Jumanne, 24 Julai 2018

Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka(1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, wokovu,

Shahidi uzoefu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Tong Xin    Mkoa wa Fujian
💓💓💓💓    *************         🌺🌺🌺🌺

Nilizaliwa vijijini. Nilitoka kwa nasaba ya wakulima wanyenyekevu na zaidi ya hayo familia yetu ilikuwa na watu wachache, kwa hiyo mara nyingi tulikuwa tunadhulumiwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 13, kulikuwa na mtoto aliyepigwa na mtu fulani kutoka nje ya kijiji chetu. Wanakijiji walimlaumu kwa uongo baba yangu kwa kuchochea hilo na wakasema walitaka kupekua nyumba yetu na kuchukua ngawira mali yetu, kuchukua nguruwe wetu na hata kumpiga baba yangu. Kulikuwa na wakati pia ambapo mwanakijiji mwingine alichukua wavu wetu wa uvuvi na kuuweka kama wake mwenyewe.
Wakati baba yangu alipokwenda kuurudisha, mwanamjiji huyo kwa kweli alimgonga baba yangu, akitegemea nguvu na ushawishi wake mwenyewe. Baba yangu alilazimika kujidhalilisha tu kwa kuwa alijua kwamba hakuwa na fedha wala nguvu. Mama yangu akawaambia ndugu zangu wa kiume nami kwamba ni lazima tujipiganie wenyewe katika siku zijazo, na kamwe tusiishi maisha ya ukandamizwaji kama huu. Nikiwa mchanga na mwenye kuchukia udhalimu katika jamii, nilidhamiria kuwa siku zijazo ningejitokeza na kuwa bora kuliko wengine na kupata heshima yao, na kamwe nisikandamizwe. Kwa hiyo nilisoma kwa bidii sana, lakini sikuwa mwerevu kutosha na sikuweza kuingia katika vyuo vikuu vyovyote, kwa hiyo nilichagua kufuatilia ustawisho katika jeshi na kujiunga kwa urahisi kwa njia ya ahali.
Wakati kwanza nilijiunga, nilisombera kuchukua kazi zote ngumu na chafu na kuonyesha uamilifu wangu kuwavutia viongozi wangu na kupandishwa cheo katika siku zijazo. Hata hivyo, bila kujali nilijaribu kwa bidii kiasi gani, sikuweza hata kupata nafasi ya kiongozi wa kikosi. Pia nilitaniwa na kudhulumiwa daima na wanajeshi wenza kwa sababu ya nguo zangu chakavu na iktisadi, jambo ambalo lilizidisha tu hamu yangu ya kujitokeza. Baadaye, kwa kuegemea ushauri kutoka kwa mwanakijiji mwenzangu, nilijifunza kwamba tathmini na kupandishwa cheo katika jeshi havitegemei kazi ngumu, lakini badala yake ni utoaji zawadi. Ingawa niliona kitu cha aina hii kikiwa chukizo, ilinibidi nichukue njia ya pekee ya kupandishwa cheo. Kwa hiyo, nilidhamiria kuchukua akiba yangu yote ili kutoa zawadi kwa viongozi wangu na kufanya miunganisho, kama kila mtu mwingine yeyote karibu nami; baada ya hapo niliweza kujiandikisha katika chuo cha kijeshi. Lakini baada ya kuhitimu, nilipewa kazi kupika katika kantini kwa sababu sikuwa na fedha za kutosha za kutoa zawadi, na baadaye nikawa Afisa Mgavi, lakini kwa jina tu. Baada ya miaka kadhaa ya maisha ya kijeshi, nilielewa kuwa warasimu hawakuwaadhibu watoa zawadi na huwezi kufanikisha chochote bila ya kujipendekeza sana kwao. Ukitaka kuendelea, unapaswa kujaribu kila njia za kutengeneza pesa na kutoa zawadi, vinginevyo huwezi kufanikisha chochote bila kujali uwezo wako ni mkubwa kiasi gani. Ili kufanikisha hamu yangu ya kupata, nilianza kutengeneza pesa na kuchangisha fedha kila mahali: Nilitaja bei ya juu na kutia chumvi kiasi kwa makusudi wakati wa kununua chakula, nikipata pesa kidogo ya ziada ya haramu; kuona Afisa Wagavi wengine wakiuza mchele, niliuza kwa siri lori moja ya mchele kutoka kwa jeshi na kutengeneza yuan elfu kadhaa, na kadhalika. Ingawa nilikuwa nimemwamini Yesu tangu utotoni na nilifahamu wazi kwamba vitu hivi nilivyokuwa nikivifanya vilikuwa ni uhalifu, nilikuwa pia na wasiwasi daima kuhusu kupatikana na kuhukumiwa siku moja, nia ya kupandishwa cheo ilinielekeza kufanya mambo hayo kinyume cha dhamiri yangu. Mara nilipokuwa nimekwisha kuweka akiba pesa kiasi, nilianza kuwapendeza viongozi wangu na kuwapa zawadi zilizowaauni kwa upendeleo wao. Kila wakati kiongozi fulani alipokuja kuniona ningejishughulisha nikienda kunywa pombe naye, kuimba, kuwasiliana na makahaba …. Nilifanya kila kitu kilichowezekana ili kujipendekeza kwake. Nilijaribu kumpendeza kwa njia yoyote iliyowezekana. Wakati wowote viongozi walipohitaji msaada fulani, nilifurahi kuwapa huduma zangu. Yeyote aliyekuwa na uhusiano mzuri na viongozi hao, ningejaribu kuwa karibu naye ili kupata pendekezo zuri. Katika miaka hiyo, nilipanda haraka hadi kwa cheo cha kamanda wa batalioni kwa kukimbilia aina hii ya falsafa ya kidunia. Hatimaye nilijitokeza na niliweza kurudi nyumbani kwa utukufu! Baada ya hapo, kila wakati niliporudi nyumbani, wanakijiji wangenizunguka, wakinipendeza na kunisifu, jambo ambalo liliridhisha majisifu yangu sana. Malengo yangu na tamaa zangu zilikua wakati huo. Kama vile watu wangesema, "Maafisa wengine wana yatetea masilahi yao wenyewe tu, sio umma," "Tumia mamlaka ukiwa nayo, kwa sababu yakishaondoka, huwezi kuyatumia," na "Hakuna kitu kama afisa ambaye hahongeki." Kwa hiyo, nilianza kufurahia marupurupu ya kuwa afisa. Ningepata vitu vya bure popote nilipoenda, na kama mtu angetafuta msaada kutoka kwangu, ningewataka wanipe zawadi na singewasaidia kama zawadi zilikuwa duni. Nilianza kufuatilia chakula na mavazi ya kupendeza, na kuanza kujidai. Nikitegemea ukweli kwamba nilikuwa kama "mtoto wa bidii anayependwa na wote" nikijuana na viongozi muhimu kama kamanda na kamissa wa kisiasa, hata nikawa na kiburi sana hivi kwamba ningewadhulumu watu kwa kuringia uhusiano wangu na wenye nguvu, kuomba zawadi kutoka kwa wasaidizi wangu nikitumia majina ya viongozi hawa. Hivi ndivyo jinsi nilivyopotoka kutoka kuwa kijana sahili Mkristo wa mashambani hadi kuwa mtu mwenye shauku, mwenye udanganyifu wa shetani.
Nikiwa mpotovu na aliyeanguka, hata nilionyesha asili yangu ya kuogofya kwa wengine. Mara nyingi nilishuku bila sababu nzuri kwamba mke wangu mrembo ambaye alifanya kazi kwa kampuni ya kigeni alikuwa na uhusiano wa kando; hili lilisababisha mgogoro zaidi kati yetu na utengano uliokuwa ukizidi. Mnamo mwaka 2006, mambo yalimzidi sana mke wangu na akaanzisha mchakato wa talaka; hili lilikuwa kama fedheha kubwa kwangu, hivyo singelikubali. Usiku wa maname daima ningekuwa nikifikiri kuhusu maisha yangu. Nilifikiri mwenyewe: Nimekuwa nikidhamiria kujitokeza tangu utotoni na mke wangu na mimi sote tumefanikiwa katika kazi zetu. Hali katika nyumba yetu ni nzuri kwa kila njia na watu wengine wanatuonea wivu, hivyo kwa nini ninaishi katika maumivu kama hayo, na kwa nini imefika kiasi kwamba mke wangu anataka kunitaliki? Hata mwana wetu wa kiume anateseka pamoja nasi. Je, maisha yangu yako jinsi ninavyotaka yawe? Ninaishi hasa kwa sababu ya nini? Nilipokuwa tu nikihisi kupotea na kuchanganyikiwa, mke wangu aliukubali wokovu wa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Kwa njia ya mikutano ya mara kwa mara na ushirika na ndugu wa kike na wa kiume, akawa mwenye matumaini mema zaidi na zaidi, aliacha kubishana nami, na kamwe hakutaja talaka tena. Badala yake, alijishughulisha na kuihubiri injili na kutimiza wajibu wake. Baadaye, nikielekezwa na mke wangu na mama yangu, pia nilianza kumwamini Mwenyezi Mungu.
Kwa sababu ya maisha katika kanisa, nilielewa kwamba Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, na kwamba Yeye huchukia zaidi uchafu na upotovu wa wanadamu. Nilifikiria njia chafu ambazo kwazo nilikuzwa katika jeshi na kwamba labda singeweza kuokolewa na Mungu kama singebadilisha tabia yangu ya zamani, hivyo nikaanza kusoma maneno ya Mungu kwa shauku, nikitumaini kuwa ningeweza kupata suluhisho ndani yayo. Siku moja, nilisoma maneno haya kutoka kwa Mungu: “Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameagamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika ‘taasisi za elimu ya juu.’ Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa, uwepo usio na thamani, na hali ya maisha potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga” (“Kuwa na Tabia Isiyobadilika ni Kuwa Katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalifichua siri katika asili ya moyo wangu; nilitetemeshwa vibaya. Miaka yote ya kuhudumu kati jeshi, nilikuwa nimefuata "sheria zisizosemwa" za ulimwengu kwa ajili ya kujitokeza. Nilikuwa nimefanya mambo mengi ambayo yaliisumbua dhamiri yangu. Nilikuwa nimekuwa tajiri kutokana na mapato yasiyo halali na kuishi maisha ya giza na mapotovu—siku zote nilijiingiza katika dhambi lakini sikuona haya. Halafu, maneno ya Mungu hayakuniruhusu tu kutofautisha mema na mabaya, bali pia yalinifanya nione kwa dhahiri asili ya kuanguka kwangu na upotovu wangu. Ilielekea kuwa mabaa haya yalitoka kwa Shetani. Ilikuwa ni Shetani aliyegeuza nchi hii kuwa kinamasi cha uovu na ukatili ambapo watu wasiokuwa na nguvu na waliokuwa waaminifu walikandamizwa na walijitahidi kuishi huku walio na nguvu, ushawishi na wenye udhalimu walisitawi. Katika jamii hii kulijaa uasi na uongo kama "Kila mtu ajitetee mwenyewe bila kujali jaala ya wengine," "Maafisa huwa hawafanyi mambo kuwa magumu kwa wale ambao hubeba zawadi," "Huwezi kufanikisha chochote bila kujipendekeza sana kwao," "Baadhi ya maafisa wanazingatia tu masilahi yao, sio umma," "Tumia mamlaka ukiwa nayo, kwa sababu yakishaondoka, huwezi kuyatumia," na kadhalika. Nilidanganywa na misemo hii ya kuogofya, na kwa sababu ya ukandamizaji karibu nami nilipoteza njia yangu, nikaziacha kanuni za kibinadamu, kutafuta vyeo vya juu kwa njia isiyo na maadili, na nikafanywa madhubuti katika kinamasi cha dhambi. Hatimaye nikawa pepo mchafu ambaye hakutafuta chochote ila utajiri, nikatumia mamlaka vibaya kwa faida ya kibinafsi, na kufuja fedha za umma. Kutoka kwa hukumu katika maneno ya Mungu, niliona ghadhabu kali na utakatifu wa Mungu, na kuelewa kuwa kukosea tabia Yake ya haki haikuruhusiwa. Nilijutia vitendo vyangu viovu na moyo wangu ulijazwa hofu. Nilihisi kwamba kama haingekuwa kwa ajili ya Mungu kuniokoa wakati ufaao na kunivuta kutoka kwa kinamasi cha uovu, ningelaaniwa na kuadhibiwa na Mungu kwa sababu ya yale niliyoyatenda. Asante Mungu kwa kuniruhusu nione mwanga tena, na kuelewa kanuni za binadamu. Kuanzia wakati huo na kwendelea, sikuwahi tena kamwe kufanya mambo hayo yaliyoleta aibu kwa jina la Mungu.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

0 意見:

Chapisha Maoni