Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 44 na 45
Tangu Mungu alipomwambia mwanadamu kuhusu "upendo wa Mungu”—somo la maana zaidi kati ya yote—Alilenga kuzungumza juu ya mada hii katika "matamko ya Roho mara saba," kusababisha watu wote kujaribu kujua utupu wa maisha ya mwanadamu, na hivyo kuchimbua upendo wa kweli ulio ndani yao.
Na wale wanaoishi katika hatua ya sasa wanampenda Mungu kiasi gani? Je, mwajua? Hakuna mipaka kwa somo la "kumpenda Mungu." Na je, kuhusu ufahamu wa maisha ya mwanadamu ndani ya watu wote? Mtazamo wao kwa kumpenda Mungu ni upi? Wako radhi au hawako radhi? Je, wao hufuata halaiki kubwa, au huchukia sana mwili? Haya yote ni mambo mnayopaswa kuelewa kuyahusu na kuyafahamu, Je, kwa kweli hakuna chochote ndani ya watu? "Nataka mwanadamu anipende kweli, lakini leo, watu bado wanasitasita, wasiweze kunipa upendo wao wa kweli. Katika mawazo yao, wao huamini kwamba iwapo watanipa upendo wao wa kweli, wataachwa bila chochote." Katika maneno haya, "upendo wa kweli" hasa una maana gani? Kwa nini Mungu bado anataka upendo wa kweli wa watu katika enzi hii wakati "watu wote wanampenda Mungu"? Hivyo, kusudi la Mungu ni kumtaka mwanadamu aandike maana ya upendo wa kweli juu ya karatasi ya majibu, na kwa hiyo, haya hasa ni matayarisho ambayo Mungu amempangia mwanadamu. Kuhusu hatua hii ya leo, hata ingawa Mungu hafanyi madai makuu kwa mwanadamu, watu bado hawajafikia matakwa ya Mungu ya asili kwa mwanadamu; kwa maneno mengine, bado hawajaweka nguvu zao zote katika kumpenda Mungu. Hivyo, katikati ya kutokuwa radhi kwao, Mungu bado anatoa matakwa Yake kwa watu, mpaka wakati kazi hii imekuwa na matokeo, na Yeye kutukuzwa katika kazi hii. Kweli, kazi iliyo duniani inahitimishwa kwa upendo wa Mungu. Hivyo, wakati ambapo Mungu anahitimisha kazi Yake tu ndipo Anaashiria kazi muhimu zaidi ya wanadamu wote. Kama, wakati ambapo kazi Yake itaisha, atampa mwanadamu kifo, nini kitamfanyikia mwanadamu, nini kitamfanyikia Mungu, na nini kitamfanyikia Shetani? Ni wakati ambapo upendo wa Mungu duniani unashawishiwa ndio inaweza kusemekana kwamba "Mungu amemshinda mwanadamu." La sivyo, watu wangesema kwamba Mungu humdhulumu mwanadamu, na Mungu angeaibishwa hivyo. Mungu hangekuwa mjinga hivyo kuihitimisha kazi Yake bila mnong'ono. Hivyo, wakati ambapo kazi inakaribia kuisha, shauku ya upendo wa Mungu hutokea, na upendo wa Mungu hugeuka kuwa mada motomoto. Bila shaka, huu upendo wa Mungu haujatiwa mawaa na mwanadamu, ni upendo usio ghushiwa, kama upendo wa mke mwaminifu kwa mme wake, au upendo wa Petro. Mungu hataki upendo wa Ayubu na Paulo, bali upendo wa Yesu kwa Yehova, upendo kati ya Baba na Mwana. "Kufikiria tu kuhusu Baba, bila uzingatiaji wa hasara na faida za mtu binafsi, kumpenda tu Baba, na sio mwingine, na kutotaka kingine chochote"—je, mwanadamu anaweza hili?
Tukilinganisha kile ambacho Yesu alifanya, Yule ambaye Hakuwa na ubinadamu kamili, tunaonaje? Mmefika umbali gani katika ubinadamu wenu kamili? Je, mnaweza kufikia sehemu moja kwa kumi ya kile Yesu alifanya? Mna sifa zinazostahili kwenda msalabani kwa ajili ya Mungu? Je, upendo wenu kwa Mungu unaweza kumwaibisha Shetani? Na mmetoa kiasi gani cha upendo wenu wa mwanadamu? Je, umebadilishwa na upendo wa Mungu? Ninyi hustahamili yote kwa kweli kwa ajili ya upendo wa Mungu? Hebu fikirini kuhusu Petro wa nyakati zilizopita, na mjitazame, ninyi ambao ni wa leo—kuna tofauti kubwa kwa kweli, hamstahili kusimama mbele ya Mungu. Ndani yenu, je, kuna upendo zaidi kwa Mungu, au upendo zaidi kwa ibilisi? Huu unapaswa kuwekwa kwa zamu upande wa kushoto na kulia wa mizani ya kupimia, kuona ni upi uko juu zaidi—je, kiasi gani cha upendo kwa Mungu kiko ndani yenu kwa kweli? Je, ninyi ni wa kufaa kufa mbele ya Mungu? Sababu ya Yesu kuweza kubaki msalabani ilikuwa kwa sababu uzoefu wake duniani ulitosha kumwaibisha Shetani, na ni kwa sababu hiyo tu ndiyo Mungu Baba alimruhusu kwa ujasiri kukamilisha hatua hiyo ya kazi; ilikuwa kwa ajili ya taabu Alizokuwa Amepitia na upendo Wake kwa Mungu. Lakini hamna sifa za kustahili jinsi hiyo. Hivyo, lazima mwendelee kupitia, kutimiza kuwa na Mungu, na si kingine chochote, ndani ya mioyo yenu—je, mnaweza kufanikisha hili? Kutokana na hili inaweza kuonekana unamchukia Mungu kiasi gani, na unampenda Mungu kiasi gani. Si kwamba Mungu anataka mengi sana kwa mwanadamu, lakini kwamba mwanadamu hafanyi kazi kwa bidii. Je, hiki ndicho kinaendelea kwa kweli? La sivyo, ungegundua ndani ya Mungu kiasi gani kilicho cha kupendeza, na ungepata ndani yako kiasi gani kilicho cha kuchukiza sana? Unapaswa kufikiria kwa makini kuhusu mambo haya. Ni haki kusema kwamba ni wachache tu chini ya mbingu wanampenda Mungu—lakini unaweza kuwa mtangulizi, kuvunja rekodi ya dunia, na kumpenda Mungu? Mungu hataki chochote kutoka kwa mwanadamu. Mbona mwanadamu asimheshimu kwa hili? Je, huwezi kutimiza hata hili? Kuna nini lingine la kusema?
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
0 意見:
Chapisha Maoni