Alhamisi, 18 Oktoba 2018

Hukumu ya Neno la Mungu ni Kumwokoa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Nyimbo

Hukumu ya Neno la Mungu ni Kumwokoa Mwanadamu

I
Ingawa Mungu amenena maneno mengi kwako
ya kuadibu, ya hukumu,
hayajafanyika kwako,
naam, hayajafanyika kwako kweli.
Mungu alikuja kufanya kazi Yake na kunena maneno.
Ingawa maneno Yake yanaweza kuwa makali,
yananenwa kwa hukumu
ya upotovu wako, uasi.
Kusudi la Mungu kufanya hivi
sio kumdhuru mwanadamu,
ila kumwokoa kutoka kwa miliki ya Shetani.
Maneno ya Mungu ni makali ili kusaidia kupata matokeo.
Kwa njia hii tu ya kufanya kazi
ndiyo wanadamu wanaweza kujitambua,
wanaweza kujitenga na tabia yao ya uasi.
Ingawa maneno ya Mungu yanaweza kuwa makali,
yananemwa kwa wokovu wa mwanadamu,
kwa kuwa Ananena maneno tu,
bila kuadhibu mwili wa mwanadamu.
Maneno haya yanamsaidia mwanadamu kuishi katika nuru,
kujua nuru ipo na ni ya thamani,
kujua ni ya manufaa kwa mwanadamu,
na kujua kwamba Mungu ni wokovu.
II
Kazi ya maneno ina maana kubwa:
Mwanadamu anaweza kutambua na hivyo kutenda ukweli,
kufanikisha mabadiliko ya tabia,
kujijua wenyewe na kazi ya Mungu.
Kufanya kazi huku kupitia kuzungumza tu
ndiko kunaweza kujenga uhusiano
uliopo kati ya Mungu na mwanadamu.
Na maneno tu yanaweza kueleza ukweli.
Ni njia bora zaidi ya kumshinda mwanadamu.
Mbali na kunena maneno,
hakuna kinachoweza kumsaidia mwanadamu kutambua vizuri
ukweli wote na kazi yote ya Mungu.
Mungu ananena katika hatua ya mwisho ya kazi Yake
kufunua ukweli usiojulikana, siri,
kumfanya mwanadamu kupata njia ya kweli, uzima,
na hivyo kuridhisha mapenzi ya Mungu.
Ingawa maneno ya Mungu yanaweza kuwa makali,
yananemwa kwa wokovu wa mwanadamu,
kwa kuwa Ananena maneno tu,
bila kuadhibu mwili wa mwanadamu.
Maneno haya yanamsaidia mwanadamu kuishi katika nuru,
kujua nuru ipo na ni ya thamani,
kujua ni ya manufaa kwa mwanadamu,
na kujua kwamba Mungu ni wokovu.
kutoka kwa "Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu" katika Neno Laonekana katika Mwili
Tazama zaidi: Umeme wa Mashariki | Nyimbo za Neno la Mungu

0 意見:

Chapisha Maoni