Kanisa la Mwenyezi Mungu Vitabu | Ufafanuzi wa Tamko la Kumi na Saba
Kwa kweli, maneno yote kutoka katika kinywa cha Mungu ni mambo ambayo wanadamu hawayajui; yote ni lugha ambayo watu hawajasikia, kwa hiyo inaweza kusemwa hivi: Maneno ya Mungu yenyewe ni siri. Watu wengi kwa kutojua wanaamini kwamba ni mambo tu ambayo watu hawawezi kutimiza kimawazo, mambo ya mbinguni ambayo Mungu anawawezesha watu kuyajua sasa, au ukweli kuhusu kile Mungu anachofanya katika ulimwengu wa kiroho ni siri. Hili linaonyesha kwamba watu hawachukulii maneno yote ya Mungu kwa usawa, wala hawayathamini, lakini wanalenga kile wanachoamini kuwa "siri."
Hili linathibitisha kwamba watu hawajui maneno ya Mungu ni nini au siri ni nini—wao husoma tu maneno ya Mungu kutoka kwa fikira zao wenyewe. Ukweli ni kwamba hakuna hata mtu mmoja ambaye anapenda maneno ya Mungu kweli—kiini cha kwa nini inasemwa kwamba "Watu ni mabingwa wa kunihadaa Mimi" iko papa hapa. Hakika si kwamba Mungu anasema watu hawana ustahili wowote, au kwamba wao ni takataka kabisa. Hii ndiyo hali halisi ya wanadamu. Watu wenyewe hawaelewi vyema kuhusu kiasi gani Mungu anamiliki katika mioyo yao—Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kwa ukamilifu. Kwa hiyo sasa hivi watu wanafanana na watoto wadogo wanyonyao—hawajui kabisa kwa nini wanakunywa maziwa na kile wanachoishia. Ni mama yao tu anayefahamu mahitaji yao, hatawaruhusu kufa njaa, wala hatawaruhusu kula chakula kingi kupindukia. Mungu anajua mahitaji ya watu bora zaidi, kwa hiyo wakati mwingine upendo Wake hujumuishwa katika maneno Yake, wakati mwingine hukumu Yake hufunuliwa ndani ya maneno hayo, wakati mwingine maneno Yake huumiza mioyo ya ndani kabisa ya watu, na wakati mwingine maneno Yake ni ya kweli sana na ya dhati. Hii huwaruhusu watu kuhisi fadhili Zake na upatikanaji Wake, na kwamba Yeye si "mtu wa kulazimisha" ambaye Anafikiriwa, Yule ambaye hawezi kuguswa, wala Yeye si "Mwana wa Mbinguni" katika akili za watu, ambaye Hawezi kutazamwa moja kwa moja usoni, na hasa Yeye si "muuaji" Ambaye watu wanadhani Huwaua wasio na hatia. Tabia yote ya Mungu imefunuliwa katika kazi Yake, tabia ya Mungu aliye katika mwili leo bado inajumuishwa kupitia kwa kazi Yake, kwa hiyo huduma ambayo Mungu huifanya ni huduma ya maneno, si kile Anachofanya au jinsi Anavyoonekana nje. Mwishowe watu wote watapata ujenzi wa maadili kutoka kwa maneno ya Mungu na kufanywa kamili kwa sababu ya maneno hayo. Katika uzoefu wao, kwa sababu ya uongozi wa maneno ya Mungu, watapata njia ya kufanya mazoezi, na kupitia maneno kutoka katika kinywa cha Mungu watu watajua tabia Yake yote. Kwa sababu ya maneno hayo kazi yote ya Mungu itatimizwa, watu watachangamka, na maadui wote watashindwa. Hii ndiyo kazi ya msingi, na hakuna mtu anayeweza kuipuuza. Tunaweza hata hivyo kuangalia maneno Yake: "Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya." Wakati Mungu anapokifungua kinywa Chake maneno hutoka tu. Yeye hufanikisha kila kitu kupitia kwa maneno, na vitu vyote vinabadilishwa kwa maneno Yake, watu wote wanafanywa upya kwa maneno Yake. Je, "radi na umeme" zinahusu nini? Na "nuru" inahusu nini? Hakuna kitu hata kimoja ambacho kinaweza kuepuka maneno ya Mungu. Anatumia maneno Yake kuweka wazi akili za watu na kuonyesha ubaya wao; Anatumia maneno kushughulikia asili ya kale ya watu na kuwafanya watu Wake wote wawe kamili. Je, huu sio umuhimu wa maneno ya Mungu? Katika ulimwengu mzima, ikiwa hapangekuwa na msaada na kutegemezwa kwa maneno ya Mungu, wanadamu wote wangekuwa wameangamizwa zamani kiasi cha kutokuwepo. Hii ni kanuni ya kile Mungu anachofanya, na ni mbinu ya kufanya kazi kwa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Umuhimu wa maneno Yake unaweza kuonekana wazi kupitia kanuni hii. Maneno ya Mungu hupenya moja kwa moja katika kina cha nafsi za wanadamu. Mara tu wanapoona maneno Yake wanashangaa na kujawa na hofu na kukimbia haraka. Wanataka kutoroka ukweli wa maneno Yake, ndiyo sababu "wakimbizi" hawa wanaweza kuonekana kila mahali. Baada tu ya maneno ya Mungu kutamkwa watu hutimua. Hii ni hali moja ya sura ya ubaya wa wanadamu ambayo Mungu anaonyesha. Hivi sasa, watu wote wanaamka polepole kutoka kwa mzubao wao. Ni kama kwamba hapo awali watu wote walikuwa wamepata kichaa, na sasa wanaona maneno ya Mungu na ni kama kwamba wana athari za kudumu baada ya ugonjwa huo na hawawezi kurejelea hali yao ya zamani. Hii ni hali halisi ya watu wote, na pia ni picha halisi ya sentensi hii: "watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani." Hii ndiyo maana Mungu alisema: "Wanadamu wengi wanashtuliwa na ujio wa ghafla wa mwangaza." Kulisema hivi kunafaa kabisa. Maelezo ya Mungu kuhusu wanadamu hayatoi nafasi hata kidogo—kwa kweli Amefanya hili kwa usahihi na bila kosa, ndiyo sababu watu wote wameridhishwa kwa ukamilifu na bila kujua, upendo wao kwa Mungu umeanza kujengeka kutoka ndani kabisa ya mioyo yao. Kwa njia hii pekee ndiyo nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu inazidi kabisa kuwa ya kweli, na hii pia ni njia mojawapo ambayo Mungu hufanya kazi.
"Wanadamu wengi wamechanganyikiwa tu; wamejeruhiwa machoni na kutupwa chini matopeni na mwangaza." Kwa sababu wanaenda kinyume cha mapenzi ya Mungu (yaani, wanampinga Mungu), mtu wa aina hiyo hupitia kuadibu kwa sababu ya uasi wake wakati maneno ya Mungu yanakuja; hii ndiyo sababu inasemekana kwamba wamejeruhiwa machoni na mwangaza. Mtu wa aina hii tayari amepeanwa kwa Shetani, hivyo wakati anaingia katika kazi mpya hana nuru au mwangaza wowote. Wale wote ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wamemilikiwa na Shetani, na ndani kabisa ya mioyo yao hakuna mahali pa Mungu, kwa hiyo inasemekana kwamba "wametupwa chini matopeni." Wale ambao wako katika hali hii wote wako katika hali ya mchafukoge. Hawawezi kuingia katika njia sahihi, hawawezi kurudia tena hali ya kawaida, kile wanachofikiria katika akili zao yote ni kinyume. Watu wote duniani wamepotoshwa na Shetani kupita kiasi. Hawana uhai na wao wamejaa harufu ya maiti. Watu wote duniani wanaendelea kuishi katikati ya tauni ya viini vya maradhi na hakuna mtu anayeweza kuepuka. Hawana nia ya kuendelea kuishi duniani, lakini daima wanahisi kwamba kuna kitu kikubwa zaidi kitakachotendeka ili kuwasababisha watu wakione wenyewe, kwa hivyo watu wote wanajilazimisha kuendelea kuishi. Watu hawajakuwa na nguvu mioyoni mwao kwa muda mrefu, wanatumia tu matumaini yao yasiyoonekana kama nguzo ya kiroho, kwa hiyo wanashikilia tu vichwa vyao wenyewe wakitenda kama mwanadamu, ili kukamilisha siku zao duniani. Ni kama kwamba watu wote ni wana wa shetani mwenye mwili. Ndiyo maana Mungu alisema: "dunia imefunikwa na vurugu, ikifanya mtazamo wa kusikitisha usiovumilika ambao, ukichunguzwa kwa kina, unamtesa mtu na huzuni nyingi." Kwa sababu ya kuonekana kwa hali hii Mungu alianza "kutawanya mbegu za Roho Wangu" kuelekea ulimwengu wote, na Alianza kutekeleza kazi Yake ya wokovu duniani kote. Ni kwa sababu ya kuendeleza kazi hii ndio Mungu alianza kumimina kila aina ya maafa, hivyo kuwaokoa wanadamu wenye mioyo migumu. Katika awamu za kazi ya Mungu, njia ya wokovu bado ni kupitia kwa maafa mbalimbali na wale wote ambao wamehesabiwa hawawezi kuyaepuka. Ni mwisho tu ndio hali ya "kutulia kama mbingu ya tatu: Hapa viumbe vilivyo hai vikubwa na vidogo vinaishi pamoja kwa amani, bila kushiriki katika 'migogoro ya mdomo na ulimi hata mara moja'" kuwa na uwezo wa kuonekana duniani. Hali moja ya kazi ya Mungu ni kuwashinda wanadamu wote na kuwapata watu waliochaguliwa kupitia kwa maneno Yake. Hali nyingine ni kuwashinda wana wote wa uasi kupitia kwa maafa mbalimbali. Hii ni sehemu moja ya kazi kubwa ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndio ufalme ulio hapa duniani ambao Mungu anataka unaweza kutimizwa kwa ukamilifu, na hii ni sehemu ya kazi ya Mungu ambayo ni kama dhahabu nzuri.
Daima Mungu anahitaji kwamba watu waelewe elimumwendo ya mbinguni. Wanaweza kulitimiza jambo hilo kweli? Ukweli ni kwamba, kwa kutegemea hali halisi za watu sasa, baada ya kupotoshwa na Shetani kwa zaidi ya miaka 5,900, hawawezi kulinganishwa na Petro na hivyo hawawezi tu kufanya hivyo. Hii ni mojawapo ya mbinu za kazi ya Mungu. Hangewafanya watu wasubiri kwa kukaa tu, lakini Angewahitaji kutafuta kwa vitendo. Ni kwa njia hii tu ndiyo Mungu atakuwa na fursa ya kufanya kazi ndani ya watu. Hili linaweza pia kuelezewa kidogo zaidi, la sivyo watu watakuwa tu na ufahamu wa juu juu. Baada ya Mungu kuwaumba wanadamu na kuwapa roho, Aliwaagiza kwamba ikiwa hawangemwita Mungu, basi hawangeweza kuunganishwa na Roho Wake na hivyo "televisheni ya setilaiti" kutoka mbinguni haingepokelewa duniani. Wakati Mungu hayupo tena katika roho za watu kuna kiti kitupu kinachoachwa wazi kwa ajili ya vitu vingine, na hivyo ndivyo Shetani anavyotwaa fursa hiyo kuingia ndani. Wakati watu wanapowasiliana na Mungu kwa mioyo yao, Shetani huingia katika hofu kubwa na huharakisha kuhepa. Kupitia wa vilio vya wanadamu Mungu huwapa kile wanachohitaji, lakini “Hakai” ndani yao kwanza. Yeye daima huwapa tu msaada kwa sababu ya vilio vyao na watu hupata ujasiri kutoka kwa nguvu hizo za ndani ili Shetani asithubutu kuja hapa "kucheza" apendavyo. Kwa njia hii, ikiwa watu daima wanaunganishwa na Roho wa Mungu, Shetani hathubutu kuja kuvuruga. Bila vurugu ya Shetani, maisha yote ya watu ni ya kawaida na Mungu ana fursa ya kufanya kazi ndani yao bila vizuizi vyovyote. Kwa njia hii, kile Mungu anataka kufanya kinaweza kutimizwa kupitia kwa wanadamu. Kutokana na hili inaweza kujulikana kwa nini Mungu daima Amewahitaji watu wazidishe imani yao, na pia Amesema: “Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi 'kukamua damu ya mtu yeyote' ili kujiridhisha.” Watu wengi sana wanakanganywa na matakwa ya Mungu, wakisema, kwa kuwa watu hawana akili hiyo na wamepotoshwa na Shetani kiasi cha kutotengenezeka tena, kwa nini Mungu anaendelea kutoa matakwa kwao? Je, Mungu hawaweki watu katika hali ngumu? Unapoona nyuso za watu za dhati, na kisha kuona mtazamo wao wenye kufedhehesha, huna budi kucheka. Ubaya mbalimbali wa watu ni wa kuchekesha sana—wakati mwingine wao ni kama mtoto anayependa kucheza, na wakati mwingine wao ni kama msichana mdogo akimwigiza "mama." Wakati mwingine wao ni kama mbwa akimla panya. Hali zao zote mbaya ni za kuchekesha kwa mzaha tu, na mara nyingi kadri watuwanavyoshindwa kuelewa mapenzi ya Mungu, ndivyo wanavyozidi kustahili kuingia kwenye shida. Ndiyo sababu inaweza kuonekana kutoka kwa maneno ya Mungu, "Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe?" Jinsi watu walivyo wajinga, na inaonyesha kwamba hakuna mtu anayeweza kuelewa mapenzi ya Mungu. Hata Akieleza mapenzi Yake ni nini, hawawezi kuyazingatia. Wanafanya tu kazi ya Mungu kulingana na mapenzi ya binadamu, hivyo wanawezaje kuelewa mapenzi Yake kwa njia hiyo? "Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma." Hii itakuwa hali wakati ufalme utaundwa. Kwa kweli, katika sehemu kadhaa Mungu ametabiri uzuri wa utambuzi wa ufalme, na kama wote utajumuishwa, ni picha kamili ya ufalme. Lakini watu hawaizingatii—wao huiangalia tu kama katuni. Kwa sababu ya miaka elfu kadhaa ya kutposhwa na Shetani, watu daima wameishi katika giza, hivyo hawana wasiwasi na giza wala hawaitamani nuru. Hii ndiyo imesababisha hili wakati nuru imefika leo: "wote wanakirihishwa na ujio Wangu, wote wanaufukuza mwangaza usije, kana kwamba Mimi ni adui ya mwanadamu mbinguni. Mwanadamu ananisalimu na mwangaza wa kujikinga machoni mwake." Ingawa watu wengi wanampenda Mungu kwa moyo wa kweli, bado Hajaridhika na bado Anawashutumu wanadamu. Hili linawakanganya watu. Kwa sababu watu wanaishi katika giza, huduma yao kwa Mungu bado inafanywa kwa njia sawa na katika hali ya kukosa mwanga. Yaani, watu wote humtumikia Mungu kwa kutumia fikira zao wenyewe, na wakati Mungu anapokuja watu wote wako katika hali hii na hawawezi kumhudumia Mungu kwa kukubali nuru mpya, lakini wanatumia uzoefu wao wote kumhudumia. Mungu hapati furaha kutoka kwa "kujitolea" kwa wanadamu, hivyo nuru haiwezi kusifiwa na wanadamu katika giza. Ndiyo maana Mungu alisema hivi—bila shaka sio kinyume na ukweli, na sio Mungu anayewadhulumu wanadamu, wala sio Yeye anayewakosea. Tangu uumbaji wa ulimwengu mpaka leo, hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kuonja joto la Mungu—wamekuwa wakijikinga dhidi ya Mungu, wakiogopa sana kwamba Mungu atawaangusha, kwamba Atawaangamiza. Kwa hiyo kwa zaidi ya miaka hii 6,000 daima Mungu ametumia uchangamfu kwa kubadilishana na uaminifu wa watu, na daima Amewaongoza kwa uvumilivu kila wakati. Hii ni kwa sababu watu ni dhaifu sana, na hawawezi kufahamu mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, na hawawezi kumpenda kwa moyo wote, kwa sababu hawana budi kuwa chini ya utawala wa hila wa Shetani. Lakini ingawa huu ni ukweli, Mungu bado Anavumilia, na wakati Anapovumilia hili hadi siku fulani, yaani, wakati Atakapoufanya upya ulimwengu, Yeye hatawatunza tena watu kama mama afanyavyo. Badala yake, Atawapa wanadamu adhabu inayofaa ndiyo sababu baada ya hayo kutakuwa na: "Maiti wanasongasonga juu ya bahari," huku "mahali ambapo hakuna maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, wakicheka na kuimba, ahadi ambazo Nimewapa." Huu ni ulinganishi kati ya hatima za wale ambao wanapewa thawabu na wale ambao wanaadhibiwa. "Juu ya bahari" inahusu kuzimu ya kuadibu kwa wanadamu ambako Mungu alizungumzia. Ni hatima ya mwisho ya Shetani, na ni "mahali pa kupumzika" ambapo Mungu amewaandalia wote wanaompinga Yeye. Daima Mungu ametaka upendo halisi wa wanadamu, lakini bila kujua, watu bado wanafanya kazi yao wenyewe. Ndio maana, katika maneno Yake yote, daima Mungu ametoa matakwa Yake kwa watu na Ameelezea dosari zao pamoja na njia yao ya mazoezi, ili waweze kutenda kulingana na maneno haya. Mungu pia Amefafanua juu ya mtazamo Wake mwenyewe kwa watu: "Lakini Sijawahi kuchukulia mzaha maisha ya binadamu hata mmoja kana kwamba ni kitu cha kuchezea. Nachunguza damu ya moyo wa mwanadamu, nami Naelewa bei ambayo amelipa. Anaposimama mbele Yangu, Sitamani kujinufaisha na kutokuwa na ulinzi kwa mwanadamu ili kumwadibu, wala kumtawaza vitu visivyohitajika. Badala yake, Nimemtunza tu mwanadamu, na kumpa mwanadamu, wakati huu wote." Watu wanapoyasoma maneno haya kutoka kwa Mungu, wao huhisi uchangamfu Wake mara moja: Kwa kweli, zamani Nimelipa gharama kwa Mungu lakini pia Nimemtendea kwa uzembe, na wakati mwingine Nimelalamika Kwake. Daima Mungu ameniongoza kwa maneno yake na Yeye huzingatia sana maisha yangu, lakini wakati mwingine Mimi hucheza nayo kama kwamba ni mwanasesere. Kwa kweli si haki. Mungu ananipenda sana, kwa hivyo kwa nini Siwezi kujitahidi vya kutosha? Wakati wanapofikiri juu ya jambo hili, watu hutaka kujipiga nyuso zao, au, kuhusu watu wengine, pua zao hata hutetemeka na wao hulia kwa sauti kubwa. Mungu anaelewa mioyo ya watu na Husema ifaavyo, na maneno haya machache ambayo si magumu wala mororo huhimiza upendo wa watu kwa ajili ya Mungu. Hatimaye, Mungu alitabiri mabadiliko katika kazi Yake wakati ufalme unapoanzishwa duniani: Wakati Mungu yupo duniani, watu wataweza kuwa huru kutokana na balaa na maafa na wataweza kufurahia neema, lakini wakati Anapoanza hukumu ya siku kuu, itakuwa wakati Anapoonekana kati ya watu wote, na kazi Yake yote duniani itakuwa imekalimilika kabisa. Wakati huo, kwa sababu siku imefika, itakuwa sawasawa na ilivyosema katika Biblia: "Yule aliye dhalimu, basi aendelee kuwa dhalimu; na yeye aliye mtakatifu, na awe mtakatifu bado." Wasio haki watarudi kwa kuadibu, na watakatifu watarudi mbele ya kiti cha enzi. Hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kupata mahali Pake, hata wana na watu wa ufalme. Yote itakuwa haki ya Mungu, na yote itakuwa ufunuo wa tabia Yake. Hataonyesha kujihusisha kwa ajili ya udhaifu wa wanadamu kwa mara ya pili.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Soma zaidi Matamshi ya Mwenyezi Mungu.
0 意見:
Chapisha Maoni