Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI
Utakatifu wa Mungu (III)
Sehemu ya Kwanza
Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu.
Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita. Shetani hutumia maarifa, sayansi, ushirikina, desturi ya kitamaduni, na mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu; hizi ndizo njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Hizi ni njia ngapi kwa jumla? (Tano.) Ni njia zipi tano? (Sayansi, maarifa, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii.) Mnafikiri Shetani anatumia nini zaidi kumpotosha mwanadamu, kitu ambacho kinampotosha kwa kina zaidi? (Desturi ya kitamaduni.) Kaka na dada wengine wanadhani kwamba ni desturi ya kitamaduni. Kuna nyingine? (Maarifa.) Inaonekana kwamba mna kiwango cha juu cha maarifa. Kuna mengine zaidi? (Maarifa.) Mnashiriki mtazamo sawa. Kaka na dada waliosema desturi ya kitamaduni, mnaweza kutueleza mbona mnafikiri hivi? Je, mna uelewa wowote wa jambo hili? Je, hamtaki kueleza uelewa wenu? (Filosofia za Shetani na mafundisho ya Confucius na Mencius zimetopea sana katika akili zetu, kwa hivyo tunahisi kwamba haya yanatupotosha sana.) Wale wanaofikiria kwamba ni maarifa, mnaweza kueleza mbona? Semeni sababu zenu. (Maarifa hayawezi kuturuhusu kumwabudu Mungu. Yanapinga kuwepo kwa Mungu, na yanapinga kanuni ya Mungu. Yaani, maarifa yanatuambia tusome kuanzia umri mdogo, na kwamba ni kupitia tu kusoma na kupata maarifa ndipo siku zetu za baadaye na kudura zetu zinahakikishwa. Kwa njia hii yanatupotosha.) Kwa hivyo Shetani anatumia maarifa kudhibiti siku zako za baadaye na kudura yako, kisha anakuongoza kuendelea kupitia pua lako; hivi ndivyo unavyofikiria Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Kwa hivyo wengi wenu wanafikiri Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu kwa kina. Kuna mengine zaidi? Je, sayansi na mienendo ya kjamii, kwa mfano? Kuna yeyote anayekubaliana na haya? (Ndiyo.) Leo Nitashiriki tena kuhusu njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu, na, baada ya Mimi kumaliza, Nitawauliza baadhi ya maswali ili kuona ni katika kipengele kipi hasa Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Mnaelewa mada hii, siyo?
Upotovu wa Shetani wa mwanadamu unadhihirika kimsingi katika vipengele vitano; hivi vipengele vitano ni njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Ya kwanza kati ya njia hizi tano tulizotaja ni maarifa, kwa hivyo wacha kwanza tuchukue maarifa kama mada ya kushiriki. Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuboreka kila siku,” kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unapopata maarifa zaidi, ndivyo utavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, kwa wakati sawa wanaposoma maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na maadili. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanatembea njia ya aina hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na maadili yao. Hatua kwa hatua, watu bila kujua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani kufikiria kwa watu wakubwa ama maarufu, na kukubali fikira hizi. Wanajifunza pia jambo moja baada ya lingine kutoka kwa matendo ya wengine ambao watu wanachukulia kuwa “mashujaa.” Mnaweza kujua baadhi ya yale ambayo Shetani anatetea kwa mwanadamu katika matendo ya hawa “mashujaa,” ama kile anachotaka kuingiza kwa mwanadamu. Ni kipi ambacho Shetani anaingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya rafiki ya mtu ama kwa rafiki. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi, na anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya Shetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana kuwapata watu, kuchukua chambo polepole. Kwa njia hii, watu wanakuwa na mambo yao ya kupitisha muda na shughuli katika mkondo wa kujifunza kwao: Wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda theolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa na nyote mmepatana nayo. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua yalivyo na mambo haya, kila mmoja amepatana nayo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo kuhusu moja yao fulani. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapenda sehemu ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu amependa kwa dhati mojawapo, basi bila kujua anaendeleza maadili: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, maadili yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya maadili na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Mbona Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi, kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.
Sasa wacha tuzungumze kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kutokana na yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, mmeanza kutambua malengo husuda ya Shetani? (Kidogo.) Mbona Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Anataka kufanya nini kwa mwanadamu kutumia maarifa? Kumwongoza mwanadamu kufuata njia ya aina ipi? (Kumpinga Mungu.) Bila shaka ni kumpinga Mungu. Hii ni athari unayoweza kuona kwa watu wanaojifunza maarifa, na matokeo unayoyaona baada ya kujifunza kwa maarifa—kumpinga Mungu. Hivyo ni nini malengo husuda ya Shetani? Hujayaelewa, sio? Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote ili watu waridhishe tamaa yao wenyewe na kutambua maadili yao. Je, uko wazi kuhusu njia hasa anayotaka Shetani kukuongoza? Bila kutia chumvi, watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Wanafikiri kwamba kukuzaa maadili ya juu ama kuwa na matarajio kunaitwa tu kuwa na hamu ya kupata, na kwamba hii inapaswa kuwa njia sawa ya watu kufuata katika maisha. Iwapo watu wanaweza kupata maadili yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Sio tu kuheshimu babu za mtu kwa njia hiyo bali pia kuacha alama yako katika historia—hili si jambo zuri? Hili ni jambo zuri na linalofaa katika macho ya watu wa kidunia. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake husuda, anawapeleka watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi yalivyo juu maadili ya mwanadamu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa maisha ya kila mtu, na haya ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Moja ni “umaarufu” na nyingine ni “faida”: Ni umaarufu na faida. Shetani anatumia njia ya hila sana, njia ambayo iko pamoja sana na dhana za watu; si aina ya njia kali. Katikati ya kutoelewa, watu wanakuja kukubali njia ya Shetani ya kuishi, kanuni zake za kuishi, kuanzisha malengo ya maisha na mwelekeo wao katika maisha, na kwa kufanya hivyo wanakuja pia bila kujua kuwa na maadili katika maisha. Haijalishi maadili haya yanaonekana kusikika kuwa ya juu kiasi gani katika maisha, ni kisingizio tu ambacho kinahusiana kwa kutochangulika kwa umaarufu na faida. Mtu yeyote aliye mkubwa ama maarufu, watu wote kwa hakika, chochote wanachofuata maishani kinahusiana tu na haya maneno mawili: “umaarufu” na “faida.” Sivyo? (Ndiyo.) Watu hufikiri kwamba punde tu wanapata umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Baada ya wao kuwa na umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao katika kutafuta kwao raha na kufurahia kwao kwa fidhuli mwili. Watu kwa hiari, lakini bila kujua, wanachukua miili na akili zao na vyote walivyonavyo, siku zao za baadaye, na kudura zao na kuzikabidhi zote kwa Shetani ili kupata umaarufu na faida wanayotaka. Watu hufanya hivi kamwe bila kusita kwa muda, kamwe bila kujua haja ya kupata tena yote. Je, watu bado wanaweza kujidhibiti baada ya wao kwenda upande wa Shetani kwa njia hii na kuwa mwaminifu kwake? Bila shaka, la. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Hawawezi kikamilifu na kabisa kujinusuru kutoka kwa bwawa ambamo wamezama ndani. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili silo ukweli? Watu wengine watasema kwamba kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hawajui tayari, wakisema kwamba wanafanya hivi ili wasiwe nyuma ya nyakati ama wasiwachwe nyuma na dunia. Watasema kwamba maarifa yanafunzwa tu ili waweke chakula mezani, kwa sababu ya siku zao za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi. Sasa unaweza kuniambia iwapo kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? (La, hakuna.) Hakuna watu kama hawa! Kwa hivyo ni nini anatesekea matatizo haya na kutesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamgoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia haya yanayoitwa maarifa kwa hakika ni nini? Si kanuni za kuishi na njia ya kupitia maisha iliyoingizwa kwa watu na Shetani, iliyofundishwa kwao na Shetani katika kujifunza kwao maarifa? Je, si maadili ya juu ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri ya watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye panga katika riwaya za kareti; mawazo haya yanashawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya, kuishi kwa sababu ya mawazo haya na kuyafuata bila kikomo. Hii ndiyo njia, mbinu, ambayo Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa hivyo baada ya Shetani kuwaongoza watu kwa njia ya umaarufu na faida, inawezekana wao kumwamini Mungu bado, kumwabudu Yeye? (La, haiwezekani.) Je, maarifa na kanuni za kuishi zilizoingizwa kwa mwanadamu na Shetani zina fikira yoyote ya kumwabudu Mungu? Zina fikira yoyote ya ukweli? (La, hazina.) Je, zina uhalisi wowote wa kumcha Mungu na kuepuka uovu. (La, hazina.) Mnaonekana kuongea kwa uhakika kidogo, lakini haijalishi. Tafuteni ukweli kwa mambo yote na mtapata majibu sahihi; ni kwa majibu sahihi tu mnaweza basi kutembea njia sahihi.
Wacha turejelee tena kwa ufupi: Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa katika miili ya watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo watu kamwe wanatembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa, wakibeba pingu hizi bila kujua. Kwa ajili ya umaarufu na faida, binadamu hutenganishwa na Mungu na anamsaliti. Kwa kupita kwa kila kizazi, binadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mweusi wa moyo zaidi na zaidi, na hivyo kwa njia hii kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, ni nini hasa nia zake husuda? Ni wazi sasa, sivyo? Shetani si wa kuchukiza? (Ndiyo!) Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu; hapo tu ndipo utaweza kutembea njia sahihi ya uhai katika ufuataji wa ukweli.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
0 意見:
Chapisha Maoni