Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Tamko la Sita
Kwa masuala ya ndani ya roho, mnapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, mnapaswa kuwa wasikivu kwa makini.
Mnapaswa kulenga hali ambayo mnaona Roho Wangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, ili ubinadamu wote utaweza kuniridhisha mbele Yangu. Nimeukanyaga ulimwenguni kwa miguu Yangu, Nikinyoosha macho Yangu juu ya anga yake nzima, na Nimetembea miongoni mwa wanadamu wote, Nikionja ladha tamu, ya asidi, chungu, na kali za uzoefu wa binadamu, lakini mwanadamu hakuwahi kweli kunitambua, wala hakuniona Nikitembea ng’ambo. Kwa sababu Nilikuwa kimya, na Sikutekeleza matendo ya mwujiza, kwa sababu ya hili hakuna yeyote aliyeniona kwa kweli. Mambo hayako sasa kama yalivyokuwa wakati mmoja: Naenda kufanya mambo ambayo, tangu mwanzo wa uumbaji, dunia haijawahi kuyaona, Naenda kusema maneno ambayo, kotekote katika enzi nyingi, wanadamu hawajawahi kuyasikia, kwa sababu Nataka ubinadamu wote uje kunijua katika mwili. Hizi ndizo hatua katika usimamizi Wangu, ambazo ubinadamu hauzijui hata kidogo. Hata Ninapozizungumzia wazi, mwanadamu bado amechanganyikiwa sana kwa akili yake mpaka haiwezekani kumwelezea katika kila utondoti. Katika jambo hili kuna hali duni kabisa ya mwanadamu, sivyo? Hili hasa ndilo Nataka kurekebisha kwake, sivyo? Hii miaka yote, Sijafanya kazi yoyote kwa mwanadamu; hii miaka yote, hata waliowasiliana moja kwa moja na mwili Wangu hawakusikia sauti iliyotoka moja kwa moja kwa uungu Wangu. Na kwa hiyo haiwezi kuepukika kwamba wanadamu wanapungukiwa katika ufahamu wao Kwangu, lakini hiki kitu kimoja pekee hakijaathiri upendo wa ubinadamu Kwangu katika enzi. Sasa, hata hivyo, Nimewafanyia kazi nyingi ya kimiujiza na isiyoeleweka na pia Nimewaambia maneno mengi. Na bado, hata chini ya hali kama hizi, watu wengi bado wananipinga mbele Yangu. Wacha Niwape mifano michache:
Kila siku mnasali kwa Mungu asiye dhahiri, mkijaribu kufahamu nia Zangu, kupata hisia ya maisha. Lakini, wakati maneno Yangu kweli yanakuja chini, mnayaangalia tofauti: mnayachukua maneno Yangu na Roho Wangu kama kitu kimoja kisichogawanyika, lakini mnamweka kando mwanadamu, mkifikiria kwamba mwanadamu Niliye hawezi kuyatamka maneno ya aina hii, na kwamba badala yake ni matokeo ya kupanga kwa Roho Wangu. Mngejuaje kuhusu hali kama hii? Mnayaamini maneno Yangu kwa kiasi fulani, lakini kwa mwili Ninaovaa, kwa kiasi kikubwa au kidogo mnayafikiria mawazo yenu wenyewe, mnayoyatafakari siku baada ya siku, mkisema: “Mbona Anafanya mambo kwa njia hiyo? Inawezekana kwamba hili linatoka kwa Mungu? Haiwezekani! Kwa mtazamo wangu, Yeye ni sawa nami—mtu wa kawaida,” Tena, mnawezaje kuelezea hali kama hii?
Kuhusu Niliyoyasema hapo juu, kuna yeyote miongoni mwenu asiyeandaliwa nayo? Yeyote asiyeyamiliki? Ingeonekana kuwa kitu unachoshikilia kama kipande cha mali binafsi, na wakati huu wote umekuwa ukisita kukiachilia. Bado hamjakuwa tayari kufuatilia juhudi amilifu; badala yake mnanisubiri Nifanye kazi binafsi. Kusema ukweli, hakuna binadamu hata mmoja ambaye, bila kunitafuta, anakuja kunijua kwa urahisi. Hakika, haya si maneno ya juujuu ambayo Nawahubiria somo, kwa sababu Naweza kutoa mfano kutoka kwa pembe tofauti kwa ili urejelee.
Punde tu anapotajwa Petro, kila mtu anajawa na sifa, akikumbushwa mara moja hizi hadithi zote kumhusu Petro—jinsi alikana kumjua Mungu mara tatu na zaidi ya hayo akamhudumia Shetani, na hivyo akamjaribu Mungu, lakini mwishowe alipigiliwa misumari msalabani juu chini kwa ajili Yake, na kadhalika. Sasa Naweka umuhimu mkubwa katika kuwasimulia jinsi Petro alikuja kunijua na pia matokeo yake ya mwisho. Huyu mwanadamu Petro alikuwa na ubora wa tabia sana, lakini hali zake zilikuwa tofauti na zile za Paulo. Wazazi wake walinitesa, walikuwa wa mapepo yaliyomilikiwa na Shetani, na kwa sababu hii mtu hawezi kusema kwamba walipitisha njia kwa Petro. Petro alikuwa na busara nyepesi, alipewa akili asili, alipendwa sana kutoka utotoni na wazazi wake; baada ya kukua, hata hivyo, akawa adui yao, kwani daima alitaka kunijua, na hili lilimfanya awapuuze wazazi wake. Hii ilikuwa kwa sababu, kwanza kabisa, aliamini kwamba mbingu na dunia na vitu vyote viko mikononi mwa Mwenyezi, na kwamba vitu vyote vya hakika vinatoka kwa Mungu na vinakuja moja kwa moja kutoka Kwake, bila kupitia usindikaji wowote na Shetani. Na mfano usiofaa wa wazazi wake kuwa kama foili,[a] hili lilimwezesha kwa urahisi kutambua upendo Wangu na huruma, na hivyo kuchochea ndani yake hamu kubwa zaidi ya kunitafuta. Alikuwa makini sana sio tu kula na kunywa maneno Yangu, lakini hata zaidi kufahamu nia Zangu, na daima alikuwa na busara na mwenye kutahadhari katika mawazo yake, ili daima alikuwa mwerevu kwa makini ndani ya roho yake, na hivyo aliweza kuniridhisha kwa yote aliyofanya. Katika maisha ya kawaida, alikuwa makini kuunganisha masomo ya wale walioshindwa katika siku za nyuma ili kujichochea kufanya juhudi kubwa zaidi, akihofia sana kwamba anaweza kuanguka ndani ya nyavu za ushinde. Alikuwa pia makini kupata imani na upendo wa wote ambao kupitia enzi nyingi walikuwa wamempenda Mungu. Kwa njia hii, aliharakisha maendeleo ya ukuaji wake sio tu kwa masuala hasi, lakini hasa kwa masuala ya hakika, hadi akawa mbele Yangu mwanadamu pekee aliyenijua bora zaidi. Kwa sababu hii, si vigumu kuwazia jinsi alivyoweza kuweka yote aliyokuwa nayo mikononi Mwangu, kukosa kuwa tena bwana wake mwenyewe hata kwa kula, kuvaa, kulala, ama mahali aliishi, lakini alifanya kuniridhisha kwa mambo yote msingi ambao alifurahia fadhila Yangu. Mara nyingi Nilimweka chini ya majaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema Nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni kutekeleza kanuni zake ili kutimiza pendo lake Kwangu. Nilipomwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa mikononi mwa Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake bali yalikuwa majaribio kwa njia ya maneno, bado alisali Kwangu: Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; Unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu waweza kuteseka, nafarijiwa ndani ya roho yangu. Ningewezaje kukosa kusifu hekima Yako na matendo Yako? Hata nikifa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari na radhi. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniacha nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Yawezekana kwamba kuna kitu ndani yangu Usichotaka kuona? Katikati ya majaribio ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu kwake binafsi kutumiwa na Mimi (iwe ni kupokea tu hukumu Yangu ili ubinadamu uweze kuona uadhama na ghadhabu Yangu), na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Je, huu hasa si mfano mnaopaswa kufuata? Wakati huu, mnapaswa kufikiria sana na kujaribu kutatua ni kwa nini Nimepeana ripoti ndefu ya Petro kama hii. Hii inapaswa kutumika kama kanuni ya maadili.
Hata kama kuna watu wachache sana wanaonijua, Sitatoa, kwa ajili ya hayo, hasira Yangu kwa ubinadamu, kwa sababu wanadamu wana dosari nyingi sana mpaka ni vigumu kwao kufikia kiwango Ninachotaka kwao. Na kwa hiyo Nimekuwa na huruma kwa ubinadamu kwa maelfu ya miaka, hadi siku hii. Lakini Natumai kwamba hamtakuwa tayari sana, kwa sababu ya huruma Yangu, kujiendekeza ; mnapaswa badala yake, kupitia Petro, kuja kunijua na kunitaka, na kupitia hadithi zote za Petro, mpate ufunuo kwa njia ya pekee, na kwa njia hii kufika kwa ulimwengu ambao haukufikiwa na ubinadamu awali. Kotekote katika ulimwengu na maeneo yasiyo na kikomo ya anga, mambo lukuki ya uumbaji, mambo lukuki duniani, na mambo lukuki mbinguni yote yanatakasa nguvu yao yote kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kazi Yangu. Hakika hamtamani kubakia watazamaji walio kando, wanaoendeshwa hapa na pale na nguvu za Shetani? Shetani daima anagugumia maarifa ambayo wanadamu wameshikilia kunihusu mioyoni mwao, na siku zote, kwa meno na makucha wazi, akishiriki kwa maumivu ya mwisho ya mapambano yake ya kifo. Je, mnataka kukamatwa na mipango yake danganyifu wakati huu? Mnataka, wakati awamu ya mwisho ya kazi Yangu imekamilika, kukata maisha yenu wenyewe? Hakika bado hamnisubiri Nitoe huruma Yangu mara nyingine tena? Kutaka kunijua ndilo jambo muhimu sana, lakini hampaswi pia kupuuza kuzingatia utendaji halisi. Nafichua ufahamu kwenu moja kwa moja kwa maneno Yangu, kwa matumaini kwamba mtaweza kuukubali mwongozo Wangu, na kukoma kuyafikiria matarajio ama miundo yenu wenyewe.
Februari 27, 1992
Tanbihi:
a. Foili. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kulinganishwa.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Soma Zaidi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?
0 意見:
Chapisha Maoni