodhesha—ushahidi na ushahidi wa kukabili—huwafanya watu wote washawishike kabisa. Hili ndilo kusudi la maneno yote ya Mungu, na ni kwa sababu ya hili ndio Mungu kwa kawaida huyatupa maneno haya ya siri kwa mwanadamu. “Mimi, kwa kifupi, Sina thamani kabisa moyoni mwa mwanadamu, Mimi ni kitu cha nyumba kisicho cha muhimu.” Baada ya kusoma maneno haya, watu hawana budi ila kutamka ombi ndani ya mioyo yao, na wao huja kujua hali yao ya kuwa wadeni kwa Mungu, ambalo huwafanya wajishutumu, huwafanya kuamini kuwa mtu anapaswa kufa, na hana thamani hata kidogo. Mungu anasema, “ni kwa sababu ya jambo hili ndio Najikuta katika hali Niliyo ndani leo,” ambayo, inapounganishwa na hali halisi ya leo, huwafanya watu kujishutumu. Je, huu si ukweli? Iwapo ungefanywa kujijua, je, maneno kama “Napaswa kweli kufa!” yangetoka kinywani mwako? Hizo ndizo hali za kweli za mwanadamu, na hili halifai kufikiriwa sana— ni mfano tu unaofaa.
Kwa maana moja, Mungu anapoomba msamaha na uvumilivu kwa mwanadamu, watu huona kuwa Mungu anawafanyia mzaha, na kwa maana nyingine, wao pia huona uasi wao wenyewe—wanangojea tu Mungu ajitahidi Mwenyewe iwezekanavyo kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, tukizungumzia dhana za watu, Mungu anasema Yeye si hodari katika falsafa ya maisha au lugha ya mwanadamu. Hivyo, kwa namna moja hili huwafanya watu kufananisha maneno haya kwa Mungu wa vitendo, na kwa namna nyingine, wao huona nia ya Mungu katika maneno Yake—Mungu anawadhihaki, kwa maana wanaelewa kuwa Mungu anafichua sura ya kweli ya mwanadamu, na Hawaambii watu kwa kweli kuhusu hali za kweli za Mungu. Maana ya asili ya maneno ya Mungu imejawa na dhihaka, mzaha, kicheko, na chuki kwa mwanadamu. Ni kana kwamba, katika kila analolifanya, mwanadamu anaipotosha sheria na kuchukua rushwa; watu ni makahaba, na Mungu anapofungua kinywa Chake kunena, wao hutetemeka kwa hofu, wakihofu kabisa kuwa ukweli kuwahusu utafichuliwa kwelikweli, ukiwaacha na aibu kuu wasiweze kumtazama yeyote. Lakini ukweli ni ukweli. Mungu haachi matamshi Yake kwa ajili ya “toba” ya mwanadamu; kadri watu wanavyoona haya na aibu isiyoweza kuelezeka kwa maneno, ndivyo Mungu huimarisha kukazia macho Kwake kwa kuchoma juu ya nyuso zao. Maneno kutoka kwa kinywa Chake huyaweka wazi matendo yote mabaya ya mwanadamu —huku tu ndiko kuwa na haki na bila upendeleo, hii tu ndiyo inaitwa Qingtian,[b] hii tu ndiyo hukumu kutoka kwa mahakama kuu zaidi ya watu. Hivyo, wakati ambapo watu wanasoma maneno ya Mungu, wao wanakumbwa ghafla na mshtuko wa moyo, shinikizo lao la damu hupanda, ni kana kwamba wanaugua ugonjwa wa moyo, ni kana kwamba utokaji wa damu ya ubongo unataka kuwarudisha katika paradiso ya magharibi kukutana na mababu zao—huu ndio mjibizo wao wanaposoma maneno ya Mungu. Mwandamu anafanywa dhaifu kwa miaka mingi ya kazi ngumu, yeye ni mgonjwa ndani na nje, kila sehemu yake inaugua, kutoka moyoni mwake hadi kwa mishipa yake ya damu, utumbo mpana, uchango, tumbo, mapafu, figo, na kadhalika. Hakuna chochote katika mwili wake wote kilicho na afya. Hivyo, kazi ya Mungu haifiki kiwango ambacho mwanadamu hawezi kukifikia, lakini huwasababisha watu kujijua. Kwa sababu mwili wa mwanadamu umezungukwa na kushambuliwa na virusi, na kwa sababu amekuwa mzee, siku ya kifo chake hukaribia, na hakuna namna ya kurudi nyuma. Lakini hii ni sehemu tu ya hadithi; maana ya ndani bado haijafichuliwa, kwa kuwa asili ya ugonjwa wa mwanadamu inatafutwa. Kwa kweli, wakati ambao ukamilifu wa kazi ya Mungu unakamilishwa sio wakati ambao kazi Yake duniani inakamilika, kwa maana mara tu hatua hii ya kazi inapokamilika, hakutakuwa na njia ya kutekeleza ile kazi ya wakati ujao katika mwili, na Roho wa Mungu atahitajika kuikamilisha. Hivyo, Mungu anasema, “Wakati ambapo Mimi ninafungua rasmi kitabu ndipo watu kote ulimwenguni wanaadibiwa, wakati ambapo kazi Yangu hufika kilele chake, wakati ambapo watu kote duniani wanapitia majaribio.” Wakati ambapo kazi katika mwili inaisha sio wakati ambapo kazi ya Mungu hufikia kilele chake—kilele cha wakati huu kinahusu tu kazi wakati wa hatua hii, na sio kilele cha mpango wote wa usimamizi. Hivyo, mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu si ya juu. Yeye anauliza tu watu wajijue, hivyo kutumikia hatua ifuatayo ya kazi, ambayo kwayo mapenzi ya Mungu yatakuwa yametimizwa. Kadri kazi ya Mungu[c] inavyobadilika, ndivyo “kitengo cha kazi” cha watu[d] kinavyobadilika. Leo ni hatua ya kazi ya Mungu duniani, na hivyo lazima wafanye kazi kule mashinani. Katika wakati ujao, itakuwa lazima kusimamia taifa, na hivyo watatumwa katika Kamati ya Kati. Wakienda kutembea ng’ambo, itawabidi washughulikie taratibu za kwenda nchi za kigeni. Katika nyakati hizo watakuwa katika nchi za kigeni, mbali kutoka kwa nchi yao— lakini hii hata hivyo itakuwa kwa ajili ya mahitaji ya kazi ya Mungu. Kama watu walivyosema, “Tutayatoa maisha yetu kwa Mungu ikibidi”—je, hii siyo njia ambayo itatembelewa katika siku za usoni? Ni nani amewahi kufurahia maisha kama hayo? Mtu anaweza kusafiri kote, atembelee nchi za kigeni, apeane mwongozo kule mashambani, ajifanye mwenyeji miongoni mwa watu wa kawaida, na anaweza pia kuzungumza juu ya maswala muhimu ya taifa na wanachama wa mashirika ya ngazi za juu; na ikibidi, anaweza binafsi kuonja maisha katika jahanamu, kisha baadaye anaweza kurudi na bado aweze kufurahia baraka za mbinguni—je, hizi si baraka za mwanadamu? Ni nani amewahi kufananishwa na Mungu? Ni nani amewahi kusafiri katika mataifa yote? Kwa kweli, watu wangeweza kuelewa kidogo juu ya baadhi ya maneno ya Mungu bila ishara wala maelezo—ni kwamba tu hawajiamini, ndiyo ambayo imeipanua kazi ya Mungu mpaka leo. Kwa sababu watu hukosa mengi sana—kama Mungu alivyosema, “hawana chochote”—kazi ya leo husababisha matatizo makubwa mno kwao; na zaidi, udhaifu wao, kwa kawaida, umekizuia kinywa cha Mungu—na je, vitu hivi sivyo hasa vinavyoizuia kazi ya Mungu? Je, bado huwezi kuona hili? Kuna maana fiche katika yote asemayo Mungu. Mungu anaponena, Yeye hufahamu vizuri suala lililoko mbele yake na kulitumia ipasavyo, na kama hekaya, maneno yote Anenayo huwa na ujumbe wa kina. Maneno haya rahisi yana ujumbe wa kina, na hivyo huelezea maswala muhimu—je, hili silo ambalo maneno ya Mungu ni bora kwalo? Je, unajua hili?
Tanbihi:
a. Makala ya asili yanasoma “hii huonekana kuwa dhana za mwanadamu kumwelekea Mungu”
b. Qingtian: Neno hili limetumika kutaja hakimu mwenye haki wakati wa kifalme.
c. Makala ya asili yanaacha “ya Mungu”
d. Makala ya asili yanaacha “ya watu”
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
0 意見:
Chapisha Maoni