Jumapili, 16 Desemba 2018

Ufafanuzi wa Tamko la Ishirini na Nane

Hali ya watu ni kwamba kadri wanavyoelewa maneno ya Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyoshuku zaidi njia ya sasa ya Mungu ya kufanya kazi. Lakini hii haina athari kwa kazi ya Mungu; maneno Yake yanapofikia kiwango fulani, kwa kawaida mioyo ya watu itabadilika.  Katika maisha yao, kila mtu huyakazia macho maneno ya Mungu, na pia wao huanza kutamani sana maneno Yake—na kwa sababu ya mfichuo wa Mungu wa siku zote, wanaanza kujidharau. Hata hivyo Mungu pia ametamkaaina nyingi za maneno yafuatayo: "Wakati ameelewa maneno Yangu yote kwa undani, kimo cha mwanadamu kiko sawa na matakwa Yangu, na maombi yake yanazaa matunda, na sio bure au batili; Ninabariki maombi ya mwanadamu yaliyo ya kweli, na sio kujifanya." Kwa kweli, watu hawawezi kuelewa kabisa maneno ya Mungu, wanaweza tu kuelewa juujuu. Mungu hutumia tu maneno haya kuwapa lengo la kufuatilia, ili kuwafanya wahisi kwamba Mungu hafanyi mambo kwa mzaha, lakini Yuko makini kuhusu kazi Yake, na ni wakati huo tu ndipo watakuwa na imani ya kufuatilia. Na kwa sababu watu wote huomba tu kwa ajili yao wenyewe, sio kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, lakini Mungu haghairi, maneno Yake daima yameelekezwa kwa asili ya mwanadamu. Ingawa watu wengi leo wanaomba, si waaminifu—ni kisingizio tu. Hali ya watu wote ni kwamba wao "wanauchukulia mdomo Wangu kama utoaji wa mambo mema ya namna maalum. Watu wote wanatamani kupata kitu kutoka kwenye kinywa Changu. Kama ni siri za taifa, au siri za mbinguni, au mienendo ya ulimwengu wa kiroho, au hatima ya mwanadamu." Kwa sababu ya udadisi wao, watu wote wako tayari kutafuta vitu hivi, na hawataki kupata kitu chochote cha ruzuku ya maisha kutoka kwa maneno ya Mungu. Hivyo Mungu anasema, "Vitu vingi vinakosekana ndani ya mwanadamu: Hahitaju tu 'nyongeza ya lishe' bali 'usaidizi wa kimawazo' na 'usambazaji wa lishe ya kiroho.'" Ni dhana zilizo ndani ya watu ndizo zimesababisha uhasi wa leo, na ni kwa sababu macho yao ya kimwili ni "kikabaili" sana ndio maana hakuna nguvu kwa kile wanachosema na kufanya, na wao ni wazembe na wapurukushani katika mambo yote. Je, hizi si hali za watu? Je, watu hawapaswi kuharakisha na kurekebisha hili, badala ya kuendelea jinsi walivyo? Kuzijua siku za baadaye kuna faida gani kwa mwanadamu? Kwa nini watu huwa na athari baada ya kusoma baadhi ya maneno ya Mungu, lakini maneno Yake yaliyosalia hayana athari? Wakati Mungu anaposema, kwa mfano, "Ninatoa uponyaji kwa ugonjwa wa mwanadamu ili matokeo bora yatimizwe, ili watu wote wawe na afya nzuri, na ili, kupitia uponyaji Wangu warejelee hali ya kawaida," inakuaje kwamba maneno haya hayana athari kwa watu? Je, kila kitu kinachofanywa na Mungu si kile kinachopaswa kutimizwa na mwanadamu? Mungu ana kazi ya kufanya—kwa nini watu hawana njia ya kutembea? Katika hili, je, hawamwachi Mungu? Kuna kazi nyingi kweli ambayo watu wanapaswa kufanya—kwa mfano, ni kiasi gani wanachojua kuhusu "joka kubwa jekundu" katika maneno "Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu"? Maneno ya Mungu ya "Mbona Nimewauliza mara nyingi?" yanaonyesha kwamba bado watu hawaijui asili ya joka kubwa jekundu, kwamba bado hawawezi kuingia ndani zaidi. Je, hii sio kazi ileile ambayo mtu anapaswa kufanya? Inawezaje kusemwa kwamba mwanadamu hana kazi? Ingekuwa hivyo, umuhimu wa Mungu kupata mwili ungekuwa upi? Je, Mungu anakuwa mzembe na mpurukushani kwa ajili ya kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati? Joka kubwa jekundu linaweza kushindwa kwa njia hii?
Mungu anasema, "Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu." Maneno haya yanaelezwa kwa kazi iliyo katika uungu; watu wa leo tayari wameingia katika kuadibu mapema, na hivyo Mungu anasema hii ni hatua ya kwanza ya kazi Yake. Yeye hawafanyi watu wavumilie kuadibu kwa maafa, bali kule kwa maneno. Kwa sababu, wakati sauti ya maneno ya Mungu inabadilika, watu huwa wasiojua kabisa, baada ya hilo wote huingia katika kuadibu. Na mara wakishapitia kuadibu, ni kama tu anavyosema Mungu[a] "Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!" Hii ni hatua ya kazi ya Mungu—ni mpango Wake. Zaidi ya hayo, watu hawa wa Mungu wataona wenyewe mbinu ambazo kwazo joka kubwa jekundu linaadibiwa, hivyo msiba unaanza rasmi katika ulimwengu wao wa nje. Hii ni mojawapo ya njia ambazo kwazo Mungu huwaokoa watu: Ndani wanaadibiwa, na nje msiba unawafika—ambalo ni kusema, maneno ya Mungu yanatimizwa. Kwa hivyo, watu wangependelea kupitia kuadibu badala ya msiba, na ni kwa sababu ya jambo hili ndio wanabaki. Kwa upande mmoja, hiki ni kiwango ambacho kazi ya Mungu imefikia; kwa upande mwingine, ni ili watu wote waweze kufahamu tabia ya Mungu. Hivyo Mungu anasema, "Wakati watu Wangu wananifurahia ni wakati joka kuu jekundu linaadibiwa. Kuwafanya watu wa joka kubwa jekundu kusimama na kuliasi joka ndiyo nia Yangu, na ndiyo njia ambayo Ninawakamilisha watu Wangu, na ni nafasi nzuri ya watu Wangu wote kukua maishani." Ni kwa nini Mungu ananena maneno haya lakini hayawavutii watu?
Nchi ziko katika machafuko makubwa, kwa sababu fimbo ya Mungu imeanza kutimiza wajibu wake duniani. Kazi ya Mungu inaweza kuonekana katika hali ya dunia. Mungu anaposema "maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika," hii ni kazi ya kwanza ya fimbo duniani, na matokeo yake ni kwamba "Nyumba zote duniani zitasambaratishwa; mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani." Hiyo ndiyo itakuwa hali ya jumla ya familia duniani. Kwa kawaida, haingeweza kuwa hasa hali ya wote, lakini ni hali ya wengi wao. Kwa upande mwingine, inahusu hali ambazo watu wa mkondo huu wamepitia katika siku za baadaye. Inatabiri kwamba, mara wakishapitia kuadibu kwa maneno na wasioamini wamepatwa na msiba, hakutakuwa tena na mahusiano ya familia miongoni mwa watu duniani; wote watakuwa watu wa Sinim, na wote watakuwa waaminifu katika ufalme wa Mungu. Hivyo, siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Na kwa hiyo, familia za watu duniani zitatenganishwa, zitapasuliwa vipande vipande, na hii itakuwa kazi ya mwisho ambayo Mungu anafanya katika mwanadamu. Na kwa sababu Mungu ataeneza kazi hii kotekote ulimwenguni, Anachukua fursa ya kuwafafanulia watu neno "hisia," hivyo Akiwawezesha kuona kwamba mapenzi ya Mungu ni kuzitenganisha familia zote za watu, na kuonyesha kwamba Mungu hutumia kuadibu ili kutatua migogoro yote ya familia miongoni mwa wanadamu. La sivyo, hapangekuwa na njia ya kuimaliza sehemu ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani. Sehemu ya mwisho ya maneno ya Mungu huonyesha udhaifu mkubwa kabisa wa wanadamu—wote huishi katika hisia—na hivyo Mungu haepuki hata mmoja wao, na Hufunua siri zilizofichwa mioyoni mwa wanadamu wote. Kwa nini ni vigumu sana kwa watu kujitenga na hisia? Je, ni muhimu zaidi kuliko viwango vya dhamiri? Je, dhamiri inaweza kufanikisha mapenzi ya Mungu? Je, hisia inaweza kuwasaidia watu kupitia shida? Machoni pa Mungu, hisia ni adui Yake—hili halijanenwa wazi katika maneno ya Mungu?
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha “ni kama tu anavyosema Mungu.”
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 意見:

Chapisha Maoni