Sura ya 35
Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kwa bako.” Hii ni kweli kabisa, lakini watu bado hawawezi kulielewa kabisa wazo hili. Kutokana na hili, sehemu ya kazi ambayo wamefanya imekuwa si lazima.
Mungu alisema, “Mimi husaidia na kuwaruzuku kwa mujibu wa kimo chao. Kwa kuwa wanadamu ndio wahusika wakuu wa mpango Wangu wote wa usimamizi, Natoa ushauri zaidi kwa walio katika hii nafasi ya ‘binadamu’ ili waweze kuiigiza kwa moyo wote na kwa uwezo wao wote,” pamoja na, “Hata hivyo, Nakataa kukosoa dhamiri zao moja kwa moja; badala yake, Naendelea kuwaelekeza kwa uvumilivu na utaratibu. Hata hivyo, wanadumu ni dhaifu, na wasioweza kutekeleza kazi yoyote.” Kufikiri kwa Mungu ni huku: Hata Akiishia kuwaangamiza binadamu hawa wote, kazi Yake duniani bado itaendelea kwa mujibu wa mpango Wake wa asili. Mungu hafanyi kazi bure; kila kitu ambacho Yeye hufanya ni kizuri. Kama Petro alivyosema, “Hata Mungu angekuwa Anacheza na binadamu kana kwamba wao ni vitu vya kuchezea watoto, wanadamu wangewezaje kulalamika? Wangekuwa na haki gani?” Je, hiki si kile ambacho Mungu ametamani kutimiza na binadamu leo[a]? Wanadamu wanaweza kuwa na mtazamo huu kwa kweli? Kwa nini Petro wa miaka elfu kadhaa iliyopita aliweza kusema jambo kama hilo, ilhali “Petro” katika enzi ya leo yenye teknolojia ya hali ya juu, iliyofanywa kuwa ya kisasa hawawezi? Siwezi kusema kwa hakika kama historia inaendelea mbele au inarudi nyuma. Kama sayansi imechukua hatua kwenda mbele au kurudi nyuma, hadi sasa, bado ni swali ambalo hakuna anayeweza kulijibu. Kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa binadamu kimekuwa kuwafanya wazuri na kuwakubalia kukua maishani. Je, watu hawawezi kulifahamu hili? Kila kitu kinachokufanya uwe mbaya ni kiwango chako dhaifu; ni kiwango kikuu cha kuweza kudhuriwa, kilicho wazi kwa mashambulio ya Shetani. Je, unaelewa hili? Kwa nini Mungu alinena hivi? “Nawasihi kwa juhudi na uaminifu wote. Hawawezi kwa kweli kufanya Nilichowauliza?” Maneno haya yana maana gani? Kwa nini Mungu aliuliza swali hili? Linaonyesha kwamba kuna hali nyingi sana mbaya za binadamu, na aina moja tu ya hali mbaya inatosha kusababisha binadamu kujikwaa. Unaweza vilevile kutazama na uone kile ambacho kuendelea katika njia zako mbaya kitakuletea wewe. Yote ambayo Mungu hufanya huelekea kwa ukamilishaji wa binadamu. Je, hili linahitaji ufafanuzi wowote zaidi? Sidhani! Hoja inaweza kujengwa kwamba binadamu wamemilikiwa na Shetani, lakini ingekuwa bora zaidi kusema kwamba binadamu wamemilikiwa na ukanaji. Hii ni njia ambayo binadamu hujionyesha wenyewe; ni kiambatisho cha mwili wao. Kwa hivyo, wote wameingia katika ukanaji bila kufahamu, na pamoja na hilo, kuadibu. Huu ni mtego uliotayarishiwa binadamu na Mungu, na huu ni wakati ambao binadamu huyaona mambo kuwa ya kufadhaisha zaidi. Kwa vile watu huishi katika ukanaji, ni vigumu wao kuachana na kuadibu. Je, hivi sivyo mambo yalivyo hasa siku hizi? Lakini binadamu wanawezaje kuyapuuza maneno ya Mungu: “Siku hizi, Shetani amekithiri kupita kiasi. Kwa nini Sichukui fursa hii kuringia kiini cha kazi Yangu ili kufichua nguvu Zangu?” Punde Nisemapo jambo fulani kuwakumbusha, watu kutoka makanisa huingia katika kuadibu mara moja. Hili ni kwa sababu baada ya miezi miwili ya kazi ya Mungu, watu bado hawapitii mbadiliko wowote wenye maana ndani. Wao huchambua tu maneno ya Mungu na mawazo yao wenyewe. Hata hivyo, katika ukweli halisi, hali zao hazijabadilika kabisa; wao bado ni wabaya. Hali ikiwa hii, Mungu anapotaja kwamba nyakati za kuadibu ziko karibu, watu huhuzunishwa sana, wakifikiria[b]: “Mimi sijui kama nimejaaliwa na Mungu au la, wala sijui kama naweza kusimama imara chini ya kuadibu huku. Hata ni vigumu zaidi kujua ni mbinu gani ambazo Mungu atatumia kuwaadibu watu.” Binadamu wote wanatishwa na kuadibu, lakini hawawezi kubadilika. Wao huteseka tu kwa kimya, lakini pia wanaogopa kwamba hawataweza kusimama imara. Katika kutokuwako huku kwa kuadibu na mateso ya maneno, binadamu wote wameteleza katika kuabidu bila kufahamu. Hivyo, wote ni wenye wasiwasi na waliofadhaishwa. Hii inaitwa, “kuvuna walichopanda,” kwa kuwa binadamu hawaelewi kazi ya Mungu kabisa. Kwa kweli, Mungu hapendi kupoteza maneno yoyote zaidi kwa watu hawa; inaonekana Mungu amechukua njia tofauti ya kuwashughulikia ambayo si kuadibu halisi. Ni kama wakati ambapo mtu hushika kifaranga na kukiinua kuona ikiwa ni kuku jike au jogoo; hili huenda lisionekane kama jambo kubwa, lakini kifaranga mdogo atatishwa sana atang’ang’ana kuwa huru, kana kwamba anaogopa binadamu atamuua na kula nyama yake, kwa kuwa kifaranga hana ufahamu kujihusu. Mtu anawezaje kumuua na kumla kifaranga mwenye uzito wa aunsi chache tu. Huo haungekuwa upuuzi? Ni kama alivyosema Mungu kabisa: “Kwa nini, basi, watu huniepuka Mimi daima? Je, ni kwa sababu Nitawachukulia kama vifaranga wadogo, kuuawa punde washikwapo?” Kwa hivyo, mateso ya binadamu yote ni kujitolea “bila ubinafsi,” na yanaweza kusemekana kuwa ni gharama bure kulipa. Ni kwa sababu hawajijui wenyewe ndiposa wao huhisi woga; kutokana na hilo, hawawezi kukosa kutahadhari. Huu ni udhaifu wa binadamu. Je, maneno yanayonenwa na Mungu, “Mwishowe, acha binadamu wajijue wenyewe. Hili ni lengo Langu la mwisho,” yamepitwa na wakati? NI nani anajijua mwenyewe kwa kweli? Ikiwa mtu hajijui mwenyewe, basi ni nini kinachompa haki ya kuadibiwa? Chukua mfano wa wanakondoo. Wanawezaje kuchinjwa kama hawajakua kuwa kondoo? Mti ambao haujazaa matunda unawezaje kufurahiwa na binadamu? Kila mtu huchukulia “chanjo” kuwa za maana sana. Hivyo, watu wote wanafanya kazi ya kufunga, na kisha wanaona njaa. Huu ni mfano wa kuvuna walichopanda; wanajiangamiza wenyewe. Si kwamba Mungu ni katili au wa kinyama. Ikiwa siku moja wanadamu watajijua wenyewe na kutetemeka kwa woga mbele ya Mungu, basi Mungu ataanza kuwaadibu. Ni kwa njia hii pekee ndiyo binadamu watakubali taabu kwa utii na kwa radhi. Na kuhusu leo je, hata hivyo? Watu wote hupokea kuadibu kinyume na hiari yao, kama watoto wanaolazimishwa kupika chakula. Watu kama hao wanawezaje kukosa kujihisi wasio na raha? Kila mtu hufikiria, “Haidhuru! Maadamu ninaadibiwa, naweza vilevile kuinamisha kichwa changu na kukiri kosa! Nitafanyaje? Hata kama nalia, bado lazima nimridhishe Mungu, kwa hiyo nitafanyaje? Nani aliniambia nitembee moja kwa moja kwa njia hii? Haidhuru! Nitajichukulia kama asiyekuwa na bahati!” Hivi sivyo wanavyofikira watu?
Kama alivyosema Mungu, “Kila mtu ana tabia nzuri, na hakuna anayethubutu kupinga. Wote wako chini ya uongozi Wangu, wakifanya kazi zao Nilizowapa.” Kwa dhahiri, hakuna binadamu hata mmoja hupokea kuadibu kwa radhi, na zaidi ya hayo, hili hutoka kwa Mungu, kwa sababu binadamu wote hutaka kuishi katika raha badala ya ghasia na vurugu. Mungu alisema, “Ni nani asiye na hofu ya kifo? Je, watu wako tayari kweli kujitoa mhanga?” Hii ni kweli kabisa; kila mtu huogopa kufa isipokuwa, bila shaka, wakati ambapo ameliwa na hasira au kukata tamaa. Hii ni dutu ya binadamu, na ndiyo ngumu zaidi kuihepa. Leo Mungu amekuja hasa kusuluhisha mashaka haya. Binadamu wote ni wadhaifu, kwa hiyo Mungu amefanya kila juhudi kuja miongoni mwao kuanzisha hospitali ya kitaalam ili kuwatibu aina hii ya ugonjwa. Watu hawawezi kujinasua wenyewe kwa ugonjwa huu wa kutatiza, ndiyo kwa sababu wote hupata wasiwasi sana mpaka wakawa na uvimbeuchungu wa mdomo, na tumbo zao kupanuka. Baada ya muda wingi wa gesi waliyonayo hukua, na kusababisha ongezeko la shinikizo. Hatimaye, tumbo zao hupasuka na wote hufa. Kwa hivyo, wakati huo, Mungu ametibu haya maradhi mabaya ya binadamu, kwa sababu kila mtu amekufa. Je, huku si kutibu hali ya binadamu? Mungu kwa makusudi amekuja kuifanya kazi hii. Kwa sababu watu huogopa kifo kupita kiasi, Mungu Mwenyewe amekuja kushiriki kazi sawa na binadamu; kwa sababu wana ujasiri kidogo sana, Ameanza kwa kutoa maonyesho ya watu kutazama. Ni baada tu ya kuona kitangulizi hiki ndipo mtu yeyote huwa radhi kutii. Kwa sababu hii, Mungu alisema, “Kwa kuwa hakuna mtu ambaye angeifanya kazi Yangu, Nimeingia vitani binafsi kukumbana na mapambano ya kufa na kupona dhidi ya Shetani.” Hivi ni vita vya kuamua mshindi na mshinde, kwa hiyo ama samaki wafe au wavu ukatike[c]. Hili ni hakika. Kwa kuwa roho itashinda mwishowe, mwili lazima uwe shabaha ya kifo. Je, mnaelewa athari za hili? Hata hivyo, msiwe wepesi kuathirika kupita kiasi. Labda sentensi hii ni rahisi, au labda ni changamano. Hata hivyo, binadamu bado hawawezi kuielewa. Hili ni hakika. Binadamu wanaweza, kutokana na kuteseka kwao, kukubali usafishaji wa neno la Mungu; kisha mtu angeweza kusema kwamba hii ni bahati yao nzuri. Hata hivyo, ingeweza pia kusemekana kuwa ya bahati mbaya kwao. Ningependa bado kumkumbusha kila mtu, hata hivyo, kwamba kusudi la Mungu ni sahihi, hata hivyo—tofauti na makusudi ya binadamu, ambayo kila mara ni kuhusu kujifanyia wenyewe mipango na matayarisho. Mnapaswa kuelewa hili, na kutozama katika tafakari zisizoisha. Je, huu sio udhaifu wa binadamu kabisa? Wote wako hivi; badala ya kumpenda Mungu kwa kiwango fulani, wao hujipenda wenyewe kwa kiwango fulani. Kwa kuwa Yeye ni Mungu ambaye ni mwenye wivu kwa binadamu, Yeye kila mara huwawekea matakwa. Kadri ambavyo watu hujipenda wenyewe, ndivyo Mungu huwahitaji zaidi wampende Yeye, na ndivyo matakwa Yake kwao huwa makali. Ni kana kwamba Mungu anawachokoza watu kwa kudhamiria. Kama watu wanampenda Yeye kweli, basi inaonekana Yeye hajali kuhusu hilo. Kwa sababu ya hili, watu wote wanakwaruza vichwa vyao na kubinya masikio yao wanapozama katika tafakari. Hii ni hadithi ya tabia ya Mungu, kutaja kwa ufupi tu kwa jambo moja au mawili. Haya ni mapenzi ya Mungu. Ni kile ambacho Mungu huwataka watu kujua; ni muhimu. Ni kazi mpya inayohitaji ninyi watu kuweza kufanya bidii kupenya na kufanya maendeleo mengine mapya. Je, unaelewa hili? Unataka Nisema mengi zaidi kuhusu mada hii?
Kuhusu enzi za awali, Mungu alisema, “hakuna mtu hata mmoja aliyechaguliwa na Mimi; kila mmoja alikataliwa na kimya Changu. Hii ni kwa sababu watu hao wa kale hawakunitumikia kwa kujitolea kwa roho moja; hivyo basi Nami wala sikuwapenda kipekee. Walikuwa wamechukua ‘vipawa’ vya Shetani na kisha wakageuka na kunitolea Mimi; kwa kufanya hivyo, je, huu haukuwa udanganyifu Kwangu?” Maneno haya yanawezaje kuelezwa? Ni kama alivyosema Mungu: “Vipaji vyote hutoka kwa Shetani.” Vizazi vya zamani vya mitume na manabii walitegemea kabisa vipaji vyao walipofanya kazi yao, na kotekote katika enzi, Mungu ametumia vipaji vyao kuendesha kazi Yake. Hii ndiyo maana inasemekana kwamba huduma ya watu wote wenye vipaji hutoka kwa Shetani. Hata hivyo, kama asemavyo Mungu[d], “Natumia ujanja wa Shetani kama foili[e]” kwa ajili ya hekima Yake. Hivyo, Mungu ametaja huduma ya watu wenye vipaji kama zawadi kutoka kwa Shetani. Kwa sababu wao ni wa Shetani, Mungu huwaita waliojaa kashfa. Hii si shutuma isiyo na msingi dhidi ya binadamu; ni ufafanuzi wenye msingi mzuri na wa kufaa. Kwa sababu hii, Alisema, “Sikufichua ghadhabu Yangu; badala yake, Nilijaribu kubadili mpango wao kwa matumizi Yangu mwenyewe kwa kuongezea ‘vipawa’ hivi kwa vifaa vinavyotumika katika usimamizi Wangu. Baadaye, mara tu vilipokuwa vimesindikwa na mtambo, Ningechoma masalio yote ya takataka.” Hiki ndicho cha ajabu sana kuhusu kazi ya Mungu. Wazo hili ni la chini mno kukubaliana na fikira za binadamu, kwa sababu hakuna ambaye angefikiri kwamba wale wanaotawala kama wafalme si watu wenye vipaji, ni watu wasio na vipaji ambao Mungu huwapenda. Kama inavyoweza kuonekana, mawazo au matumaini ya Witness Lee na Watchman Nee yote yamegeuka kuwa jivu—na watu wenye vipaji katika siku za sasa sio jambo la pekee. Sasa Mungu ameanza kazi hii, na Anachukua polepole kazi yote ya Roho Mtakatifu ndani ya binadamu ambao huhudumu kama foili kwa kazi Yake. Kazi ya Mungu itakapomalizika kabisa, watu hawa wote watarudi mahali pao pa asili. Hata hivyo, Nawasihi binadamu wasitende kwa kutojali kutokana na kile ambacho Nimesema. Lazima mfuate mkondo, kuzifuata hatua za kazi ya Mungu ili kuepuka kuikatiza. Je, mnaelewa hoja hii? Kwa sababu hii ni hatua na mbinu ya kazi ya Mungu. Wakati ambapo Mungu “atatengeneza” “zawadi” hizi ziwe “bidhaa zilizokamilishwa,” makusudi Yake yote yatakuwa wazi, na zawadi zinazomfanyia Yeye huduma zitaondoshwa zote; hata hivyo, Mungu atakuwa na bidhaa zilizokamilishwa kufurahia. Je, mnaelewa hili? Kile ambacho Mungu hutaka ni bidhaa zilizokamilishwa, sio zawadi za fahari ambazo hutolewa na binadamu. Ni wakati ambapo tu kila mtu amechukua pahali pake pa kufaa, kumaanisha wakati ambapo Mungu amerudi katika nafasi Yake ya asili na shetani, pia, ameketi katika kiti chake, na vilevile malaika, bila kinzano—wakati huo tu ndipo tabasamu ya kupendezwa itaonekana katika uso wa Mungu, kwa sababu makusudi Yake yatakuwa yameridhishwa, lengo Lake limetimizwa. Mungu hatatafuta tena “usaidizi” kutoka kwa “shetani,” kwa sababu makusudi ya Mungu yatakuwa yamefichuliwa kwa dhahiri kwa binadamu, na binadamu kamwe hawatalazimika kuyawasilisha. Wakati huu, miili yao ya tamaa za mwili itakuwa kitu kimoja na roho zao. Hili ndilo Mungu huwafichulia binadamu; ni makusudio ya mwisho ya roho, nafsi, na mwili. Ni muhtasari wa wazo la asili la “ubinadamu.” Hili halihitaji kuchunguzwa kwa utondoti; inatosha kujua jambo moja au mawili kulihusu. Je, mnaelewa?
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanasoma “Je, hiki si kile ambacho Mungu hutimiza na binadamu leo?”
b. Maandishi ya asili yanaacha “wakifikiria.”
c. Ama samaki wafe au wavu ukatike: nahau ya Uchina, yenye maana “mapambano ya kufa na kupona.”
d. Maandishi ya asili yanaacha “kama asemavyo Mungu.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili
Kujua zaidi: Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
0 意見:
Chapisha Maoni