Jumatatu, 26 Novemba 2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu,

Matamshi ya Mwenyezi MunguTamko la Thelathini

Mwenyezi Mungu alisema, Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri.  Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!
Ni wa kusikitisha jinsi gani! Jinsi gani walivyo duni! Jinsi gani walivyopofuka! Jinsi gani wanadamu walivyo wakatili! Kwa kweli mnalipuuza neno Langu—je, Ninazungumza nanyi bure? Bado ninyi ni wazembe sana, kwa nini? Kwa nini hivyo? Je, hamjawahi kufikiria kuhusu hilo kabla? Ninasema mambo haya kwa ajili ya nani? Niamini! Mimi ni Mwokozi wenu! Mimi ni Mwenyezi wako! Kesheni! Kesheni! Muda uliopotea hautakuja tena kamwe, kumbuka hili! Hakuna mahali popote duniani ambapo unaweza kununua dawa ambayo itapoza majuto! Kwa hiyo Nitawaambiaje hili? Je, neno Langu halistahili uzingatifu wenu wa makini na kutafakari kwa kurudia? Ninyi ni wazembe sana kwa maneno Yangu na ni msiowajibikia maisha yenu sana; Ninawezaje kustahimili haya? Ninawezaje?
Kwa nini inawachukua muda mrefu sana kuwa na maisha sahihi ya kanisa? Ni kwa sababu mnakosa imani, hamko tayari kulipa gharama, hamtaki kujitoa wenyewe, na hamko radhi kujitumia wenyewe mbele Yangu. Amkeni, wanangu! Niamini, wanangu! Wapendwa Wangu, kwa nini hamuwezi kufikiria yaliyo ndani ya moyo Wangu?
kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili 

 Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

0 意見:

Chapisha Maoni